Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,305
- 11,165
Wengine wanaweza kusema swali hilo ni kichekesho, lakini hali ilivyo sasa ni swali linalokwenda na wakati na kutaka kupatiwa jibu lake.
Tangu wanamgambo wa Houthi waanze kuingia kwenye mapambano kuwasaidia wenzao wa Gaza, Marekani imekuwa ikikasirika sana na hata kuwahi kusema Yemen ni rogue nation inayopasa kushughulikiwa.
Wanamgambo wa Houthi ambao ndio wanaoitawala Yemen hawajaonekana kutishika na maneno hayo ya Marekani kwani hapo juzi walizitia mchakamchaka meli 4 zenye mahusiano na Israel ikiwemo meli ya kivita ya Marekani yenyewe. Meli hiyo ya USS corney ilirushiwa kombora na droni na haijajulikana kwa uhakika madhara iliyopata.
Katika hali hiyo jee Marekani ina uwezo wa kuingia vitani na wanamgambo hao ili iwaondoe madarakani na kuihakikishia usalama wake Israel.
Hali za kisiasa duniani na uwezo wa kijeshi na kiuchumi wa Marekani jee unaipa nguvu nchi hiyo kupigana na Houthi na kuishinda na mwishowe kuweka kiongozi kibaraka watakayemchagua?
Ikumbukwe kuwa Houthi ni watawala wa taifa dhaifu sana lakini wamekalia eneo muhimu sana kiuchumi wa dunia na mienendo ya kijeshi. Kupambana nao mpaka kuwashinda moja kwa moja kunaweza kukamaliza nguvu zote za mtu huyo atakayejaribu kuingia vitani nao