Je Laana ya Umasikini wa Tanzania Haijaletwa na CCM?Tanzania?

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Imeelezwa na watu mbalimbali, mabalozi wanchi za nje na taasisi kadha za ndani na nje ya Tanzania; kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini na fukara duniani. Ingawa nchi hii ni tajiri kwa raslimali inayomezewa mate na mataifa mengi duniani. Imesemwa Tanzania ina utajiri katika maeneo yafuatayo:
  1. Ina akiba ya madini ya dhahabu nyingi. Ni ya tatu kwa utajiri wa dhahabu Afrika.
  2. Inaongoza duniani kwa kuwa na madini adimu ya Tanzanite yasiyopatikana pengine pote duniani.
  3. Ni ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vya kitalii duniani(mbuga za Serengeti na Ngorongoro zimetukuka kuliko mbuga nyingine zote duniani.
  4. Ni ya kwanza Afrika mashariki kwa kuwa na mito na vianzo vingi vya maji( maziwa zaidi ya 10)
  5. Ina mlima mrefu kuliko yote Afrika
  6. Ina utajiri wa aina mbali mbali za madini( almasi, urani, rubby, cobati, makaa ya mawe, chuma nk)
  7. Ni nchi ya tatu duniani inayopokea misaada kwa wingi toka nje.
  8. Ni ya tatu katika Afrika kwa kuwa na mifugo mingi mfano ng'ombe nk
  9. Ni kati ya nchi chache duniani yenye watu kidogo kwa kila kilometa moja ya mraba ya ardhi yenye rutuba.
  10. Ni ya kwanza katika Afrika ambayo ina vyanzo vingi vya nishati ya umeme( maji, gesi asili, makaa ya mawe, upepo wenye kasi, joto ardhi nk)

Swali langu ninalojiuliza imekuwaje Tanzania inaishi kwenye lindi la ufukara na umasiki? Shule hazina vifaa, walimu, nyumba za walimu nk. Hospitali hazina vifaa, hazina madawa, hazina watumishi nk.

Je, sio kwamba tumelaaniwa kwa kuwa tumeichagua CCM kututawala? Kumbuka wana wa Israel walitaka watawaliwe na mfalme badala ya Mungu. Wakampata mfalme Sauli. Ufisadi ukaivaa nchi-Biblia. Naona hata sisi tunakwenda hivyo. Viongozi wetu hawamtumaini Mungu wa Mbinguni kuiongoza nchi, badala yake wanatawala kwa kupitia mizimu na matambiko.
 
Back
Top Bottom