Je, kwa haya maamuzi tukisema kuwa huenda GSM alikuwa anatafuta vita ya kibiashara na Azam siku nyingi tutakuwa tunakosea?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,128
110,523
GENTAMYCINE sitaki kabisa kuamini kuwa haya maamuzi ninayoyaita ya kipumbavu na kishamba yaliyofanywa na Kiongozi wa Matawi wa Yanga SC Mkoa wa Dar es Salaam ya kuwataka wana Yanga SC wote kususia kununua bidhaa zozote zile za Azam yamefanywa kwa ama bahati mbaya au kwa kukurupuka tu.

Ukituliza akili yako vizuri hapa utagundua ya kwamba GSM alikuwa anaitafuta siku nyingi sana hii Hhli itokee ili sababu ipatikane na yeye atumie huo mwanya kujiimarisha kibiashara lakini pia nae kuanza kuuza bidhaa baadhi ambazo Kampuni ya Azam inatengeneza na hata kubumi zaidi.

Kuna taarifa nimepenyezewa kuwa kumbe hata GSM nae yuko mbioni kuanzisha Kampuni ya kutengeneza bidhaa (products) zote anazotengeneza Azam akiwa na lengo kuu la kutaka kuliteka Soko la Tanzania.

Ambapo kwa msaada mkubwa anaopewa na Mstaafu mmoja mwenye ushawishi mkubwa katika Awamu ya Sita hii huenda hili likawezekana na hata dalili fulani fulani zimeshaanza kujitokeza.

Sasa ni wazi vita ya GSM na AZAM ndiyo imeshaanza hivyo na kuna Uwezekano mkubwa kuanzia sasa Utajiri mkubwa wa Mzee Bakhressa ukawa tempered Kimakusudi na Watu wa Kodi kwa Maagizo ya Watu wa Mamlaka wenye Uyanga Uliotukuka kwa Ushawishi mkubwa wa Mstaafu ambaye inasemekana katika Utajiri wa GSM Yeye ana Share kama 75% hivi ila GSM anapaishwa Kimkakati ili Kuwazuga Watanzania wasimjue Mmiliki Mkuu aliye nyuma ya GSM.
 
GSM Mimi GENTAMYCINE nitakuona nawe ni Hamnazo ( yaani huna Akili ) kama ukiyafurahia Maamuzi ninayoyaita ya Kipumbavu na Kiuwendawazimu yaliyofanywa na Uongozi wa Matawi ya Yanga SC Mkoa wa Dar es Salaam ya kuwataka wana Yanga SC wote Wasusie Kununua Bidhaa ( Products ) za Kampuni ya Azam.

Najua kwa sasa GSM unaweza ukaiona hii Kwako ni kama vile Opportunity ya Kujiimarisha zaidi Kibiashara ila nakuhakilkishia kuwa hata Wewe inaweza kuja Kukuathiri pakubwa Kibiashara na usije Kuamini.

Sitaki Kuamini kuwa wanaonunua Bidhaa ( Products ) za GSM ni wana Yanga SC tu peke yao bali GENTAMYCINE naamini kuwa hata wana Simba SC na wana Azam FC na wengi tu wananunua tena huenda Wao ndiyo wakawa Wananunua Vingi na kwa Uwingi kuliko wana Yanga SC.

GSM kama Watu wenu wa Matawi wa Yanga SC wamekuja na Uamuzi huu je, unadhani kwa Urafiki mkubwa na Uhusiano uliopo kati ya Tajiri wa Kampuni ya Azam Mzee Bakhressa ( ambaye pia ni Mwanachama Hai wa Simba SC ) nae pia akiamua Kuingia katika Vita hii ya Kukomoana huku Kibiashara nae akiwashawishi wana Simba SC wote nchini nao Wasusie Kununua Bidhaa ( Products ) zozote zile za GSM utakuwa Salama Kibiashara na Sokoni?

Ombi langu Jema Kwako GSM waambie upesi hawa wana Yanga SC ( hasa Uongozi wa Matawi ) waliofanya Maamuzi haya Jana waache mara moja na ikiwezekana hata hiyo Kauli waifute kwani Kwanza si ya Kimichezo halafu waambie kuwa Adui yao Yanga SC ni Azam FC na siyo Azam Company hivyo Siku zingine watumie Akili ( ambazo hawana ) kabla hawajakurupuka na kutufanya tuyaamini maneno ya Mhamasishaji Mkuu wenu Haji Manara kuwa Yanga SC nzima Wenye Akili ni Rais Mstaafu Kikwete, Baba yake Mzee Manara na Mama Karume ila waliobaki wote ( nawe ukiwemo ) hamna Akili.
 
Ila biashara za hawa wawili haziingiliani sana labda kwenye ICD

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Ushaambiwa kuwa GSM nae anataka aanze kuzalisha GSM Energy drink, GSM Cola, GSM Ukwaju, GSM Embe, GSM Unga, GSM Chapati, GSM Sukari na mataka taka yote unayoyajua kuwa Azam anatengeneza. Inshort wanataka kuwa direct competitors wa Azam products.
 
Mafala sana haya ma Gsm..binafsi ni shabiki wa Simba lakini nilinunua godoro lao sasa kwa hasira ninaenda kumpa mwanautopolo. Godoro lilikua zuri na lina viwango, sasa kwa utopolo huu bora nikamkabidhi mwanautopolo yoyote bure.
Genta pendekeza mwanautopolo nimpe bure godoro hili la inch 12.
 
Lini hivi vilabu vya simba na yanga, vitauzwa na vimilikie na watu binafsi?,kinyume cha hapo maendeleo ya soka nchi hii itakua zero na politicians wanatumia mgongo wa vilabu hivi kuendelea ile status ago yao, piga mnada hizi clubs ili ziendeshwe kikampuni, CEOs wawajibike kwa owners sio haya ya sasa
 
Mafala sana haya ma Gsm..binafsi ni shabiki wa Simba lakini nilinunua godoro lao sasa kwa hasira ninaenda kumpa mwanautopolo. Godoro lilikua zuri na lina viwango, sasa kwa utopolo huu bora nikamkabidhi mwanautopolo yoyote bure.
Genta pendekeza mwanautopolo nimpe bure godoro hili la inch 12.
Mpe Frank Wanjiru atakushukuru sana kwani kwa sasa analalia Mkeka tu.
 
Back
Top Bottom