analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 729
- 612
Ndugu wana JF, Tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia jinsi kituo cha TV cha TBC kinavyokandamiza upinzani, hasa chama kilichojidhihirisha kuwa ni tishio kwa chama tawala mwaka huu,kwa kuwalimit ni mambo gani wazungumzie kwenye kampeni, na hata kuonyesha habari za kampeni zilizochakachuliwa. Mimi nafikiri ni wakati muafaka, kwa vyama hivi kuanzisha vituo vya TV ili kuhakikisha ujumbe wa ukombozi ambao chama tawala usingependa wananchi uwafikie, unawafikia wananchi kama inavyokusudiwa.