Je kukondeana ni dalili ya kuwa na roho mbaya...................?

Nahisi kuna ukweli hapa, mtu mwenye roho mbaya hali akashiba, roho yake huwa inasononeka akiona mwenzie kaapata, yaani roho yake iko juu juu tu. hii inatokana na kutokuwa na peace of mind.
 
Hii ni kweli kabisa.
Lakini ni generalisation tu so sio wote ni hivyo.
Hayo mambo ya wivu, kutosamehe, etc. hayo yote ni dhambi tu
Na mshahara wa dhambi ni......
Mwili hukosa nguvu na mtu anakuwa mgonjwa mgonjwa tu.
 
Kumbe...asante mtambuzi ila wngine wanazaliwa kamwili kako hivi mpaka wanakuwa hawabadiliki
sometimes nadhani ni maumbile na sometimes ni mambo kama hayo uliyosema
 
si kweli! kwa mana walioishikilia hii nchi wengi ni wanene na wanaroho mbaya sana sana sana! lakini wanao itetea hii nchi wengi ni wembamba na wanaroho safi sana sana sana! mpaka wanaamua kuitetea nchi yao.
angalieni watu maarufu wote ambao wenye roho nzuri wengi ni wembamba, na wengi wanene ni roho mbaya mnooo.
hata adamu na eva walikuwa wembamba! na manabii wengi walikuwa wembamba.
dunia ya sasa wengi ni wanene kwa vya uharamu! pombe,ufisadi, kula vyakula kwa kudhulumu n.k
anayekuwa mwembamba kwasababu ya mtu fulani, ujue anachukia yale mabaya yanayofanywa na mtu huyo.
mifano tazameni nchi yenu na viongozi wake,celebrit wake n.k na pia angalienie viongozi wa nje wenye roho nzuri na maceleb wao na watu maarufu wenye roho safi.
Kukondeana na wembamba ni vitu viwili tofauti. sio kweli kwamba mtu mwembamba amekondeana. Ila wengi ya waliokondena wana roho mbaya...naungana na mtoa mada.
 
Naomba kujua maana ya kukondeana na wembamba. Kuna watu ni wembamba kwa sababu za kibiolojia (genetics) kama mimi. Moyo wangu ni msafi, hata mtu akinikwaza huwa sioni sababu ya kubeba mizigo ya mawazo au kutumia nguvu kupambana, nimekuwa nikila mlo sahihi lakini nyama haziongezeki jkabisa. Tumekuwa tukiandamwa sana kwa kuwa na miili mwembamba, hata kutaka kuanzisha chama cha watu wembamba Tanzania.
 
kuna mtu akiona hata inzi kaingia chooni kwake au ametua kwenye kinyesi chake atakasrika na lazma amfukuze, si sababu ya usafi, la hasha anaumia kwa nini anafaidi jasho lake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom