zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Baada ya ufafanuzi uliopewa hapo juu ndio umepata hitimisho kuwa kiswahili ni CHOTARA?.
Mkuu kiswahili ni KIBANTU full stop.
Kwanini kibantu? lugha zote duniani zina asili yake na asili ya kiswahili ni kibantu kwa maana ya kuwa iliasili utamkwaji aka rithm au kwa maana nyingine pronaunciation yake ni ya kibantu licha ya kukopa maneno lukuki kutoka katika kiarabu.
Moja ya sifa ya lugha ni namna unavyotamka maneno pronaunciation, ndio maana mengi ya hayo maneno ya kiarabu hayatamkwi exactly kama waarabu wenyewe wanavyo yatamka na kuyaandika.
Kibantu si kabila ila inamaana ujumla wa makabila yaliyozaliwa katika asili moja yanayo share baadhi ya maneno na utamkwaji na hii inafanya kiswahili kuwa kibantu.
Najua kwanini katika wote waliotoa michango umemkubali zaidi ZOMBA ni kwasababu unaelekea kuipeleka hoja hii ktk udini, ionekane atutaki kusema ni kiarabu kwakuwa kiarabu kina uislam ndani yake(which is not true) naamini ndugu yangu umepitia madrassa unaweza kulinganisha maneno mliyojifunza huko kimatamshi yapo sawa na yaliyotoholewa kuwa kiswahili? mfano sahil na mswahili, ni wazi utamkwaji upo tofauti yaliyotoholewa yanatamkwa ktk tone ya kibantu.
Mwisho mkuu zomba inferiority complex ndio inayo kusumbua wewe na wenzio mnaodhani watu wapo kupinga uislam tu, hapana watu wapo bize kujenga mahospitali, mashule, mavyuo mabenki nk ili watu kama ninyi mpate huduma huko serikali iliposhindwa na si kukomalia kiswahili ni kiarabu, haiwasaidii
Naomba pitia hiyo risala yako utazame ni maneno mangapi humo unaweza kusema ya asili ya kiarabu na mangapi yana asili ya ubantu.
Point yako ya lafdhi, haina mantiki kwa sababu hiki kiswahili chenyewe lafdhi tofauti hutumika kulinganisha na sehemu kitumiwacho. Mfano, kiswahili ni lugha mama ya waswahili (watu wa pwani ya Afrika Mashariki), lakini hubadilika lafdhi mji mpaka mji wa pwani hiyo hiyo. Kwa hiyo huwezi kusema kuwa lafdhi ndio inakifanya kiswahili kuwa Kibantu. Kiswahili ni maneno ya lugha nyingi lakini kiarabu ndio chenye maneno asilimia kubwa katika kiswahili kuliko lugha nyingine yeyote. Kama unabisha kwa hilo tuanze kuhisabu maneno ya kiswahili.
Pia napenda ujuwe kuwa kiswahili kilijulikana kama lugha ya waIslam, kwani hao waswahili wenye asili ya kiswahili wengi wao 99% ni waIslam.