Je, huu sio uvunjaji wa haki za msingi za binadamu unaofanywa na serikali ya Magufuli?

Na wala hakuna mabadiliko yanayotokea overnight. Kama akili yako imeganda kwenye MRI na CTS basi reasoning capacity yako ni tatizo.

Katika nchi za kibepari una uhakika kila kitu huwekwa wazi hata katika initial stages? Kumbe na wewe ni mweupe kiasi hiki!!? Ikiwa hivi utakavyo wewe unafikiri intelligence agencies zitafanyaje kazi? Kwamba kila kinachotokea umeshaambiwa sababu yake. Mengine yanafichwa kwanza ili jambo muhimu likamilike. Hii ni standard dunia nzima hata kwa hao unaowasifia. Angalia mambo waliyoyatoa akina Snowden and learn something. Usiwe mtu wa kulalamika lalamika tu. Waliomzuia wanaelewa haki za binadamu kuliko wewe unayetazama kitabu kwa nje na kuhukumu.

Now this is what we call "Comparing apples with oranges"

Snowden alifanya espionage.US kuna taasisi imara za uwajikaji.Rais amedhibitiwa kikatiba na mamlaka yake yapo checked.

Hapa unalinganisha na nchi ambayo watawala wanataka kujifanya miungu watu na kutozingatia hata sheria na katiba mbovu iliyopo

Hujui hata unachotetea/pigania. Uko confused !
 
ni ngumu sana kumwelewa magufuli kwa mtu mwenye akili kama yako.
Kwakuwa akili yako inafikiria hapa ulipo sasa na si wakat ujao hutakuja kumwelewa magufuli na utaishia kulalamika tu.

Mambo mengne sio kila mtu ajue kuwa kwann inakuwa hivi. Kwakuwa hujui yanayoendelea ndan ya nchi hii na htajua kuwa kwann magufuli amezuia hizo safari ila secret service ndio inayoweza kujua kuwa kwann kazuia safar.

Na ujue hata ndan ya nyumba ukishaona mkeo ni mlopokaji inatakiwa sio kila unalofanya alijue na inatakiwa hata mshahara wako asijue kias flan kinaenda wapi. Japo ataweza kulalamika kuwa unamnyima uhuru wa kujua mambo yenu lakn siku ya siku atakapokuja kuona matokeo mazuri ya kias cha mshahara ulichokuwa unamficha hapo ndio ataanza kukusifia.

Kwa maelezo na picha unayoijenga hapa,ulipaswa kuwa mume/baba wa familia karne tatu zilizopita
 
Ni nyie nyie mnaonung'unika kuwa haki za binadamu zinavunjwa ndio hamuishi kutuambia kuwa Balali yupo hai ila kaminya tu sehemu. Wote tunafahamu kuwa BoT ndiko kuna chumvi ya Taifa, sasa mbona msitie shaka kuwa yawezekana kajamaa kanataka kusepa mamoja?

Hakuna kupumzika wala nini, kama ni beach aende Coco kabla haijauzwa. Umeshaambiwa ni KIGOGO, tena haikupaswa kuzuiwa tu, angecharazwa na bakora kwa kosa la kuondoka darasani huku mwalimu anafundisha
Kuna mijitu iko kwenye Payroll ya madalali.
 
Ben Saanane na Pasco ni vyema mkawa mnasoma sheria vinzuri na mkazielewa. Pia badala ya kuangalia katiba tu mlipaswa kuangalia na HR policy ya BOT inasemaje, pamoja na hayo pia mlipaswa kuangalia sheria ya utumishi wa umma inasemaje.
attachment.php

Maboso,

Ikitokea mkanganyiko kati ya Katiba na Sheria au kanuni ndogondogo ni kipi hutamalaki?

Constitutional Supremacy !
 
Last edited by a moderator:
Sheria za Utumishi wa Umma zipo nyingi tu na hiyo inayomtaka mtumishi kupata ridhaa ya likizo na pia akiwa anataka kusafiri nje ya nchi ipo. Sababu zinaeleweka kwa watumishi husika. Kwa kuwa wewe si Mtumishi wa Umma ndio huelewi. Hajatunga Magufuli amezikuta na anazisimamia. Uvivu uliokidhiri kwa mtumishi kuto kusoma, kuzielewa na kufuata taratibu zilizopo. Sasa kila mfanyakazi aamke ajielimishe na kanuni za Utumishi sio kulalamika bila kufuata sheria. Ni aibu kwa Mtumisi wenye cheo cha Mkurugenzi kutoifahamu hilo je atasimama vipi walio chini yake. Narudiani ni aibu.
 
Binafsi nimefanya kazi kwa muda mrefu na serikali na nafahamu vizuri sheria za kusafiri nje ya nchi. Kwanza tujue kuwa kuomba kibali cha kusafiri kwenda nje ya nchi hakijaanza leo, ni tangu enzi za Mwalimu. Kilichokuwepo ni kukosa usimamizi. Tangu miaka hiyo, unajaza fomu 2 moja inaishia wizarani au kwa mwajiri wako (mkurugenzi, Katibu Mkuu). Ya pili inakwenda Ikulu. Na unajaza tu unapokuwa kwa shughuli za kikazi.

Najua, wengi mnajua, airport kuna taratibu gani za kuasafiri. Hakuana anayeangalia kibali cha kusafiri mtu zaidi ya Visa na pengine kama kuna kitu kinaleta sintofahamu barua ya mwaliko.

Kama kunatokea kitu kama hiki hasa kwa mtumishi wa umma, kuna cha zaidi. Tujipe muda, nchi inafukuta na watu wengine wanatafuta pa kutokea. Kama hana shida kwani alijitambulisha au kuna reja ya wafanyakazi Airport. Hakuna!!!!

Hatuwezi kuja na majibu ya jumla hata aliyekataliwa tunafahamiana sana naye.

mkuu ni nani huyo aliyekataliwa?
 
Mkuu waweza nithibitishia mahali nilikotaka tuwe na rais wa aina hii?

Mkuu Ben

Sikutarajia ungeomba nithibitishe hili. Maana implication ya maandiko yako kadhaa imejidhihirisha kuhitaji kiongozi mwenye uthubutu wa kuongoza kwa "mkono wa chuma". Hitaji lako kwamba nithibitishe pengine ukimaanisha ninukuu andiko lako linanipa picha tofauti kidogo kuhusu consistency ya uchambuzi wako makini.
 
Mkuu Ben

Sikutarajia ungeomba nithibitishe hili. Maana implication ya maandiko yako kadhaa imejidhihirisha kuhitaji kiongozi mwenye uthubutu wa kuongoza kwa "mkono wa chuma". Hitaji lako kwamba nithibitishe pengine ukimaanisha ninukuu andiko lako linanipa picha tofauti kidogo kuhusu consistency ya uchambuzi wako makini.

Absurd conclussion....
 
Labda watendaji wanaitekeleza vibaya kama kawawa wakati wa vijiji vya ujamaa, nia ya mwalimu Jk ilikuwa njema bali baadhi ya watendaji watekelezaji walihamisha watu kwa nguvu hata kuchoma makazi yao moto.
Huenda zuio hili halijafafanuliwa vizuri.
 
Ndo Atumie Pesa Za Umma? Ndo Atumie Muda Wa Kazi Kwenda Nje? ALIPOULIZWA GHARAMA ZA SAFARI KAZIPATAJE HAKUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA ALIKOTOA PESA ZA KUGHARAMIA SAFARI YAKE, Alijichanganya Kwenye Maelezo Yake Na Ndiyo Maana Akazuiliwa, Sasa Hapo Ni Haki Ipi Iliyovunjwa? Sana Sana Yeye Ndo Alitaka Kuiibia Serikali Muda, Pesa Na Nguvu Kazi Yake Angetoweka Nayo, HEKO MAGUFULI, HEKO MLOMZUIA HUYO KIGOGO UCHWALA.
 
Hiyo hela anayokwenda kutumia ulaya ameitoa wapi kama siyo fisadi pia. Watu kama hawa ndiyo wanatafutwa waseme hizo hela ambazo hazilinganyi na mishahara yao wameitoa wapi?
 
Back
Top Bottom