Je, huu sio uvunjaji wa haki za msingi za binadamu unaofanywa na serikali ya Magufuli?

Subiri UKAWA wakichukuwa nchi ndo mfanye manayoona. Najua hakuna anayependezwa na haya awe CCM au UKAWA ila mabadiliko ya kweli ndo haya. Mtumishi wa serikali inatakiwa ndo awe kioo cha kutii sheria.
mkuu[MENTION]pasco[/MENTION] itafika kipindi tuujue ukweli kuwa mpaka sasa tuko kwenye an undeclared state of emergency lakini wachache hawaoni taa nyekundu za uongozi huu kuanza kuonea watu na kuvunja haki za msingi za raia huku wakitumia media kujionyesha kuwa wako serious na kazi.

haya yanaweza kuonwa na wachache na wanaoweza kukosoa kama wewe. wengine hawana habari nayo hawajali kwa sababu hakuna mwingine anayejali. wao likifanyika baya mradi liwe limefanywa na kiongozi katika utawala mpya wanashangilia likifanyika jema wanashangilia hawaelewi wanaelekea wapi.

kwa awamu ya tano hii naanza kuliona wazi tatizo la kukosa vision, decision making style na delegation yenye tija muda utasema huko tuendako tusubiri tuone.
kuna watu watakuja kusema tunakosoa kwa sababu sisi tuna wivu wa kike hatuyaoni mazuri ya awamu ya tano badala yake tunaona mapungufu tu hawa nao tusiwakatie tamaa tuendelee kusema tunapoona pamefanyika fyongo.

namna ya utendaji wanayoanza nayo viongozi wetu itaumiza wengi hasa pale watakapokabidhi nyundo kwa vichaa bila kuwapa speed governor.
 
Aende tena na tena...mbuga ni kubwa sana hizi...hawezi kuzimaliza na hapo bado hajaenda mapango ya amboni, Udzungwa, mawe ya Isimila, Maporomoko ya maji kalambo (ya pili kwa ukubwa Africa), Mt. Kilimanjaro, Pori la ugalla, Katavi, Serengeti, Mikumi,Selou, Tarangire,Ruaha, Gombe, Saadani, Saanane (visiwa), Zanzibar, Pangani.......dah yaani hadi mkono unauma
IQ ikiwa ndogo, kila kitu kinakua sawa na IQ yenyewe
 
Pasco , Ben Saanane

Nyie sio miongoni mwa waliotaka tuwe na Raisi Mkali?

Raisi atakayeongoza kwa mkono wa chuma?

Ndio tunaanza kuziona faida na hasara za kiongozi wa namna hii mliyemtamani. Au kama vipi tumrejeshe Kikwete
 
Hili ndilo nililotaka kulisema.
Kutaka kujionesha kuwa unamwelewa na unaendana na bosi wako ni kazi ngumu sana kwa wengine.
Alichofanyiwa huyo bosi wa BOT ni uharamia.
Halafu nchi sasa inaonekana kuendeshwa kwa amri binafsi hata za viongozi wasiona mamlaka.
Magufuli atashindwa kwa sababu hajawaandaa watendaji na wasaidizi wake.
Anataka kila mtu atumie intuition binafsi kuongoza.
Pasco, umesahau utekelezaji wa sera ya ujamaa vijijini? Kuna baadhi ya watendaji wa serikali wataenda mbali zaidi ya kile wanachotakiwa wafanye na hivyo kuangukia kwenye huo uvunjaji wa haki za binadamu: umesikia pia sehemu fulani watumishi waliokuwa likizo warudi kazini na kwamba likizo zao zimefutwa na kwamba pia watumishi fulani walichelewa kikao na kuswekwa ndani na DC na tena akaamuru wasipewe dhamana. Just imagine! Kuna msemo kwamba mtu "anakupa mkono wewe unashika bega" - wapi na wapi?
 
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata katika na utawala wa sheria!.

Ndani ya katiba ya JMT kuna vifungu rasmi vya haki za msingi za binaadamu!. Moja ya haki hizo ni kipengele hiki

Kama jambo hili ni kweli limefanyika,
Kigogo wa BoT azuiwa Airport kutokana na kukosa vibali vya kusafiri nje ya nchi

then
Haiwezekani mtu ambaye yuko huru, tena yuko likizo, ameamua kwenda kujipumzikia zake nchi za wenzetu, azuiliwe!.

Nafahamu kuna wafanyakazi wa serikali, na baadhi ya idara nyeti, au hata madakitari, jeshi, polisi na zimamoto, hata wakiwa likizo, wanawajibika kumtaarifu mwajiri wao, likizo yake atakuwa wapi, ili in case of anything, aweze kuwa reached out!, lakini kitendo cha maofisa uhamiaji, kumzuia mtu mwingine yoyote wa serikali, asisafiri nje ya nchi, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu!.

Pasco



Ni mapema mno kutoka Mapovu na kurusha lawama !


 
Ilikuwaje hao wana usalama wakajua huyo bwana ni mtumishi wa BOT, kuna kuna kujitambulisha siku hz hapo Airport au kuna harufu mbaya juu ya huu mkasa?
 
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata katika na utawala wa sheria!.

Ndani ya katiba ya JMT kuna vifungu rasmi vya haki za msingi za binaadamu!. Moja ya haki hizo ni kipengele hiki

Kama jambo hili ni kweli limefanyika,
[h=1]Kigogo wa BoT azuiwa Airport kutokana na kukosa vibali vya kusafiri nje ya nchi[/h] then
Haiwezekani mtu ambaye yuko huru, tena yuko likizo, ameamua kwenda kujipumzikia zake nchi za wenzetu, azuiliwe!.

Nafahamu kuna wafanyakazi wa serikali, na baadhi ya idara nyeti, au hata madakitari, jeshi, polisi na zimamoto, hata wakiwa likizo, wanawajibika kumtaarifu mwajiri wao, likizo yake atakuwa wapi, ili in case of anything, aweze kuwa reached out!, lakini kitendo cha maofisa uhamiaji, kumzuia mtu mwingine yoyote wa serikali, asisafiri nje ya nchi, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu!.

Pamoja na nia nzuri, na nia njema ya Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo na tija kwa taifa, utekelezaji wa kauli hiyo, lazima uzingatie taratibu, sheria na kanuni, na sio kutekelezwa tuu kama zimamoto, na kukiuka haki za msingi za binadamu!.

Ila pia niliwahi kushauri humu, kama baadhi ya sheria, zinaweza kuwa ni kikwazo kwa rais wetu, kututengeneza Tanzania tunayoitaka, rais anayo mamlaka ya kisheria, kuandika waraka, 'decree' kuiweka kando katiba , hivyo kuitawala Tanzania kwa kutumia decree hivyo kuwa huru kufanya jambo lolote atakavyoona inafaa!.

[h=3]Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria Ongoza Kwa Kutumia Decree tuu! [/h]
Viongozi wote wanakula kiapo cha utii wa katiba!, kama katiba inatoa uhuru fulani!, haiwezekana, akaibuka mtu mwingine, kwa mamlaka aliyopewa na katiba hiyo, akauondoa uhuru fulani na haku tunamtazama tuu, au tunamshangilia!. Hili haliwezekani!.

Japo wengi wetu, tunaishi katika lindi la umasikini, uliotopea, na sio tuu hatuna hata hiyo likizo, lakini umasikini wetu, usutufanye tuwachukie, wenzetu waliobahatika kuwa wenye heri, wenye uwezo wa kwenda kujipumzikia zao ulaya wakati wa likizo zao!.

Nashauri serikali itoe waraka wa ufafanuzi wa hili katazo la safari za nje, unless itamkwe wazi, watumizi wote wa umma, hata safari zao binafsi kujipumzikia, au kuwatembelea wapendwa wao, wapenzi wao au hata vimada wao, sasa lazima waombe kibali kwa KMK!, na jee kama hivi ndivyo katiba ilivyotamka?!, kama sio kwa mujibu wa katiba, then rais atoe waraka, Tanzania tujijue tuko kama China au Urusi, enzi zile, kuingia Beijing au Moscow, mtu hujiingilii hivi hivi!.

Jee kumkumbusha rais wetu kuhakikisha watendaji wake wanazingatia katiba aliyoapa kuilinda, ni kumuingilia katika utendaji wake?!.

Pasco

Pasco pasco usiwe na upei finyu. Haunaga HAKI DUNIANI ELEWA HILO. HATA HAO WAMAREKANI WANAOSEMAA WANADEMCRASIA YA HALI YA JUU HAWAPO HIVO. SO MWACHE MR PREZDA AFANYE YAKE. ACHA UMBEYA WA KUINGILIA MAMBO. HAKI HAKI HAKI IKO WAPI ACHA UNAFIKI WEWE. MBONA NAWE HUKUTENDA HAKI KIPINDI KILE IPO SEHEMU FURANI HIVI. WE FANYA YAKO. AFU JUA SIO LAZIMA UMKUBARI MAGUFULI KWA MAMBO YOTE
 
Ni Fikra zilezile za kijima hata wananchi wa nchi za kikomunisti katika muktadha huu hawawezi ku-reason kihivi.Unadhani serikali inao uwezo wa kumnya'anya mtu haki zake tu na ikabakia kuwa serikali inayoheshimika?

Kama la Bade nili-spin,vipi safari za kushtukiza Muhimbili zime-fix MRI na CT-Scan?Mana hilo pia nililikosoa
Na wala hakuna mabadiliko yanayotokea overnight. Kama akili yako imeganda kwenye MRI na CTS basi reasoning capacity yako ni tatizo.

Katika nchi za kibepari una uhakika kila kitu huwekwa wazi hata katika initial stages? Kumbe na wewe ni mweupe kiasi hiki!!? Ikiwa hivi utakavyo wewe unafikiri intelligence agencies zitafanyaje kazi? Kwamba kila kinachotokea umeshaambiwa sababu yake. Mengine yanafichwa kwanza ili jambo muhimu likamilike. Hii ni standard dunia nzima hata kwa hao unaowasifia. Angalia mambo waliyoyatoa akina Snowden and learn something. Usiwe mtu wa kulalamika lalamika tu. Waliomzuia wanaelewa haki za binadamu kuliko wewe unayetazama kitabu kwa nje na kuhukumu.
 
Ni nyie nyie mnaonung'unika kuwa haki za binadamu zinavunjwa ndio hamuishi kutuambia kuwa Balali yupo hai ila kaminya tu sehemu. Wote tunafahamu kuwa BoT ndiko kuna chumvi ya Taifa, sasa mbona msitie shaka kuwa yawezekana kajamaa kanataka kusepa mamoja?

Hakuna kupumzika wala nini, kama ni beach aende Coco kabla haijauzwa. Umeshaambiwa ni KIGOGO, tena haikupaswa kuzuiwa tu, angecharazwa na bakora kwa kosa la kuondoka darasani huku mwalimu anafundisha
 
Reason nikweda kufanya nn jaman mmesafiri sana miaka kumi ya jk tena kwa kutumia pesa zetu uku wagonjwa wakikosa dawa muhimbili na vitanda mkiwa ngazi hiyo hiyo ya juu now mwezi mmoja mmeahaha hapana kuna kitu kikubwa nje ya pazia msije kuwa mnajijua mapema
 
Pasco umesema kazuiliwa sababu hana vibali je mtu km hana vibali aruhusiwe tu sababu sheria imetamka? je sheria inasema mtu yuko huru kwenda atakakko bila hata kua na vibali? mbona mi nona ni sahihi kabisa sababu hana vibali atafute ndio aende navyo wamzuie sijui nini tatizo hapa.
 
Last edited by a moderator:
Pasco ibara ya katiba uliyoitumia kama kumbu:- inampa mamlaka mhifadhi katiba yeyote kumzuia raia kwenda atakako ikiwa tu:-

kufanya hivyo ni kwa maslahi mapana ya taifa.

soma kwa makini sehemu hii hapa chini
PASCO said:
(2)Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenyemadhumuni ya-Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania______________________________ ______________________________ _____19(a)kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako nakumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au(b)kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtukwenda anakotaka ili-(i)kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;au(ii)kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibuwowote anaotakiwa na sheria nyinginekuutimiza; au(iii)kulinda manufaa ya umma kwa jumla aukuhifadhi maslahi fulani mahususi aumaslahi ya sehemu fulani ya umma,kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyohaitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara hii
 
Last edited by a moderator:
Sifa tu za magufuli kunyanyasa wafanyakazi kwa kutaka sympathy ya wananchi na watu wasio na mwelekeo kama wewe
Mambo mengine yanachukuliwa kama wote tuko vijiweni.ukishakuwa mtumishi wa umma uko utaratibu na hakuna namna ni lazima ufuatwe,je kwa hili ulifuatwa.watumishi wote wanajua hilo.
 
pasco pasco usiwe na upei finyu. Haunaga haki duniani elewa hilo. Hata hao wamarekani wanaosemaa wanademcrasia ya hali ya juu hawapo hivo. So mwache mr prezda afanye yake. Acha umbeya wa kuingilia mambo. Haki haki haki iko wapi acha unafiki wewe. Mbona nawe hukutenda haki kipindi kile ipo sehemu furani hivi. We fanya yako. Afu jua sio lazima umkubari magufuli kwa mambo yote

ndugu hata sielewi kwa nini huyu jamii ameleta hili bandiko hapa sababu kaandika kwa maneno yaliokolezwa kwamba huyo kigogo hana vibali ndo maana kakatazwa kwenda nje sasa hata huko ulaya watu wanatoka tu bila vibali? Labda km kuna kitu sijaelewa hapa
 
pascal hatuna katiba inayotufaa kuiheshimu.

hii ya 77 ni ya kipuuzi na wanaoapa kuilinda huapa wakichekelea upuuzi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom