Je, hii ni sahihi katika dini ya Uislamu???

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,110
52,837
Kutoka nchini Marekani Pichani ni Imam Mwanamke Amina Wadud akiswalisha kundi la Wanaume, alianza kwenye kutafsiri Qur'an hadi kuwa Imam anayesimama mbele ya mamia ya Wanaume na anaongoza Sala ya Ijumaa.

👉 I mean no malice to nobody.

FB_IMG_16846930643505077.jpg
 
Kwani kuna Aya inayowazuia wanawake kuwa ma Imamu?

Wacheni udikteta katika Dini.

La. Sivyo wekeni andiko linalo wakataza wanawake kuwa ma imamu.
 
Mbona hao waislam wa marekani hawajavaa kiislam kama waislam wengine wanaoeleweka? Kama ni kweli, uislam umeharibiwa, waliwakebehi wakristo kwa ukristo wao kuvamiwa na wahuni
 
Hata huku inawezekana. Kwani mwanamke anakasoro gani? Tatizo la waislamu wa bongo imamu akiwa mwanamke mwenye taarab la nguvu, atakapo geukia kibla huku nyuma wenye udhu watakua wachache Sana.
 
Shia hao, Imani na itikadi zinatofautiana

Ni sawa na Katoliki Mwanamke hawezi kuongoza ibada lakini kwa walokole ni sahiii
 
Kwani kuna Aya inayowazuia wanawake kuwa ma Imamu ?

Wacheni udikteta katika Dini.

La. Sivyo wekeni andiko linalo wakataza wanawake kuwa ma imamu.
Zipo, kwamba mwanaume ndy kiongozi kwa mwanamke.

Kwa Jambo lolote lile.
 
Kwani kuna Aya inayowazuia wanawake kuwa ma Imamu ?

Wacheni udikteta katika Dini.

La. Sivyo wekeni andiko linalo wakataza wanawake kuwa ma imamu.
ipo hivi, sala ni dua, ni unyenyekevu, na mawasiliano kati ya mwanadamu na muumba wake, sala inahitaji utulivu wa akili na haipaswi kuingiliwa na jambo lolote,
katika uislam sisi wanaume tunaamrishwa kuinamisha vichwa chni tuonapo mwanamke mbele yetu ambaye si mkeo na ambaye kwako wewe inafaa kumuoa, quran 24:30

Hapohapo quran 24:31 inawakataza wanawake kuonyesha maungo yao na kujisitiri maungo yao, na wainamishe nyuso zao mbele ya mwanaume.

vilevile mafundisho ya kiislam hayaruhusu mwanamke kuvaa nguo ambazo ni kishawishi kwa mwanaume, mfano zenye kitambaa chepesi ama cha mpira chenye kuweza kuchora umbo lake

sasa katika hali ya kawaida kaa chini fikiria wewe mwenyewe je inafaa kumfanya mwanamke kuwa imam

Na kwa ufupi katika uislam mwanaume ndio kiongozi daima, imamu ni kiongozi
 
Kwani kuna Aya inayowazuia wanawake kuwa ma Imamu ?

Wacheni udikteta katika Dini.

La. Sivyo wekeni andiko linalo wakataza wanawake kuwa ma imamu.

Unataka Andiko Katika Biblia au Qur'an?
Au Ngoja nikupe la Biblia Maana Inaonekana wewe Ni kafiri.Nikupe La kitabu Chako

1 Timotheo 2:8
Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.

Hapo wanaume Wameambiwa Wasalishe Kila Mahali,Yaani Waongoze Kila Ibada

Naongezea Andiko
1 timotheo 2:12
Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
 
Back
Top Bottom