Mti wa mitunda ndiyo hupigwa mawe, uislamu utakuwepo na utazidi kuwepo! Allah akbar

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
Imam Mwanamke' Amina Wadud: Kutoka kufasiri Quran hadi kuongoza sala ya Ijumaa

Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Amina Wadud - ambaye alichagua kuandika jina lake kwa herufi ndogo, kulingana na herufi za Kiarabu ambazo hazitambui herufi kubwa - alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza sala ya Ijumaa nchini Marekani na Uingereza mwaka 2005 na 2008.

Jina lake linajulikana na wengi kama Bibi Imamu.

Hata hivyo, muda mrefu kabla ya hapo, mwaka 1992 alikuwa amepata mafanikio kwa kuandika kitabu cha Quran na Mwanamke

Katika kitabu hicho, Amina anafasiri Quran kwa mtazamo wa wanawake kuhusu mada mbalimbali, kama vile umuhimu wa wanawake katika Quran, na pia nafasi na haki za wanawake katika Uislamu.

'Sifanyi hivyo ili kuwa wa kwanza katika jambo lolote, au kuwa kiongozi kwa yeyote. Bali ninajali sana uhusiano wangu na Quran na jinsi unavyotofautiana na ukweli ninaoupata, kwa mfano katika jamii ya Kiislamu," alisema Amina.

Sasa anachagua kukaa Indonesia.

Kwa BBC Indonesia na mwandishi wa BBC aliyebobea katika masuala ya kidini huko Beirut, Lebanon, Amina alishirikisha safari yake kuelekea Uislamu na juhudi zake za kufikia haki ya kijinsia.

Sio tu kwa wanawake na wanaume bali pia wasiokuwa wawili katika muktadha wa Uislamu.

"Nitasherehekea miaka 70 ya kuzaliwa mwaka huu, pamoja na miaka 50 tangu kuukubali Uisilamu," alisema.

''Ninajihisi mwenye bahati sana, nilipata kitu ambacho nilikipenda, na miaka 50 baadaye upendo na haiba haijawahi kufifia.''

Alizaliwa katika familia ya wachungaji nchini Marekani

Niliingia kwenye makazi ya Amina huko Yogyakarta, nikakaribishwa na meza iliyokuwa mbele ya lango la kuingilia iliyokuwa ikionyesha vitu mbalimbali.

''Mimi ni Muislamu ambaye mawazo yangu yanachangiwa na vyano mbalimbali,'' alisema Amina, ambaye alichagua kuandika jina lake kwa herufi ndogo zote, kwa sababu alisema Kiarabu haitambui herufi kubwa.
 
.
 

Attachments

  • IMG-20230520-WA0031.jpg
    IMG-20230520-WA0031.jpg
    38.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom