Je, Ethiopia kujiunga Jumuiya ya Afrika Mashariki kutaharibu au kuimarisha jumuiya hiyo?

Ethiopia inataka kujiunga na EAC?
Nini madhara na faida?
Je Tanzania na Kenya zitakua bado na sauti ndani ya EAC au ndio mvurugano utaongezeka?
Hakuna Jumuiya yoyote ya maana itakayoweza kuboresha hali za maisha ya watu wa Afrika inayoweza kuundwa na Watawala wa nchi za Afrika. Jaribu tu kujiuliza swali dogo, Je hizi Jumuiya za ki-Afrika ambazo tayari zimeundwa na zipo hai zimewasaidia nini au zinawaletea faida gani Watu wa bara hili la Afrika?
African Union (AU) ipo ipo tu, haina faida yoyote ile kwa Waafrika, imegeuka kuwa Club ya kukutana ya 'Wazee Madikteta na Mafisadi' wanaolihujumu bara hili la Afrika. Huko wanapanga mikakati ya kuendeleza tawala zao za kidikteta na kuunda timu ya 'kulindana' endapo kama mtawala-dikteta mmojawapo atakataliwa na wananchi au kupinduliwa ktk nchi yake. Ni hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom