Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Huyu dr slaa hafai hata bure.....dr slaa ni bora raisi sio rais bora na waswahili wanasema rais huwa ghali

dah..kazi kwelikweli,kumbe maadui wa nchi hii bado wana nguvu.....yaani ujinga,maradhi,umasikini na lile lingine.
 
1. Hana mbinu wala mikakati ya kushinda
2. Anaonekana ana kaugonjwa ka ulevi na anataka kuwaambukiza watanzania wote ugonjwa huo
3. Hajui uchumi unakwendaje (labla kwa vile ni mtheolojia)
4. Hauziki
5. Hana ndoa
6. Jema pekee alilofanya (ingawa hajafanikiwa na hatafanikiwa) ni kuwataja wevi pale mwembe yanga
7. Mnafiki. Analialia eti posho za wabunge ni kuwa huku anazipokea
8. Hodari wa kulalamika lalamika
9. Anataka kuzalisha jamii yta wavuta sigara (huende na bangi pia) pamoja na walevi
10. Hakubaliki

Kwa hali hiyo, SITAMCHAGUA

Sifa zote hizi ni za JK, kaazi kweli kweli!
 
dah..kazi kwelikweli,kumbe maadui wa nchi hii bado wana nguvu.....yaani ujinga,maradhi,umasikini na lile lingine.
Na bado. Tutawaona wengi kufikia Oktoba 31. Baada ya hapo watatoweka mmoja mmoja.
 
BTW, MODS naona mngefanya la maana mkiunganisha hizi IDs za MS na kuziunganisha pamoja kwenye ban. Sioni sababu ya kumuogopa hata kama atakuwa mwana wa mfalume.
 
Zaidi ya asilimia 99 ya watz hawafuati dini na wala hawajali lolote kuhusu dini na ni unafiki na uzandiki kwa kweli kuhusisha jambo lolote na dini, na mtu yeyote anayeleta maelezo au hoja ya dini mi namuona PWAGUZI TU HANA HOJA. Hiyo midini yenu si inawaambia msiibe, msiue, msizini etc etc ..mngekuwa hamfanyi hayo maovu yote walau kwa asilimi 50 taifa letu si lingekuwa mbali sana?

Nyie na midini yenu you can all go to hell.Mnakera sana walahi.
 
Antibayotiki: Ni mapema sana kusema lolote....unaonyesha una wasiwasi na mbinu atakazotumia Slaa ndio mana unashauku ya kutaka kujua.
Mbinu gani za ushindi? Hata wiki moja haijaisha tangu campain zimeanza rasmi? Bado miezi miwili tusubiri tuone. Hata CUF na wengine hawajaanza? Mbona mchezo bado sasa ni kupasha msuli tu!
 
Mozze,

Waogopeni sana watu wa aina ya Anti-sijui nini!

Hawa ni wa kuja na kuondoka hawa!...Amekuja kikazi hapa na ni pandikizi la watu au mabwana wanaomlipa nusu-na-robo ya unga!..
Anamtumikia kafiri apate mradi wake!...
Hapa anachotaka ni kuchokonoa ili tuweke wazi baadhi ya mbinu tunazotumia, then acopy na ku-paste kwenye genge lao...
Hatudanganyiki ati broda!.

Akamwambie mume wake kwamba amegonga mwamba!..Mambo yote aliyosema hapo kwenye post yake ni kama liquid inayopatikana katika shimo la choo!..huh!
 
Wana JF,

Nadhani nimekwisha kujibu hoja hii mara nyingi na kama mwandishi husoma jamvi hili angeliweza kupata majibu ya yote aliyoeleza humu. Narudia kwa kifupi,
i) Dr. Slaa hakufukuzwa upadre wa Kanisa Katoliki, na wala hakutuhumiwa popote na kwa wakati wowote ule kuhusiana au na ubadhirifu wa mali au rasilimali za kanisa au za mtu yeyote ile. The onus of proof is on the author na niktafurahi sana kama ana chembe ya ujasiri aweke hadharani. Nadhani ndio uungwana.
ii) Dr Slaa alipotoka upadre aliitwa na wananchi wake wa Karatu kuwa mtumishi wao. nimekuwa Mbunge kwa miaka 15 yaani awamu tatu na hadi leo wanamlilia. ghafla hawezi kugeuka shetani. na hana tabia ya kujificha wala kuwa na sura ya kinyonga. Mwandishi angefika Karatu na kufanya utafiti angeligundua ukweli huo.
iii) Kuhusu Maisha yanayoitwa binafsi, Dr Slaa hajawahi kuwa na maisha binafsi ya siri. Mwandishi angelifika Karatu angelishangaa kuwa hayo anayoita maisha binafsi ya ndoa ya DR. Slaa ni public knowledge. wananchi waliomlea kwa miaka 15 ndio wanaomjua kuliko yeyote, na wana haki ya kuulizwa.
iv) MWANDISHI anaonyesha uelewa mdogo wa masuala ya Kanisa Katoliki na Taratibu zake mbalimbali. Dr Slaa anayo Decree ya Vatican ya Laicization, Mwandishi angefanya utafiti mdogo tu angeweza kuelewa maana yake nini, wala asingelizungumzia habari ya prodigal son, ambayo dhahiri haelekei kufahamu maana yake.

Nimetoa haya kwa manufaa ya wanaopenda kuelewa zaidi. Hata hivyo maswala haya yalikwisha kufafanuliwa kwa kina kwenye jamvi hili.

Nawashukuru wana jamvi wote, na wanajamvi mko huru kudodosa lolote kwa vile kiongozi hana private life, hivyo Dr Slaa anaweza kuulizwa lolote na ufafanuzi unaotakiwa utatolewa
 
Dr. Slaa wewe ni public figure hivi sasa na sidhani kama unatumia muda wako vyema kumjibu mtu anayesema 'umetumwa na kanisa kugombea urais' this is too low..Hivi ndivyo nionavyo.

Ungefanya la busara kuelezea mikakati yako na kuelezea kinagaubaga jinsi utavyoshape sera zako za kiuchumi ziadi. Haya mambo ya uswazi waachie akina Malaria Sugu.
 
Wana JF,

Nadhani nimekwisha kujibu hoja hii mara nyingi na kama mwandishi husoma jamvi hili angeliweza kupata majibu ya yote aliyoeleza humu. Narudia kwa kifupi,
i) Dr. Slaa hakufukuzwa upadre wa Kanisa Katoliki, na wala hakutuhumiwa popote na kwa wakati wowote ule kuhusiana au na ubadhirifu wa mali au rasilimali za kanisa au za mtu yeyote ile. The onus of proof is on the author na niktafurahi sana kama ana chembe ya ujasiri aweke hadharani. Nadhani ndio uungwana.
ii) Dr Slaa alipotoka upadre aliitwa na wananchi wake wa Karatu kuwa mtumishi wao. nimekuwa Mbunge kwa miaka 15 yaani awamu tatu na hadi leo wanamlilia. ghafla hawezi kugeuka shetani. na hana tabia ya kujificha wala kuwa na sura ya kinyonga. Mwandishi angefika Karatu na kufanya utafiti angeligundua ukweli huo.
iii) Kuhusu Maisha yanayoitwa binafsi, Dr Slaa hajawahi kuwa na maisha binafsi ya siri. Mwandishi angelifika Karatu angelishangaa kuwa hayo anayoita maisha binafsi ya ndoa ya DR. Slaa ni public knowledge. wananchi waliomlea kwa miaka 15 ndio wanaomjua kuliko yeyote, na wana haki ya kuulizwa.
iv) MWANDISHI anaonyesha uelewa mdogo wa masuala ya Kanisa Katoliki na Taratibu zake mbalimbali. Dr Slaa anayo Decree ya Vatican ya Laicization, Mwandishi angefanya utafiti mdogo tu angeweza kuelewa maana yake nini, wala asingelizungumzia habari ya prodigal son, ambayo dhahiri haelekei kufahamu maana yake.

Nimetoa haya kwa manufaa ya wanaopenda kuelewa zaidi. Hata hivyo maswala haya yalikwisha kufafanuliwa kwa kina kwenye jamvi hili.

Nawashukuru wana jamvi wote, na wanajamvi mko huru kudodosa lolote kwa vile kiongozi hana private life, hivyo Dr Slaa anaweza kuulizwa lolote na ufafanuzi unaotakiwa utatolewa

Halafu "the onus of proove' ndiyo kitu gani mkuu? Kama Kiingereza mambo fulani tuandike Kiswahili tu tutaelewana, hii mikogo ya Kiingereza cha kuunga unga inakuaibisha tu.

Kiswahili cha first person na third person kinachanganywa humo humo wakati mtu (Dr.) anajiongelea mwenyewe !

Na inakuwaje CHADEMA mkawaachia CCM kuchukua majimbo 10 bila kupingwa, mengine wagombea hawarudishi fomu, mengine wanarudisha fomu lakini wagombea dhaifu kama kina Regia Mtema, hivi mkipeleka wabunge dhaifu kama hawa mnatuambia nini kuhusu uimara wa chama?

Zaidi ya hapo, je ukweli kwamba hamna wagombea madhubuti unachangia CHADEMA kuchukua mapandikizi ya watu walioshindwa kupata nafasi kugombea ubunge kwa tiketi za CCM ?
 
Mbona unaandika na kujijibu mwenyewe kama vile unapiga p... Acha kujidhalilisha, inaelekea usivyokuwa na akili kwa kuanzisha thread ambayo haina viwango, yaani umeonyesha chuki na kutumwa. Halafu mwanaume kutumwa bwana, yaani unakuwa ka nyoka, kutumwa, kama vile kukatuma katoto sigara dukani, lol aibu sana mtu mzima, eti antibayotiki, lol. Haya maneno hayana tofauti na Makamba hivi, manake ndio anaongea bila kufikiri
 
Halafu "the onus of proove' ndiyo kitu gani mkuu? Kama Kiingereza mambo fulani tuandike Kiswahili tu tutaelewana, hii mikogo ya Kiingereza cha kuunga unga inakuaibisha tu.

Kiranga,
Wewe usijione kwamba haki ya mtu kueleza jambo kwa kiingereza ni YAKO WEWE BINAFSI(kIRANGA)!
Wewe ndiye namba 1 kwa kuandika andika vitu visivyoeleweka hapa jamvini kwa lugha hiyohiyo unayomlaumu nayo Dr Slaa...what a mess!:eyeroll2:

Umembiwa kwamba mwandishi anatakiwa kufanya utafiti kidogo ili kuyajua hayo!..Hata wewe ukifanya utafiti kidogo tu utajua maana ya "the onus of proof"!...huh!
 
Thanks Dr. W Slaa... mwenye macho kaona, mwenye masikio kasikia...

Abdulhalim nadhani ujumbe umemfikia Dr.

Kiranga... waswahili wanasema kuchamba kwingi, kutoka ma m@vi, wewe katika post yoote hiyo umeona paragraph, na lugha tu??? kuna mwalimu wa chemistry alishawahi kuniambia "Acid.. ukishaona unakagua benzene ring kuangali tofauti ya pembe na kama ile ring haiko uniform basi kimbia haraka psychiatry, maana wawez kuwa tayari...."

wakatabahu
 
Kiranga,
Wewe usijione kwamba haki ya mtu kueleza jambo kwa kiingereza ni YAKO WEWE BINAFSI(kIRANGA)!
Wewe ndiye namba 1 kwa kuandika andika vitu visivyoeleweka hapa jamvini kwa lugha hiyohiyo unayomlaumu nayo Dr Slaa...what a mess!:eyeroll2:
Umembiwa kwamba mwandishi anatakiwa kufanya utafiti kidogo ili kuyajua hayo!..Hata wewe ukifanya utafiti kidogo tu utajua maana ya "the onus of proove"!

1. Mostly naandika vitu vinavyoeleweka, kama huelewi niulize.

2. Hata ikitokea kwa nadra nimekosea, sijawahi kukosea kuandika "the onus of proove" instead of 'the onus of proof"

3. Hata ningekosea hivyo, sijaomba urais na standard ya kunibana mimi ni tofauti na standard ya kumbana Dr. Slaa

Dr. Slaa anataka kuwa colloquial sasa, na anatutia shaka kuhusu uwezo wake. Kiingereza hajui, kuandika kwa paragraph hajui, kutochanganya kiswahili na kiingereza hajui, kuwapa proofreaders wamsomee mambo hajui.

Anaweza kuwa rais akafanya vituko kama mambo yenyewe ndiyo haya.

Watanzania twafwa, Kikwete kilaza, Dr. Slaa mwenyewe watu wanaomtegemea awe kiongozi mbadala ndiye huyu au mtu tu kaja kuchukua hilo jina ?
 
Thanks Dr. W Slaa... mwenye macho kaona, mwenye masikio kasikia...

Abdulhalim nadhani ujumbe umemfikia Dr.

Kiranga... waswahili wanasema kuchamba kwingi, kutoka ma m@vi, wewe katika post yoote hiyo umeona paragraph, na lugha tu??? kuna mwalimu wa chemistry alishawahi kuniambia "Acid.. ukishaona unakagua benzene ring kuangali tofauti ya pembe na kama ile ring haiko uniform basi kimbia haraka psychiatry, maana wawez kuwa tayari...."

wakatabahu

Unaweza usichambe kabisa ukabaki na gundu vile vile, ndicho ninachokataa.

Kumwambia Dr. Slaa asijibu hakutamsaidia maana maji kashayavulia nguo, hana budi kuyaoga, ama sivyo ataonekana mtu wa ku half step, na ahadi yake ya kujibu maswala yoyote atakuwa kaivunja, kitu ambacho si kizuri hususan mapema hivi kwa mgombea urais.

Nimeuliza mengi zaidi ya lugha na sijapata majibu, soma post.

Haifagiliwi groupthink hapa, wembe ule ule unaochana uzembe wa CCM utatumika kwa upinzani.Mwendo wa zero tolerance ndio mwendo pekee utakaolinyanyua taifa letu, mimi sina chama wala ushabiki, natafuta excellence kutoka kote.
 
Dr. Slaa anataka kuwa colloquial sasa, na anatutia shaka kuhusu uwezo wake. Kiingereza hajui, kuandika kwa paragraph hajui, kutochanganya kiswahili na kiingereza hajui, kuwapa proofreaders wamsomee mambo hajui.

Hilo la Dkt. Slaa kutojua Kiingereza umelitoa wapi? Au kwa vile kaandika "the onus of proove' wewe kwako ndio imekuwa hajui Kiingereza?

Back
Top Bottom