Je CHADEMA inawaandaaje wananchi baada ya Oct 31?

Hii Mada ungeiweka katika mtazamo chanya ilikuwa nzuri lakini kwa sababu wewe unaona lazima CCM ishinde wakati kunavyama lukiki vinashindana na kurudishia mwenyewe wewe PAULSS ni mchochezi huna uzalendo
 
Mkuu Froida wala mimi sijasema CCM lazima ishinde
yasome tena kwa umakini maandiko yangu, nahakika utaelewa namaanisha nini,
Mimi ni mzalendo sana na nchi yangu na ndio maana nikaona hatari iliyopo kama mambo kama haya yataendelea kupandikizwa vichwani mwa watu
Ni haki ya kila chama kudai kitashinda, lakini si haki ya chama chochote kudai lazima kitashinda na ikitokea akimeshindwa basi kimeibiwa kura, na kusapoti kushinda kwao wanaanza kuzusha habari za uongo kuonyesha kunampango wa kuwaibia kura ili watakapo shindwa wapate sababu yakuanzisha vurugu
.
Kama umesikiliza vizuri leo mdahalo wa kiaina kati ya Slaa na Kinana ungejua kwanini CCM wanasema watashinda ukiondoa dhana ya kushinda ya CHADEMA kudhania wingi wa watu ktk kampeni na hoja za ufisadi ndio mtaji pekee wa kuwaingiza ikulu

Jibuni hoja, msijitie hamuoni
Marufuku kuikmbia jamvi baada ya uchaguzi,,,mje na vikaragosi vyenu kama kawaida,,, mkitaka kulia lia mkalie nyumbani kwenu na watoto wenu,, hapa jamvini hatutaki kusikia vilio vyenu
 
CHADEMA inatuandaa kulinda kura baada ya kupiga ili haki inapoibwa iweze kupiganiwa, hakuna tena muda wa kuacha ccm waibe.
 
CHADEMA inatuandaa kulinda kura baada ya kupiga ili haki inapoibwa iweze kupiganiwa, hakuna tena muda wa kuacha ccm waibe.
Mkuu umesoma mada ukaielewa? au unajibu kiushibiki tu
kama ni swala la la kulinda kura soma kwa uzuri post no 18
Kwenye red inaonyesha ni jinsi gani ulivyo athirika na uzushi huu wa CHADEMA, unaonyesha upo tayari kuingia hata msituni ilimradi tu CHADEMA haijashinda
 
Jibuni hoja, msijitie hamuoni
Marufuku kuikmbia jamvi baada ya uchaguzi,,,mje na vikaragosi vyenu kama kawaida,,, mkitaka kulia lia mkalie nyumbani kwenu na watoto wenu,, hapa jamvini hatutaki kusikia vilio vyenu

Na mimi nasema hivi.. FORUM HII ISIFUNGWE HAPO BAADA YA OKTOBA 31.
Maana kuna wanachama humu wanafikiri kila mtu atakipigia chama fulani, tumechoka na visingizio vya kutafuta sababu ya kushindwa hapo Okt 31. Bado siku kumi tu, itajulikana kama ni tui la nazi au maziwa....

Moderator naomba utuwekee script ya "Countdown to Election 31 Okt 2010" uwakumbushe watu hapa, wasije singizia ooh nilisahau na sikwenda piga kura ndo maana chama changu hakikushinda...
 
Mkuu umesoma mada ukaielewa? au unajibu kiushibiki tu
kama ni swala la la kulinda kura soma kwa uzuri post no 18
Kwenye red inaonyesha ni jinsi gani ulivyo athirika na uzushi huu wa CHADEMA, unaonyesha upo tayari kuingia hata msituni ilimradi tu CHADEMA haijashinda

wewe hujaelewa nini, post 18 ni mawazo ya mwanakijiji, si lazima nikubaliane nayo ama nijadili kile ambacho mwanakijiji anajadili, wee vipi,
ir2.jpg
 
Jibuni hoja, msijitie hamuoni
Marufuku kuikmbia jamvi baada ya uchaguzi,,,mje na vikaragosi vyenu kama kawaida,,, mkitaka kulia lia mkalie nyumbani kwenu na watoto wenu,, hapa jamvini hatutaki kusikia vilio vyenu

hivi kwa nini craps kama hizi za kutokea crapville zinazoletwa na watu waliotumia crap malt zisipewe neno moja tu la crap?
 
Back
Top Bottom