Elections 2010 Je CHADEMA iko tayari kuongoza nchi?

akashube

JF-Expert Member
Dec 24, 2009
401
23
Wakuu wana JF, kwa kweli nimechoshwa sana na uongozi mbovu wa sasa chini ya serikali ya chama cha mapinduzi CCM. Nimejiandaa vema kabisa kupiga kura kuiondoa madarakani.

Fikiria mara ghafla Novemba sijui tarehe ngapi...pah!...CHADEMA imechukua nchi kwa ushindi mkubwa kiasi kwamba ina wabunge wa kutosha na Rais ni Dr. Slaa.

SWALI:

Sura zote zikiwa mpya kabisa.....CHADEMA iko tayari kuongoza nchi?

Unaingia Ikulu kwa upya kabisa, Rais Mpya, Waziri Mkuu Mpya, Baraza la mawaziri jipya, Wabunge?, wakuu wa mikoa?, wakuu wa wilaya? makatibu wakuu? wakurugenzi mfano usalama wa taifa, mkuu wa majeshi... Brand New kila kitu.

Je kutakuwa na wa kumuuliza hiki tunafanyaje na hiki kinakuaje? Au je kuna utaratibu wa Rais aliyepo kuendelea kwa muda kuwezesha 'fair handover'..yaani bila shaka yapo mambo ya kuelekezana.?????

Je hiki kipindi kitachukua muda gani ili ahadi za siku 100 za kwanza muda wake usiingiliwe?

Ni wasiwasi tu wa mpiga kura...naomba tusaidiane.
 
Wala usitie shaka katika obama alipoingia madarakani kama democrat je sura ipi ya zamani ya republican ilibaki kuwaelekeza? Kanu ilipoangushwa kule kenya swala lilikuwa vivo hivyo kwa kifupi serikali hasa wizara huendeshwa na ma katibu wakuu ndo maana hawabanduki hata baada ya uchaguzi na wao ndo wanaohandover iwapo wameenguliwa katika nafasi zao mawaziri daima ni wasimamizi ndio maana hata bungeni manaibu wao ndo wanaojibu maswali japo majibu huandaliwa na katibu wa wizara husika hapa unaona jinsi fedha nyingi zinavyotumika ovyo mlundikano mkuubwa wa watu lakini mtendaji ni mmoja tu.
 
Achana na hoja hii. CHADEMA hawakuingia kwenye kinyang'nyiro kichwa kichwa
 
Back
Top Bottom