Je, CCM kuingilia uhuru wa Bunge, imevunja katiba?

Madela wa madilu,
Mkuu mimi hilo la kanzu na mvaaji wake kidogo limenibakiza kizani kwani navyojua mimi hatuzungumzii joho la Spika ila Bunge. yaani Msikiti au kanisa na upande wa pili kuna Sheikh au Padri.
Sasa ikiwa unamatatizo na Sheikh au Padri sidhani kama utakuwa unalitukana kanisa au msikiti kwa sababu ya uendeshaji ibada wa Sheikh au Padri X..na wala hutakuwa unafanya kufuru ya dini, aya au sala nzima, isipokuwa unahoji udhu (usafi) wa mwendesha ibada. Kama yeye sii msafi kuna kila sababu ya sala nzima kutopokelewa ipaswavyo..

Nikirudi ktk swala la Bunge bila shaka mnakumbuka kwamba hata hapa JF ni kama chombo chochote kinachokatazwa kujadili mambo ya Bungeni kikatiba.. lakini tumeona hoja kibao za wabunge tukizijadili jambo ambalo mimi naweza sema ni kuvunja katiba..Lakini sidhani kama ndio maana ya sheria hiyo kuwekwa kwamba wananchi ktk vyombo vyao hawaruhusiwi kudajili maswala ya Bungeni isipokuwa ibara hii imetanguliwa na maswala fulani muhimu ambayo yanakataza mjadala hiyo..
Sasa bila shaka ningependa kuisoma sheria nzima kwa mapana yake ili nipate mwanga zaidi kwani katiba yetu ina tobo nyingi sana ambazo baadaye zinaweza kutumaliza sisi wenyewe. Pia katiba ni sawa na msahafu unahitaji mwanga mkubwa sana kuelewa na kila aya inakuwa na hadithi nyuma yake meaning tunatunga sheria kutokana na matukio na sii kubuni sheria..

Nitarudia kusema maneno ya Chiligati na wabunge wengine wengi wachovu wa kufikiri, makuhadi wa Ufisadi ni maneno mazito sana (hayabebeki) kuhusiana na yale yanayotokea Bungeni, lakini pia tuwe wepesi kutazama upande wa pili wa sarafu hii kwamba what if Speaker wa Bunge atakuwa upande wa utawala wa Kidikteta. Tuwe na rais kama Mugabe ambaye Spika alikuwa akimpongeza hata katika maasi na mapungufu makubwa ya chakula nchini mwao kwa sababu tu hataki kuachia ngazi ya Utawala.. hawa watu watafungwa na sheria gani?..

pamoja na kuwepo ibara ya 100 ningependa kuona Ibara inayotengua sheria hiyo ikiwa Kiongozi, mbunge au rais amekiuka miiko ya uongozi na kalitumia Bunge kujenga sheria kinyume cha haki..naelewa vizuri sana swala la Sitta na msimamo wangu upo wazi kabisa against hao mafisadi na naomba Mungu washughulikiwe lakini hii isiwe sababu ya kutokuwa na sheria ambayo Spika wa Bunge anaweza kufanya anayotaka kuyafanya kama kumwondoa Zitto bungeni kisha isiwe ruksa kwetu wala vyombo vyovyote kujadili au kutafuta haki ya mhusika kwa sababu tu Spika analindwa na sheria za Bunge.
Waswahili tunasema Sheikh kaingia na mbwa msikitini!
 
Last edited:
Ok, assume CCM wamevunja katiba, then what?

Nadhani tuepeuke mijadala hii inayoeleweka, tujadili CCM waondoke madarakani wakitanguliwa na JK wake! hizi story ziko kila siku kila mahali na si mara ya kwanza

Spika ni mwana CCM for any how lazima ataulizwa unless ahame chama na auvue uspika!

1. Tupiganie katiba ibadilishwe ikiwemo ya tume huru ya uchaguzi na hili la spika( ikiwezekana awe mtu huru pasi chama) inawezekana
2. Ya kuwa JK ajiuzulu hata kam mtaona haiwezekani ingekuwa kila tukilala na kuamka marungu tunaelekeza kwakwe, leo hii tungekuwa mbali.

3. Uozo wa ufisadi huko kila kona mpaka umekuwa wimbo sasa people are no longer excited na hizi habari sana sana ndiyo waroho wanaongezeka , nchi inhitaji kukombolewa haraka!
 
Mmmh!
Wajameni!
Naona hii issue hata sisi wenyewe inaelekea kutushika pabaya. Katiba yetu ina mashimo ya volcano.
 
Recta, Mkuu unachozungmza wewe ni katiba ya nchi na jinsi inavyoweza kufanya kazi lakini sii within a party. kama nakumbuka vizuri Chadema walimsimaisha mwenyekiti msaidizi wao marehemu Wangwe Uenyekiti na wangeweza kwenda zaidi kumpokonya kadi ya chama kulinagana na katiba yao hata kama inapingana na katiba ya nchi.
Mkuu, ilisemekana kuwa chama cha Wangwe kilitaka kumnyang'anya uanachama Wangwe kwa sababu zao. Hilo linawezekana kwenye chama chochote na kama vikao husika vimefikia uamuzi huo, ni halali kabisa kufanya hivyo. Vile vile, Spika angeweza kabisa kupoteza uanachama wa CCM kama kikao hicho kingeridhia kwa idadi inayotakiwa kufanya hivyo (nayo bila kuvunja sheria yoyote).
Ni ktk kuchanganya mabo haya ndio maana tunashindwa kuwahukumu kina Lowassa, tunadhani kwamba maadam wao wamechaguliwa na wananchi wa majimbo yao basi chama au serikali haina ruhusa ya kuwanyang'anya Ubunge.

Mkuu, hakuna chama kinachoweza kumnyang'anya Mbunge kiti chake cha Ubunge. Katiba ya nchi haina kipengele kinachotoa ruhusa hiyo. Bali, kwakuwa Mbunge ni lazima awe ametoka katika chama chochote cha siasa, anaponyang'anywa uanachama automatically anapoteza kiti cha Ubunge. Maana ya hili ni kuwa, hata kama si nia ya chama kumnyang'anya Ubunge mtu ambae amefukuzwa kwenye chama alichokuwa akikiwakilisha Bungeni, nafasi yake ya Ubunge itakoma automatically. Hivyo basi, uwezekano uliopo wa chama kumfukuza mwanachama wake ubunge ni kwa kutumia trick hiyo tu.
 
Mkuu tuwe makini ktk hili hapa kwani tusije kumjengea ngao kubwa speaker Sitta..
Ebu nikupe mfano nje ya mada hii kidogo.. tuseme Chadema ndio wameshinda na kumchagua Spika wa bunge ambaye
Hivi kweli mnataka kusema Sitta angekuwa mbunge na spika wa Chadema na akafanya kinyume cha chama kwa kukataa kabisa mada zinazohusiana na Mafisadi kusimamishwa kinyume cha wabunge wa Chadema....basi Uongozi wa Chadema ungekuwa hauna haki kumsimamisha Uongozi Spika huyo kwa sababu analindwa na katiba ya nchi?..Meaning hivi leo Spika Sitta angekuwa anafanya kama Mafisadi wanavyotaka tungekuwa hatuna sheria ya kumwajibisha!..
Mkuu soma kipengele cha pili kinatanguliwa na maneno haya:- Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika..

Mkuu Mkandara, mfano wako ni mzuri sana.

Ni kweli kuwa chama kingeweza kumng'oa uSpika ndani ya Bunge pekee na sio kwenye vikao vya chama. Vikao hivyo vingetumika kupanga mikakati hiyo tu.

Jaribu ku-imagine mkuu (mfano mwingine), kuwa Bunge lina uwakilishi wa mchanganyiko mkubwa wa chama tawala na vyama vingi vya siasa (le's say 10). Na kati ya hivyo hakuna chenye wabunge zaidi ya theluthi moja. Baadhi ya vyama ni dhahiri vitaungana na kupitisha jina moja la mtu wanaeona anawafaa kuwa Spika na hivyo mtu huyo kushinda nafasi hiyo. Je, ni chama gani kati ya hivyo kitakachokuwa na nguvu ya kumuita Spika na kumshinikiza kufanya watakayo?
 
1. Tupiganie katiba ibadilishwe ikiwemo ya tume huru ya uchaguzi na hili la spika( ikiwezekana awe mtu huru pasi chama) inawezekana
2. Ya kuwa JK ajiuzulu hata kam mtaona haiwezekani ingekuwa kila tukilala na kuamka marungu tunaelekeza kwakwe, leo hii tungekuwa mbali.

3. Uozo wa ufisadi huko kila kona mpaka umekuwa wimbo sasa people are no longer excited na hizi habari sana sana ndiyo waroho wanaongezeka , nchi inhitaji kukombolewa haraka!
Mkuu Waberoya, uko sahihi kabisa. Katiba yetu ina mapungufu makubwa, na labda hiyo ndio nguvu inayofanya chama tawala kisiwe na wasiwasi na hatua mbalimbali inazozichukua.

Ila Mkuu wangu, ni kivipi unampata mtu asie na chama? Unajuaje kuwa mtu huyu hana chama? Kumbuka, Tume ya uchaguzi inaongozwa na watu wanaotakiwa wasiwe na chama chochote cha siasa. Je, unadhani (kwa matendo yao) hilo ndivyo lilivyo?
 
Dr. Slaa,
Neno "chombo" katika Art.100 ya Katiba yetu inamaanisha vyombo (branches) vitatu vinavyotajwa na Katiba - Bunge (Parliament), Rais (Executive) na Mahakama (Judiciary). Art.100 ni mojawapo ya "checks and balance" tool iliyowekwa na Katiba kulinda upekee wa hivi vyombo vitatu. NEC sio chombo kulingana na maana ya "chombo" katika Ibara 100 ya Katiba. Ndio maana, comment yangu ya awali ni ya bado ya msingi. Sub article (2) ya ibara hii inaendelea kukaza uhuru wa mbunge kutoa maoni bila la hofu ya kushtakiwa mahakamani kwa lolote atakalolisema akiwa kwenye vikao vya Bunge.
Sungi,
Nakushukuru kwa tafsiri yako ya neno "chombo" naomba ufanye utafiti wa kina kuhusu neno "chombo" kama inavyotumika ndani ya Katiba, na ni pana kuliko unavyotaka kuonyesha. Rejea vile vile Ibara ya 63(2). Lakini Tafsiri yako hai hold kama utafanyia utafiti maneno yote yaliyoko Ibara ya 100 na 101 katika ujumla wake. Ni hatari sana kuchukua sehemu tu ya Ibara ya Katiba au ya sheria yeyote kwa lengo tu la kutaka kuhalalisha unachotaka wewe, au unachoamini wewe. Ukiisha kufanya utafiti wa kina na kutoa tafsiri ya maneno yote yaliyotumika katika Ibara ya 100 tunaweza kuendelea kujibizana vinginevyo ni malumbano yasiyo na tija.
 
63(2) inasema, " (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."[Mkazo ni wangu]. tafsiri yangu ya chombo bado inashawishi hivi vyombo vitatu vya dola, Bunge, Rais na Mahakama.
Ibara 101 sio relevant to the question at issue, whether NEC ni "chombo" kwa maana "chombo kwenye Ibara 100. Hivyo nahitimisha kwamba CCM haijaingilia uhuru wa Bunge na kwa hiyo haijavunja Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Ninachokubaliana nawe ni kwamba articles 100 - 101 ni provisions zinazoelezea Mamlaka ya Bunge.
Asante :)
 
Dr. Slaa,
Mkuu wangu mimi nipo ktk kuuliza zaidi ili swala hili liwe wazi kwa sisi wote. Umesema Ibara ya 100 ya katiba ya Jamhuri inakataza kuhojiwa kwa mijadala ya Bunge na chombo chochote.. sawa nakubali lakini je, kuna mjadala au hoja yoyote ya Bungeni iliyojadiliwa na Kikao hicho cha CCM?..ama walimjadili Spika ktk Utendaji kazi wake na sii hoja, muswada ila mtazamo wa baadhi wabunge kuwa anakiuka sheria za chama kwa kuchukua upande wa wapinzani..ndio maana nauliza kuwa hivi Spika angekuwa upande wa Mafisadi ni wakati gani chama kinatakiwa kumjadili Spika nje ya Bunge.. Na let's say mkitaka motion of no confidance mafisadi wanaipinga pia.. where do we go from here!
Na statement kama za wajumbe wanaosema Spika anawaunga mkono wapinzani nadhani hii ni slaha kubwa kwa vyama vya Upinzani kwani yaonyesha wazi swala la Ufisadi ni nguzo ya Upinzani na CCM ipo ktk kuji defend!.. ushindi wenu hapa mkuu wangu, nukuu kama hizi ni matunda kwa Chadema.
Mkuu wangu nasema hivi kwa sababu ya huko tulikotoka, mfano mzuri ni Mkapa na mashtaka yote yanayomkabili yanalindwa na katiba (according to..) na kama ujuavyo, wewe mwenyewe umekwama kutokana na Bunge kutoafiki hoja yako na hawawezi kukuunga mkono..Sote tumebakia kushika matama wakati mzee mzima akistaafu na mabillioni..
Bahati nzuri Spika yupo upande wetu na tutaendelea kumtetea lakini what if ingekuwa kinyume, sio ndio ya Mkapa tena hayo!
Mkandara,
Nashukuru kwa maswali na hoja zako nzuri.
i) Kama tumefuatilia vizuri hoja za Chiligati, Spika amejadiliwa na NEC kwa kuruhusu Mijadala dhidi ya Chama, na kuwa ameshindwa kuizuia. Hivyo, swala hapa sio la Maadili ya Spika. Ni utendaji kazi wa Spika, katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ndio yanahojiwa. Swala lingelikuwa tofauti iwapo wangelikuwa wanajadili conduct ya Spika dhidi ya Sera au ilani ya CCM.
2) Ieleweke pia kuwa ndani ya Bunge hakuna Sera wala ilani ya Chama chochote inayojadiliwa. There is a serious misconception on this issue tu. Jambo likiingia Bungeni ni Sera ya Taifa. Sera na Ilani za CCM zinaishia pale maandalizi yanapomalizika ndani ya Serikali, yaani Sera ya Chama Tawala inapogeuzwa kuwa mswada wa Serikali au Bajeti ya Serikali. Chama Tawala kinategemea uwingi wa wabunge wake kupitisha Sera hiyo ya Taifa( ya Serikali). Lakini, Wabunge wanajukumu kwa Dhamira yao, kwa Taifa lao, na pale wanapoona Mapendekezo ya Serikali ( Japo Serikali hiyo imetokana na Chama chao) yanaenda kinyume na Maslahi ya Taifa na kwa dhamira yao wanaona hivyo, ndipo inapotokea katika mabunge yote kitu kinachoitwa Back Bencher Rebellion. Utafiti wa utendaji katika Mabunge yote, ikiwemo la Westminster ambalo sisi tumechukua mambo mengi kwao ndivyo unavyodhihirisha. Ndani ya Bunge letu, japo kwa jambo dogo sana kulikwisha kutokea Back Bencher Rebellion wakati wa Mhe. Spika Msekwa. Hoja ya Serikali iliangushwa na Wabunge kutokana na Schedule of Ammendment iliyowasilishwa na Mheshimiwa V.P. Kone, Mbunge wa Simanjiro wakati ule, if my memory carries me correctly. Hivyo si jambo jipya.
4) Kifungu cha 64 ya Kanuni za Bunge Toleo la 2007 iko wazi kabisa,
a) Kinakataza mambo ambayo hayaruhusiwi kujadiliwa ndani ya Bunge (prohibited).
b) iwapo jambo linalojadiliwa na Mbunge ni kati ya mambo yanayokatazwa kuna utaratibu uliowekwa na Kanuni ya 64(2) ambayo inamtaka Mbunge yeyote, kusimama na kutoa taarifa kwa Spika kuwa jambo linalojadiliwa limekatazwa na Kanuni, na Spika kwa mujibu wa Kanuni anachukua hatua. Kama hakuna Mbunge aliyesimama Spika, kwa Kanuni hawezi kuchukua hatua "Suo Motu" ( yaani kwa hiari yake mwenyewe- ni hiki kipengele kimewekwa kulinda maximum freedom ya Mbunge Ibara ya 100 ya Katiba). Ikumbukwe kuwa Wabunge waliomshambulia Spika walikuwepo Bungeni (au walitegemewa kuwepo) na hawakuchukua hatua yeyote. Hivyo Spika hawezi kubebeshwa lawama so long as taratibu zote za Kanuni zimefuatwa. Kanuni zinaifanya Bunge kuwa Self Regulating katika mambo yake kwa principle ile ile ya Separation of Powers and to provide maximum/ absolute protection kwa Bunge ili kutimiza jukumu lake la Oversight au Watchdog kwa "Serikali na vyombo vyake vyote". Tusipoelewa dhana hii nzima tutatukuwa tunazunguka kama pia, na hatutapata scientific/legal solution. Si vema katika mambo mazito kama haya kujadili bila kujua misingi, na au tukaweka ushabiki wa vyama ( ndiyo maana mimi pamoja na Tofauti zangu nyingi na Spika, na mara nyingine hata kuzuia hoja zangu kwa nguvu, simtetei Spika Sitta kama Sitta bali ninaitetea Taasisi ya Bunge kama Taasisi, na hivyo "Uspika" badala ya Spika.
c) Katika hoja zilizoibua mjadala ndani ya NEC kwa wanaofuatilia wanafahamu ni hoja ambazo Serikali inaona inaziaibisha Serikali mathali, hoja nzito zilizotolewa na Wabunge na "kuibana" Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Richmond, Majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Kiwira ( ambayo Mhe. Mkapa anahusika moja kwa moja, japo katika Taarifa ya Serikali walikwepa kumwonyesha Mhe. Mkapa Mwenyewe alivyohusika kupitia Kampuni yake ya ANBEM lakini walionyesha ushiriki wa watoto wake, lakini pia wakajikoroga zaidi Serikali ilipotoa Tamko kuwa inataka kuwalipa hao wanaotuhumiwa kukiuka sheria ya Maadili kama Fidia-japo baadaye imerekebisha Kauli hiyo na kusema itafanya Tathmini), Hoja ya Uuzaji wa Nyumba za Serikali. Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 64 Hoja hizo zimeanzishwa na Wabunge, na Serikali ikatakiwa kujibu. Serikali yenyewe ikaahidi kutoa Taarifa ya Utekelezaji. Hivyo Taarifa hiyo ya Utekelezaji ambayo haikukidhi hoja za Bunge ziliwekwa kwenye "Order Paper" yaani "Orodha ya Shughuli za Bunge kwa Siku husika, jambo ambalo linafanya hoja hizo kuwa miongoni mwa hoja ambazo hazikuzuiliwa kujadiliwa, hata kama Mhusika ni Rais, ikizingatiwa kuwa Rais ni Mwenyekiti wa Executive yaani Serikali, na huwezi kuilaumu Executive( Mawaziri na Makatibu Wakuu, bila kumgusa Rais, ambaye ni Mwenyekiti na maamuzi yote yanafanyika na Baraza la Mawaziri, ambalo Rais ndiye Mwenyekiti). Katika Hoja ya Aina hiyo Spika hana mamlaka ya kumzuia Mbunge yeyote kuijadili kwa kina, alimradi anatumia " Parliamentary Language" na Parliamentary Language, inapata Tafsiri pana kutokana na historia ya Mabunge yote duniani, siyo Bunge la Tanzania tu. Hivyo, si sahihi kumbana Spika kwa msingi wowote ule kwa "kuwa ruhusu wabunge kujadili" he is not just a referee, he is a Referee that should meticulously observe the rules of the Game, and not to arbitrarily decide on the performance and operations of Parliament. Natumaini nimetoa mwanga kidogo kwa wale ambao hawakuwa na details za kwanini tumelinda "Speakership as an Institution". This is paramount if we want to protect real democracy in this country and not a lip-service democracy. We are of course still a long way to go, but we have to have a starting point.
 
Madela wa madilu,
Mkuu mimi hilo la kanzu na mvaaji wake kidogo limenibakiza kizani kwani navyojua mimi hatuzungumzii joho la Spika ila Bunge. yaani Msikiti au kanisa na upande wa pili kuna Sheikh au Padri.
Sasa ikiwa unamatatizo na Sheikh au Padri sidhani kama utakuwa unalitukana kanisa au msikiti kwa sababu ya uendeshaji ibada wa Sheikh au Padri X..na wala hutakuwa unafanya kufuru ya dini, aya au sala nzima, isipokuwa unahoji udhu (usafi) wa mwendesha ibada. Kama yeye sii msafi kuna kila sababu ya sala nzima kutopokelewa ipaswavyo..

Nikirudi ktk swala la Bunge bila shaka mnakumbuka kwamba hata hapa JF ni kama chombo chochote kinachokatazwa kujadili mambo ya Bungeni kikatiba.. lakini tumeona hoja kibao za wabunge tukizijadili jambo ambalo mimi naweza sema ni kuvunja katiba..Lakini sidhani kama ndio maana ya sheria hiyo kuwekwa kwamba wananchi ktk vyombo vyao hawaruhusiwi kudajili maswala ya Bungeni isipokuwa ibara hii imetanguliwa na maswala fulani muhimu ambayo yanakataza mjadala hiyo..
Sasa bila shaka ningependa kuisoma sheria nzima kwa mapana yake ili nipate mwanga zaidi kwani katiba yetu ina tobo nyingi sana ambazo baadaye zinaweza kutumaliza sisi wenyewe. Pia katiba ni sawa na msahafu unahitaji mwanga mkubwa sana kuelewa na kila aya inakuwa na hadithi nyuma yake meaning tunatunga sheria kutokana na matukio na sii kubuni sheria..

Nitarudia kusema maneno ya Chiligati na wabunge wengine wengi wachovu wa kufikiri, makuhadi wa Ufisadi ni maneno mazito sana (hayabebeki) kuhusiana na yale yanayotokea Bungeni, lakini pia tuwe wepesi kutazama upande wa pili wa sarafu hii kwamba what if Speaker wa Bunge atakuwa upande wa utawala wa Kidikteta. Tuwe na rais kama Mugabe ambaye Spika alikuwa akimpongeza hata katika maasi na mapungufu makubwa ya chakula nchini mwao kwa sababu tu hataki kuachia ngazi ya Utawala.. hawa watu watafungwa na sheria gani?..

pamoja na kuwepo ibara ya 100 ningependa kuona Ibara inayotengua sheria hiyo ikiwa Kiongozi, mbunge au rais amekiuka miiko ya uongozi na kalitumia Bunge kujenga sheria kinyume cha haki..naelewa vizuri sana swala la Sitta na msimamo wangu upo wazi kabisa against hao mafisadi na naomba Mungu washughulikiwe lakini hii isiwe sababu ya kutokuwa na sheria ambayo Spika wa Bunge anaweza kufanya anayotaka kuyafanya kama kumwondoa Zitto bungeni kisha isiwe ruksa kwetu wala vyombo vyovyote kujadili au kutafuta haki ya mhusika kwa sababu tu Spika analindwa na sheria za Bunge.
Waswahili tunasema Sheikh kaingia na mbwa msikitini!
Mkandara,
Kifungu nadhani cha 4 na 5 cha Kanuni za Bunge zina provide, avenues, pale Spika anapokuwa ametoa uamuzi na agreeved party, ana uhuru wa kukata Rufaa kwa Kamati ya Kanuni. Kamati hiyo inayo mamlaka ya kumwita (summon) Spika, na kusikiliza pande zote husika, na uamuzi wa Kamati hiyo utatolewa Bungeni. Hivyo kama nilivyosema, Bunge inayo Self Regulating mechanism, iwapo Wabunge tutafuata Kanuni vizuri, Arbitrariness haipaswi kuwepo. Kanuni za 2007 zimetoa nafasi hata kwa mtu mwingine yeyote asiye Mbunge, akiumizwa na Kauli iliyosemwa ndani ya Bunge, kupeleka Malalamiko yake kwa Spika, na Kamati ya Maadili ya Bunge inalitazama swala hilo na au itamshauri Spika, au itatoa Taarifa yake ndani ya Bunge. Hivyo Mechanism ipo kama itafuatiliwa kikamilifu. Taratibu hizo za Rufaa dhidi ya Spika zimekwisha kufanyika ndani ya Bunge letu, japo process hiyo nadhani haijafikia mwisho wake.
 
Mkandara,
Nashukuru kwa maswali na hoja zako nzuri.
i) Kama tumefuatilia vizuri hoja za Chiligati, Spika amejadiliwa na NEC kwa kuruhusu Mijadala dhidi ya Chama, na kuwa ameshindwa kuizuia. Hivyo, swala hapa sio la Maadili ya Spika. Ni utendaji kazi wa Spika, katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ndio yanahojiwa. Swala lingelikuwa tofauti iwapo wangelikuwa wanajadili conduct ya Spika dhidi ya Sera au ilani ya CCM.
2) Ieleweke pia kuwa ndani ya Bunge hakuna Sera wala ilani ya Chama chochote inayojadiliwa. There is a serious misconception on this issue tu. Jambo likiingia Bungeni ni Sera ya Taifa. Sera na Ilani za CCM zinaishia pale maandalizi yanapomalizika ndani ya Serikali, yaani Sera ya Chama Tawala inapogeuzwa kuwa mswada wa Serikali au Bajeti ya Serikali. Chama Tawala kinategemea uwingi wa wabunge wake kupitisha Sera hiyo ya Taifa( ya Serikali). Lakini, Wabunge wanajukumu kwa Dhamira yao, kwa Taifa lao, na pale wanapoona Mapendekezo ya Serikali ( Japo Serikali hiyo imetokana na Chama chao) yanaenda kinyume na Maslahi ya Taifa na kwa dhamira yao wanaona hivyo, ndipo inapotokea katika mabunge yote kitu kinachoitwa Back Bencher Rebellion. Utafiti wa utendaji katika Mabunge yote, ikiwemo la Westminster ambalo sisi tumechukua mambo mengi kwao ndivyo unavyodhihirisha. Ndani ya Bunge letu, japo kwa jambo dogo sana kulikwisha kutokea Back Bencher Rebellion wakati wa Mhe. Spika Msekwa. Hoja ya Serikali iliangushwa na Wabunge kutokana na Schedule of Ammendment iliyowasilishwa na Mheshimiwa V.P. Kone, Mbunge wa Simanjiro wakati ule, if my memory carries me correctly. Hivyo si jambo jipya.
4) Kifungu cha 64 ya Kanuni za Bunge Toleo la 2007 iko wazi kabisa,
a) Kinakataza mambo ambayo hayaruhusiwi kujadiliwa ndani ya Bunge (prohibited).
b) iwapo jambo linalojadiliwa na Mbunge ni kati ya mambo yanayokatazwa kuna utaratibu uliowekwa na Kanuni ya 64(2) ambayo inamtaka Mbunge yeyote, kusimama na kutoa taarifa kwa Spika kuwa jambo linalojadiliwa limekatazwa na Kanuni, na Spika kwa mujibu wa Kanuni anachukua hatua. Kama hakuna Mbunge aliyesimama Spika, kwa Kanuni hawezi kuchukua hatua "Suo Motu" ( yaani kwa hiari yake mwenyewe- ni hiki kipengele kimewekwa kulinda maximum freedom ya Mbunge Ibara ya 100 ya Katiba). Ikumbukwe kuwa Wabunge waliomshambulia Spika walikuwepo Bungeni (au walitegemewa kuwepo) na hawakuchukua hatua yeyote. Hivyo Spika hawezi kubebeshwa lawama so long as taratibu zote za Kanuni zimefuatwa. Kanuni zinaifanya Bunge kuwa Self Regulating katika mambo yake kwa principle ile ile ya Separation of Powers and to provide maximum/ absolute protection kwa Bunge ili kutimiza jukumu lake la Oversight au Watchdog kwa "Serikali na vyombo vyake vyote". Tusipoelewa dhana hii nzima tutatukuwa tunazunguka kama pia, na hatutapata scientific/legal solution. Si vema katika mambo mazito kama haya kujadili bila kujua misingi, na au tukaweka ushabiki wa vyama ( ndiyo maana mimi pamoja na Tofauti zangu nyingi na Spika, na mara nyingine hata kuzuia hoja zangu kwa nguvu, simtetei Spika Sitta kama Sitta bali ninaitetea Taasisi ya Bunge kama Taasisi, na hivyo "Uspika" badala ya Spika.
c) Katika hoja zilizoibua mjadala ndani ya NEC kwa wanaofuatilia wanafahamu ni hoja ambazo Serikali inaona inaziaibisha Serikali mathali, hoja nzito zilizotolewa na Wabunge na "kuibana" Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Richmond, Majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Kiwira ( ambayo Mhe. Mkapa anahusika moja kwa moja, japo katika Taarifa ya Serikali walikwepa kumwonyesha Mhe. Mkapa Mwenyewe alivyohusika kupitia Kampuni yake ya ANBEM lakini walionyesha ushiriki wa watoto wake, lakini pia wakajikoroga zaidi Serikali ilipotoa Tamko kuwa inataka kuwalipa hao wanaotuhumiwa kukiuka sheria ya Maadili kama Fidia-japo baadaye imerekebisha Kauli hiyo na kusema itafanya Tathmini), Hoja ya Uuzaji wa Nyumba za Serikali. Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 64 Hoja hizo zimeanzishwa na Wabunge, na Serikali ikatakiwa kujibu. Serikali yenyewe ikaahidi kutoa Taarifa ya Utekelezaji. Hivyo Taarifa hiyo ya Utekelezaji ambayo haikukidhi hoja za Bunge ziliwekwa kwenye "Order Paper" yaani "Orodha ya Shughuli za Bunge kwa Siku husika, jambo ambalo linafanya hoja hizo kuwa miongoni mwa hoja ambazo hazikuzuiliwa kujadiliwa, hata kama Mhusika ni Rais, ikizingatiwa kuwa Rais ni Mwenyekiti wa Executive yaani Serikali, na huwezi kuilaumu Executive( Mawaziri na Makatibu Wakuu, bila kumgusa Rais, ambaye ni Mwenyekiti na maamuzi yote yanafanyika na Baraza la Mawaziri, ambalo Rais ndiye Mwenyekiti). Katika Hoja ya Aina hiyo Spika hana mamlaka ya kumzuia Mbunge yeyote kuijadili kwa kina, alimradi anatumia " Parliamentary Language" na Parliamentary Language, inapata Tafsiri pana kutokana na historia ya Mabunge yote duniani, siyo Bunge la Tanzania tu. Hivyo, si sahihi kumbana Spika kwa msingi wowote ule kwa "kuwa ruhusu wabunge kujadili" he is not just a referee, he is a Referee that should meticulously observe the rules of the Game, and not to arbitrarily decide on the performance and operations of Parliament. Natumaini nimetoa mwanga kidogo kwa wale ambao hawakuwa na details za kwanini tumelinda "Speakership as an Institution". This is paramount if we want to protect real democracy in this country and not a lip-service democracy. We are of course still a long way to go, but we have to have a starting point.

This is a well expounded response. Asante
 
Mkuu, ilisemekana kuwa chama cha Wangwe kilitaka kumnyang'anya uanachama Wangwe kwa sababu zao. Hilo linawezekana kwenye chama chochote na kama vikao husika vimefikia uamuzi huo, ni halali kabisa kufanya hivyo. Vile vile, Spika angeweza kabisa kupoteza uanachama wa CCM kama kikao hicho kingeridhia kwa idadi inayotakiwa kufanya hivyo (nayo bila kuvunja sheria yoyote).

Mkuu, hakuna chama kinachoweza kumnyang'anya Mbunge kiti chake cha Ubunge. Katiba ya nchi haina kipengele kinachotoa ruhusa hiyo. Bali, kwakuwa Mbunge ni lazima awe ametoka katika chama chochote cha siasa, anaponyang'anywa uanachama automatically anapoteza kiti cha Ubunge. Maana ya hili ni kuwa, hata kama si nia ya chama kumnyang'anya Ubunge mtu ambae amefukuzwa kwenye chama alichokuwa akikiwakilisha Bungeni, nafasi yake ya Ubunge itakoma automatically. Hivyo basi, uwezekano uliopo wa chama kumfukuza mwanachama wake ubunge ni kwa kutumia trick hiyo tu.
Recta,
Statement yako kuwa mtu akinyang'anywa uanachama Ubunge wake una cease automatically siyo kweli sana. Nadhani turudi kwenye Historia ya Bunge letu, ambapo CUF kupitia vikao vyake halali viliwafukuza uanachama wabunge wake wa Viti Maalum. Wabunge hao walienda mahakamani na Wakarudishwa na Mahakama, na wakaendelea kuwa Wabunge hadi mwisho wa uhai wa Bunge hilo. Nadhani tufanye utafiti kuona kuwa kinachosemwa kuwa Chama kina absolute power siyo kweli. Tatizo ni kuwa wengi hawafahamu "avenues" nyingi za haki katika Sheria zetu. Tujenge utamaduni wa kufanya utafiti wa kina ili tuweze kuisadia jamii yetu na Taifa kwa ujumla. Tunaweza kuwakatisha Tamaa, wakati Precedence ipo.
 
Dr. Slaa,
Neno "chombo" katika Art.100 ya Katiba yetu inamaanisha vyombo (branches) vitatu vinavyotajwa na Katiba - Bunge (Parliament), Rais (Executive) na Mahakama (Judiciary). Art.100 ni mojawapo ya "checks and balance" tool iliyowekwa na Katiba kulinda upekee wa hivi vyombo vitatu. NEC sio chombo kulingana na maana ya "chombo" katika Ibara 100 ya Katiba. Ndio maana, comment yangu ya awali ni ya bado ya msingi. Sub article (2) ya ibara hii inaendelea kukaza uhuru wa mbunge kutoa maoni bila la hofu ya kushtakiwa mahakamani kwa lolote atakalolisema akiwa kwenye vikao vya Bunge.
Mkuu, sijui umepata wapi tafsiri ya neno chombo kama lilivyoumiwa na Katiba ya nchi kiasi cha kuamua kuizuia kwa nguzo hizo tatu za uongozi (Bunge, Mahakama na Serikali). Katiba ya nchi haijasema kuwa maana ya neno hilo (chombo) ni kuhusiana na taasisi hizo tu.

Kimsingi, kama taasisi hizo kubwa kabisa nchini zinazuiwa kufanya majadiliano, au kufungua mashauri yoyote kuhusu kauli zinazotolewa ndani ya Bunge au utendaji wa Bunge, ni taasisi gani nyingine (labda tusiyoijua) ambayo kwa mtazamo wako sio chombo ambayo ina mamlaka na haihuzuiwi na Katiba kuingilia uhuru wa Bunge?

Kwa mtazamo wangu, neno chombo lina maana pana zaidi ya kumaanisha serikali, bunge na mahakama. Nadhani neno hili kwa uwazi wake, lina maanisha muundo wowote wa kitaasisi, kundi lolote la watu au vinginevyo.
 
Dr Slaa

Heshima Mbele! Naomba kuuliza:

Hivi haiwezi tolewa hoja binafsi bungeni, kumtaka Chiligati achukuliwe hatua za kisheria kwa kulidharau bunge kwa matamshi yake tata hadharani tena akiwa ni mtumishi wa ngazi ya ya juu serikalini? Mpaka sasa hajatoka hadharani kukanusha au kuweka mambo sawa, kwanini asishughulikiwe ili kuondoa mbegu mbaya inayopandwa kwa kizazi hiki na kijacho?

Na kuhusu NEC kulidhalilisha Bunge thru Spika, mtu yeyote anaweza kwenda mahakamani au inabidi swala hili lirudi Bungeni? Lazima awepo mtu wa kuanzisha hoja ndani au nje ya Bunge...huu ni muda mwafaka wa kusafisha nyumba.
 
Mnyoofu,
Uko sahihi, kuna njia za "redress" kwa kutumia i) Sheria na 3 ya Mwaka 1988 (RE), yaani, Parliamentary Immunities and Privileges, Act, 2) Lakini pia kutumia Kifungu cha Kanuni kinachohusu "hoja ya dharura inayohusu Haki na Hadhi ya Bunge". Hoja hii inaweza kuwasilishwa wakati wowote, na kwa mujibu wa Kanuni inavunja/Kusimamisha shughuli zingine zote zinazokuwa zinaendelea. Nadhani kwa sasa niishie hapo, bila kuingia ni kitu gani hasa kitafanyika. Tungelitegemea wakereketwa wa CCM watali pick up, na kuli raise, kwa vile wao ndio wanaonyamazishwa kimsingi. Opposition, kama mnavyofahamu tumezoea kuzuiwa kwa utaratibu wa uwingi wa Wabunge wa CCM ambayo ni hoja tofauti na si hoja inayojadiliwa hapa.
 
Ningependa kukushukuru Dr Slaa kwa point zako. Umeeleza hili jambo vizuri na kwa unyeyekevu kwa wadau humu ndani. Nimepata somo zuri hapa leo.

Ivi spika anaweza kuleta hoja ya dharura (au hoja nyingine yeyote bungeni)? Maana yeye si bado mbunge wa eneo lake, hivyo ningetegemea angeweza kufanya hivi.
Kweli sisi bado ni demokrasia changa. Na taratibu tunajifunza mengi.
 
Mkuu Mkandara, mfano wako ni mzuri sana.

Ni kweli kuwa chama kingeweza kumng'oa uSpika ndani ya Bunge pekee na sio kwenye vikao vya chama. Vikao hivyo vingetumika kupanga mikakati hiyo tu.

Jaribu ku-imagine mkuu (mfano mwingine), kuwa Bunge lina uwakilishi wa mchanganyiko mkubwa wa chama tawala na vyama vingi vya siasa (le's say 10). Na kati ya hivyo hakuna chenye wabunge zaidi ya theluthi moja. Baadhi ya vyama ni dhahiri vitaungana na kupitisha jina moja la mtu wanaeona anawafaa kuwa Spika na hivyo mtu huyo kushinda nafasi hiyo. Je, ni chama gani kati ya hivyo kitakachokuwa na nguvu ya kumuita Spika na kumshinikiza kufanya watakayo?
Mkuu Shukran maadam tunakwenda kwa kituo nadhani nitakuwa na nafasi nzuri ya kujieleza point by point kuliko kuzunguka mji mzima ktk kujieleza hoja hii.

Ni hivi mkuu wangu swala hapa sii USPIKA na kamam sikosei hakuna mahala CCM wanasema wanataka kumvua Sitta - Uspika au Ubunge, isipokuwa wanataka kumnyang'anya kadi ya chama...madaia haya ni vitu viwili tofauti kabisa, Na kwa sababu sisi tunafahamu matokeo ya kunyang'anywa Sitta kadi ya chama ndio tumefikia conclusion ya kile kitakachofuata..

Nikirudi ktk mfano wako, ikiwa Huyo Spika ni mwanachama wa chama chochote kile cha Siasa, chama hicho kina kila haki ya kumweka kitimoto Spika yaani anasimama kizimbani kama mwanachama wa chama hicho na kwa kutumia sheria za chama hicho. Ila tu kesi yake haitakiwi kuzungumzia (jambo lolote linalohusiana na ibara ya 100) lakini haikatazwi kumzungumzia Spika kama mwanachama ambaye anasaidia upande wa upinzani kwa kuuza siri za chama chake.. (hata kama siri hizo ziwe Ufisadi).

Kwa mfano Spika kama ni mwanachama wa CUF anauza siri za chama hicho kwa CCM au hata Chadema ktk maswala yao nyeti.. kisheria (katiba) siwezi kuona kosa kabisa CUF wakimwita kiongozi huyo na Kumshinikiza kwani kuuza siri za chama sio agenda ya kikao chochote cha Bunge, ila mhusika ndiye Mbunge na Spika.. Nje ya hapo yeye ni mwanachama wa CUF alivua joho lake la Uspika na kutumia kadi ya chama CUF kuuza siri za chama akiwa bungeni..

Hivyo, madai ya wajumbe mafisadi wa CCM ni kwamba Sitta anawasaidia wapinzani (vipi?..) na pengine Ufisadi ni siri ya chama CCM..Kwa hiyo mnapo quote sheria za Kitaifa (Katiba) inaonyesha wazi mnashindwa kuelewa kwamba Sitta ni mwanachama wa CCM na anashtakiwa kwa makosa ya uanachama wa CCM kulingana na katiba ya CCM..pamoja na kwamba yeye ni Spika.

Mkuu wewe na mimi tunaelewa wazi kuwa Ufisadi ndio unatumaliza ni ushenzi mkubwa na wanatakiwa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo lakini kiongozi ndio hatuna.. JK muungwana, msanii asiyeweza kutawala nchi bali kiushikaji..hivyo tukubali kwamba hilo kanisa la CCM wameamua kusali uchi na Ufisadi ni moja ya ibada zao za siri..(The skull) Spika kakiuka miiko yao anatoa siri za kanisa nje, nasema CCM wana kila haki ya kumwadhibu kulingana na katiba (ushetani) wao..
Na ndio mfano wangu kwa Wangwe ulipoingia, kwani kama sikosei ilisemakana kwamba Mahehemu Wangwe alikuwa akiuza baadhi ya siri za chama au kuzungumza uongo kukipaka chama na kadhalika!..
Mimi sijui kitu kuhusu ukweli/Uongo huo na sintapenda kutumia ushahidi wa Chadema kuitazama haki ya chama hicho kumsimamisha Uenyekiti au kumnyang'anya kadi Ila nachotazama ni makosa yaliyojengwa ili kusimamisha mashtaka kisheria..

Chadema walikuwa na kila haki kujenga mashtaka hayo na motion iliyoombwa ni kummwondoa marehemu ktk Uenyekiti..Sasa walipotangaza tu hiyo motion, tayari wananchi tukavamia Chadema kama vile tayari Marehemu alikwisha hukumiwa...Oooh haiwezekani Wangwe kunyang'anywa Uenyekiti na kundi la Mbowe, Dr. Slaa na Zitto tukasahau kwamba haya yalikuwa ni madai ambayo kisheria yalihitaji kupata sheria na ufumbuzi kwa kutumia ushahidi na sio hisia za watu ama sheria nje ya sheria za chama hicho.

Mimi kama Mkandara au mwanaCCM naweza kuona ubaya mkubwa wa majungu na mengineyo lakini kisheria kulingana na katiba ya chama Chadema, ipo miiko ambayo mwanachama anaweza kupoteza uanachama au kti chake through hatua kadhaa ambazo sii lazima siwe sawa na za CCM au CUF.

Kikatiba CCM hawawezi kumnyang'anya Sitta Uspika wala Ubunge isipokuwa wanaweza kumnyang'anya Uanachama na matokeo ya kitendo hico kinaweza kabisa kuzua matokeo mengine ya kupoteza Ubunge na hata kupoteza Uspika..Inatisha na haipendezi lakini ndio ukweli wenyewe kwamba Mafisadi wanaweza kutumia njia ya mkato, kisheria na kupitia vichochoro vya makosa ya kichama kumng'oa Sitta bila kupitia barabara kuu. Na matokeo yakawa na uzito sawa kabisa!

Mimi, wewe na wengine wote tunafahamu fika kwamba ikiwa Sitta atanyang'anywa uanachama CCM, dhahiri wataweza kuifikisha bungeni hoja hii ipigiwe kura ya motion na atashindwa kutokana na hofu ya ushindi wa mafisadi ktk mkutano huu, baadaye miezi inayofuata 2010 Ubunge pia ungepotea...

Ni mbinu chafu sana lakini sidhani kama wanavunja sheria ikiwa watatumia Ujanja wa chama. Nina hakika hawa jamaa wanajua fika kwamba Ukitaka kumwondoa Spika ni kuwakilisha hoja Bungeni na kura za motion of no Confidence zitaamua lakini kwa kufahamukwamba njama hiyo haiwezi kushinda na hawatapata kura za kutosha wamechagua kuanza na mkutano mkuu ambako kuna Makabuntas, Washabikia wali wa Maulidi, na kina hamnazo kibao ambao watabuya Ulevi wa Rostam kirahisi..Wakiweza kumshinda Sitta ktk kikao cha chama na kumyang'anya uanachama basi mengine yote yatakuwa rahisi kabisa na hata kama wakishindwa kufanya hivyo---Most important - Ujumbe utakuwa umefika!.

Ujumbe wao utakuwa umefika kwa mwenyekiti, Sitta na wajumbe wengine wote wapinzani wa Ufisadi..Na kusema kweli UJUMBE UMEFIKA... maanake sote tunateteleka sasa hivi, nchi nzima inachemsha na kukimbilia sheria wakati hawa jamaa wamekuja na silaha mpakani kupigana vita.. Sisi ndio kwanza tunalilia haki na UN wako wapi...Hakika Ujumbe wa kina Rostam umefika kwa wabunge wote..That they can take U out anytime na serikali, JK wala mshenzi yoyote hawezi kuzuia kitu.

Sasa mchezo alocheza JK pia ulikuwa kinyume cha mategemeo ya Mtandao kwani kawasikiliza akaona vitisho vyao na hakika Sitta, Mwakyembe na wengine wajumbe wote against Ufisadi matumbo moto.. Ujumbe wa mafisadi uli hit haswa kama walivyokusudia ila nilichoweza kugundua ni kwamba JK pia alikuwa na mtego wake for his own survival.. Kawaacha walolonge weee kwa hesabu na ukubwa wa kundi zima akawajua wote wabaya wake kwani alompa kichwa Sitta ni yeye. Mwisho wa mjadala kawachagua Mwinyi, Mzee Msekwa, Kinana ambao wote ni watu wake hivyo sioni kesi yoyote zaidi ila nahofia zaidi plan B ya mafisadi kama Ipo..
 
Last edited:
Back
Top Bottom