BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
absolutely! kwa sababu hatujaathirika moja kwa moja na hayo yote unayoyasema. Sasa hivi tunaishi kwa misingi kuwa endapo mimi na familia yangu tumepata chakula cha jioni, na watoto waemeenda shule na tuna nguo na mahali pa kulala hayo mengine mimi sijali. Hatukasirishwi na kuona mwingine anahangaika na mahitaji yake ya kila siku.
Wakati mwalimu aliongoza kwa sera ya "kabla wachache hawajishi katika anasa, wengi wapate mahitaji yao muhimu" leo hii kina Kikwete wanahakikisha "wachache wanazidi kuishi katika anasa huku wengi wakiahidiwa mahitaji yao muhimu". Matokeo yake, leo hii tunategemea wageni kutuchimbia visima; tunatarajia watu binafsi kuendesha shule za msingi na sekondari, n.k
Watu wakikataa kuridhika na wakatamani makubwa zaidi, mazuri zaidi na mema zaidi kwa sababu wanastahili wataona umuhimu wa cha kufanya. Lakini tukipewa kanga na tsheti huku tunaburudishwa na wimbo wa "nambari wani eeh" tunaridhika na kufurahia kuwa na sisi tumepata vikofia vya chama!
Mkjj umesema kitu kikubwa sana hapo. Nimeliona hili kwa marafiki wengi sana ambao ukiongelea matatizo yanayotokana na uongozi mbovu nchini mweru wanakuwa hawakuelewi kabisa na kutaka kukuonyesha kwamba hujui unaongea nini basi watakwambia "Wewe unaishi nje hali hapa nyumbani si mbaya kiasi hicho usiyaamini sana yote unayoyasikia au kusoma kwenye magazeti." Wengi wa hawa ni wale ambao wameridhika na maisha yao wana mishahara minono wanaweza kuafford shule za kulipia wana magari wengine zaidi mawili. Mimi huwaambia kwamba mficha ugonjwa maradhi yatamuumbua kwa maana kwamba ncghi yetu ina matatizo makubwa sana na Watanzania wengi wamekata tamaa ya maisha kutokana na utendaji mbovu wa Vuongozi wa juu ndani ya Serikali ambao wameweka mbele maslahi yao au ya CCM na kuwasahau kabisa mabilioni ya Watanzania ambao wanaishi maisha ya dhiki ya kutisha, siku ambayo hawa waliokata tamaa ya maisha wakisema sasa basi liwalo na liwe hata hao ambao wana maisha mazuri basi maisha yao yatakuwa hatarini na watajuta kwa nini walifumbia macho uongozi mbovu kwa miaka mingi nchini kwetu.