annamaria
Senior Member
- Apr 1, 2009
- 135
- 15
Mkuu tupeane pole, maana kwa kweli haya majambo yanauma. Nafikiri jambo moja ambalo hatujafanikiwa kulifanya ni kuhusisha ubovu wa uongozi tulio nao na shida ambazo wananchi wanazipata. Kila nipitapo vijijini nikiongea na wananchi unawaona wanavyosononeka, lakini ukiwauliza mnafikiri tufanyeje hatuongei lugha moja kama hii hapa JF. Hawaoni kabisa kama mazira yaliyopo yamesababishwa au yanasabishwa na uongozi na serikali tuliyo nayo kwa kiasi kikubwa na hawaoni kama hii serikali ndiyo inapaswa kuwa kinara wa kuyatatua. Ndio kusema wanapoenda kupiga kura hawaendi kuchagua mtu wa kutatua matatizo yao na ya taifa; wanaangalia vigezo vingine--mostly the most visible party and we all know which party this is. Na kama kuna sehemu watawala wamefanikiwa ni hapa-'keep them in dark for ever strategy'. Na hapa ndipo walipoanzia akina Raila. Leo hii wakenya wapo clear na kipi cha serikali na kipi cha mwananchi, na wanajua wanapokwama wapi wajilaumu wao na wapi waijabishe serikali yao.
Leo hii watanzania, tena wasomi kabisa, hata kazi za bunge hatuzijui--kama umefuatilia mjadala wa wanabidii. Utachoka!!
Mkuu Kitila tuanze na elimu ya uraia huko basi manake ndiyo tatizo.I mean tusisubiri mwezi ujao uchaguzi ndiyo tuanze kujitokeza kwa wananchi na kuwaambia kuwa umasikini wao unasababishwa na CCM.Hawawezi wakakuelewa,watajua umeenda kutafuta kura(read kula)tu!Na ndipo balaa inaanza hapo kwa vile walishazoea kupewa elfu mbili ili 'watoe kula' basi lazima na wewe wakuulize vipi unazo hizo 2000?Kama huna anza kuhesabu maumivu!!
Kuna sehemu nyingine Mkuu siyo siri wananchi wamechoka na wabunge wa CCM,isipokuwa hakuna potential alternatives,inafikia wanaona heri wachague yule yule wa CCM.Kuna mkulu mmoja wa NCCR nakumbuka 2005 nilishiriki kampeni yake kwenye jimbo ninakotoka.Sisi vijana tulimsaidia sana tena bila ya kulipwa hata senti tano.Na kizuri ilikuwa yule mgombea wa CCM aliyekuwa kipenzi pale na alishinda kwenye kura za maoni,jina lake likaja kuondolewa.CCM wakaja kutuletea Mbunge yuleyule ambaye tulikuwa hatumtaki.Lakini mkulu wa NCCR pamoja na hii golden chance aligalagazwa sana na yule babu wa CCM.
Sababu kubwa hakujiandaa.Maandalizi yake yalikuwa finyu sana na alichelewa kuonyesha nia yake ya kugombea.