Je, CCM Itatawala Milele Au?

Status
Not open for further replies.
- Wakuu wote JF heshima mbele sana, nimekuwa nikisumbuliwa sana na swali moja tunalalamika sana kuhusu matatizo ya uongozi wa CCM kwa taifa letu. Ni miaka 47 sasa CCM imetutawala Tanzania, nikiangalia historia inaonekana wenzetu yaani wazee wa zamani pamoja na uchache wao kielimu na tools, sio siri kwamba walikuwa wanatoa upinzani mzito sana kwa TANU/CCM kuliko sisi vijana wa sasa.

- Inaonekana kama wenzetu hawakuwa na maneno mengi sana, ila walikuwa na vitendo vizito sana na siku zote walikuwa wakiilaza macho serikali na CCM, tizama kina Anangisye, Mwabulambo, Kambona, Bibi Titi, Kassanga Ntumbo, wazee kama kina Chipaka, Magee, Lugangira yaani huyu pamoja na kumfunga jela alitoroka anyways, Nyirenda na wengineo, I mean mbona inaonekana kama they were more effective kuliko sisi wenye akili sana katika kuipigisha magoti serikali na TANU/CCM? Kila walipomaliza kufanya vitu vyao kuna mabadiliko flani yalikuwa yakifanyika kuitikia vilio vyao kuhusu taifa, infact ni wao ndio walishinikiza Sokoine kupewa power na ile vurugu ya mafisadi, sasa nini kimetokea sasa tena ukitilia maanani kwamba sisi tuna tools nyingi in our hands zaidi ya walizokuwa nazo wao! Hebu soma historia yetu utasikia kila wakati kulikuwa na tafrani somehow somewhere!

- Tuna vyama vingi vya siasa, tuna uhuru wa kuongea na kuandika, I mean wale hawakuwa na yote haya lakini they were more effective na vitendo vyao bubu kuliko sisi, WHY? Hebu tuambiane nini challenge ya maana iliyowahi kufanyika against CCM na serikali yake toka tuingie vyama vingi Mwaka 1995 to this date katika kuwafahamisha kwamba wananchi tumechoka na upupu mwingi wanaoufanya mpaka kuwashitua ili watusikilize kama wale wenzetu wa zamani?

- I mean I could be wrong vile vile, lakini this is what I see, we are just not effective enough or convincing to watawala, WHY? Halafu kumbuka kwamba milele ni pale tu mwisho wa maisha yako unapofika na sio anything esle!

Respect.

FMEs!

Hivi ndivyo vinavyofanya hali iwe hivi.Mivyama kibao,uhuru wa kuongea nao kila mtu anaropoka anavyopjisikia akiulizwa ana kwambia ana haki ya kuzungumza chochote ili mradi tu asivunje sheria.Kuonge kumekuwa kwingi kwani ukiongea siku hizi ndio watu wanakuona wewe wa maana.
 
Mkuu wewe unashauri tufanye nini ili tuwe more effective katika kufikisha ujumbe wetu kwamba haturidhiki na utendaji wa Viongozi wa juu wa Serikali.
 
- Not there yet mkuu wangu, just think for a second, Anangisye na Chipakas wamefufuka leo na kuanzisha chama chao cha siasa, wewe unafikiri patatosha kwenye hili taifa? Si patachimbika hapo! Sisi tunafanya nini wrong!

Respect.

FMEs!
 
Hawawezi tawala milele, mpasuko mbona ushaonekana? ila kwa sasa sisi wapiganaji uzalendo haupo ila ubinafsi ndo umetujaa, tujaze kwanza matumbo yetu, lakini ndo mwisho wa dunia wenyewe hata Paulo mtume alisema upendo wa mwanzo utapoa na watu wtakitafutia njia zao wenyewe. Yuko wapi Zito, Ane Kilango, Sita, Mwakyembe and the like.
 
- Mkuu wangu hata mimi I am lost kama wewe if you will, I mean ninaona jinsi Health Care bill ilivyokwama tena over the most popular ever president wa US, na hii inafanywa na the minority party, sasa swali langu ni kwamba sisi tunashindwa nini?

- Look kina Raila Odinga sasa hivi, hawa ni nini they are doing right mpaka wanasikilizwa na watawala wao ambacho sisi tunashindwa?

Kwa kweli patachimbika.Mi nadhani kuwe na ukomo wa vyama kwani watu tunadhani kuanzisha chama kipya ndio kukomboa nchi.Ndio maana leo kuna CCJ inataka kuja wakiwa na dhamira ya dhati kabisa ya kukomboa nchi.Hivi kwani hatuwei kukomboa nchi kwa hivi hiv vyama tulivyonavyo?kwanini nchi imetushinda?mbona karibu sera za vyama vyote na malengo yao ni mazuri mno tena tamu kuliko asali.Tatizo mi nadhani liko kwetu sisi wapiga kura.Tunadanganyika na maneno badala ya vitendo ndo maana leo hii kuna uhakika mkubwa wa wale waliotajwa kuwa ni mafisadi wakashinda majimbo yao tena kwa kura nyingi tu.Pia hata Wabumge walioshindwa kutekelzea yale waliyoyaahidi kwa kipindi cha miaka mitano watajitetea kwa wapiga kura na watashinda.
 
Hawawezi tawala milele, mpasuko mbona ushaonekana? ila kwa sasa sisi wapiganaji uzalendo haupo ila ubinafsi ndo umetujaa, tujaze kwanza matumbo yetu, lakini ndo mwisho wa dunia wenyewe hata Paulo mtume alisema upendo wa mwanzo utapoa na watu wtakitafutia njia zao wenyewe. Yuko wapi Zito, Ane Kilango, Sita, Mwakyembe and the like.

Ni jambo jema tukaangalia kinachowakwamisha hao hapo juu kabla hatujasema nani hamnazo nk....Maswali ni mengi,kama kuna wanaoweza kuunganisha dots watajua nachosema,hata MKJJ alishawahi kuuliza swali muhimu sana,je wanapigania nini?Maana ni vigumu kupima ufanisi kama huo endapo taifa halina dira wala mwelekeo....Kama ni kweli tunataka tujuwe kwanini tumekwama basi twende hatua kwa hatua,yani ni kipi kimesababisha kipi and so forth
Lazima tutambue kuwa malengo ya kutawala kwasasa ni tofauti sana na hapo nyuma,kwenye uchumi unaoendeshwa na watu binafsi bila kuwa na taratibu za kumonitor ili kuyalinda maslahi ya Taifa na wananchi zimebadilisha kabisa reasons ni kwanini watu wanataka uongozi,jiulize kwanza ni kwanini watu walio wengi wanataka uongozi kabla ya kujiuliza watafanya nini wakishapata uongozi.
 
- Mkuu wangu hata mimi I am lost kama wewe if you will, I mean ninaona jinsi Health Care bill ilivyokwama tena over the most popular ever president wa US, na hii inafanywa na the minority party, sasa swali langu ni kwamba sisi tunashindwa nini?

- Look kina Raila Odinga sasa hivi, hawa ni nini they are doing right mpaka wanasikilizwa na watawala wao ambacho sisi tunashindwa?

Respect.

FMEs!

Hata mimi I am lost too. Tukiacha individuals ambao ili kupata haki zao lazima wajiunge katika vikundi, kama wanaharakati, vyama vya upinzani n.k unafikiri ni organisation gani zinaweza kulaumiwa? maana kuna watu wamevaa nguo wakisema ukombozi unakuja, hatuuoni

Au which way ambazo tunaweza kuwapata akina Raila Odinga?

Or is it because we are so kind and good hearted citizen kwa hiyo issue za magomvi kama Kenya hatuziwezi, hivyo hatutaweza kuwapata akina Odinga?

Ni jambo jema tukaangalia kinachowakwamisha hao hapo juu kabla hatujasema nani hamnazo nk....Maswali ni mengi,kama kuna wanaoweza kuunganisha dots watajua nachosema,hata MKJJ alishawahi kuuliza swali muhimu sana,je wanapigania nini?Maana ni vigumu kupima ufanisi kama huo endapo taifa halina dira wala mwelekeo....Kama ni kweli tunataka tujuwe kwanini tumekwama basi twende hatua kwa hatua,yani ni kipi kimesababisha kipi and so forth
Lazima tutambue kuwa malengo ya kutawala kwasasa ni tofauti sana na hapo nyuma,kwenye uchumi unaoendeshwa na watu binafsi bila kuwa na taratibu za kumonitor ili kuyalinda maslahi ya Taifa na wananchi zimebadilisha kabisa reasons ni kwanini watu wanataka uongozi,jiulize kwanza ni kwanini watu walio wengi wanataka uongozi kabla ya kujiuliza watafanya nini wakishapata uongozi.

So tulikosea misingi? au kubadili mfumo wa siasa ndio umesababisha haya? swala lako muhimu na gumu pia, inabidi nitafute pain killer!
 
Heshima kwako Mkuu FMES,

Kwa hakika kwa mwenendo uliopo,yayumkinika kubashiri utawala wa milele wa CCM.Wakati wengi tunasononeshwa na hali ya huko nyumbani kuhusiana na mwamko mdogo wa kujikomboa dhidi ya ufisadi,uonevu,na madhambi mengine ya mfumo dhalimu,kuna upande wa pili wa tatizo hili ambao unasikitisha zaidi.Hapa nazungumzia hali ya kupuuza/kutojali hatma ya taifa letu miongoni wa Watanzania wengi walio nje ya nchi.

Tukiweka kando kundi la walio nje ya nchi kutokana na nafasi za wazazi/ndugu zao au ukaribu wao na mfumo fisadi,kuna mwamko mdogo sana miongoni mwa walalahoi kama mie ambao tunapaswa kutambua kuwa hata kama maisha ya huku yana nafuu,ndugu jamaa na marafiki zetu huko nyumbani wanaendelea kuathiriwa na mfumo dhalimu.Hiyo ni sababu tosha ya kulifanya tatizo hilo kuwa letu pia hata kama halitugusi moja kwa moja.Lakini ukipita kwenye mitandao mbalimbali (with exception of JF) utabaini kwamba kwa asilimia ya walio nje aidha hawajali kinachoendelea huko home au wanasapoti utawala uliopo madarakani.

Mfumuko wa matawi ya CCM nje ya nchi pia ni kielelezo kizuri,sambamba na kujitokeza kwa wingi kwa "wananchi" wanapokuja viongozi wa CCM.Kuna ujio wa Msekwa hapa Uingereza in next few days na tayari ujio huo umewavutia "wananchi" kadhaa japo natambua kuwa hiyo ni haki yao ya kidemokrasia.

Kwanini "nawalaumu" baadhi ya wa-tz walio nje ambao aidha wanapuuza matatizo ya nyumbani au wanakumbatia mfumo dhalimu?Jibu langu ni jepesi: kwa wengi wetu,uwepo wetu hapa unapaswa kuwa darasa tosha kuhusu namna serikali zinavyopaswa kuwajibika kwa wananchi au chama kilichopo madarakani kinavyopaswa "kuwanyenyekea" wapiga kura at all times na sio nyakati za chaguzi pekee.Japo simaanishi kuwa kila jambo maeneo haya ni perfect lakini kwa kiasi kikubwa tunaona namna siasa inavyotengenishwa na maslahi ya taifa na nchi inavyowekwa mbele badala ya chama.Kwa lugha nyingine,uwepo wetu huku unatupatia kioo kizuri cha kutusaidia kwanini tunasuasua kimaendeleo (hata kama kioo hicho sio absolutely perfect).

Wazalendo wa aina ya Mwanakijiji ni sauti adimu kutoka nje ya nchi.Hiyo ni tofauti sana na wenzetu Wakenya au Wazimbabwe (na wengineo).Hawa wanasaidia sana katika jitihada za kuwafahamisha "wafadhili wetu" namna watawala wetu wanavyotupelekesha.Najua kuna watakaosema hakuna haja ya "kuwapigia magoti ex-wakoloni wetu" lakini ni muhimu kufahamu kuwa misaada yao inatumika sana katika kudhoofisha jithada za kung'oa tawala dhalimu sambamba na kudumisha ufisadi.

Ndio maana,kama unakumbuka Mkuu FMES,niliwahi kuunga mkono "wazo la kiuendawazimu" kuwa mapinduzi kama ya huko Niger yanaweza kuwa relevant kwa Tanzania.Nafahamu madhara ya mapinduzi (hususan ya umwagaji damu) lakini binafsi nimeanza kukata tamaa ya uwezekano wa kupatikano msukumo kutoka ndani ya Tanzania utakaopelekea kuing'oa CCM au kupambana kwa dhati na ufisadi plus ku-consolidate efforts za kutuondoa kwenye umasikini wa kupindukia.

Correct me if I'm wrong,asilimia kubwa inayounda middle class ya Bongo inatamani zaidi kuwa sehemu ya upper class (isomeke ufisadi) than kujumuika na tabaka la walalahoi kujenga jamii tunayohitaji.Picha zinaelezea maneno 1000: tembelea blogu mbalimbali za picha uone "jitihada" za middle class kuji-portray kama members wa the upper class.

Lakini kikwazo kingine ni mentality inayosherehesha matendo dhalimu.Mhasibu anayeishi kwa kadri ya kipato chake atachekwa mtaa mzima kwamba "yani huwezi kuamini kuwa huyu ni mhasibu.Hata gari hana,na ana nyumba moja tu..." waki-imply sifa ya kuwa mhasibu ni kuwa na fleet ya magari ya kifahari,vibakauchumi lukuki,na vitu kama hivyo visivyoendana na kipato cha mhasibu huyo.Wahalifu wanaouza madawa ya kulevya wanaheshimika kama "mapedejee" na kutukuzwa kwenye tungo za bendi zetu huku mitaani wakipambwa na sifa za kuitwa "mzungu wa unga","bosi","kigogo",na sifa nyingine kama hizo za kipuuzi.

Naweza kuandika kwa kirefu zaidi lakini nimalizie kwa kuungana na baadhi ya wachambuzi wa siasa za Tanzania wanaodai kuwa Ujamaa kama itikadi ililenga zaidi kumtengeneza mwananchi aishi kama bepari lakini kwa misingi ya usawa na haki.As Kikwete said,wazo la Maisha Bora kwa Kila Mtanzania lilikuwepo tangu uhuru,ila ukiingia kwa undani namna ya ku-attain maisha hayo bora unaweza kuafikiana na wachambuzi hao kuwa Ujamaa katika namna isiyo wazi ungeweza kuzalisha (na ulifanikiwa kuzalisha) mabepari uchwara na hatimaye kusababisha contradictions ambazo zingepelekea kifo cha itikadi hiyo.
 
Sherehe za Miaka 33 ya Chama Cha Mapinduzi - Tawi la CCM Uingereza

CHAMA CHA MAPINDUZI

TAWI LA UINGEREZA SHEREHE YA KUZALIWA KWA
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
MIAKA 33 YA CCM
Wanachama Wote - C C M
Wakereketwa Wote - C C M
Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote
Tarehe: 06/03/2010

saa: 10 jioni Hadi Saa 5 usiku

WAPI:
UKUMBI WA: THE WAREHOUSE
1 CUMBERLAND ROAD
READING
RG1 3LB

Mgeni Rasmi
Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara:

Mhe Pius Msekwa

Watanzania ambao wangependa kujiandikisha, mnaombwa kuleta picha zenu za passport size mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya uanachama ya mwaka mzima).

Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:
Moses Katega - 07727475313
Victor Mgoya – 07501083328
Maira Migire – 07799212095
Wote Mnakaribishwa – Kutakuwa na Vinywaji, Vitafunio, na Muziki Baada ya Shughuli Zote
.
- Well here we go!

Respect.

FMEs!
 
- Now check this out, wote tunakuablaliana kwamba Sarakikya, Mayunga, Mwakalindile, na Nyirenda hawa walipelekwa nje ya nchi kuwakilisha serikali kwa sababu they were feared na watawala, watawala walikuwa wanawaogopa sana ndio maana wakaweka mbali, leo nitajie kiongozi au mwananchi mmoja tu unayemjua ambaye amewekwa mbali na watawawala wa sasa kwa sababu wanamuogopa? Ukweli ni kwamba hakuna wanayemuogopa wala kutishika naye, WHY?

- Wale wa zamani hawakuwa na vyama vya siasa, na walikuwa wakifuatwa fuatwa na mashushu kila wakati, lakini bado waliweza kuonyesha ukali wao wa kukataa kuburuzwa kama wajinga, they resented Mwalimu's policies kwa kumuonyesha sio kujificha ficha kama siku hizi, they were dead serious, wale waliokuwa hawataki siasa zake walifahamika na jamii nzima na wote tuliwajua kwa majina hata kama bado walikuwemo kwenye serikali ya Mwalimu. Mwalimu na misimamo yake kuna sehemu alikubali kubadilika mpaka kuachia power kutokana na kushinikizwa na matukio mbali mbali ya wazee wetu.

- Ninakumbuka at onetime Mwalimu akimshambulia Mwinyi na policies zake, kwa ujasiri sana Mwinyi alijibu kwamba policies zake zinakubalika sana na wananchi na taifa zima, ndio maana hata mara moja katika miaka yake 10 ya utawala hakujatokea any attempt ya kutaka kumpindua, as opposed na waliomtangulia, bing! this is a fact!

- Wananchi wa sasa nina wasi wasi sana kwamba we do not have it, I mean what it takes kupata attention ya watawala wetu, je tukubali tu yaishe?

Mkuu FMES kama nilivyosema hapo awali,nadhani taratibu tutakuwa kwenye ukurasa mmoja.....Ukweli ni kwamba mbinu ni za tofauti kama nilivyosema hapo awali,sasa hivi wanaingiza mamluki kwenye upinzani,wapinzani wengine wananunuliwa,wengine wanaingizwa kwenye tume nk,yote hiyo inatokana na ile kasumba ya ubinafsi,yani whats in there for me,Taifa na uchumi ulipokuwa mikononi mwa wananchi wenyewe,viongozi walikuwa automatically wanapigania maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla,sasa hivi hayo hayapo tena na ukifurukuta dawa si kukimbizwa nje tena,alternatives ni nyingi zaidi.

Mifumo ilikuwa ni ya tofauti sana na Mwinyi hakuwa na presha kwasababu sasa tuliukumbatia ubepari officially na kwahivyo shinikizo kwenye utawala wa juu halikuwepo tena na hivyo Mwinyi hakuwa fair alipotoa madai hayo kwa mwalimu,wala haina maana kabisa kwamba kauli ya Mwinyi ilikuwa right....Mwinyi kazi yake during his tenure na mwalimu zilikuwa tofauti kabisa,Mwinyi yeye alisimamia transition period wakati mwalimu yeye alikuwa against it.

Ofcourse sababu zao za kupingana na mwalimu ndio zimetufikisha hapa,kama hakuna dira hakuna mwelekeo,then hakuna uongozi makini.

All in all conditions ni za tofauti sana compare to then,kama ingekuwa ni rhuksa kumiliki mali za umma ie ubinafsishaji kwa wakati ule certainly tungekuwa tuazungumzia mengine hapa kuhusiana na walichokuwa wanakifanya viongozi hao....Dhana ya kwamba kuna maslahi ya Taifa imeshaanza kufutika kwa kasi miongozi mwa mawazo ya viongozi kadri muda unavyozidi kwenda na utafsiri wetu wa ubepari,na kusema kweli wengi wa viongozi ni wale wale tu.

Kwahiyo tunapo compare na wakati wa mwalimu, tusisahahu kuwa upinzani ulikuwa ni wa ndani ya chama,upinzani huo umejitokeza tena wakati huu kutoka kwa wanaojiita wapiganaji,tofauti ni kwamba sasa pia kuna upinzani hata nje ya chama ie chadema nk,ambako nako ni vurugu tupu, kutokana na mabadiliko yote hayo na sababu ambazo nimekuwa nikizi mention kuanzia hapo nyuma kwenye mjadala huu,utaweza kuona mwenyewe kuwa system sasa imeshakuwa kama njia za panya ambapo huwezi kuingia ndani na kushidana na panya hao,dawa ni ku wa flush out na ku destroy kabisa mtandao huo wa njia za panya...

Same with ccm,kipindi cha mwalimu,maslahi ya Taifa yalikuwa ni majukumu ya kila siku ya viongozi kwasababu uchumi na rasilimali vilikuwa chini ya serikali yenyewe kwa niaba ya wananchi,sasa hivi ni tofauti sana na hata sheria nyingine zinawalinda mafisadi,sheria haziwabani viongozi hao ili waweze kujali maslahi ya wananchi,na hatua ya kujaribu kupambana na mtandao huo wa kifisadi ni sawa na kujaribu kushindana na panya kwenye njia zake,hutamweza kamwe.

Mabadiliko ni possible only through some sort of a revolution.
 
- Mkuu wangu tupo pamoja, lakini bado sioni kubeba kwetu responsibility!

Respect.

FMEs!
 
Mzee mwenzangu; siri imebakia kwenye kuridhika. Wazee wetu wale walikuwa hawaridhiki kirahisi rahisi; sisi leo tunaridhika kirahisi rahisi. Tukijengewa uwanja wa mpira wa kisasa tunaridhika japo kina mama wanarundikana kwenye wodi ya wazazi! Tumejengewa shule za sekondari za kata tukaridhika japo kiwango cha elimu kimeshuka na kufaulu kunazidi kushuka.

Hadi pale tutakapokataa kuridhika kirahisi na kutaka zaidi na kudai zaidi ndipo tutaweza kuwafikia wazee wetu. Wote uliowataja katika historia yetu ni watu ambao hawakuridhika kirahisi rahisi; they wanted more so they asked for more!
 
Siyo na uoga pia?Kwamba sisi wa sasa pamoja na umasikini wetu lakini tunaogopa sana kufa na ndiyo maana ikifikia kwenye kutenda,wote tunategea kwenda frontline!
 
hakuna woga; ni kuridhika tu. Mtu aliyeridhika haitaji kufanya lolote. Mpaka atakapoona kuwa hajatosheka hapo ndiyo kitakuwa kimbembe.
 
Umasikini wote unaotutafuna,dawa hakuna hospitali,matibabu ya kubahatisha,elimu ndiyo hiyo inazidi kuporomoka kila kukicha,wengine milo mitatu kwa siku ni kama anasa etc huku kina Chenge wanaita mamilioni ya pesa vijisenti,Ndulu anakarabati nyumba kwa Bilioni 2,Richmond sijui bado wanaendelea kulipwa ile 152M kwa siku???du du du the list goes on..halafu bado tumeridhika?Wenzetu wanaridhika walau hata wakiweza ku afford zile basic necessities,lakini sisi tumeridhika na njaa zetu,mhhh huku kuridhika si bure,nadhani tumerogwa!!
 
absolutely! kwa sababu hatujaathirika moja kwa moja na hayo yote unayoyasema. Sasa hivi tunaishi kwa misingi kuwa endapo mimi na familia yangu tumepata chakula cha jioni, na watoto waemeenda shule na tuna nguo na mahali pa kulala hayo mengine mimi sijali. Hatukasirishwi na kuona mwingine anahangaika na mahitaji yake ya kila siku.

Wakati mwalimu aliongoza kwa sera ya "kabla wachache hawajishi katika anasa, wengi wapate mahitaji yao muhimu" leo hii kina Kikwete wanahakikisha "wachache wanazidi kuishi katika anasa huku wengi wakiahidiwa mahitaji yao muhimu". Matokeo yake, leo hii tunategemea wageni kutuchimbia visima; tunatarajia watu binafsi kuendesha shule za msingi na sekondari, n.k

Watu wakikataa kuridhika na wakatamani makubwa zaidi, mazuri zaidi na mema zaidi kwa sababu wanastahili wataona umuhimu wa cha kufanya. Lakini tukipewa kanga na tsheti huku tunaburudishwa na wimbo wa "nambari wani eeh" tunaridhika na kufurahia kuwa na sisi tumepata vikofia vya chama!
 
Mzee mwenzangu; siri imebakia kwenye kuridhika. Wazee wetu wale walikuwa hawaridhiki kirahisi rahisi; sisi leo tunaridhika kirahisi rahisi. Tukijengewa uwanja wa mpira wa kisasa tunaridhika japo kina mama wanarundikana kwenye wodi ya wazazi! Tumejengewa shule za sekondari za kata tukaridhika japo kiwango cha elimu kimeshuka na kufaulu kunazidi kushuka.

Hadi pale tutakapokataa kuridhika kirahisi na kutaka zaidi na kudai zaidi ndipo tutaweza kuwafikia wazee wetu. Wote uliowataja katika historia yetu ni watu ambao hawakuridhika kirahisi rahisi; they wanted more so they asked for more!

- Sawa sawa Mkuu, hayo ni maneno ya kubeba responsibility na sio kulaumu wengine, tunaridhika na machache sana na yasiyo ya muhimu kwa maisha yetu!

Respect.

FMEs!
 
Umasikini wote unaotutafuna,dawa hakuna hospitali,matibabu ya kubahatisha,elimu ndiyo hiyo inazidi kuporomoka kila kukicha,wengine milo mitatu kwa siku ni kama anasa etc huku kina Chenge wanaita mamilioni ya pesa vijisenti,Ndulu anakarabati nyumba kwa Bilioni 2,Richmond sijui bado wanaendelea kulipwa ile 152M kwa siku???du du du the list goes on..halafu bado tumeridhika?Wenzetu wanaridhika walau hata wakiweza ku afford zile basic necessities,lakini sisi tumeridhika na njaa zetu,mhhh huku kuridhika si bure,nadhani tumerogwa!!

- Saawa sawa mkuu ninakusikia sana!

Respect.

FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom