Jawabu kwa Lord Denning: Mikataba mithili ya IGA inayotaja gharama halisi za miradi ipo hapa Tanzania

Kwa hiyo kumbe shida yako ni waarabu? Umepuyanga kwenye uzi kuleta maneno matupu kumbe shida yako kubwa ni uarabu tu!

Finally nimekuelewa!

Ujumbe wangu kwako. Waambie waliokutuma ukaburu hauna nafasi Tanzania.

Case closed!!

1690708027736.png
 
Anataka kulazimisha eti Kila mwanamke akojoe amechuchumaa anasahau kuwa wanawake wazee sana nyonga zao haziruhusu kuchuchumaa, wanajisaidia wamesimama!!!
Wajinga hawa wamepewa fungu huko kuja kutushawishi upuuzi wakupoteza haki zetu zakumiliki hata aridhi
 
IGA ya Italia na Algeria mwaka 2022 kwenye masuala ya nishati iliwekwa wazi kwamba Italia wangwekeza $4billions kwenye mashirikiano hayo.

Unauliza swali la kitoto sana, hata watu kukujibu wanaona uvivu. Kuna malaki ya IGA dunia na wewe sio ajabu hujawahi kuona hata zaidi ya tatu, halafu IGA za uwekezaji haziwezi kuwa sawa na za utamaduni, sheria, mazingira n.k
Wanaoleta upuuzi wa Uchama, Udini, Ukabila katika mambo ya msingi ya nchi nashauri wapuuzwe tu. Yani mtu anakomaa na kamstari kamoja tena akitaka mifano ya kwengine akijua fika nchi zinatofautiana sheria, tamaduni,katiba etc. wakati kuna document nzima yenye mapungufu.
 
Mama Amon kiasi umepotoka kulinganisha mkataba tambuka wa kampuni kwa kampuni na wa nchi kwa nchi. Hata vile ufafanuzi wako umetoa picha halisi ya tofauti ya mkataba tambuka (IGA )na wa utekelezaji (HGA) kimataifa.

Nakubaliana nawe kuwa TPA na DP World, kwa kuwa tayari wamesaini MoU, waingie kwenye mikataba ya utekelezaji (HGAs) ambayo italindwa na sheria za nchi husika kupitia IGA yenye vifungu vyenye "nipe-nikupe", kulinda maslahi ya Mataifa yote.

Pamoja na pendekezo langu hilo, hoja yangu kuu Serikali iweke na kutekeleza mikakati ya kuwezesha makampuni ya ndani ya kuwekeza na wageni watumike tu kiubia kuongeza ufanisi na tija. Kuendelea kutegemea mataifa ya kigeni, kwa maendeleo, ni kudumisha ukoloni-mamboleo
Amepotoka vipi sasa.. kwani Dubai Ni nchi?..
 
Dah.

Mafundi mchundo hizi lugha zinatuacha.

Sisi tunafuata Upepo, yaani wasiwasi ndo akili. Heri nusu shari kuliko shari kamili.

Hatutaki Huu mkataba wa mwarabu
 
Nani kakwambia kwamba IGA zote ni identical?
Each case has to be argued in isolation.
We have a stable legal and political framework.
Uwekezaji wa bandarini za Tanzania hauhitaji IGA, as shown above.
Hivi hizo HGA baada ya IGA zinatua na msaada gani once tumeshindwana na kwenda kwenye kesi nje...Je itatazamwa hizo HGA ama IGA?kama ni IGA je hizi ngojera kua HGA itakua nzuri zina msaada gani, badala ya kukomaa ku solve IGA ndio iwe nzuri
 
Haya mambo yanahitaji twenda taratibu na kuelekezana. Maana hii ni taaluma na inahitaji utaalamu na uzoefu wa muda mrefu. Kuna baadhi ya mambo hapa, hata mtoa mada wetu ameteleza sana na yamenipa ukakasi, sema sintayasema. Ila kwenye hili, watanzania tunahitaji kwenda taratibu sana bila kutunishiana misuli. Kuna giza kubwa sana huko mbeleni...
Sijui kwanini umeamua kufumbia macho upotoshaji alioleta mleta mada, hii JF ipo kwa ajili ya kujifunza na kurekebishana, sioni sababu kwanini tuoneane aibu, naamini kufaya hivyo, tutakuwa tunazidi kuharibu.
 
View attachment 2702775
Picha ya antena za Vodacom, Tigo, Airtel na TTCL zikiwa zimesimikwa kwenye mnara wa Helios baada ya makampuni haya kusaini mkataba wa upangishaji na Helios

Kuna mtu, Lord Denning, ameuliza swali lifuatalo: Je, kuna mkataba mithili ya IGA iliyosainiwa kati ya Tanzania na Dubai unaotaja gharama halisi za miradi kama vile bei ya huduma na kodi ya pango?

Jawabu kwa swali hili ni "ndiyo," na ufafanuzi ufuatao ni kwa ajili ya kuthibitisha hilo.

IGA na HGA ni mikataba mtambuka (framework ontracts)

Mikataba ya IGA na HGA ni mikataba mtambuka, yaani "framework contracts." Kimsingi, mkataba mtambuka unaweza kuwa na sura mbili.

Kwanza, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi unafahamika, kiasi kwamba ikishasainiwa HGA hakuna haja ya mikataba mingine.

Mfano mzuri ni ule mradi wa bomba la mafuta linalounganisha Tanzania na Uganda, yaani radi wa EACOP.

Pili, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi haufahamiki kikamilifu, kiasi kwamba, kushasainiwa kwa HGA hakuondoi haja ya mikataba mingine. Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu aina hii ya mikataba mtambuka:

View attachment 2702567

Na tatu, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unatambuka miradi tofauti inayotekelezwa ndani ya nchi ile ile moja, lakini miradi hiyo inatekelezwa kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti na watekelezaji tofauti, lakini pasipo ulaiza wa kubadilisha sheria za nchi husika, kiasi kwamba kusainiwa kwa "Framework Contract" pamoja na "Project Contracts" kunaondoa mahitaji ya mikataba mingine, na hivyo kuondoa sababu ya uwepo wa IGA na HGA. Mchoro ufuatao unafafanua zaidi.

View attachment 2702566

Mifano ya Mikataba mtambuka isiyohitaji IGA wala HGA

Hapa nchini, kuna mifano mingi ya "mikataba mtambuka" ya aina hii ya pili. Mikataba hii inaonyesha gharama halisi za miradi husika, hata kabla mikataba ya miradi husika kusainiwa. Mifano mizuri hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:
  1. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na kampuni ya Vodacom,
  2. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Tigo,
  3. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Airtel,
  4. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya TTCL.
  5. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Halotel.
Makampuni ya Halotel, Vodacom, Tigo, Airtel, na TTCL hutoa huduma za mawasiliano ya simu.

Lakini makapuni haya hayana mitaji ya kutosha kwa ajili ya kujenga minara nchi nzima.

MInara ya kurusha mawimbi ya sauti (signal relay stations) huhitajika kwa ajili ya kusimika antena za kupokea na kurusha upya mawimbi ya sauti kutoka kwa mpigaji hadi kwa mpokeaji.

Lakini, Helios ni kampuni ya Uingereza yenye mtaji wa kujenga na kukodisha minara kwa makapuni mbalimbali.

Helios wanamiliki minara zaidi ya 1000, katika Afrika mashariki na Kati. Hivyo, haya makampuni yetu yanakodisha nafasi kwenye minara ya Helios ili yaweze kuweka antena zao kwenye minara hiyo, na kuwahudumia wateja wake.

Kampuni inapoanza kukodisha nafasi kwenye minara ya Helios inakuwa haijui kwa uhakika inahitaji minara mingapi na iliyo wapi.

Kwa hiyo, busara ni kukodisha minara ya Helios kwa awamu, kulingana na wateja wanavyopatikana na wanakopatikana.

Hivyo, mchakato wa kuingia mkataba kati ya kampuni ya Helios na kampuni kama vile Vodacom inachukua hatua nne. Yaani:
  1. Kusainiwa kwa mkataba mtambuka mmoja (framework contract) wenye kutaja taarifa chache za jumla, zitakazoweka singi wa mikataba ya saiti moja moja katika siku za usoni.
  2. Kampuni yenye mahitaji kuiandikia Helios ikiomba huduma ya kukodishwa mnara kwenye site mpya.
  3. Kusainiwa kwa mikataba ya saiti maalum (site cocntract), na hivyo kuongeza idadi ya minara ya Helios iliyokodishwa kwa kampuni pale tu mahitaji ya kampuni yanapoongezeka kwa sababu wateja wapya wamepatikana.
  4. Helios kuandaa mnara kwenye saiti kulingana na mahitaji, na hatimaye kampuni kukabidhiwa saiti hiyo.
Kwa ujumla, mikataba mtambuka kati ya Kampuni ya Helios na makampuni yaliyotajwa hapo juu, inafanana katika muundo na maudhui.

KImsingi, kila "mkataba mtambuka" kati ya Helio na kampuni yoyote hapo juu, una sehemu zifuatazo:
  1. Maelezo ya msingi kuhusu makubaliano: Sehemu hii inaongelea wahusika katika mkataba, malengo ya wahusika, na mwongozo wa jumla kuhusu mahusiano ya siku za usoni.
  2. Kiammbatanisho cha kwanza ("schedule 1"): Kinaongelea "configuration", yaani aina ya huduma ambazo Helios anapaswa kuhakikisha zinapatikana kwenye kila saiti. Mfano:-- kuna sharti kwamba, kama mnara unaotaka kukidishwa uko sehemu ambako hakuna umeme wa gridi ya Taifa, basi Helios aweke jenereta; -- kuna sharti kwamba, kampuni itapewa ukubwa wa eneo la meta moja ya mmraba kwa ajili ya kusimika antena yake; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba tambuka; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba mahsusi utakaosainiwa katika siku za usoni; -- na kadhalika.
  3. Kiambatanisho cha pili ("schedule 2"): Kinaongelea kodi ya pango inayotajwa kwa kutumia kizio cha "TZS/site/month". Gharama hizi ziko katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yenye umeme wa gridi ya Taifa (bei nafuu). Na Kundi la pili ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya Taifa (bei kubwa).
  4. Kiambatanisho cha tatu ("schedule 3"): Kinaongelea muundo na maudhui ya mkataba utakaosainiwa kwa ajili ya kukidisha saiti moja tu, yaani kukodisha mnara mmoja pekee. Kwa hiyo, kama kampuni ya Vodacom itakodisha minara 100, kutasainiwa mikataba mahsusi 100.
  5. Kiambatanisho cha nne ("schedule 4"): Kinaongelea utaratibu wa kuongeza mnara mpya, yaani jinsi kampuni yenye mahitaji itakavyowasiliana na Helios na kuonyesha huduma ya mnara mpya ianze kutolewa lini.
  6. Kiambatanisho cha tano ("schedule 5"): Kinaongelea utaratibu wa kukabidhiana huduma kwenye saiti.
  7. Kiambatanisho cha sita ("schedule 6"): Kinaongelea protokali ya kutumia saiti, maana kwenye mnara mmoja kuna wakodishaji wengi. Yaani, unakuta kuna antena za Tigo, Airtel, Vodacom, na kadhalika.
Hakuna haja ya IGA kati ya Tanzania na Dubai

Baada ya kusema hayo hapo juu sasa nafanya majumuisho muhimu kwa kuzingatia hoja yafuatayo:

Njia mojawapo ya kusanifu hoja, ni kuanzia kwenye ufanano wa vitu viwili. Njia hii huzalisha hoja yenye muundo ufuatao:
  1. Kitu X na kitu Y vinafanana kwa sababu kila kimoja kinazo sifa sifa kadhaa zinazounda seti Z.
  2. Kitu X pia kinaonekana kuwa na sifa nyingine P.
  3. Kwa hiyo, kitu Y pia kinapaswa kuwa na sifa hiyo P.
Kwa kutumia mantiki hiyo hapo juu, sasa nawea kumjibu Lord Denning kikamilifu kama ifuatavyo:

Mosi, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza na kammpuni ya DPW kutoka Dubai zinafanana kwa kuwa zote ni Kampuni za wawekezaji wa Kigeni wanaotaka mazingira tulivu ya uwekezaji ili wafanikiwe kuwekeza, kuvuna na kuhamisha faida kutoka nchini Tanzania, ambapo HELIOS anajenga na kuendesha minara kwa kuikodisha kwa makampuni yanayosafirisha mawimbi ya simmu hapa Tanzania, wakati DPW anajenga na kuendesha bandari za mmajini na nchi kavu kwa kuzikodisha kwa watu wanaosafirisha mizigo.

Pili, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza inao uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) na "mikataba ya miradi mmahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Uingereza.

Na tatu, kwa hiyo, Kampuni ya DPW kutoka Dubai inapaswa kuwa na uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) na "mikataba ya miradi mmahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai.

Yaani, timu ya Johari Hamza haikuwa na weledi katika mambo haya.

Hitimisho na mapendekezo

Mkataba mtambuka (framework contract) kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba kati ya nchi na nchi (IGA). Na mkataba wa saiti kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba wa ngazi ya miradi kati ya nchi mwenyeji na mwekezaji wa kigeni (HGA).

Kwa hiyo, inawezekana, na ni lazima, kutaja gharama za mradi kama vvile kodi ya pango na pia ukomo wa muda kwenye IGA.

Na kama ambavyo Helios na makampuni ya simu yanasaini "Framework Agreements" na baadaye "Project Site Agreements," vivyo hivyo DPW na TPA wanaweza na wanapaswa kusaini nyaraka za aina hii.

Hakuhitajiki IGA wala HGA kamwe ili kuiwezesha DPW au kampuni yoyote iwayo kuwekeza katika bandari za Tanzania!

Mama Amon Desk
"Summbawanga Town"
Sumbawanga.
30 Julai 2023.
Hivi yule Zwazwa alikushighulisha kabisa ukahangaika kumtafutia mifano ambayo yeye mwenyewe anajua ipo? Wiki 2 zilizopita iliwekwa hapa BIT Kati ya UAE na UK na Kila Mtu alisoma jinsi benefits za Kila upande zilivyoainishwa. Huyo Lord wa Machongo ni Chawa tasa asikusumbue Mkuu.
 
Haya mambo yanahitaji twenda taratibu na kuelekezana. Maana hii ni taaluma na inahitaji utaalamu na uzoefu wa muda mrefu. Kuna baadhi ya mambo hapa, hata mtoa mada wetu ameteleza sana na yamenipa ukakasi, sema sintayasema. Ila kwenye hili, watanzania tunahitaji kwenda taratibu sana bila kutunishiana misuli. Kuna giza kubwa sana huko mbeleni...

Mie nimewasilisha hoja yenye kutetea rai kwamba uwekezaji kwenye bandari zilizo ndani ya nchi yetu hauhitaji IGA wala HGA.

Hoja hii inaweza kuboreshwa kwa njia tatu: kuondoa tatizo la kimmuundo (soundness) au kuondoa tatizo la kimaudhui (validity) au yote matatu.

Uboreshaji wa aina hiyo huwa na faida kwa jamii pana, kama hii iliyopo hapa JF

Usisite kutekeleza wajibu wako kama mwanazuoni.
 
Daa! Kila nikikaribia kuelewa najikuta tena Chali! "Katika IGA nchi zimekubaliana DP World ndio kampuni itakayowekeza ikiwakilisha Dubai na TPA kampuni pokezi ya uwekezaji huo ikiwakilisha JMT." Ni nchi gani hizi tena? Mi mbona naona IGA ni kati ya Tanzania na DP WORLD!? Ngoja niisubirie mahakama tu. Ila mleta bandiko kwangu upande wangu ni moja ya watu waliolieleza jambo hili kwa rugha rahisi sana kueleweka (kwa anayetaka kujifubza)
1. Hakukuwa na haja ya IGA katika issue hii.
2. Kinachotafutwa kwenye IGA na HGA kipo kwenye framework contract na project contracts
3. IGA hii inatengeneza hatari kwa Tanzania
4. Mkataba ulipaswa uwe kati ya TPA na DPW na si vinginevyo.
5. Swali la Lord denning linatafuta UBISHI zaidi kuliko kuleta weredi kwa wadau.
Tunaongea lugha moja kwa maana kwmba hoja hazipingani.

Tangu awali nimekuwa nasema IGA ni batili. DPW iingie ubia na TPA kwa MoU waliosaini, na ijisajiri TIC na BRELA.

Hivyo basi, maelezo yangu, ya awalli, unayoona yanatatiza, ni majibu kwa watetezi wa IGA wakidai kuwa HGAs ndio zitakuwa na majibu ya maswali ya wanaopinga baadhi ya vifungu vyake.
 
Nimefanya utafiti wangu ndo mana nikaja na ilo swali.

Fanya utafiti wako then Jibu swali langu kama lilivyoulizwa!
Weka hapa matokea ya utafiti wako tuone kama ushahidi uliyopata una mashiko. Yaani ufanye utafiti halafu matokeo hutaki kuyaweka wazi ili wachangiaji wayapitie? Wewe ni msomi wa wapi? Eti «fanya utafiti wako», wakati wewe ndiyo una burden of proof kuthibitisha hoja yako kwa ushahidi? Hoja yako wewe ndiyo nothing but an opinion: haina factual basis yoyote. Ukiambiwa uweke ushahidi unakwepa. Unajibu: «fanya utafiti wako».
 
Nikupongeze Mama Amon kwa uchambuzi wako mzr, ila kuna maelekzo umeyatoa na mifano ya mkataba ambayo inakinzana na hoja iliyopo na hoja ya mtu uliyemnukuu kwenye andiko lako hili.

Kwanza, ufafanuzi wako umeanza kwa kuandika bayana "Mifano ya Mikataba isiyohitaji IGA na HGA.." Kisha ndio ukaanza kuitaja kwa kuchambua Mikataba ya Kampuni ya Helios na Mitandao ya Simu ya Tanzania na ukaenda kueleza na vifungu vya ghrama, Pango nk. (Kwa maelezo yako, mifano hiyo ya mikataba ndio hiyo ya kundi hilo ulilokoleza la kutohitaji IGA na HGA).

Lakini, mkataba wa DPW na Tz una IGA na pia inaelezwa kuwa utakuwa na HGA. Sasa tulitegemea kuwe na Mkataba wenye nature ya namna hiyo aidha serikali ilishawahi ingia huko nyuma hapa Tz au nchi nyingine ambayo imeingia mkataa wa namna hii halafu ndani ya hiyo IGA kuwe na vifungu vya gharama, malipo, muda, mgawanyo wa fedha, na mengine yote kama ambavyo itakuwa ktk actual site contracts/aggreement.

Mifano uliyotoa sio sahihi na inajicontradict.
Mimi nimemwelewa vyema pia..

Kwa lugha rahisi zaidi, Mama Amon anamaanisha kwamba, kampuni ya DP World haikuhitaji kuingia kuwekeza Tanzania kwa njia mkataba wa IGA..

DP World kama inataka kuwekeza Tanzania, basi ingekuja kwa kufuata utaratibu uleule wa kawaida ambao Kila mwekezaji anaufuata. Wangesaini mkataba wa kibiashara (commercial contract) kimya kimya tu na TPA.

Kila mtu anajiuliza, iweje DP World (kampuni binafsi ya kibiashara) itake kuja kuwekeza nchi kwetu kwa mgongo wa "nchi" Kwa kutumia mkataba wa IGA unaotaka sisi kama nchi tubadili sheria zetu ili tu ziwa - accommodate wao?

Tunaendelea kujiuliza, hii DP World ina umaluumu gani kuzidi wawekezaji maelfu wengine waliopo na watakaokuja kuwekeza hapa nchini? Na kwanini mkataba wa kibiashara upelekwe kuwa ratified na Bunge?

Na tukajiuliza tena, mbona mikataba ya makampuni makubwa makubwa mengine kama ya madini, gas nk hayakupitia njia hii? Kulikoni kwa DP World..?

Haya ndiyo maswali yanayosumbua vichwa vya watu na bahati nzuri majibu ya kilicho nyuma ya huu mpango, yalishapatikana...!!

Ni kwamba, kwa kutumia mgongo wa ujinga wa viongozi wetu na tamaa zao, mfalme wa UAE kupitia Dubai na kwa kuitumia kampuni binafsi ya mfalme wa Dubai (DP World) wanataka kuifanya Tanganyika koloni lao..!!
Lord denning FaizaFoxy njooni na huku na mseme kitu kwa Mama Amon
 
Hatukubaliani na wazo lako. Kelele za wenye nchi sio "kelele tu." Ukoloni wa walowezi kwa mara ya pili hapana. Hoja yetu iko hivi:

The Dubai Investors want to implement the projects within a policy and legal framework whose objective is to create an environment for foreign investment that protects the companies against changes in national priorities, together with the changes in law that can result.

In order to achieve this, IGA and HGA requires the state to make an agreement with the investor that contains what are called "stabilization clauses."

An Intergovernmental Agreement (IGA) between the states through whose territories an identified project system is to be operated. It addresses horizontal issues concerning the pipeline infrastructure as a whole – cooperation, land rights, tax structures, issues relevant to the implementation of the project.

The Host Government Agreements (HGA) between individual states within whose territory the project system is to be realized and the project investor(s). It addresses vertical issues concerning the project activity within the territory of each state – governmental obligations, investor duties, relevant standards, liability, issues relevant to the implementation of the project in each specific territory.

The stabilization clauses under IGA and HGA demand that there be no changes in the state’s policies that would alter the terms for the project initially agreed, without the consent of the other contracting party.

Sometimes the intention is to avoid the risks of nationalization, or the effects of changes in tax rates.

In other cases, the intention is much wider because the host government is required to undertake, for at least 66 and possibly 99 years, not to apply any fresh legislation or other measures if these will affect the profitability of the project.

This includes measures having their origin in international treaties to which the host government is a party and measures aimed at improvements in environmental and social protection, except for certain qualifications.

It is a framework that poses a clear and present threat to human rights and national sovereignty. We disagree.
Bimkubwa , IGA mbona imesema wazi kabisa, Kwamba Tanzania tunalazimika kumtaarifu DP World na Hata DPW pia anapaswa kututaarifu pale anapoona anataka kuwekeza kwene Gati Flani ya Bandari, Kisha Ana Frame proposal na kumpa Tanzania, So Tanzania ,apo ana maamuzi mawili, either aikubali na kuweke saini au aikatae .
Halazimiki kuikubali ile Proposal ,Bali anaweza kutoikubali na Akampa kampuni nyingine eneo hilo hilo.

Hakuna sehemu iliosema Tanzania Haturuhusiwe kushirikiana na Makampuni mengine.
 
View attachment 2702775
Picha ya antena za Vodacom, Tigo, Airtel na TTCL zikiwa zimesimikwa kwenye mnara wa Helios baada ya makampuni haya kusaini mkataba wa upangishaji na Helios

I. Utangulizi

Makubaliano ya Kiserikali kati ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari za Tanzania yanaongozwa na Sheria za Kimataifa, Katiba ya Taifa la Tanzania, Sheria za Kitaifa zilizotungwa na Bunge la Tanzania, na mikataba mbalimbali inayoongozwa na sheria hizi.

Mikataba muhimu ni pamoja na mkataba wa IGA, mkataba wa HGA, mikataba ya wakandarasi, mikataba ya mikopo ya mabenki, na kadhalika, kama mchoro ufuatao unavyoonyesha:

View attachment 2704138
Mchoro: Uhusiano kati ya Tanzania, Dubai, Kampuni zitakazotekeza miradi, na mikataba husika

Katika mazingira haya, kuna mtu, Lord Denning, ameuliza swali lifuatalo: Je, kuna mkataba wa IGA ambao uliwahi kusainiwa kati ya pande bili wnye kutaja gharama halisi za miradi kama vile bei ya huduma na kodi ya pango?

Jawabu kwa swali hili ni "ndiyo," na ufafanuzi ufuatao ni kwa ajili ya kuthibitisha hilo.

II. IGA na HGA ni mikataba mtambuka (framework contracts)

Mikataba ya IGA na HGA ni mikataba mtambuka, yaani "framework contracts." Kimsingi, mkataba mtambuka unaweza kuwa na sura mbili.

Kwanza, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi unafahamika, kiasi kwamba ikishasainiwa HGA hakuna haja ya mikataba mingine.

Mfano mzuri ni ule mradi wa bomba la mafuta linalounganisha Tanzania na Uganda, yaani mradi wa EACOP.

Pili, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi haufahamiki kikamilifu, kiasi kwamba, kushasainiwa kwa HGA hakuondoi haja ya mikataba mingine. Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu aina hii ya mikataba mtambuka:

View attachment 2704015

Na tatu, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unatambuka miradi tofauti inayotekelezwa ndani ya nchi ile ile moja, lakini miradi hiyo inatekelezwa kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti na watekelezaji tofauti, lakini pasipo ulazimma wa kubadilisha sheria za nchi husika, kiasi kwamba kusainiwa kwa "Framework Contract" pamoja na "Project Contracts" kunaondoa mahitaji ya mikataba mingine, na hivyo kuondoa sababu ya uwepo wa IGA na HGA. Mchoro ufuatao unafafanua zaidi.

View attachment 2704010

Kwa kifupi, tunaweza kusanifu hoja ifuatayo juu ya uhusiano uliopo kati ya "mkataba mtambuka," unaoitwa IGA" na "mkataba wa HGA"

Mosi, mkataba mtambuka (framework contract) ni mkabata wa jumla kati ya pande mbili, mfano, kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Uganda; kati ya serikali ya Tanzania na taasisi ya kimataifa isiyo nchi kama vile Benki ya Dunia; au kati ya kampuni ya usafirishaji na kampuni ya mafuta.

Pili, mkataba mtambuka (framework contract) kati ya serikali na serikali, unaitwa "Intergovernmental agreement (IGA)" au "Heads of States Agreement (HSA)" au "Bilateral International Treaty (BIT)."

Tatu, na kwa hiyo, kimuundo, IGA, HGA na BIT zinafanana kwa sababu zote zinao muundo wa mkataba mtambuka (framework contract).

Nne, kuna mkataba mtambuka (framework contract) kati ya kapuni ya Vodacom inayotoa huduma za simu and kampuni ya HELIOS inayojenga na kukodisha minara ya masafa,

Na tano, tukipata mkataba mtambuka (framework contract) kati ya Vodacom na Helios, tunakuwa tumepata mfano hai wenye kuonyesha muundo wa mkataba wa IGA, unavyopaswa kuwa.

III. Mkataba kati ya Helios na Vodaco ni mifano hai wa mikataba mtambuka isiyohitaji IGA wala HGA

Hapa nchini, kuna mifano mingi ya "mikataba mtambuka" ya aina hii ya pili. Mikataba hii inaonyesha gharama halisi za miradi husika, hata kabla mikataba ya miradi husika kusainiwa. Mifano mizuri hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:
  1. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na kampuni ya Vodacom,
  2. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Tigo,
  3. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Airtel,
  4. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya TTCL.
  5. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Halotel.
Makampuni ya Halotel, Vodacom, Tigo, Airtel, na TTCL hutoa huduma za mawasiliano ya simu.

Lakini makapuni haya hayana mitaji ya kutosha kwa ajili ya kujenga minara nchi nzima.

MInara ya kurusha mawimbi ya sauti (signal relay stations) huhitajika kwa ajili ya kusimika antena za kupokea na kurusha upya mawimbi ya sauti kutoka kwa mpigaji hadi kwa mpokeaji.

Lakini, Helios ni kampuni ya Uingereza yenye mtaji wa kujenga na kukodisha minara kwa makapuni mbalimbali.

Helios wanamiliki minara zaidi ya 1000, katika Afrika mashariki na Kati. Hivyo, haya makampuni yetu yanakodisha nafasi kwenye minara ya Helios ili yaweze kuweka antena zao kwenye minara hiyo, na kuwahudumia wateja wake.

Kampuni inapoanza kukodisha nafasi kwenye minara ya Helios inakuwa haijui kwa uhakika inahitaji minara mingapi na iliyo wapi.

Kwa hiyo, busara ni kukodisha minara ya Helios kwa awamu, kulingana na wateja wanavyopatikana na wanakopatikana.

Hivyo, mchakato wa kuingia mkataba kati ya kampuni ya Helios na kampuni kama vile Vodacom inachukua hatua nne. Yaani:
  1. Kusainiwa kwa mkataba mtambuka mmoja (framework contract) wenye kutaja taarifa chache za jumla, zitakazoweka singi wa mikataba ya saiti moja moja katika siku za usoni.
  2. Kampuni yenye mahitaji kuiandikia Helios ikiomba huduma ya kukodishwa mnara kwenye site mpya.
  3. Kusainiwa kwa mikataba ya saiti maalum (site cocntract), na hivyo kuongeza idadi ya minara ya Helios iliyokodishwa kwa kampuni pale tu mahitaji ya kampuni yanapoongezeka kwa sababu wateja wapya wamepatikana.
  4. Helios kuandaa mnara kwenye saiti kulingana na mahitaji, na hatimaye kampuni kukabidhiwa saiti hiyo.
Kwa ujumla, mikataba mtambuka kati ya Kampuni ya Helios na makampuni yaliyotajwa hapo juu, inafanana katika muundo na maudhui.

KImsingi, kila "mkataba mtambuka" kati ya Helio na kampuni yoyote hapo juu, una sehemu zifuatazo:
  1. Maelezo ya msingi kuhusu makubaliano: Sehemu hii inaongelea wahusika katika mkataba, malengo ya wahusika, na mwongozo wa jumla kuhusu mahusiano ya siku za usoni.
  2. Kiammbatanisho cha kwanza ("schedule 1"): Kinaongelea "configuration", yaani aina ya huduma ambazo Helios anapaswa kuhakikisha zinapatikana kwenye kila saiti. Mfano:-- kuna sharti kwamba, kama mnara unaotaka kukidishwa uko sehemu ambako hakuna umeme wa gridi ya Taifa, basi Helios aweke jenereta; -- kuna sharti kwamba, kampuni itapewa ukubwa wa eneo la meta moja ya mmraba kwa ajili ya kusimika antena yake; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba tambuka; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba mahsusi utakaosainiwa katika siku za usoni; -- na kadhalika.
  3. Kiambatanisho cha pili ("schedule 2"): Kinaongelea kodi ya pango inayotajwa kwa kutumia kizio cha "TZS/site/month". Gharama hizi ziko katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yenye umeme wa gridi ya Taifa (bei nafuu). Na Kundi la pili ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya Taifa (bei kubwa).
  4. Kiambatanisho cha tatu ("schedule 3"): Kinaongelea muundo na maudhui ya mkataba utakaosainiwa kwa ajili ya kukidisha saiti moja tu, yaani kukodisha mnara mmoja pekee. Kwa hiyo, kama kampuni ya Vodacom itakodisha minara 100, kutasainiwa mikataba mahsusi 100.
  5. Kiambatanisho cha nne ("schedule 4"): Kinaongelea utaratibu wa kuongeza mnara mpya, yaani jinsi kampuni yenye mahitaji itakavyowasiliana na Helios na kuonyesha huduma ya mnara mpya ianze kutolewa lini.
  6. Kiambatanisho cha tano ("schedule 5"): Kinaongelea utaratibu wa kukabidhiana huduma kwenye saiti.
  7. Kiambatanisho cha sita ("schedule 6"): Kinaongelea protokali ya kutumia saiti, maana kwenye mnara mmoja kuna wakodishaji wengi. Yaani, unakuta kuna antena za Tigo, Airtel, Vodacom, na kadhalika.
IV. Hakuna haja ya IGA kati ya Tanzania na Dubai

Baada ya kusema hayo hapo juu sasa nafanya majumuisho muhimu kwa kuzingatia hoja yafuatayo:

Njia mojawapo ya kusanifu hoja, ni kuanzia kwenye ufanano wa vitu viwili (argument by analogy). Njia hii huzalisha hoja yenye muundo wa kimantiki ufuatao:
  1. Kitu X na kitu Y vinafanana kwa sababu kila kimoja kinazo sifa kadhaa zinazounda seti Z.
  2. Kitu X pia kinaonekana kuwa na sifa nyingine P.
  3. Kwa hiyo, kitu Y pia kinapaswa kuwa na sifa hiyo P.
Kwa kutumia mantiki hiyo hapo juu, sasa tunaweza kumjibu Lord Denning kikamilifu kama ifuatavyo:

Mosi, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza na kammpuni ya DPW kutoka Dubai zinafanana katika sifa zifuatazo:
  • zote ni Kampuni za wawekezaji wa Kigeni;
  • zote zinaotaka mazingira yenye utulivu wa kisheria na kisiasa kwa ajili ya uwekezaji ili wafanikiwe kuwekeza, kuvuna na kuhamisha faida kutoka nchini Tanzania;
  • zote zinahitaji kimilikishwa ardhi kwa ajili ya kuitumia kama saiti ya miradi yake;
  • na zote zinajenga saiti zinazoitwa minara, kuziboresha na kisha kukodisha nafasi yenye eneo maaluma kwa muda fulani kwa makampuni kadhaa. Kwa upande mmoja, HELIOS wanasimika minara na kuikodisha kwa makampuni yanayosafirisha mawimbi ya simu hapa Tanzania. Kwa upande mwingine, DPW wanajenga saiti zinazoitwa bandari, kuziboresha na kuvikodisha kwa watu wanaosafirisha mizigo kwa kutumia meli.
Pili, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza inayo sifa ya ziada kwa sasa, yaani uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutumia "mkabata mtambuka" (framework agreement) ambao ni mwavuli wa "mikataba ya miradi mingi," kila saiti ya mnara ikiwa na mkataba wake (project site agreements), lakini pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Uingereza wala kuhitaji mkataba wa HGA kati ya Helios na serikali ya Tanzania.

Tatu, kwa hiyo, Kampuni ya DPW kutoka Dubai inapaswa kuwa na uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) pamoja na "mikataba ya miradi mahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai wala mkataba wa HGA kati ya DPW na serikali ya Tanzania.

Nne, kuipa kampuni ya DPW unafuu unaotokana na mikataba ya IGA na HGA na kuzinyima unafuu huo kampuni baki za wawekezaji wa kigeni ni ubaguzi usio na sababu za msingi dhidi ya baadhi ya wawekezaji wa kigeni.

Na tano, kwa hiyo, kwa ajili ya kutenda haki sawa kwa wawekezaji wote wa kigeni, Tanzania inapaswa kuepuka mikataba ya IGA na HGA.

V. Hitimisho na mapendekezo

Mkataba mtambuka (framework contract) kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba kati ya nchi na nchi (IGA). Na mkataba wa saiti kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba wa ngazi ya miradi kati ya nchi mwenyeji na mwekezaji wa kigeni (HGA).

Kwa hiyo, inawezekana, na ni lazima, kutaja gharama za mradi kama vvile kodi ya pango na pia ukomo wa muda kwenye IGA.

Na kama ambavyo Helios na makampuni ya simu yanasaini "Framework Agreements" na baadaye "Project Site Agreements," vivyo hivyo DPW na TPA wanaweza na wanapaswa kusaini nyaraka za aina hii.

Hakuhitajiki IGA wala HGA kamwe ili kuiwezesha DPW au kampuni yoyote iwayo kuwekeza katika bandari za Tanzania!

Mama Amon Desk
"Summbawanga Town"
Sumbawanga.
30 Julai 2023.
Lord denning atakuelewa? Maan ashakula mlungula wa kupush agenda ya DP world!!
 
Makubaliano ya Kiserikali kati ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari za Tanzania yanaongozwa na Sheria za Kimataifa, Katiba ya Taifa la Tanzania, Sheria za Kitaifa zilizotungwa na Bunge la Tanzania, na mikataba mbalimbali inayoongozwa na sheria hizi
 
Back
Top Bottom