Jaribio la mauaji kwa Tundu Lissu: Maadui zetu wamebaini kupenyezewa "kirusi"?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Wengi wameshaandika kuhusu kinachoweza kuwa asili ya jaribio la mauaji kwa ndugu yetu Tundu Lisu. Mawili makubwa na mojawapo ni kwamba yawezekana ikawa ni Serikali(eti kwa sababu "anaishambulia" na kuisakama.Pili,yawezekana wauaji wakawa ni wabaya Wa Lisu waliojenga chuki naye eti kwa sababu wanaona anaiandama Serikali ya JPM.

Mimi naandika upande mwingine ambao watu hawauoni.Ninaandika kwa kutumia ukweli wa kihistoria.Ukweli wasioujua watu wengi wa jinsi vyama vya Siasa vinavyofanya kazi hapa nyumbani. Ninaandika kwa kutumia jicho langu la tatu na sense ya sita juu ya jinsi nilivyokuja kubahatika kumfahamu Mrema,Lipumba,Dr.Slaa, Cheyo, Marando na wengineo. Ninaandika kwa kuongozwa na 35% ya Kauli za Magufuli Jana wakati akipokea ripoti za Kamati Teule za Bunge,Ikulu. Ninaandika kwa kuongozwa na 65% ya lugha ya mwili ya Lisu katika utendaji kisiasa.

Ninaandika kwa kuangalia yale maudhui yanayoonekana lakini yasioneshe maudhui kusudiwa(yaliyojificha) katika utendaji wa Tasnia ya Usalama.

Baada ya Mwalimu kuzongwa na Mataifa Beberu wakimtaka aruhusu mfumo Wa Vyama vingi kama njia ya kusaidiwa kurekebisha mwenendo Wa kiuchumi kwa wakati ule,Serikali iliazimia kuruhusu mfumo huo u-take shape(licha ya wananchi wengi kuwa wameukataa) kwa Kuchukua "machineries" kadhaa na kuzichomeka huko na waanzilishi vya vyama hivyo na hata viongozi Wanaorithi nafasi mbalimbali ndani vya vyama vya siasa. Hili wengine wanalijua na wengine hawalijui.

Lisu ni miongoni mwa watu wenye akili sana.Ukweli huo haubainishwi tu na ufaulu katika masomo yake bali hata aina yake ya kufikiri na kujenga hoja.Lisu amekuwa "akinyofoa" mambo mazito na nyeti ya nchi. Katika Tasnia ile ya "kunyemelea" unyofoaji wake huo ni classified info lakini ambazo hazina madhara.Ni mbinu ya kuwafanya wasioona kwa jicho la tatu waamini kuwa jamaa kweli ni Anti-system. Ni mbinu ya "nipe nikupe".

Ninamuona Lisu katika mbinu sawa na mbinu ya sawa na kumtwaa panya na kumfundisha jinsi ya Kubaini vitu mbalimbali kwa urahisi na hata ikilazimu panya huyo atumike kuangamiza panya wengine waharibifu.Panya kama huyo anapewa mnofu wa uhakika wa nyama anakuwa analanda landa nao. Panya walafi (na wasiojua chochote kama huyo panya ametegeshewa) wakiona mnofu kama huo wanakimbilia haraka haraka kwa panya huyo wakidhani ni mwenzao ambaye amefanikiwa kumuweza mwenye nyumba kumbe sivyo.
Jana Raisi Magufuli, alifunua ukweli kama huu wa mbinu ya panya alipoeleza jinsi Operative Prof.Mruma alivyofanikisha kuwadukua wawekezaji katika sekta ya madini.Mruma yeye alijiweka upande wa "kula" pamoja na Wawekezaji.Niliwahi ku-comment humu kuwa taarifa zote ama ziwe za audio au video za toka uwekezaji katika uchimbaji madini uanze zilikuwepo panapostahili.Taarifa za kila kitu zilikuwa zinakusanywa kila Siku na kuwasilishwa kwa "Babu" ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuwasilisha taarifa kwa Sponsor.

Niliandika hivyo kwamba Raisi Magufuli alikuwa na taarifa zote nyeti juu ya wawekezaji " uchwara" hao na hata za wawekezaji wenye nia njema. Nilisema Raisi hakuwa anajiamini burebure tu. Nilivyosema ndivyo Raisi alivyosema Jana. Nilijua mwisho wa ACACIA ungekuwa mbaya sana maana walikuwa wameshikwa mithili ya mtu aliyebinywa korodani. Na ndivyo inavyotokea.
Tundu Lisu ni mzalendo sana.Ukichunguza kauli zake na vitendo vyake unauona uzalendo wake unaoanzia kwenye kitako cha moyo wake. Ukimfuatilia sawa sawa utaona Lisu huwa anafukunyua mambo yenye maslahi tu kwa nchi.Orodha iko wazi.Anawezaje kupata mambo hayo kama si kutoka kule kwa "Babu"?

"Panya" waliopenyezwa kwenye mambo ya wawekezaji,mintarafu mikataba ya Kimataifa,sio Mruma pekee. Wako panya waliopewa kazi ya kuonyesha jinsi tulivyokuwa tunapigwa na hao wawekezaji lakini kwa nia tu ya kutaka kuwa-hook hao wezi. Tundu Lisu,amekuwa professional katika eneo hilo na mwenyewe hujigamba kuwa ameshafanya kazi ya maana sana katika kuibua wizi Wa wawekezaji katika sekta ya madini.
Shambulio la Lisu lina dalili na mazingira kama ya kifo cha Mch.Mtikila. Juzi juzi kuna spy anayesemekana amekamatwa hapa nyumbani na kwamba alikuwa anahojiwa na vyombo vya usalama. Huyo jamaa inasemekena amehusika na nyendo nyingi sana za kijinga hapa nyumbani kwa muda mrefu.Hivi kundi hilo haiwezekani likawa liko nyuma ya hiyo hiting?

ACACIA na wenzao nao wameshagundua kuwa walikuwa wanadukuliwa na pengine hata watu walliotumika kuwadukua. Katika mazingira kama haya ya Kivita ya kiuchumi yanayoendelea nchini,maadui zetu wanapogundua kuwa kuna watu "wamewaliza" njia kama hii ya tukio la jana kwa Lisu,ni lazima itatumika.Upande wa pili wa adui, wanaweza kuazima kundi la Hit-men ili watekeleze kazi hiyo.

Wengine wanasema pengine Serikali inahusika kutaka kumumaliza Lisu ndio maana imeweka masharti katika kumuhudumia kwenye matibabu. Mimi nasema,sio kwamba Serikali imekataa kumgharimia. Itamgharimia kupitia njia za michango zilizotangazwa na zingine zisizotangazwa.Jicho la tatu limenionyesha kuwa kauli ya Raisi Magufuli (kuhusiana kuharakishwa uchunguzi) juu ya tukio la kuhujumiwa Lisu ni ishara ya kwamba Lisu ni Mshirika wa Tanzania katika vita hii ya kiuchumi. Huku kuparurana kwa Lisu na Magufuli na Serikali yake kusiwatishe. Ndivyo tasnia hiyo inavyotaka.
 
Heshima kwako mkuu tusiwe wavivu kufikiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upuuzi mtupu. Mnamtetea Magufuli wakati yote yanaanzia kwake?

Huhitaji hata kuwa na pH D kujua kwamba vyombo vya dola kwa kutumwa toka juu au kujituma wenyewe wanahusika. Mbinu ni zile za kutekwa kwa wana music, akina Saanane na watu wengine
Serikali inajua ndio maana haitaki kuchunguza au hata kutoa taarifa.
Wale waliopiga risasi kwa Nape wako wapi?

Hakuna cha maadui wetu. Ni serikali ya Magufuli ambayo haiko tayari kukubali challenges. Maneno yake yamewapa Uhuru usalama wa taifa kutisha watu hata kama hawajaruhusiwa moja kwa moja na yeye mwenyewe.

Kitendo cha serikali kukaa kimya watu wanapotekwa kimetoa ishara kwa rogue police na tiss kwenda hatua moja mbele ya kutaka hata kuua.

Serikali inawajibu was kulinda raia. Ina wajibu wa kutoa majibu kwa familia ya Mawazo. Ina wajibu wa kutoa majibu kwa familia ya Saanane, kwa Roma nk.
 
" WASHUGHULIKIENI BUNGENI NASI TUTAWASHUGHULIKIA URAIANI"

" HIVI NI VITA VYA UCHUMI ANAETUPINGA YUPO UPANDE WAO NA ADHABU YAKE INAJULIKANA"

" NI HERI MVUNJE SHERIA KULINDA RASILIMALI ZETU"
Hebu jaribu kuunganisha doti
 
Upuuzi mtupu. Mnamtetea Magufuli wakati yote yanaanzia kwake?

Huhitaji hata kuwa na pH D kujua kwamba vyombo vya dola kwa kutumwa toka juu au kujituma wenyewe wanahusika. Mbinu ni zile za kutekwa kwa wana music, akina Saanane na watu wengine
Serikali inajua ndio maana haitaki kuchunguza au hata kutoa taarifa.
Wale waliopiga risasi kwa Nape wako wapi?

Hakuna cha maadui wetu. Ni serikali ya Magufuli ambayo haiko tayari kukubali challenges. Maneno yake yamewapa Uhuru usalama wa taifa kutisha watu hata kama hawajaruhusiwa moja kwa moja na yeye mwenyewe.

Kitendo cha serikali kukaa kimya watu wanapotekwa kimetoa ishara kwa rogue police na tiss kwenda hatua moja mbele ya kutaka hata kuua.

Serikali inawajibu was kulinda raia. Ina wajibu wa kutoa majibu kwa familia ya Mawazo. Ina wajibu wa kutoa majibu kwa familia ya Saanane, kwa Roma nk.
Mkuu, first of, I always respect you, second, ebu pitia kwanza hii link...
Tundu Lissu: Am told, People at the top aren't thinking and acting rationally anymore...

Jingine ni kuhusu ulinzi. Kama una imply kuwa Lissu na Maruma were the same kwenye issue ya ACACIA, basi naona ama serikali imembagua na kutokujali kazi yake, ama umekosea kwenye uchambuzi huu.

Dhana ya kulazimishwa kuhusu vyama vingi na mabepari ili watutawale vizuri nakubaliana nayo kabisa. Upinzani walikuwa ni wana usalama waliopelekwa na mwalimu ili isije kutokea nchi ikachukuliwa na "maadui wa taifa"

Ila kuna pahala tumekosea, napo ni kwenye hizi siasa za vyama. Kumekuwa na uadui wa kweli kabisa na matukio mengi tu ni ushahidi tosha. Hata wanaojiita wasomi, nao huwa wanajidhalilisha kabisa inapokuja kwenye siasa za vyama. Yani watu ufahamu unawatoka kabisa.

Kina Mrema na Marando ndiyo. Lissu I don't think so.
 
.... [B said:
Baada ya Mwalimu kuzongwa na Mataifa Beberu wakimtaka aruhusu mfumo Wa Vyama vingi kama njia ya kusaidiwa kurekebisha mwenendo Wa kiuchumi kwa wakati ule,Serikali iliazimia kuruhusu mfumo huo u-take shape(licha ya wananchi wengi kuwa wameukataa) kwa Kuchukua "machineries" kadhaa na kuzichomeka huko na waanzilishi vya vyama hivyo na hata viongozi Wanaorithi nafasi mbalimbali ndani vya vyama vya siasa. Hili wengine wanalijua na wengine hawalijui.
....[/B]

cc Mwanahabari Huru, Salary Slip
 
mkuu hizo ni sababu za kusadikika, tuko hapa wote hautakuja kusikia mtuhumiwa kakamatwa mbali na kudhan kama unavyodhan ww, usitake kutufanya sisi mambulula hata tusijue ukwel uko wapi, nan mwenye ujasiri wa kwenda kumshambulia hadhalani mchana kweupe mtu maarufu na mzito ktk jamii kama Lissu na asikamatwe? hebu achani dhahania zenu hizo za kubadili ukweli kuwa uongo ili tu kuupotosha uuma.
 
Binadamu wengine ni roho za wanyama na shetani. Wakati Mungu na binadamu wema wanataka maisha marefu. Mijitu shetani inafikiri kukatisha/kutesa binadamu wenzao. Mambo ya uharamia huu yanatoka wapi ??? UHAI NI ZAIDI ya Mipesa au Chochote unachojua ni cha thamani.... inaumiza sana kwa watu wema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom