Januari Makamba asema CCM inalifanyia mzaha tatizo la umeme Tanzania

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati ameilalamikia serikali ya CCM kwa kile kilichoelezwa ni mzaha kwani mapendekezo ya tume yake hayajafanyiwa kazi hata kidogo huku tatizo la umeme likiwa linaendelea.

Hajui kesho bungeni atasema nini!

Hakubaliani na serikali kukodi mitambo ya kufua umeme kwa gharama ya sh 5billion, badala yake hizo pesa zingewekezwa katika mitambo mipya ya kuzalisha umeme wa maji katika mito ya Rusumo au Rufiji na kuwa mali yetu moja kwa moja!!

Source Channel10 news.
 
Huyu dogo kuna kipindi kichwa yake ina hoji vitu vya ukweli sana. Ni kweli serikali yetu inafanya mzaha na umeme, haijui kila kitu siku hizi ni umeme, ona jinsi serikali ilivyopata hasara ya mabillion katika siku hizi ambao umeme ni karibu 16hrs mgao. Big up Makamba.
 
Naomba wenye kulifaham hili watujuze.

Hivi mito ya Rusumo na Rufiji maji yake hayapungui? Maana utegemezi kwenye maji umeligharim saana taifa hili. Umeme rahisi wa upepo vipi? Lakini pia kwanini wasihakikishe wanahimiza solar kwa kutoa hata subsidy au kwenye ofisi za serikali ukizingatia mazingira yetu yalivyo?

Lakini je, pendekezo lake ni la muda mfupi kuliko umeme wa kukodi?
 
Back
Top Bottom