mimi kistobe
Member
- Nov 25, 2023
- 99
- 277
Nina kaka yangu anapitia kipindi kigumu cha mawazo na maumivu juu ya jambo linalomsibu.
Kaka yangu alikuwa anatoka kimapenzi na mama mmoja mke wa tajiri hapa mjini, kutokana na tamaa za mali akawa amejisahau na kujiachia
Baada ya mahusiano yao ya muda mrefu, kaka akaanza kuumwa sana na kutoka vipele mwili mzima, nikamshauri aende kupima.
Vipimo vikatoka ila akasema anaumwa typhoid na vipele ni mchafuko wa damu, Baada ya mm kurudi nyumbani kumsalimia bimkubwa, nikamkuta kaka amebadilika sana amekuwa mlevi wa kupindukia.
Nikapata mashaka na ulevi wake ikabidi siku moja niende nae kunywa pombe tulilewa sana, na nilifanya makusudi ili aropoke kinachomsibu.
Dhumuni langu lilifanikiwa kweli na akaniambia ameathirika, nilishtuka na kuumia sana.
Maisha yakasogea, mm nikarudi kwenye majukumu yangu mkoa mwingine, yeye akabaki home na bimkubwa makazi ya kaka makubwa ni Nairobi.
Sasa jambo ambalo linaniumiza kichwa ni ulevi wa kaka, yaani huyu jamaa anakunywa pombe sijawahi kuona wakuu, asee amekuwa mlevi sana si mchana wala usiku muda wote yeye gage inasoma.
Mpaka sasa sijamshirika bimkubwa wala kaka zangu wengine wakubwa, na mbaya zaidi hatumii vizuri dawa za ARV.
Nawaza sana nifanyaje juu ya hili swala, naweza nikampoteza kaka yangu alafu mimi ndo nimebaki na hii siri.
Angalau angepata mtu mzima amshauri na kumpa moyo akubaliane na hali atumie dawa na maisha yaendelee, ila hataki kumshirikisha hilo swala mtu yoyote.
Tafadhali naombeni ushauri wakuu.