Uthibitisho wa kazi maalum ya Ben Saanane na hujuma za Dr. Slaa kwenye siasa za Juliana Shonza

Status
Not open for further replies.

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
Ndugu wana JF,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa kashfa zinazoenezwa dhidi yangu juu ya yale yaliyoandikwa na exaud mamuya na Ben Saanane kuhusu mimi kama mmoja wapo wa kundi la masalia kutumika na zitto kuwachafua viongozi wa chama pamoja nakuratibu mipango[movement]ya kuhujumu chama.

Ndugu wana JF, nimewaunganisha wote kwa maana ya ben na mamuya kwasababu ni dhahili kabisa kwamba lao ni moja,wamelenga kunichafua mimi na wenzangu Mchange, Mwampamba, Gwakisa, Sanga akiwemo kiongozi mwandamizi wa chama naibu katibu mkuu na mbunge mh Zitto Zubery kabwe. Huku wakimtuhumu zitto kuwa ndiye mmiliki wa masalia katika harakati za kuhujumu chama na kuwachafua viongozi mtandaoni.

Ndugu wana JF,
Sio mara ya kwanza majina haya kuandikwa vibaya mtandaoni na watu ambao wamekuwa wakijificha sura zao kwa kuvaa vinyago[mask]wakidhani kwamba hawafahamiki.

Kabla sijaanza kujibu hoja za Ben na mamuya niweke wazi kwamba Zitto ni kiongozi wangu. Namheshimu kabisa kabisa kama ninavyo mheshimu mbowe na slaa na wengine wote ndani na nje ya chama.

Ndugu wana JF,
Hoja alizotoa mamuya dhidi yangu ni hoja zisizo na mashiko yoyote kwa mstakabali wa vijana, chama na taifa kwa ujumla maana ni hoja mufitini, ambazo zimelenga kuwagawa baadhi ya vijana waonekane kwamba wao ndio bora zaidi ya wenzao huku wakiwachafua wenzao kwa majina mbalimbali kama vile mamluki, wasaliti na masalia.

Exaud Mamuya naweza kumuelezea kwamba ni kijana ambaye akili yake haijiongezi,asiye na msimamo, mkurupukaji, na mpika majungu. Katika kuthibitisha hili mamuya atakumbuka kipindi cha uchaguzi wa bavicha alipokuwa anagombea nafasi ya naibu katibu mkuu bavicha alinipigia simu akiniomba tushirikiane ashinde kwakuwa ametelekezwa na viongozi wakuu wa chama na Godbless Lema baada yakugundua kuwa kawasaliti na kuhamia kambi ya Zitto. Akajinadi kwamba ni kweli amehamia kambi ya zitto. Kwakuwa mimi si mnafiki kama alivyodhani majibu niliyomjibu najua anayakumbuka na matokeo yake aliyapata Dodoma baada yakujikuta umeambulia kura sifuri.

Exaud Mamuya
nikwambie wazi kwamba huna dira maana umechagua kufanya siasa za majitaka. Napata shida kidogo nikifikiria wapi hasa umetoa ujasiri wakumzushia zitto maneno ya uwongo pamoja na hao mnaowaita masalia. Kama suala ni kundi la Zitto basi lazima kuna uwepo wa kundi jingine ambalo wewe unapigania maslahi yake ukiwa kama muumini wa kundi hilo.

Wewe sio wa saizi yangu, endelea kutuita masalia jina la Kubenea kupitia mwanahalisi .

BEN SAANANE

Huyu namfahamu kama kijana wa chadema japo sijawahi kumuona kwenye shughuli yoyote ya kujenga chama zaidi ya kubomoa na kufitinisha viongozi na wanachama kama alivyofanya kutimiza matakwa ya maboss wake.

Swali: Kama kuna yeyote amewahi muona Ben Saanane kwenye kazi za chama yoyote ile ya shina au ta kitaifa aje hapa na ushaidi wake.

Shutuma ulizozielekeza kwangu kwamba tulikaa kikao chakujadili kwenda kula kiapo kwa waganga. Ben ni wapi tulikaa kujadili suala la kwenda kwa waganga? Nakana wazi kwamba hakuna kikao chochote nilichokaa na wewe nikakuunga mkono suala la kutokwenda kwa waganga au kwenda. Wewe ni mwongo unapaswa kupuuzwa maana shughuli yako imejionyesha wazi kwamba una lengo mahususina sio kujenga chama na ndio maana hujawahi kuonekana kwenye shughuli za ujenzi wa chama zaidi yakuzunguka kwenye mahotel kufanya vikao na ndugu zako kupitia ruzuku ya chama unayolipwa pale makao makuu.

Ben saanane katika kukutana kwangu mm na wewe hakuna siku tuliyowahi zungumzia,au mhusisha Zitto na swala lolote la kuharibu au kuhujumu chama zaidi ya kumsifia kwamba ni kiongozi anayefaa kuigwa ndani ya chama.

Nina ushahidi wakutosha kwamba ben saanane analipwa na chama cha chadema na yupo kwenye payrol ya chama kila mwezi kwa kazi hii ya kumchafua zitto kabwe na kufanya kazi ya kijasusi ndani ya chama.(nipo tayari kuwasilisha udhibitisho huu mbele ya chama)


NAMNA DR SLAA ANAVYONIHUJUMU KISIASA:

Namuheshimu dr slaa kama katibu wangu wa chama ambaye alipaswa kuwa dira yangu ya kisiasa na kiungozi ndani ya chama. lakini chakushangaza siku hadi siku amekuwa akinihujumu moja kwa moja yeye mwenyewe na kupitia kwa ben wa sanane kwakumtuma aje kunishawishi tuanzishe movement nje ya chama kitu ambacho nilikikataa nayeye ni shahidi katika hili.


Dr slaa amekuwa akiligawa baraza la vijana kama ifuatavyo

Kwanza yeye kama mtendaji mkuu mtendaji wa shughuli zote za chama amemuidhinishia bwana Heche mshahara wa shilling laki saba kwa mwezi kinyume cha katiba ambayo inamtambua katibu wa baraza pekee kupokea mshahara kwa mwezi.

Kumlipa mshahara heche ni kuligawa baraza la vijana kwasababu ni ukiukwaji wa katiba ya chama.Pia ni wazi anaonesha anamlipa fadhira heche kwa yale aliyoyafanya ya kuendesha baraza kwa misingi ya kauli za katibu mkuu.

Pia katibu mkuu ndg Peter Slaa aliruhusu mwenyekiti wa vijana bwana John Heche apewe kiasi cha shilingi milioni mbili kama malipo ya pango la nyumba aliyotafutiwa na chama baada ya kupewa uenyekiti wa baraza la vijana.

Hii ni ishara tosha kwamba viongozi wa vijana tunawekwa kimatabaka katika mamcho ya viongozi wetu.Kumlipia heche pango ni wazi mm na viongozi wengine tumetengwa na hatuonekani kama watu mbele ya chama.

Vilevile mh.naibu katibu mkuu ndg Zito Zuberi Kabwe alitoa gari aina ya Nissan patrol rangi nyekundu kwaajiri ya shughuri za baraza la vijana kwani hapo kabla chama kilikuwa na uhaba wa magari,lakini jambo la kushangaza na aibu na linalochukuliwa na wengi kama ufisadi,bwana Heche amekuwa akilitumia gari hilo kwa shughuri zake binafsi huku dereva mkuu wa gari hilo akiwa ni mdowake wa kuzaliwa aitwae Chacha Heche, visingizio vimekuwa vikitolewa na kufumbiwa macho na katibu mkuu kuwagari ni bovu,jambo ambalo si la kweli.

Katibu mkuu ndg Peter Slaa amekuwa akinizuia kutekeleza majukumu yangu ya kiongozi huku akinitisha kwa simu ya mkononi kwa kunipigia na kunitumia meseji ili nikate tamaa na kuwavunja moyo walionichagua na kisha nisusie chama kama ambavyo mh. Arfi alitaka kufanya jana mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa na viongozi wakuu ndani ya chama kama silaha ya kudhoofisha watu ambao wanahisi wanakinzana nao kimtazamo.


Ushahidi wa meseji ujumbe mfupi wa maandishi ninao ,nanipo radhi kuupeleka mbele ya chama itakapo bidi.

moja ya mambo aliyoniambia dr.slaa ni kwamba
"huta kaa ukashiriki kazi yoyote ya chama, hadi pale mbowe atakapoondoka madarakani"



Wanajf hii meseji ni kutoka kwa Dr. Slaa kuja kwangu makamu wa baviha taifa.

Mfano mwezi wa nane mwaka huu nilijitolea kwenda kujenga chama Mbeya kwa rasilimali zangu lakini cha kushangaza Slaa alinitumia meseji ya vitisho(ninayo)akidai nimeenda kufanya m4c ambayo anadai eti yeye ndiye mwenye mamlaka nayo,yaani ndiye mwenye kupanga nani afanye na nani asifanye.

Wakati huohuo alishanipigia simu nakunitamkia kwamba sitakaa nishiriki shughuri yoyote ya ujenzi wa chama kwani eti mimi ni mfuasi wa Zito Zuberi Kabwe,na hiyo ni baada ya mimi kumuuliza kwa nini mimi sipangwi kwenye shughuri za ujenzi wa chama, na katika kipindi hicho m4c ilikuwa imeelekea Lindi na Mtwara huku washiriki toka Bavicha wakiwa ni walewale Munishi na Heche, nalijibia hili kwasababu nimekuwa nikiulizwa na viongoz na wanachama kwa nini sionekani kwenye ujenzi wa chama.

Hakuishia hapo slaa amekuwa akinifitinisha na viongozi wangu wa wilaya ya mbozi, wilaya niliyotumia nguvu yangu na uwezo wangu mkubwa kukujenga chama kwakupitia mwenyekiti wa wilaya bwana john mwambigija .

Mfano ni hivi majuzi wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani kama kawaida sikupangwa kwenye kata yeyote huku viongozi wenzangu wakipangiwa ndipo nilipoenda wilaya ya mbozi kata ya muyovizi lakini katika hali yakushangaza mwenyekiti huyo wa wilaya alikataa kunisimamisha kuhutubia kwa madai ya kwamba ameambiwa na dr.slaa mm simuungi mkono ndani ya hama hivyo asinisimamishe kuhutubia.

Katika mazingira ya kawaida ni wazi kuna mazingira yakubaguliwa labda kutokana na ukanda na ukabila ambayo kwa hali ilivyo sasa haifichiki.Dr slaa ndiye injinia wa mipasuko ndani ya chama kitu ambacho kimelenga kubomoa na kudhoofisha jitihada zangu,dhamira yangu safi ,na utumishi uliotukuka kwa chama changu.


KUHUSU BEN SAANANE NA KUTUMIKA KUMUUA ZITTO KABWE

Wana jf,Nakili wazi hili swala lilitokea mnamo mwezi wa 5 mwaka 2012 tukiwa Lunch time hotel external kwenye mazungumzo ya kawaida(ambavyo ben saanane anaita ni vikao vya kuhujumu chama). Siku ya tukio tukiwa meza moja na Ben Saanane mkono wake wa kushoto alifunga bandeji akidai ameumia mkono(nakumbuka). Kwa babati mbaya sana katika maongezi yale Ben alilewa pombe (alikuwa anakunywa bia(kilimanjaro). Kulewa kwake pombe alijisahau na kutoa bahasha ya kaki yenye fedha, ndani ya bahasha ile wakati wa kutoa fedha alipe huduma ya chakula na vinywaji alidosha karatasi ya nailoni ndogo ikiwa na unga mwekundu ndani.

Tulimuuliza ni nini hicho akadai ni kuberi,na kuing'ang'ania tusifungue(aliyekiokota ni mwampamba).Lakini Mwampamba aligoma kumpa na kudai lazima ifunguliwe pale pale.

Ben saa nane akiwa katika hali yake ya kulewa alifura kwa hasira kutaka arudishiwe ilekaratasi,haliiliyopelekea uvunjifu wa amani pale lunch time hotel.Mwampamba aliondoka na mzigo ule kwa kukimbia nao, usiku ule Ben alitafutana na mwampamba hadi nyumbani kwake(temeke) akidai huo mzigo(ikumbukwe mwampamba na mm nimeishi kwake na nikaka yangu) . Lakini katika hali ya kusikitisha ben aliomba mzigo ule usiende mbali na kuahidi atasema kweli kile ni nini.

Ben saanane alikili wazi kwamba ile ni sumu lakini anapeleka nyumbani kwa ajili ya kuulia panya, Swala hili halikuishia usiku ule,ben hakufanikiwa kupata mzigo ule kesho yake asubuhi(jumapili) alikwenda kumsihi mwampamba ampatie mzigo.

Sharti lilikuwa aseme ni nini kwasababu huwezi kuwa na sumu eneo la starehe kama pale hotelini huku akisisitiza kuonana na zitto ambaye alisafiri usiku ule kwenda marekani bila kuonana na yeyote kati yetu?

Ndipo Ben saanane akakili ile ni sumu akilenga kumpatia zitto akiwa ametumwa na Dr.slaa.Tulihamaki kusikia kile kitu(hapa tulikua tabata reli stand tukisubiri usafi).Nilimuuliza uthubutu wake wa kufanya kitu kama hicho na kwanini afanye unyama huo,akadai ametumwa Kisa kikiwa ni zitto kumsakama dr.slaa ndani ya vikao vya chama.

Swala hili lilifika mbali kwa kuwekeana mipaka ya kula vyakula mahotelini na kutoshirikiana tena katika ushikaji wetu kama masalia.

Lakini urafiki wetu na ben uliendelea na tukayamaliza haya mambo kishikaji kawa wanasiasa vijana,Ben alifurahi sana ndipo akaja na wazo la PM7 kama movement ya kuendesha harakati huru ndani ya chadema zikilenga kukataa kutumika na viongozi wa chama kama ben alivyotumika kutaka kumuua zitto.

Hilo wazo la PM7 lilikaliwa mazungumzo mara nne lakini likaaishia hewani mara baada ya kuona halitakuwa na manufaa ndani ya chama na litaleta mtafaruku.

Tokea kupigwa kwa hoja hii ya ben saanane ya PM7,ndipo tulipo anza kutengenezeana uadui wa kisiasa hadi hii leo tumefikia hapa .




HITIMISHO:

Hii issue ya mamuya na ben saanane ni maalumu kuzima sakata la kadi mbili lililomuandama mwezi mzima dr.slaa,Na hizi shutuma,uongo na uzandiki umekaliwa vikao kwaajili ya kuandaa hizi shutuma

NOTE:
1.Nimewasilisha barua yangu ya malalamiko kwa mwenyekiti wa chama freeman mbowe kupitia ofisi za kambi rasmi ya upinzani bungeni kuanzia mwezi 10 kwa namna Dr.slaa anavyo nihujumu ili likajadiliwe kamati kuu.

2.Ninaushahidi wa malipo ya Ben saanane juu ya hii kazi ya kuchafua viongozi wa chama hasa mh.zitto zuberi kabwe.(nitawasilisha)

3.Jana nimepigiwa simu mfululizo toka makao makuu ya chama(VIONGOZI WAKUU WA CHAMA) kuhusu kukaa kimya kuzungumzia shutuma hizi ambazo zimelenga kuchafua viongozi ndani ya chama.(ushahidi ninao na nipo tayari kuuwasisilisha)


Juliana Daniel Shonza
Makamo Mwenyekiti BAVICHA - Taifa.


MAJIBU YA BEN:
Sikupenda kuingia tena katika majadiliano haya zaidi ya kusubiri vikao vya Chama. Kwa kuwa kundi hili linaendeleza mjadala na upotoshaji wa pale alipoishia kiongozi wa kundi nimeona si vyema kukaa kimya. Mchange anasema hakuwa wa kwanza kunitafuta mimi as if hii ni hoja ya Msingi sana. Hata Zitto sikuanza kumtafuta mimi ila yeye hasa baaada ya kuenguliwa uchaguzi wa BAVICHA. Nitaweka baadhi ya mawasiliano yake ya kwanza yakiwemo ya tarehe 29/05/2011 siku iliyofuata baada ya kuenguliwa BAVICHA.

Kwanza NI KWELI kundi hili la PM7 lilikuwepo. Ni kweli tulishirikana kaktika mpango huu.Kwanza jina PM7 ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa miongoni mwa majina mengine. E-Mail aliyotuma Mchange hapo juu ni e-mail ambayo nilimtumia Zitto Kabwe na tulikubakliana mimi na yeye isajiliwe taasisi ambayo tutakua tukiendesha harakati bila kujipambanua waziwazi na malengo ya taasisi hiyo. Lengo kuu la Taasisi hii lilikua ni kuanzisha vuguvugu la vijana na kulitumia kama platform ya kisiasa na kijamii ambayo ingekuwa non-partisan baada ya taasisi ya ADO kutokuwa active. Pia ingekuwa taasisi ambayo ingefanya harakati za baraza huru la vijana. Zitto alipokea wazo hili kwa furaha.Hata hivyo lengo la Taasisi lilibadilika na kuwa na malengo ya kisiasa ndani ya chama na wakati huo huo tukitafuta njia ya kubeba kundi la masalia kisiasa. Zitto alikuwa ameshaanza kuzunguika na kundi hili kwenye mikutano ya hadhara mikoani. Mimi ndiye niliye-draft contents zote ambazo hata hivyo Mchange hajathubutu kuziweka zote hapa.Tulitohoa jina la PM kutoka katika taasisi hiyo niliyoipa jina la Youths Patriotic Movement

Ninayo mawasiliano yangu na Zitto kuhusu kundi hili na alinihimiza wakati huo akiwa Songea kwenye kampeni za udiwani kwenye chaguzi ndogo za udiwani akiwa na akina mwampamba na Shonza.Tulikubaliana kwamba hii taasisi isajiliwe haraka sana iwezekanavyo namnukuuu YPM MUST BE REGISTERED SOON AND GO COUNTRYWIDE mwisho wa kunukuu. Ndugu Zitto, bila shaka anaweza kuthibitisha hili

Nikiwa Geita wanachama wa kundi la Masalia walikua wakinipigia simu mara kwa mara na hata Message za kunitaka nirudi Dar haraka hata kwa muda mfupi tu tuweke mipango ya kuanzisha kundi hili pamoja na kufungua bank account. Tarehe 01/05/2012 nilifika Dar es Salaam kikazi. Siku hiyo hiyo tulikutana na Habib mchange, Mtela Mwampamba, Juliana Shonza na Festo Sanga pale Lunch time hotel. Siku hii ndiyo niliyotambulishwa kwa Festo Sanga. Wote walikua na shauku ya kupata mawazo yangu kwa kuwa zitto alishawadokeza juu ya mkakati huu hasa baada ya kikao cha kamati kuu.Nadhani ilikua ni matokeo ya kikao cha kamati kuu na mambo yaliyotokea humo ambayo sitaki kuyaandika hapa kwa sababu ni siri za vikao.

Tulikubaliana katika kundi hili tuwe na mkakati wa siri na tukusanye fedha nje na ndani ya chama.suala la kukusanya fedha nje ya chama nililipinga sana.Nakumbuka Mchange ndiye aliyeleta wazo la kukusanya fedha nje ya chama.miongoni mwa walengwa walikua
-David Kafulila
-Mwigulu Nchemba
-Deo Filikunjombe
na baadhi ya wafanyabiashara

Draft niliyoandika ilionekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wale ambao walikua potential donors.

Pia Habibu Mchange alileta taarifa kwenye kikao kwamba Zitto amemwambia tuandae bajeti ya kundi hili. Zitto alisafiri siku hiyo bila kutuambia na tulilalmika sana sana. Baada ya hapo alikua akiwasiliana na mtu mmoja mmoja. Hata hivyo kwa kuwa ulikua mpango wa siri nilipendekeza tutumie code names au namba zilizochanganywa na herufi kama mbinu mojawapo ya kijasusi. Mwishowe kila mmoja alikubaliana tutumie tu majina kwa kuwa walihofia kusahau code names.tulibatizana majina na jina langu likawa COBRA, Mchange-Mdude, Shonza-Benazir, Mwampamba-Kony na code name ambayo tuliitumia kwa Zitto ni Prezzo au Dogo

Role yangu mimi ilikua katika fedha baada ya majadiliano kwa kuwa kila mjumbe alisema Ben ndiye tunayemuamini pekee katika usimaizi wa fedha na kubuni vyanzo vya fedha. Nilipewa kazi ya kuandaa bajeti.Lakini nilikataa kwa kuwa nilisema bado siridhishwi na mwenendo wa kukusanya fedha nje ya chama.

Shonza Alikuwa Mwenyekiti wa PM7 strategically ili awe na wajibu mkubwa kwa kuwa alikua kiongozi wa juu wa BAVICHA. Mchange alijichagulia kuwa makamu Mwenyekiti, Mwampamba Katibu, Festo Sanga alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE akisaidiana na mchange na Mwampamba. Tulikubaliana iwe taasisi kwa kundi lote la Masalia ili itumike panapolazimika. Sikuwahi kuitumia kwa kuwa niliwaambia nitaendelea kutumia ID yangu kwa kuwa siatamtukana mtu au kuzusha kitu hata kama michango yangu ingeniweka matatani

Hata hivyo baadae nilikubali na niliandaa bajeti ya Sh. 25,000,000 kwa awamu ya kwanza na tukachora ramani ya jinsi tutakavyogawana mikoa.

Lengo lilikua kuingia mikoani hata kwa lazima na kufanya mikutano ya hadhara na kujenga mtandao. PM7 ilikuja kubadilika na malengo yakawa too narrow kwa kuwa yalilenga kuimarisha kundi ndani ya chama. Badala ya Patriotic Movement ilikuja kuwa PINDUA MBOWE-7. Lengo hapa lilikua kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu ili kundi liweze kuimarika na kupenya kati kati. Hapa ndipo kazi ambayo ilikua imekwisha anza mwezi wa 4 katika kampeni za Arumeru Mashariki ya kumchafua Mbowe na Katibu mkuu kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE iliposhamiri

Actually, niliona hatari ya kukichafua chama hasa tuhuma zilizokuwa ziktumika zilikua tuhuma za uongo na uzushi.Wakati tunafanya maandalizi ya kufungua akaunti benki, nilikutana na Dr. Kitila kwa haraka na kumweleza kama zitto au yeyote amemweleza kuhusu kundi hili. Alinijibu kwamba hana taarifa hizo.Hata hivyo tulikubaliana tukutane haraka na Zitto tuweke mikakati mipya kwa kuwa alishangaa ni kwa nini amewahusisha akina Mchange na Mwampamba huku akijua siyo watu makini katika strateggy na ni waropokaji. Aliniomba nifanye mpango wa kulivuruga kundi hili na Pm-7 ife taratibu. Baadae alinieleza kwamba tutapanga siku tutoke nje ya Dar mimi, yeye na zitto tuweke mikakati upya kwa kuwa hapa dar tulikua tunafuatiliwa sana sana. Nilifanikiwa katika mipango hii ya kuiua Pm-7 taratibu na hata wakati mwingine tuligombana sana na baadae kwenye kiakao karibu na Pacific hotel pale Manzese, Mchange na Mwampamba waliibuka na hoja kwamba kuna haja ya kwenda kula viapo kwa mganga ili tusisalitiane katika kazi hii pm-&. Kwa bahati nzuri shonza, Mimi naMwakajila tulipinga vikali upuuzi huu. Shonza hili unalijua na unajua ni kiasi gani nilikasirika siku hiyo. Uliniandikia Message na kunisihi tuendeleze kundi hili

Baada ya hapo wakati kikao cha bajeti kinaendelea Shonza na Mwampamba walinipigia simu kuhusu kikao cha dgharura na David Kafulila. Ilikuwa Tarehe 4/07/2012. Tulikutana Tamal Hotel. Kafulila alitudokeza juu ya kusajiliwa kwa chama cha CHAUMMA, tulijadili mambo mengi.Nilishirikishwa juu ya kujiunga na CHAUMMA na kuhakikisha kinasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu. Kafulila alinisihi sana na kuniambia ndani ya CHADEMA yatanikuta yaliyomkuta yeye kwa hiyo tuungane. Nilimwambia nitafikiria. Hussein Bashe alikuja dakika za mwisho kwenye kiako kile. Yeye ni miongoni mwa mashuhuda. Kafulila aliniambia mzee Hashim Rungwe pia atajiunga na anafanya mawasiliano na Zitto. Tulipanga kukutana siku iliyofuata. Mwampamba alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao pamoja na Shonza. Siku hii mchange hakuwepo

Tarehe 7/07/2012 nilikuwa ndani ya Ofisi ya CHAUMMA. Nilitambulishwa kwa viongozi wote tukaweka mikakati. Mingine sitaiandika hapa kwa sasa. Walinipa kazi ya kuandika sera ya Vijana na sera ya mambo ya nje huku Kafulila akisema kwenye uchumi sera ya gesi atashirikiana na Zitto kwa kuwa wote wana utaalamu kutoka holand na Norway. Niliwakubalia kimkakati hasa nilipogundua wanapanga kupunguza kura za CHADEMA mwaka 2015 huku akiniahidi kwamba kundi kubwa litatoka CCM na CHADEMA baada ya chaguzi za ndani mwaka huu na mwaka ujao respectively. Aliniambia hata akina Hashim Rungwe wapo nyuma ya kundi hilo na vigogo wa CCM. Mliniambia CHAUMMA kitakua chama darasa. Kafulila anaweza kuthibitisha hili.

Katibu Mwenezi wa CHAUMMA ndg.Mawazo Athanas kutoka kigoma alinisihi sana nimsaidie na Zitto akiwa nje amemuhakikishia kwamba sisi tutamsaidia yaani masalia group au PM-7. Hapa Dr. Kitila mkumbo hakuhusika.Ikumbukwe Mawazo athanas alikua Mgombea Ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi huko kigoma na baada ya kuhama alitaka kujiunga na CHADEMA. Nilimshawishi sana ajiunge na CHADEMA lakini baadae nilimsikia yupo CHAUMMA. Nilikuwa nikifahamiana naye hapo kabla. Tuliendelea kuwasiliana nae kwa karibu na pia nikamuahidi Kafulila na uongozi wa juu wa CHAUMMA kwamba nitatoa ushirikiano ila waandae vitendea kazi. Nitaweka baadhi ya mawasiliano yetu hapa. Hata ID ya CHAUMMA hapa JF niliifungua mimi nikiwa ndani ya Ofisi za CHAUMMA na tulipeana Password. Kafulila alitaka nimpe paswd yeye, Katibu Mwenezi na katibu mkuu huku akiahidi kwamba atampa zitto itakapobidi. Alinisihi nisiwape akina Mchange na wengine kwa kuwa wanaweza kuharibu na kuonyesha wazi kwamba lengo la CHAUMMA ni kuigawa CHADEMA. Alitaka tuende kimya kimya. Akina Mchange na Mwampamba waliendelea kutumia ID Fake na ID ya TUNTEMEKE. Hii ni sehemu ndogo tu,sitaki kuharibu mambo mengi hapa hasa nyeti kwa kwa chama.

Nitaendelea....Nikihitajika nitakuja tena

attachment.php

attachment.php

 
Mwenendo unavyoenda Chadema ni aibu saana... Sijajua katika hili uongozi wa juu na wafuasi wa Chadema wanalichukulia vipi ila ukweli unabaki kuwa ni AIBU. Haijalishi nani ni mkweli... Haijalishi nani ni muhalifu... Mchawi, msafi ama mchafu; ila namna mambo yanavyoenda it is too Low.

Bado miaka miwili tu kwa wao uwezekano mkubwa wa kushika nchi, huu ndio wakati pekee wa kurekebisha huu uchafu na kashfa za kutiana aibu... Chadema so far ime prove viongozi wameshindwa kabisa KUDHIBITI Nidhamu (tena ya watu wachache) tokana na kuwa yeyote yule anaweza toa kauli ambayo ina smear mmoja/baadhi ya viongozi katika Chama hadi kwa Dr. Slaa mwenyewe let alone Zitto. In a way inacheza nafasi hasi ya kuonesha kuwa hawapo tayari kama wanashindwa kudhibiti subordinates wao.

Kila anae shutumu anadai ana ushahidi tosha.... Tunaombeni huo ushahidi. Na madame Juliana Shonza hapa umemgusa Dr. Slaa ambaye yeye katika macho ya Chadema hanaga makosa kwa wengi na Saanane (ambaye anaonekana kajutia makosa na kujisafisha) tena kwa kujaribu kumtetea Zitto... Ni sawa na kumpigia mbuzi guitar bila ushahidi wowote.
 
mimi naamini yote kama mtu ,upadiri ulimshinda hawezi kuwa muadilifu.kweli mungu mkubwa yaani huyu ndiyo angekuwa rais
 
Ndugu Juliana shonza,Naona umeamua kuvujisha mambo nyeti.Yaani umemtoa nyoka pangoni kwa kuanika ukweli huu hapa.
D.slaa pole sana mkuu wangu naona hali si hali(I.C.U) wameshatuma ambulance
 
Hivi umesomea wapi hiyo shule yako? Hivi mpaka andike kuwa amekubali? Kwani alicho kiandika si kimeonekana!

AMEKUBALI WAPI?NAOMBA U QUOTE alipo kubali..Juliana nilikuwa nakusubiria kwa hamu kamanda
 
mimi naamini yote kama mtu ,upadiri ulimshinda hawezi kuwa muadilifu.kweli mungu mkubwa yaani huyu ndiyo angekuwa rais

tungempa urais tumekwisha,Naona anahujumu vijana ndani ya chama.Au kwasbabu ni binti?
 
Sasa hii ndio kitu tunataka. Mods please msizifunge hizi mada mpaka wote waje wateme nyongo zao zote. Huu ndio ukweli na uwazi tunaoutaka mpaka kila mtu aambiwe mapungufu yake na hapo ndio chama kitakaa sawa. Kama kuna mtu yoyote ambaye pia anajua jinsi gani wanapata ufadhili toka CCM kwaajili ya kuharibu chama naye auweke hapa. Hii italeta kuheshimiana na chama chetu kitakuwa imara sasa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom