Jamani sijajua kuwa hili tatizo au kitu gani, sijui ni kwangu tu au tupo wengi wanaume wa hivi?

big dreamer

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
398
1,059
Samahanini kwa kutowasalimia

Yani ipo hivi yani hiki kitu kina nitokea sana kwa upande wangu,,,ni hali ambayo nakutana nayo sana unakuta binti niliempenda leo kutoka moyoni baada ya miaka kadhaa et nakuwa simpendi tena kama mwanzo na upendo unapungua kwa asilimia kubwa,,sio kwamba nilimtamani laasha na simaanisha mimi ni player hapana,,na kwamba hata sometimes sio kwamba mpaka niingie nae kwenye mahusiano hapana hata kwa kumpenda tu bila kupata nafasi ya kumweleza,,,

Yani sometimes unakuta kuna mwanamke ambae nimemtongoza kwa wataki huo alafu labda akanikataa lakini mimi nimempenda sana na nasema nikipata nafasi kuwa nae huyu moja kwa moja ni ndoa lakin bahati mbaya hakupi hiyo nafasi sasa tunapoteana baada ya miaka,,nikikutana nae yani moyoni huwa najiuliza daah hivi ni mimi nilikuwa silali kisa huyu mwanamke mbona saa hizi hata simpendi hata namba yake sichukui,,,na moyoni nasemaga ni bora hakunikubali maana ningemweka ndani kipindi kile saa hzi sijui ingekuwaje maana moyoni hayupo tena.

Upande wa ma ex yani (baadhi yao tume follow each other kwenye social media) mpaka nasema hadi hivi huyu nilimpenda kinoma kipindi kile saa hzi mbona hata moyoni hayupo kabisa wakati kipindi kile alikuwa ananikosesha usingizi huyu (karibia wote imenitokea hivyo)

Upande wa ma superstars/celebrities yan kuna ma star ambao kipindi hicho nilikuwa nasema huyu mimi Mungu akitenda muujiza nimekuwa nae daaah sitalala siku hiyo,nahisi nitazilahi walahi ila sasa miaka zinavyozidi kwenda unakuta et hadi najishangaa kuwa mimi ndio nilikuwa namuwazia hivyo huyu binti mfano mzuri WEMA SEPETU,JACKLINI WOLPER HATA ZARI THE BOSS LADY yani saa hzi nawaona wa kawaida sana bora hata madem wa kitaa hapa

Schoolmates unakuta kipindi niko shule hadi chuo kuna wanawake nilikuwa nasema badi hii pisi no konyo yani nikipata bahati nahizalisha fasta tuweke parmanent bond lakini inakuwa hata salamu tu kutoka kwake ni shida lakini saa hizi nikitutana nao nawaona wakawaida mno hadi hanishtui hata sijui kwanini

Sasa sijajua hii hali ni kutokana na nini au labda ni mambo ya ujana na vijana wezangu mnapitia kama ninvyipitia mimi (sipo peke yangu au sijui nifanye nini hii hali ipungue)

Ila kuna binti mmoja tu ambae nilimpenda sana ila alinizinguaga miaka mingi sana na kwasasa ameshaolewa yule tulikutana mara moja miaka ya karibuni ndio bado upendo uliwepo kwa asilimia fulani za kutosha tu ila wengi inakuwa hivyo jaman sijui kwanini


Uzi tayari
 
Mi hali hiyo hunikuta nikitongoza halafu akaninyima, yaani namwona mbaya hadi najilaumu hivi ilikuwaje hadi nikajidhalilisha kumtongoza
 
Wewe bado hujatulia, mda ukifika na umri ukakwambia now is too late inabd uwe na mke wako wa kuishi naye , hutafanya huo ujinga ..... Kuna Aina ya mwanamke unamtaka Ila unaokutana nao sio hitaji lako, Ila umri ukisonga mbele utatulia tuu
 
Tatizo lako usipofanikiwa kua na binti hua unajenga chuki dhidi yake,

Unaonekana ni mtu uliyeumizwa sana kwenye mahusiano ndio maana umejijengea chuki dhidi ya mabinti,hua unatamani tu na hupendi na baadae hua nafsi yako inajiambia what for? Unateseka sana mkuu,sahau yaliyopita na uenjoy ur life,life is too short,

Kingine unaweza kua una stress sana za maisha,take easy tu.
 
Wewe bado hujatulia , mda ukifika na umri ukakwambia now is too late inabd uwe na mke wako wa kuishi naye , hutafanya huo ujinga ..... Kuna Aina ya mwanamke unamtaka Ila unaokutana nao sio hitaji lako, Ila umri ukisonga mbele utatulia tuu
Okay inawezekana kabisa ulichosema mkuu,kina ukweli fulani nashukuru
 
Sio uzinzi mkuu,,,nimekuwa honestly tu kwa upande wangu niliyoya experience kwangu mimi
Upo kwenye hatari ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, mara nyingi watu ambao hawawezi kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu au kuchoshwa na mwezi(msichana & mvulana) hutafuta kitu tofauti

Chukua hatua kaka bado mapema tafuta mwenzako utakaeweza kumvumilia madhaifu yake kwani kila mmoja ana udhaifu wake
 
Tatizo lako usipofanikiwa kua na binti hua unajenga chuki dhidi yake,

Unaonekana ni mtu uliyeumizwa sana kwenye mahusiano ndio maana umejijengea chuki dhidi ya mabinti,hua unatamani tu na hupendi na baadae hua nafsi yako inajiambia what for? Unateseka sana mkuu,sahau yaliyopita na uenjoy ur life,life is too short,

Kingine unaweza kua una stress sana za maisha,take easy tu.
Haaaah mkuu hadi ma ex inanitokea sio tu niliyowashindwa kuwa pata
 
Upo kwenye hatari ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, mara nyingi watu ambao hawawezi kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu au kuchoshwa na mwezi(msichana & mvulana) hutafuta kitu tofauti

Chukua hatua kaka bado mapema tafuta mwenzako utakaeweza kumvumilia madhaifu yake kwani kila mmoja ana udhaifu wake
Haaa hicho kitu hakiwezi kutokea mkuu yani ile kitu mbususu naipenda balaa asikuambie mtu kitu
 
Back
Top Bottom