Jamani Kwani Katiba Mpya Ndio Basi Tena?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Wanabodi naomba kuuliza swali.

Hivi ile michakato ya katiba mpya, iliyogharimu mabilioni ya shiringi za walipa kodi iliishia wapi?
Manake naona katiba mpya haizungumziwi tena!
Imefika mahali mtu mwenye akili timamu anaweza kuhoji kuwa je hawa waheshimiwa wetu waliopo madarakani leo si ndiyo walewale walionufaika na posho za vile vikao?
Ina maana walikula posho bure au ni nini?
 
vipau mbele vya sasa ni viwanda na kuhamia Dodoma bila kusahau elimu bure mpaka kadato cha 4.Katiba sahau,Siku zote katiba makini huletwa na wananchi sii watawala.Watawala hufurahia iliopo kama INA maslahi kwao
 
Tunawezaje kusahau kitu cha gharama kama kile?
 
vipau mbele vya sasa ni viwanda na kuhamia Dodoma bila kusahau elimu bure mpaka kadato cha 4.Katiba sahau,Siku zote katiba makini huletwa na wananchi sii watawala.Watawala hufurahia iliopo kama INA maslahi kwao

Kukosa maarifa maana watoto na wajukuu wao watateswa na katiba hiyo
 
Program ya serikali hadi 2020 ishatangazwa na waziri mkuu wakati akiahirisha Bunge hivi majuźi. Ni kuhamia Dodoma. Suala la katiba mpya halikuwepo, so forget it!
 
Wanabodi naomba kuuliza swali.

Hivi ile michakato ya katiba mpya, iliyogharimu mabilioni ya shiringi za walipa kodi iliishia wapi?
Manake naona katiba mpya haizungumziwi tena!
Imefika mahali mtu mwenye akili timamu anaweza kuhoji kuwa je hawa waheshimiwa wetu waliopo madarakani leo si ndiyo walewale walionufaika na posho za vile vikao?
Ina maana walikula posho bure au ni nini?
Dr. Slaa hayupo alafu ukawa wamemchukua lowassa aliyeipinga, ye ndo mwenye chama, unategemea nini??
Binafsi naitaka rasimu ya Warioba iwe katiba ya JMT.
 
Back
Top Bottom