Jamani hii ni soda gani? Fanta au Mirinda?

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
DSCF0002i.jpg
DSCF0001i.jpg
DSCF0003i.jpg
Jamani hivi hizi biashara zinafanyika vipi? Inakuwaje mtu nanunua soda ya fanta lakini iko ndani ya chupa ya mirinda? Huu ni uzembe wa hali ya juu!
Nani mwenye kosa hapa? Hivi naweza kuwachukulia hatua gani hawa?
Siku nyingine utagundua kuwa watanzania hatuko serious na biashara zetu.
utakuta mende, vifuniko vya soda na takataka kibao katika soda. Ni uzembe mkubwa sana.
Usishangae siku nyingine kukuta unakunywa konyagi mwitu ukidhani wanywa soda, maana huku kwetu wanatumia chupa hizi hizi ku bottle Konyagi!
 
Hii ni bonge la aibu meneja wa hicho kiwanda anatakiwa kujiudhuru :smash::smash::smash:
 
Kaka Bongo utelezi jamaa yangu alishaagiza castlelite wakaleta ipo kwenye chupa Tusker malt na si unajua Tusker malt ina maandishi ya kuchoma kwenye chupa lakini label na kizibo Castle lite.

Wapelekee Coca cola labda wataweza kufind a way foeward na ukalipwa kifuta jasho au bodi ya ushindani wa biashara nao pia wanahusika katika mambo haya.
 
Tatizo hatuna sera, sheria wala ufuatiliaji wa kumlinda mlaji. Umeangalia vifuniko vimejaa kutu kwa nje, ndani vitakuwaje? Iko siku nilinunua soda ndani mna filter ya sigara. Nilipokwenda kiwandani walinizuwia nisionane na mkuu wa uzalishaji. Kama tungekuwa makini hawa ni wa kupigwa faini kubwa na/au kufungiwa kabisa.
 
Hiyo ndo Bongoland. Subotage kila mahali. I can imagine hiyo pia ni mbinu inayotumiwa na haya makampunia kuharibiana biashara
 
Oops! Kuna binti huku alikunywa koka ndani kulikuwa na mavi ya mende na uchafu mwingine. Binti hoi hadi akalazwa hospitali. Alienda kushtaki akalipwa fidia.
Watu tushajitoa mhanga kunywa hayo makemikali. Bado wanatuongezea na uchafu. Lol!
 
Hiki ni kile kiwanda cha Mwanza cha yule mwana CCM mkereketwa anaitwa Gachuma ndio kinafanya madudu haya.
Jamaa yuko buzy anachakachua mambo ndani ya chama na huku biashara yake pia imechachuka. Badala ya kuwa busy na kuhakikisha biashara yake ina prosper yeye yuko busy na chama kilichokwisha kujifia! JAMANI!
 
Hivi ndugu unaona wanajf wote watoto? Au unadhani hatuna mambo ya maana ya kujadili? UMECHUKUA CHUPA YA MIRINDA ORANGE, UKAPACHIKA KIZIBO CHA FANTA, halafu unajiita great thinker, cjui ndyo ubunifu? Pole
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Hivi ndugu unaona wanajf wote watoto? Au unadhani hatuna mambo ya maana ya kujadili? UMECHUKUA CHUPA YA MIRINDA ORANGE, UKAPACHIKA KIZIBO CHA FANTA, halafu unajiita great thinker, cjui ndyo ubunifu? Pole
Nadhani una ugonjwa wa kichwa. Nibandike kizibo ili iweje wewe juha? wewe ndiye mtoto. Unadhani nina faida gani kuleta uongo hapa. Mimi nina akili timamu na kitu hiki kimetokea. Na ndio sababu nauliza. Kama huna la kusema kaa kimya. Kama wewe ni meneja wa kiwanda hicho ni PM nikwambie soda hiyo ilipo na nikudai fidia mjinga wewe.
 
mkuu .... nahisi hii ni photo shop ... photographic illusions
 
Back
Top Bottom