Jaji Ramadhani tafadhali bwana! Ama unasema kweli au la...

Hii haina tofauti na maamuzi ya Magu kuukataa sasa mradi wa Bagamoyo wakati alipokuwa waziri hakuupinga na kama aliupinga kwenye baraza la mawaziri lakini hakujiuzulu bali aliunga mkono maamuzi ya wenzake kwahiyo hana tofauti na Jaji huyu mstaafu.
Ni tofauti kabisa kama anga na bahari. Sema tu chuki na hasira yako kwa Magufuli inakufanya utafute kila sababu umchague Rais. Wewe tulia na uzoee. Magufuli ni Rais wetu mpaka 2025!
 
Siyo suala la kutaka ni suala la italiana. Ukiwaondoa na kuwaweka wasiokuwa wanachama wa chama chochote unajuaje unaowaweka hawana mapenzi au ushabiki wa chama chochote?
Kuna mambo usiyoyajua au umeamua kuwa mtetezi wa dhuluma.

Hapo zamani, upendeleo kwa CCM na maagizo ya kuwanyang'anya ushindi vyama vya upinzani, ilifanyika kwa siri lakini kwa awamu hii upendeleo unafanyika kwa uwazi kwa maagizo ya kiongozi wetu, tena kwa vitisho na kwa kukiuka sheria na katiba.

Kuna wakati kiongozi wetu aliwatangazia wateule kwa nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri, akisema, 'safari hii nimewateua wakurugenzi wengi makada wa chama ili wakasimamie ilani ya chama'. Anaongea hayo kwa uwazi huku akijua kabisa kuwa nafasi ya ukurugenzi imeelezwa wazi kwenye miongozo ya Utumishi wa umma, ni nani mwenye sifa ya kuwepo kwenye nafaai hiyo. Yeye anawateua watu toka ofisi za Lumumba, watu ambao hawajawahi kuwa watumishi wa umma, wakati nafasi hiyo kwa kadiri ya mwongozo wa utumishi wa umma inastahili kushikwa na mteule toka kwenye kundi la wafanyakazi wa umma waliofikia ngazi fulani tu.

Pili, usichokijua MMK ni kuwa tatizo kubwa ni kiongozi wetu, mbaye anateua wakurugenzi kwa kuwapa maelekezo kuwa wakapokonye haki za wananchi wakati wa uchaguzi.

Tatizo kubwa lipo kwa anayewateua wakurugenzi. Kwa sasa, mkurugenzi akiamua kutenda haki, na haki hiyo ikampa ushindi mpinzani, mkurugenzi huyo ajue hana kazi. Tuna kiongozi ambaye anafurahia unyang'anyi wa haki za raia japo kwa unafiki anatuhadaa kuwa anapenda haki.

Huku tukipiga hatua taratibu, tuendelee kumwomba Mungu azidi kuwadhalilisha na kuwaonesha kweli yake, wale wapokonya haki na mawakala wao. Taratibu tunapiga hatua, na kuna siku mavazi na picha zao wasiotenda haki, zitawekwa kwenye makumbusho kama kumbukumbu mbaya watu waliojitahidi sana kudhulumu haki za Raia.
 
Mh Jaji yuko sahihi. Unapogundua kosa, haijalishi umelifanya kwa masaa, siku, wiki, miezi au miaka mingapi! Nafasi ya kujisahihisha ikipatikana fanya hivyo. Kwa wkt huo huwezi jua ni mazingira gani yalimkumba akashindwa. Kuna mambo huwezi badilisha kwenye mfumo kama huna '' money power, people's power (influence) au political power ''
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wakati mwingine unaweza kujisikia kizunguzungu ukiwasikiliza viongozi wetu ambao sasa wanaonekana “wanajua”. Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani amenukuliwa na gazeti moja akionesha kuunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu kutangaza kuwa mfumo unaowaweka viongozi au wanachama wa chama tawala kama wasimamizi wa uchaguzi ni kinyume na Katiba. Amedai kuwa tangu 1995 (akiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi) walitoa mapendekezo ya kuondoa utaratibu huo. Lakini kwa miaka ishirini hilo halijatokea hadi hivi sasa.

Jambo ambalo linanitibua mimi zaidi ni kuwa Jaji huyu huyu ambaye anadai kuwa wana viongozi na mashabiki wa vyama vya siasa wasijiwekwe kusimamia uchaguzi alijitokeza 2015 akiwa amevaa magwanda ya CCM akitaka kugombea Urais chini ya mfumo ule ule ambao anadai wao hawakuupenda! Mfumo ambao anataka tuamini kuwa aliona hautakuwa wa haki (fair) kwa vyama vingine?

Sasa Jaji Ramadhani tafadhali bwana; hivi kama kweli ulijua kuwa mfumo huu ni mbaya kilichokufanya usimame na kutaka kugombea Urais kwa tiketi ya CCM ilikuwa ni nini? Unataka tuamini kuwa mapenzi yako kwa CCM yalikuja baada ya kuwa umeondoka Ujaji Mkuu? Je, haiwezekani kuwa kumbe mwenzetu tangu miaka “ile ya nineteen kweusi” ulikuwa ni mwanachama na shabiki wa CCM? Kwamba ulipokuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulikuwa tayari na “mahaba” na chama tawala?

Kama hili ni kweli basi kuna mambo mawili; kwamba, unaamini kuwa kwa wewe kuwa na mapenzi au uanachama wa Chama cha Mapinduzi hakukufanya uvunje uadilifu wako wa kusimamia taratibu au sheria bila kujali mgombea anatoka chama gani. Kwamba, kama Augustino Mrema angeshinda mwaka 1995 wewe na wenzako mlikuwa tayari kumtangaza mshindi hata kama CCM ingeondoka madarakani? Je hili ni kweli?

Kama hili ni kweli unataka tuamini kuwa mwanachama wa chama cha siasa akisimamia na kuzingatia viapo vyake, maadili ya kazi, sheria na haki anaweza kusimamia uchaguzi bila kupendelea chama chake. Kwamba, ndio maana wapo wabunge wa vyama vya upinzani ambao wameshinda na kurudia kushinda kwenye majimbo yao licha ya wasimamizi wa majimbo hayo kuwa ama ni wanachama wa chama tawala au mashabiki wa chama hicho.
Jambo la pili ni kuwa kama hilo la kwanza si kweli basi ni wazi kuwa hukuwa mwadilifu na kuwa ulikuwa unafanya kazi kwa upendeleo ukiongozwa na mahaba kwa chama chako. Kwamba, kwa vile tunajua sasa kuwa wewe ulikuwa ni mwana CCM ulikuwa unafanya kazi kwa kificho kumbe moyoni ulikuwa na chama unachokipendelea kishinde.

Kama hili la pili ni kweli basi hoja yako ya kuwaondoa mashabiki na wanachama (walijionesha wazi) wa CCM kwenye kusimamia uchaguzi ni jambo la msingi, la lazima na ambalo haliepukiki. Hii ina maana kuwa siyo wana CCM tu bali Watanzania wote wanapaswa kushuku kila wakati na mara zote unapofanyika uchaguzi pale ambapo wasimamizi wa uchaguzi bado ni wana CCM. Kwamba, WAtanznaia na hasa wapinzani wasidhanie hata kwa mbali kuwa wakurugenzi hawa wa uchaguzi wanaweza kutenda haki.

Nikiangalia yote mawili naamini tatizo letu kubwa haliko kwenye uanachama wa wakurugenzi wa uchaguzi au watendaji wengine. Hii ni kwa sababu huwezi kuondoa mapenzi ya mtu kwa chama Fulani hata kama mtu huyo hatovaa gwanda hilo wakati akiwa kazini. Tatizo letu ni kutokuwa na mfumo ambao uko wazi, unaoneshimika na kila mtu na ambao kila mtu anaweza kuuamini kumtendea haki. Inapotokea kwamba wapinzani wanalazimika “kulinda kura” kwa kuhofia kuibiwa ni wazi kuwa mfumo hauko sawa na hauaminiki.

Badala ya kuhangaika na “uanachama” wa Wakurugenzi wa Uchaguzi naomba kupendekeza kwa heshima na taadhima tuangalia uadilifu wa watendaji – ikiwemo kuweka adhabu kubwa kwa mkurugenzi ambaye anaonekana kuharibu uchaguzi kwa sababu za kisiasa. Ni lazima tuangalie mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kuwa wapinzani wanapata haki ile ile wanayopewa CCM. Haiwezekani wapinzani wanalazimika kutumia nguvu kubwa kweli hata kurudisha fomu za kugombea wakati CCM inaonekana wana mlango wao mwingine maalum.

Nitatoa mfano, Rais Magufuli alipozungumza (labda kwa utani au akimaanisha) kuwa yeye anateua wakurugenzi wa halmashauri halafu ati waje kumtangaza mgombea wa upinzani kashinda. Tulitarajia Tume ya Uchaguzi ingesimama na kutetea nafasi yake na kuwataka watendaji wake kutekekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na siyo matakwa ya siasa. Kama Rais Magufuli atawafukuza kazi wakurugenzi wa halmashauri kwa sababu wamemtangaza mpinzani hii ni haki na wajibu wake.

Ndio maana niliposoma habari ya kauli yako hii nimebakia kusema “Jaji Ramadhani, tafadhali bwana!”

Niandikie:mwanakijiji@jamiiforums.com
Puppet on a string...

Kwikwikwikwiii
 
Hii haina tofauti na maamuzi ya Magu kuukataa sasa mradi wa Bagamoyo wakati alipokuwa waziri hakuupinga na kama aliupinga kwenye baraza la mawaziri lakini hakujiuzulu bali aliunga mkono maamuzi ya wenzake kwahiyo hana tofauti na Jaji huyu mstaafu.
Umelenga patamu sana,sijui atakujibu nini hapo!!!!
 
Unajua ndugu hawa wazee wetu umri umekwenda,wanatakiwa kua makini sana katika kauli zao,muda mwingine unakwepa kwanza kuongea ili utafakari.

Wanasahau watanzania ni makini sana kufuatilia nyendo zao
Tujadili hoja yake.
 
Haki au Kweli haina rangi, taifa, kabila, jamii, jinsia, chama cha siasa au kundi lolote lenye mshikamano fulani.
 
Nisomapo mabandiko marefu hivi, ambayo mwanzo wake tu yananionyesha kuyapinga huwa napata taabu sana kutuliza akili yangu isiyumbe na kuwa na uvumilivu wa kusoma hadi mwisho wa maandiko.

Kwa bahati nzuri nimevuta subira kweli mpaka nilipofikia sehemu niliyokubaliana na mleta mada; hasa kwenye 'mapendekezo' ya kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha wasimamizi wanatenda haki kila mara wanaposimamia uchaguzi. Na kwamba adhabu kali itolewe kwa yeyote anayebainika kupindisha matakwa ya wapiga kura.

Sasa huo utani? wa kuwaamuru watu unaowateua! Huo uwe utani!

Hapa ndipo dharau ya watu tuliowaheshimu sana kwa misimamo ilipoanzia, haijulikani ni kitu gani kilichoingia ndani ya ubongo wao na kuukoroga kama uji.

Unapokuwa shabiki au mwanachama wa chama, halafu uwe refa wa kusimamia haki kati ya mwanachama mwenzako na mpinzani, hili halileti maana yoyote, hasa katika mazingira haya tuliyonayo sasa.

Tunazungumzia chama kilichopo kwenye madaraka, na mara baada ya uchaguzi huo, hata hao mashabiki na wanachama waliosimamia uchaguzi wanategemea teuzi za juu zaidi ili waendelee kuneemeka! Kwa nini hili watu (hasa hao walioko CCM na wanaofaidika na chama kama hicho wanaung'ang'ania... sababu ni hiyo hiyo moja, kwa sababu wanafaidika na mpango huo.

Sasa tunaona baadhi ya watu, hata kama hawashabikii chama, lakini wanashabikia mtu, hadi kumwona matamshi yake ya utata kuwa ni utani?

Nadhani mwisho nimalizie tu kwa kusema hili moja. Kama huko CCM kweli bado kuna watu wanaoamini kwa dhati ya mioyo yao kwamba kuna chama kinachosimamia hatma ya taifa hili; hao watu ni wa kuwahesabu, na huenda hata vidole vya mikono miwili huvimalizi. CCM ni ya wapigaji; ni ya maslahi. Hata hao akina Augustino ni maslahi zaidi ndiyo waliyoyaweka mbele.
Kwa hiyo kama hawakutokea kupinga anayoyahoji mwandishi, asijifanye hilo halijui.

Kati ya hao wachache waliobaki huko ni akina Mzee Sinde Warioba, ambaye naye imemlazimu sasa anyamaze na kubaki kuwa mtazamaji na kuogopa kutia mchanga kwenye kitumbua cha kijana. Hayo ndio maadili yaliyobaki huko CCM.

Na Tanzania ya watu zaidi ya milioni hamsini, Tume iliyo huru kweli itashindwa kabisa kuwapata watu wachache tu wa kusimamia uchaguzi mpaka ilazimu wawe makada wa chama waliojitambulisha?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wakati mwingine unaweza kujisikia kizunguzungu ukiwasikiliza viongozi wetu ambao sasa wanaonekana “wanajua”. Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani amenukuliwa na gazeti moja akionesha kuunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu kutangaza kuwa mfumo unaowaweka viongozi au wanachama wa chama tawala kama wasimamizi wa uchaguzi ni kinyume na Katiba. Amedai kuwa tangu 1995 (akiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi) walitoa mapendekezo ya kuondoa utaratibu huo. Lakini kwa miaka ishirini hilo halijatokea hadi hivi sasa.

Jambo ambalo linanitibua mimi zaidi ni kuwa Jaji huyu huyu ambaye anadai kuwa wana viongozi na mashabiki wa vyama vya siasa wasijiwekwe kusimamia uchaguzi alijitokeza 2015 akiwa amevaa magwanda ya CCM akitaka kugombea Urais chini ya mfumo ule ule ambao anadai wao hawakuupenda! Mfumo ambao anataka tuamini kuwa aliona hautakuwa wa haki (fair) kwa vyama vingine?

Sasa Jaji Ramadhani tafadhali bwana; hivi kama kweli ulijua kuwa mfumo huu ni mbaya kilichokufanya usimame na kutaka kugombea Urais kwa tiketi ya CCM ilikuwa ni nini? Unataka tuamini kuwa mapenzi yako kwa CCM yalikuja baada ya kuwa umeondoka Ujaji Mkuu? Je, haiwezekani kuwa kumbe mwenzetu tangu miaka “ile ya nineteen kweusi” ulikuwa ni mwanachama na shabiki wa CCM? Kwamba ulipokuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulikuwa tayari na “mahaba” na chama tawala?

Kama hili ni kweli basi kuna mambo mawili; kwamba, unaamini kuwa kwa wewe kuwa na mapenzi au uanachama wa Chama cha Mapinduzi hakukufanya uvunje uadilifu wako wa kusimamia taratibu au sheria bila kujali mgombea anatoka chama gani. Kwamba, kama Augustino Mrema angeshinda mwaka 1995 wewe na wenzako mlikuwa tayari kumtangaza mshindi hata kama CCM ingeondoka madarakani? Je hili ni kweli?

Kama hili ni kweli unataka tuamini kuwa mwanachama wa chama cha siasa akisimamia na kuzingatia viapo vyake, maadili ya kazi, sheria na haki anaweza kusimamia uchaguzi bila kupendelea chama chake. Kwamba, ndio maana wapo wabunge wa vyama vya upinzani ambao wameshinda na kurudia kushinda kwenye majimbo yao licha ya wasimamizi wa majimbo hayo kuwa ama ni wanachama wa chama tawala au mashabiki wa chama hicho.
Jambo la pili ni kuwa kama hilo la kwanza si kweli basi ni wazi kuwa hukuwa mwadilifu na kuwa ulikuwa unafanya kazi kwa upendeleo ukiongozwa na mahaba kwa chama chako. Kwamba, kwa vile tunajua sasa kuwa wewe ulikuwa ni mwana CCM ulikuwa unafanya kazi kwa kificho kumbe moyoni ulikuwa na chama unachokipendelea kishinde.

Kama hili la pili ni kweli basi hoja yako ya kuwaondoa mashabiki na wanachama (walijionesha wazi) wa CCM kwenye kusimamia uchaguzi ni jambo la msingi, la lazima na ambalo haliepukiki. Hii ina maana kuwa siyo wana CCM tu bali Watanzania wote wanapaswa kushuku kila wakati na mara zote unapofanyika uchaguzi pale ambapo wasimamizi wa uchaguzi bado ni wana CCM. Kwamba, WAtanznaia na hasa wapinzani wasidhanie hata kwa mbali kuwa wakurugenzi hawa wa uchaguzi wanaweza kutenda haki.

Nikiangalia yote mawili naamini tatizo letu kubwa haliko kwenye uanachama wa wakurugenzi wa uchaguzi au watendaji wengine. Hii ni kwa sababu huwezi kuondoa mapenzi ya mtu kwa chama Fulani hata kama mtu huyo hatovaa gwanda hilo wakati akiwa kazini. Tatizo letu ni kutokuwa na mfumo ambao uko wazi, unaoneshimika na kila mtu na ambao kila mtu anaweza kuuamini kumtendea haki. Inapotokea kwamba wapinzani wanalazimika “kulinda kura” kwa kuhofia kuibiwa ni wazi kuwa mfumo hauko sawa na hauaminiki.

Badala ya kuhangaika na “uanachama” wa Wakurugenzi wa Uchaguzi naomba kupendekeza kwa heshima na taadhima tuangalia uadilifu wa watendaji – ikiwemo kuweka adhabu kubwa kwa mkurugenzi ambaye anaonekana kuharibu uchaguzi kwa sababu za kisiasa. Ni lazima tuangalie mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kuwa wapinzani wanapata haki ile ile wanayopewa CCM. Haiwezekani wapinzani wanalazimika kutumia nguvu kubwa kweli hata kurudisha fomu za kugombea wakati CCM inaonekana wana mlango wao mwingine maalum.

Nitatoa mfano, Rais Magufuli alipozungumza (labda kwa utani au akimaanisha) kuwa yeye anateua wakurugenzi wa halmashauri halafu ati waje kumtangaza mgombea wa upinzani kashinda. Tulitarajia Tume ya Uchaguzi ingesimama na kutetea nafasi yake na kuwataka watendaji wake kutekekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na siyo matakwa ya siasa. Kama Rais Magufuli atawafukuza kazi wakurugenzi wa halmashauri kwa sababu wamemtangaza mpinzani hii ni haki na wajibu wake.

Ndio maana niliposoma habari ya kauli yako hii nimebakia kusema “Jaji Ramadhani, tafadhali bwana!”

Niandikie:mwanakijiji@jamiiforums.com
Kuna siku huyu pamoja na majaji wastaafu wenzake walialikwa ikulu kuongea na Mh Rais.
JPM aliwapa nafasi ya kumshauri kuhusu jambo lolote.
Mbona hakusema lolote kuhusu wakurugenzi kusimamia Uchaguzi Mkuu na chaguzi nyingine?
 
Kishatafuna pesa za watu huyo kwa hiyo lazima zimtokee tundu lolote lile. Ndiyo sababu anakuja hapa kuandika upuuzi wake ili kumfurahisha master wake. Ukiwa na tamaa ya pesa za haraka haraka matokeo yake ndiyo kama haya. Unapoteza reputation na credibility.
Inabidi nami nikubaliane na dhana hii. Katika mkondo ule ule uliompata Dr Mhogo, huyu naye alichukua kitu; akauza utu wake.

Inashangaza sana, hasa katika yale aliyokuwa akiyaelezea kuhusu Mwalimu Nyerere na misimamo aliyokuwa nayo, ya kutetea alicho kiamini bila ya kuteteleka. Hasa inapohusu haki za wanyonge na watu wanaoonewa.
 
Siyo suala la kutaka ni suala la italiana. Ukiwaondoa na kuwaweka wasiokuwa wanachama wa chama chochote unajuaje unaowaweka hawana mapenzi au ushabiki wa chama chochote?
Wataangaliwa historia yao. Mfano sio wanachama wa chama chochote for the past five years. Hii isimamiwe na sheria na mtu anaapa, kinyume chake anaadhibiwa vikali. Tuko mil 50+, kupata watu 200 wasimamizi wa uchaguzi ambao ushahidi unaonyesha sio wanachama yawezekana.
 
Tatizo kubwa lipo kwa anayewateua wakurugenzi. Kwa sasa, mkurugenzi akiamua kutenda haki, na haki hiyo ikampa ushindi mpinzani, mkurugenzi huyo ajue hana kazi. Tuna kiongozi ambaye anafurahia unyang'anyi wa haki za raia japo kwa unafiki anatuhadaa kuwa anapenda haki.
MUNGU WA MBINGUNI ANAYAONA HAYA
 
Jambo ambalo linanitibua mimi zaidi ni kuwa Jaji huyu huyu ambaye anadai kuwa wana viongozi na mashabiki wa vyama vya siasa wasijiwekwe kusimamia uchaguzi alijitokeza 2015 akiwa amevaa magwanda ya CCM akitaka kugombea Urais chini ya mfumo ule ule ambao anadai wao hawakuupenda! Mfumo ambao anataka tuamini kuwa aliona hautakuwa wa haki (fair) kwa vyama vingine?

Sasa Jaji Ramadhani tafadhali bwana; hivi kama kweli ulijua kuwa mfumo huu ni mbaya kilichokufanya usimame na kutaka kugombea Urais kwa tiketi ya CCM ilikuwa ni nini? Unataka tuamini kuwa mapenzi yako kwa CCM yalikuja baada ya kuwa umeondoka Ujaji Mkuu? Je, haiwezekani kuwa kumbe mwenzetu tangu miaka “ile ya nineteen kweusi” ulikuwa ni mwanachama na shabiki wa CCM? Kwamba ulipokuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulikuwa tayari na “mahaba” na chama tawala?

Kama hili ni kweli basi kuna mambo mawili; kwamba, unaamini kuwa kwa wewe kuwa na mapenzi au uanachama wa Chama cha Mapinduzi hakukufanya uvunje uadilifu wako wa kusimamia taratibu au sheria bila kujali mgombea anatoka chama gani. Kwamba, kama Augustino Mrema angeshinda mwaka 1995 wewe na wenzako mlikuwa tayari kumtangaza mshindi hata kama CCM ingeondoka madarakani? Je hili ni kweli?
...... matatizo yenyewe ndiyo hayo; sizitaki mbichi hizi
 
Hahahaa. What a weak argument. Kwenye utawala wowote wa kiimla usitegeee wanaomtumikia mtawala watafanya maamuzi au kutenda kwa utashi wao. Mtu anateuliwa kwa kuambiwa na mtawala wake kwamba asipofanya X basi Y itamtokea, halafu unaleta hoja mufilisi kwamba maadili binafsi ya watumishi wa umma ndo kigezo kinachoamua kama watafanya ufisadi wa kisiasa au hawatafanya. Unaishi kwenye pango gani Mzee ambapo hata mambo rahisi yanayoendelea ulimwenguni huwezi kuyaelewa?
 
Back
Top Bottom