Akumbushwe tena kuwa kifungu cha katiba namba 41 kinataka raisi awe amechaguliwa na kushinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa (kulingana na version ya kiingereza ya hiyo katiba). Tuna ushahidi wa kutosha kuwa Kikwete hakupata idadi hiyo ya kura kwa hiyo hakuchaguliwa kwa mujibu wa katiba, hivyo yeye siyo rais halali wa jamhuri ya Tanzania.
Uchaguzi wa Rais hauna uhusiano wowote na uchaguzi wa wabunge ingawa wote wanachaguliwa siku moja. Uchaguzi wa wabunge unatawaliwa na vifungu vya katiba namba 77 hadi 79 wakati uchaguzi wa raisi unatawaliwa na kifungu 41. Kwa hiyo tunaweza kuwatambua wabunge bila kumtambua rais na kusiwe na tatizo lolote.
Kumbe uwezo wa Bomani katika kutafsiri sheria ni sifuri kweli kweli, inatia shaka sana kwenye umakini wa mashauri aliyoamua wakati wakiwa jaji; inawezekana ndiyo maana tuna majaji wanashindwa kuamua kesi za muhimu kama ile ya mgombea huru kwa sababu uwezo wao wa kuchambua sheria ni kama ulivyo wa JAJI bomani. Nina wasi wasi wanazidiwa hata na walimu wa ngumbaru kabisa watu hawa.
Asante......clearly put!