Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,785
Tuweke record sawa hapa. Kwanza kuhusu upitishwaji wa jina la Waziri Mkuu. Wabunge wa CHADEMA walikuwa wanatuma salamu kwa Anna Makinda kwamba akae chonjo, wapo makini katika kuzingatia kanuni na taratibu za bunge, ambazo watazifuata katika kupigania kile kilichowaleta pale bungeni: maslahi ya wananchi na taifa kwa kujumla. nilivyoona katika TV jinsi mijadala ilivyoendelea, CHADEMA ilitimiza lengo lake kwa hali ya juu kabisa. mfano ule utaratibu wa kupitisha mtu anayegombea nafasi katika bunge bila kumuuliza maswali ya msingi, ulionekana kupitwa na wakati. ilichekesha pale Tundu Lissu alipotumia nafasi ya kuuliza maswali mbunge anayegombea kuwakilisha bunge letu katika bunge la SADCC, na akamuuliza swali dogo tu ni nini kirefu cha SADCC. mgombea huyo ambaye awali alipoeleza cv yake alionesha jinsi alivyoshugulika saaana na mambo ya SADCC. lakini alishindwa kueleza kirefu cha SADCC!! hii inaonesha ugonjwa mkubwa sana kwamba mtu anagombea katika jambo ambalo hata hajalifanyia kazi na kulielewa sawasawa.
kwa hiyo basi, uhakiki wao wa taratibu zinazotumika pale bungeni ni halali kabisa kufanya katika mazingira yoyote yale.
pili, CHADEMA wanayo haki ya kuamua jinsi watakavyofanya protest yao. kwa kuwa sheria ni kandamizi, kwamba huruhusiwi kupinga uteuzi wa rais akishatangazwa na tume, ni juu ya chama chochote kuamua kitumie mbinu gani mbadala. hii ni mbinu ya political pressure, ambayo ilimgusa waziri mkuu mteule Pinda, kama uliangalia runinga wakati anatoa neno la shukrani. hilo ndio lilikuwa jambo la kwanza kulizungumzia, jinsi CHADEMA walivyomweka pembeni, akakumbuka bunge lililopita walivyomuunga mkono. hata wakati wa kumpitisha wakati anateuliwa kujaza nafasi ya Lowasa, za kumpinga zilikuwa ni chache zaidi kulinganisha na za sasa. unaweza kusema, japo kura ni za siri, kwamba CHADEMA hawakumpa kura zao. ni kweli haina impact kubwa kwa upande mmoja, lakini the mere fact kwamba inazungumziwa katika duru mbalimbali, na ni mara ya kwanza kutokea kwa msisitizo mkali namna hii katika siasa za Tanzania, ni dalili kwamba ina impact tayari!! protest imefanyika na imeshafanikiwa. suala la wizi wa kura hasa za urais bado litakuwa katika ajenda mbalimbali kitaifa na kimataifa. hata hapa jf bado ni mada moto. mission accomplished!!
unasahu rais huwa anaunda tume za hawa wabunge? si unakumbuka ile ya madini,
acha siasa, anachosema Kiranga ni cha kawaida kabisa kwa akili ya kawaida na siyo kuleta philosophical arguments ambazo hazileti tija wala kubadilisha hoja.Learn from cuf walivyosusia baraza la wawakilishi.
Hii issue imekaa vibaya kuliko kawaida, is this a return to people who voted for chadema? can you heal their wounds just by talking ambiguos things?
maslahi matamu, bunge tamu ebo!!!!