Jaji Mkuu wa Tanzania awashukuru wananchi kwa fedha za kukamilisha majengo ya Mahakama Mwanga na Same

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma anazungumza kwenye Uzinduzi wa Majengo ya Mahakama za Wilaya ya Mwanga na Same leo Novemba 15, 2022




Nurdin Hassan Babu - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro
Haki siyo lazima upate wewe tu, hata mwenzako akipata haki na wewe unapaswa kukubali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba na Sheria - Dkt. Joseph Kizito Mhagama
Ushauri kwa Jaji Mkuu;
1) Kutoa mamlaka katika Mahakama za Wilaya hasa katika maeneo ambayo hakuna Mabaraza ya Ardhi ya wilaya waweze pia kushughulikia migogoro na mashauri yanayohusiana na ardhi, ili kuwapunguzia gharama wanaosafari umbali mrefu kupara huduma hizo.

2) Ili kuongeza tija kwenye maombi ya kupata Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni vyema ofisi hii ikawa pamoja na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi ya TAKUKURU kufanya kazi pamoja na kwa ukaribu ili kumsaidia Rais pamoja na Jaji Mkuu katika huduma muhimu ya utoaji haki.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania - Prof. Olisante Ole Gabriel

- Jengo lililozinduliwa leo kwaajili ya Mahakama ya Mwanga na Same kati ya majengo sita yanayojengwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 yamejengwa kwa fedha za ndani, jengo la Mwanga limegharimu Tsh milion 726.9 na jengo la Same limegharimu Tsh milioni 740.7.

Jaji Mkuu wa Tanzania - Prof. Ibrahim Hamis Juma

- Mihimili ya dola ina wajibu wa kuwasogezea huduma za utoaji haki, ikiwa ni pamoja na mhimili wa Bunge na Serikali.

- Kipimo cha utoaji haki huwa tanaangalia maswali ambayo wabunge huwa wanayauliza, na dukuduku mbalimbali ambazo wabunge huwa wanayatoa na maswali hivi karibuni yamekuwa ni kuomba majengo ya Mahakama, malalamiko katika maene mengine ya maadili ya mahakama yamepungua sana.

- Kukamilika kwa majengo ya Mahakama ya wilaya ya Same, Mwanga na kwengine ambako majengo yao yatafunguliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu ni kielelezo cha mpango mkakati wa mahakama na mpango wa ujenzi ambao Mahakama imejiwekea na kuutekeleza kwa ukamilifu kwa msaada wa serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania

- Matumizi ya TEHAMA yatumike katika kuwasaidia wananchi kupata haki kwa urahisi zaidi.

- Mwananchi una haki ya kudai huduma iliyobora, kama unaona kuna huduma inalegalega kuna namba za simu za kupiga moja kwa moja Makao Makuu, masaa ishirini na changamoto yako itatuliwa mara moja - 0752 500 400.

- Hatutegemei haki itakayopatikana katika majengo haya itakuwa haki iliyocheleweshwa, inayotokana na mrundikano wa mashauri, kuhairishwa kwa mashauri kila mara au kuwa dalili zozote za rushwa au utovu wa maadili. Tumekupa nyenzo ya kuhakikisha lalamiko lako linasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi mara moja.

- Karne ya 21 ni karne ya TEHAMA ambayo inategemea sana upatikanaji wa taarifa muhimu, huduma za mahakama siyo kusilikiliza mashauri tu, ni kutoa taarifa mjuhimu kumuwezesha mwananchi kufanya maamuzi yake akiwa na taaarifa za kutosha kuhusu maswala mbalimbali, kwahiyo majengo haya yawe ni sehemu ya elimu ya Mahakama na elimu ya sheria kwa umma.

- Mageuzi ambayo yanatokea Duniani ya kuifanya Dunia kuwa ya kidigitali sisi ni sehemu ya mabadiliko hayo, tujitayarishe kuendana na mabadiliko haya katika zama ambazo mwananchi utajitafutia taarifa wewe mwenyewe na utaweza wewe mwenyewe kuendesha mashauri yako bila hata ya kutegemea mawakili.
 
Huyu jaji mkuu tangu ajitokeze kuongelea issue ya Lissu kupigwa risasi nilimshangaa Sana.

Jaji Mkuu anaonesha upande, Tena akaonesha hayupo upande wa Lissu Bali waliomshambulia.

Tangu siku hiyo nikajua tuna jaji mkuu wa mchongo au pazia.
 
Kwa mfumo wetu ulivyo Jaji Mkuu ni mtu mdogo saana, hana mamlaka yoyote zaidi tu ya jina la cheo chake kuwa kubwa.
 
Huyu jaji mkuu tangu ajitokeze kuongelea issue ya Lissu kupigwa risasi nilimshangaa Sana. Jaji mkuu anaonesha upande, Tena akaonesha hayupo upande wa Lissu Bali waliomshambulia. Tangu siku hiyo nikajua tuna jaji mkuu wa mchongo au pazia.
Hakuna CJ, ni bure kabisa!
 
Back
Top Bottom