Jaji kiongozi Fakh Jundu amjibu Lissu kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mahakama Bungeni

hebu wana sheria tujuze juu ya hili janga. hii si itapelekea kesi au mashauri mazito ya kikatiba.itapelekea kutengua hukumu zote zilizo hukumiwa na majaji wasio na sifa hata ikiwa kwa miaka ishirini ijayo. natabiri hili jambo halitamwacha salama " JK" wakati huo akiwa rais msitaafu
 
Tumechoka na hii tabia ya kuwapa watu mikataba baada ya kustaafu. Waende wakapumzike
 
"Hoja kama hizi, zinapotolewa bungeni, hatuna namna ya kujitetea, tumenyamaza kimya kwa sababu habari za bungeni tutamjibu nani, wataendelea kuchafua majina yetu, lakini wenye akili watajua.

"Hatutaki majibizano yasiyo na faida, sijui yalizungumzwa hayo kwa kumlenga Rais au majaji, Bunge halina ubavu wa kujadili mahakama wala majaji kwa majina, kwa sababu hatuna nafasi ya kujitetea," alisema Jaji Jundu.

Toa Maoni yako kwa habari hii

Jamani ngoja mimi nifafanue understanding yangu jinsi huyu Jaji Fakhi Jundu alivyouvaa mtego wa Tundu Lissu. Ili kunielewa naomba mkazie kwenye statement niliyoweka hapo juu na hasa kwenye RED.

Ukisoma RED zote mbili ni kweli kabisa bunge halina mamlaka kujadili majaji kwa kuwataja majina. Hivyo ni kweli kabisa Jaji huyu anachokisema, hakupaswa kutajwa kabisa.

Lakini kitaalamu, huyu Jaji ndiye kaingia mtegoni kwa kuanzisha mjadala wa yeye kutajwa bungeni. Najua hoja zangu wengi hukurupuka kunipinga kama walivyokurupuka nilipoongelea mpaka wa Malawi. Na hadi hapa najua nikikomea hapa mtanipinga hadi asubuhi ninaposema Jaji huyu ndiye kalianzisha na wala si Tundu Lissu.

Watakaosema kuwa kalianzisha Tundu Lissu watasema kama Jaji huyu kwamba Tundu Lissu kaliongelea Bungeni. Wote hao na huyu Jaji wanakosea na mimi ninafafanua kama ifuatavyo.

Bunge ni nini? Bunge ni mkutano unaokaa huku Spika akiwa amevaa joho lake na lile lifimbo la askari anayewatimuaga CHADEMA likiwa limekaa mezani. Hivyo kinachozungumzwa Bungeni kinazungumzwa lile lifimbo likiwepo na kikishazungumzwa kinatunzwa kwenye kumbukumbu iitwayo Hansard.

Je, Tundu Lissu alifanyaje? Siku ya kuwasilisha mawazo ya Kambi ya Upinzani ndipo Tundu Lissu alipotumia mwanya huo kueleza udhaifu wa uteuzi katika mahakama. Ukweli si udhaifu huu tu bali udhaifu mwingi ili bunge lifanye uwezo wake serikali iurekebishe. Udhaifu si bajeti finyu tu kwa mahakama. Mwaka jana mnakumbuka jengo la mahakama kuhamishwa ndiyo ilikuwa issue. Mwaka huu zikawepo zingine na hili la udhaifu wa majaji likawa mojawapo.

Kama mnakumbuka baada ya Tundu Lissu kusoma mawazo yale mjadala ukawa mkubwa kwamba mahakama imedharauriwa. Justice Werema alidiriki kusema atamfungulia mashtaka Tundu Lissu. Mimi nina uelewa mkubwa tu kwamba kinachozungumzwa Bungeni kina haki ya kushtakiwa japo wengi wakiwemo wabunge hudanganyika na kudhani kwamba kinga inawafanya mle bungeni wasishtakiwe. Ni refu hili na silijadili zaidi. Lakini Jaji Werema yuko sahihi kama kweli ataamua kumshitaki Tundu Lissu. Narudia ana haki kumshtaki lakini sisemi kuwa Tundu Lissu ana makosa.

Lakini cha msingi kuliko vyote ninachotaka mjue au mkumbuke ni kwamba siku hiyo Tundu Lissu hakumtaja Jaji hata mmoja kuthibitisha udhaifu aliousema. Na hiki ndicho kilichoingia kwenye hansard. Kwa maana hiyo ukipekua kumbukumbu za bunge hutakuta hata nukta inamtaja jaji yoyote wa Tanzania aliyetajwa na Tundu Lissu. Mnaoelewa haraka, hadi hapa mmeshaona ninakoelekea. Ambao hamjaelewa tuendelee na maelezo.

Kilichofuata baadaye ni kiti cha Spika kuamua kwamba suala la Tundu Lissu kuwadharirisha majaji lipelekwe kwenye Kamati nadhani kamati ya Maadili. Kilichotokea ni kwamba Kamati ikakaa na ikamtaka Tundu Lissu awasilishe uthibitisho kwenye Kamati.

Tundu Lissu akawasilisha utetezi wake kwenye Kamati na kama kawaida kwenye nchi hi sasa hivi iliyojaa uwazi na ukweli kopi ya utetezi wake ikatua magazetini na huku mitandaoni.

Tumesoma wote kuwa huyu jaji na wengine tele walitajwa na Tundu Lissu. Lakini tujiulize maswali ya kutufunulia uelewa. Je, Tundu Lissu amemtaja huyu na wenzake Bungeni au mtaani?

Hakika hadi sasa Tundu Lissu hajamtaja Jaji yeyote Bungeni. Kamati ya Bunge si Bunge. Tundu Lissu kawasilisha utetezi kwenye Kamati hakuwasilisha Bungeni. Kwenye Kamati hakuna lile lifimbo. Kuna mwenyekiti wa Kamati na wajumbe wachache sana. Ikibidi hata huyu Jaji anaweza kuitwa na Kamati ile ili kujieleza alivyotuhumiwa.

Hivyo unaposema kwamba mambo haya yamezungumzwa Bungeni ukweli ni kwamba unajidhihirisha ulivyo dhaifu kupambanua mambo. Ukisikia kwamba umedharirishwa Bungeni basi tafuta hansard ya siku hiyo kuthibitisha. Hivyo, huyu Jaji hawezi kuthibitisha kuwa ni hansard ya lini iliyomtaja jina lake kupitia kwa Tundu Lissu.

Hivyo, hadi hapa mtakubaliana nami kwamba huyu Jaji ni dhaifu na kauthibitisha udhaifu wake kwa kuliparamia hili swala la Tundu Lissu. Mimi si mwanasheria lakini ninaelewa na aliyenisoma ameelewa kwamba Tundu Lissu hajamtaja jaji yeyote kwa jina. Ni uelewa finyu wa Jaji huyu.

Hata hivyo ili jambo litambulike kuwa limefikishwa Bungeni ni pale linapokuwa limewasilishwa kwenye meza ya Spika mbele ya wabunge. Muwasilishaji hulazimika kusema "Mheshimwa Spika nawasilisha".

Utetezi wa Tundu Lissu haujapitia hatua hiyo. Uko kwenye Kamati. Hata kama Kamati itaona kuna haja ya kuwasilishwa Bungeni basi siku hiyo mwenyekiti wa kamati atauwasilisha kwa kusema "Mheshimwa Spika nawasilisha".

Hivyo, kimaadili, hatutakiwi kabisa kujadili kilichowasilishwa na Tundu Lissu kwenye Kamati kwa sababu hatuna ushahidi kawasilisha nini. Hivyo kimsingi hatutakiwi kujadili tulichokiona kama utetezi wa Tundu Lissu.

Mimi nimesoma utetezi kwenye magazeti na humu JF. Lakini magazeti na jF siyo forum rasmi ya kuthibitisha alichowasilisha Tundu Lissu. Na hata hivyo bado kiko kwenye Kamati hata Spika ukimuuliza hawezi kukupa jibu.

Hivyo Jaji huyu kachemka kujadili jambo ambalo ni premature. Kwa hili tu katuthibitishia udhaifu hata kama asingetajwa na Tundu Lissu.
 
Jamani ngoja mimi nifafanue understanding yangu jinsi huyu Jaji Fakhi Jundu alivyouvaa mtego wa Tundu Lissu. Ili kunielewa naomba mkazie kwenye statement niliyoweka hapo juu na hasa kwenye RED.

Ukisoma RED zote mbili ni kweli kabisa bunge halina mamlaka kujadili majaji kwa kuwataja majina. Hivyo ni kweli kabisa Jaji huyu anachokisema, hakupaswa kutajwa kabisa.

Lakini kitaalamu, huyu Jaji ndiye kaingia mtegoni kwa kuanzisha mjadala wa yeye kutajwa bungeni. Najua hoja zangu wengi hukurupuka kunipinga kama walivyokurupuka nilipoongelea mpaka wa Malawi. Na hadi hapa najua nikikomea hapa mtanipinga hadi asubuhi ninaposema Jaji huyu ndiye kalianzisha na wala si Tundu Lissu.

Watakaosema kuwa kalianzisha Tundu Lissu watasema kama Jaji huyu kwamba Tundu Lissu kaliongelea Bungeni. Wote hao na huyu Jaji wanakosea na mimi ninafafanua kama ifuatavyo.

Bunge ni nini? Bunge ni mkutano unaokaa huku Spika akiwa amevaa joho lake na lile lifimbo la askari anayewatimuaga CHADEMA likiwa limekaa mezani. Hivyo kinachozungumzwa Bungeni kinazungumzwa lile lifimbo likiwepo na kikishazungumzwa kinatunzwa kwenye kumbukumbu iitwayo Hansard.

Je, Tundu Lissu alifanyaje? Siku ya kuwasilisha mawazo ya Kambi ya Upinzani ndipo Tundu Lissu alipotumia mwanya huo kueleza udhaifu wa uteuzi katika mahakama. Ukweli si udhaifu huu tu bali udhaifu mwingi ili bunge lifanye uwezo wake serikali iurekebishe. Udhaifu si bajeti finyu tu kwa mahakama. Mwaka jana mnakumbuka jengo la mahakama kuhamishwa ndiyo ilikuwa issue. Mwaka huu zikawepo zingine na hili la udhaifu wa majaji likawa mojawapo.

Kama mnakumbuka baada ya Tundu Lissu kusoma mawazo yale mjadala ukawa mkubwa kwamba mahakama imedharauriwa. Justice Werema alidiriki kusema atamfungulia mashtaka Tundu Lissu. Mimi nina uelewa mkubwa tu kwamba kinachozungumzwa Bungeni kina haki ya kushtakiwa japo wengi wakiwemo wabunge hudanganyika na kudhani kwamba kinga inawafanya mle bungeni wasishtakiwe. Ni refu hili na silijadili zaidi. Lakini Jaji Werema yuko sahihi kama kweli ataamua kumshitaki Tundu Lissu. Narudia ana haki kumshtaki lakini sisemi kuwa Tundu Lissu ana makosa.

Lakini cha msingi kuliko vyote ninachotaka mjue au mkumbuke ni kwamba siku hiyo Tundu Lissu hakumtaja Jaji hata mmoja kuthibitisha udhaifu aliousema. Na hiki ndicho kilichoingia kwenye hansard. Kwa maana hiyo ukipekua kumbukumbu za bunge hutakuta hata nukta inamtaja jaji yoyote wa Tanzania aliyetajwa na Tundu Lissu. Mnaoelewa haraka, hadi hapa mmeshaona ninakoelekea. Ambao hamjaelewa tuendelee na maelezo.

Kilichofuata baadaye ni kiti cha Spika kuamua kwamba suala la Tundu Lissu kuwadharirisha majaji lipelekwe kwenye Kamati nadhani kamati ya Maadili. Kilichotokea ni kwamba Kamati ikakaa na ikamtaka Tundu Lissu awasilishe uthibitisho kwenye Kamati.

Tundu Lissu akawasilisha utetezi wake kwenye Kamati na kama kawaida kwenye nchi hi sasa hivi iliyojaa uwazi na ukweli kopi ya utetezi wake ikatua magazetini na huku mitandaoni.

Tumesoma wote kuwa huyu jaji na wengine tele walitajwa na Tundu Lissu. Lakini tujiulize maswali ya kutufunulia uelewa. Je, Tundu Lissu amemtaja huyu na wenzake Bungeni au mtaani?

Hakika hadi sasa Tundu Lissu hajamtaja Jaji yeyote Bungeni. Kamati ya Bunge si Bunge. Tundu Lissu kawasilisha utetezi kwenye Kamati hakuwasilisha Bungeni. Kwenye Kamati hakuna lile lifimbo. Kuna mwenyekiti wa Kamati na wajumbe wachache sana. Ikibidi hata huyu Jaji anaweza kuitwa na Kamati ile ili kujieleza alivyotuhumiwa.

Hivyo unaposema kwamba mambo haya yamezungumzwa Bungeni ukweli ni kwamba unajidhihirisha ulivyo dhaifu kupambanua mambo. Ukisikia kwamba umedharirishwa Bungeni basi tafuta hansard ya siku hiyo kuthibitisha. Hivyo, huyu Jaji hawezi kuthibitisha kuwa ni hansard ya lini iliyomtaja jina lake kupitia kwa Tundu Lissu.

Hivyo, hadi hapa mtakubaliana nami kwamba huyu Jaji ni dhaifu na kauthibitisha udhaifu wake kwa kuliparamia hili swala la Tundu Lissu. Mimi si mwanasheria lakini ninaelewa na aliyenisoma ameelewa kwamba Tundu Lissu hajamtaja jaji yeyote kwa jina. Ni uelewa finyu wa Jaji huyu.

Hata hivyo ili jambo litambulike kuwa limefikishwa Bungeni ni pale linapokuwa limewasilishwa kwenye meza ya Spika mbele ya wabunge. Muwasilishaji hulazimika kusema “Mheshimwa Spika nawasilisha”.

Utetezi wa Tundu Lissu haujapitia hatua hiyo. Uko kwenye Kamati. Hata kama Kamati itaona kuna haja ya kuwasilishwa Bungeni basi siku hiyo mwenyekiti wa kamati atauwasilisha kwa kusema “Mheshimwa Spika nawasilisha”.

Hivyo, kimaadili, hatutakiwi kabisa kujadili kilichowasilishwa na Tundu Lissu kwenye Kamati kwa sababu hatuna ushahidi kawasilisha nini. Hivyo kimsingi hatutakiwi kujadili tulichokiona kama utetezi wa Tundu Lissu.

Mimi nimesoma utetezi kwenye magazeti na humu JF. Lakini magazeti na jF siyo forum rasmi ya kuthibitisha alichowasilisha Tundu Lissu. Na hata hivyo bado kiko kwenye Kamati hata Spika ukimuuliza hawezi kukupa jibu.

Hivyo Jaji huyu kachemka kujadili jambo ambalo ni premature. Kwa hili tu katuthibitishia udhaifu hata kama asingetajwa na Tundu Lissu.

mkuu Nikupateje,
unapoandika, andika kama asomaye hatashindwa kukuelewa, unapoanza kujishuku kuwa kutokueleweka kwako ni kosa la msomaji naona ni sawa na kujipa digirii wewe mwenyewe,

umefafanua vizuri hoja ya mkenge aliouingia Jundu (jina la kwanza sitaki kuwakwaza kulitamka mbele ya wadhungu)

wabunge wa ccm, na spika wao wako too defenceve kiasi hawajui wanadefend nini. Wanaoga mtoni Lisu kawalia timing kachukua nguo anatimua mbio, nao wanamkimbiza, tunachekaje.

kwa maneno mengine kale kamwongo alikokatoa Makinda (sina uhakika na makinda au ndugai) kuwa Lisu alipoyataja majina ya wabunge waliodaiwa kuhongwa, aliyatajia kwenye maeneo ya bunge, hivyo ile kinga ya mijadala ya kibunge kutokushitakiwa inahusu pia huo mkutano na waandishi wa habari kwani ulifanyika kwenye maeneo ya bunge, utakuwa mwongozo feki au sio Nikupateje

na kiini macho kinakuwa kikubwa zaidi unapotuambia unao uelewa wa kutosha kuwa mijadala ya bunge inaweza kushitakiwa kwa maana ya muhusika mmoja mmoja ama kundi la wahusika (wa/mbunge) hebu mshushue spika pamoja na wote wajuao kuwa mbuge hawezi kushitakiwa kwa matamshi ayatoayo bungeni!

Wala usijipe hofu ya kupingwa kama kwenye mjadala wa mpaka wa tz na malawi.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Nikupateje,
unapoandika, andika kama asomaye hatashindwa kukuelewa, unapoanza kujishuku kuwa kutokueleweka kwako ni kosa la msomaji naona ni sawa na kujipa digirii wewe mwenyewe

Nimetahadharisha nikiwa na reference ya wanaokurupuka humu JF. Wakurupukaji wamo na sisi hatutaacha kutahadharisha uwepo wao eti kwa sabbabu kwa kufanya hivyo tunajipa degree.

kwa maneno mengine kale kamwongo alikokatoa Makinda (sina uhakika na makinda au ndugai) kuwa Lisu alipoyataja majina ya wabunge waliodaiwa kuhongwa, aliyatajia kwenye maeneo ya bunge, hivyo ile kinga ya mijadala ya kibunge kutokushitakiwa inahusu pia huo mkutano na waandishi wa habari kwani ulifanyika kwenye maeneo ya bunge, utakuwa mwongozo feki au sio Nikupateje
Hakuna kinga kwa tamko linalomdhalillisha utu wa mtu, iwe limetolewa kwenye maeneo yanayozuguka bunge (Precinct) au hata ndani mle bungeni ukumbini.

Mbunge hawezi kutamka kuwa mama yangu ni malaya halafu ukasema tamko hilo lina kinga ya bunge eti siwezi kumshtaki! Naamini kwa mfano huo tu inatosha kuelewesha.
 
Back
Top Bottom