Jaji kiongozi Fakh Jundu amjibu Lissu kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mahakama Bungeni

Kwani Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imeishatoa maamuzi au huyu Jaji Jundu anaitolea maamuzi?. Jambo halijapelekwa kwake yeye unajishaua tu!. Basi alete utetezi wa kisheria, au tuwapambanishe live yeye na Lisu kama anadhani ana hoja.
Kweli amedhihirisha kuwa hakuwa na sifa ya kuwa alipo kwani anarukia mambo yasiyomhusu.
 
henge,
jaji mborouk, mmoja kati ya majaji 3 wanaosikiliza rufaa ya lema hana degree ya sheria. Je, kama yeye yuko pale kimizengwe atamtendea haki lema? Si anajipendekeza kwa mteuaji wake anayegombana na lema?


ahaaah hili linchi bana, mtu hana degree anakuwaje jaji??
Najua sifa ya kuwa jaji ni kuwa na degree ya sheria!
 
Huyu jaji kazidi kujivua nguo maana kakanusha kama watu wavijiweni wafanyavyo!
Naona mziki wa Lissu bado haujapa mchezaji!
Hadi sasa hajajibu hata hoja moja ya Mh lissu.
 
Nilidhani kweli Jaji Kiongozi katoa kile kinachoweza kuitwa majibu kwa hoja za Mhe. T. Lissu...

Kimbelembele changu changu cha kutafuta walau hoja moja iliyojibiwa kimeniacha na hasira....

Hawa watu wanazidi kuchokoza umma na ipo siku watarushiwa mayai viza!
 
Nilidhani kweli Jaji Kiongozi katoka kile kinachoweza kuitwa majibu kwa hoja za Mhe. T. Lissu...

Kimbelembele changu changu cha kutafuta walau hoja moja iliyojibiwa kimeniacha na hasira....

Hawa watu wanazidi kuchokoza umma na ipo siku watarushiwa mayai viza!

Penye Red,
Heri mayai ya viza. Unadhani mama ambaye ameonewa mumewe na Mahakama akawa Mjane wa mfumo wake mbovu ataacha kurusha mawe?
 
Henge,
Jaji Mborouk, mmoja kati ya majaji 3 wanaosikiliza Rufaa ya Lema hana degree ya sheria. Je, kama yeye yuko pale kimizengwe atamtendea haki Lema? Si anajipendekeza kwa mteuaji wake anayegombana na Lema?


kumbe huyu fisadi wa kazi yupo kwenye hii kesi? Huyu hafai hata kuwa hakimu. Alitakiwa kuwa kwenye mambo ya utawala na siyo kusikiliza kesi. Hii kesi imekwisha haribiwa
 
Penye Red,
Heri mayai ya viza. Unadhani mama ambaye ameonewa mumewe na Mahakama akawa Mjane wa mfumo wake mbovu ataacha kurusha mawe?


Unajua nini mkuu Mikael P Aweda,

Kuna watu wamesota sana kusoma na bado wanahangaika huku makazini kwa sababu ya upuuzi kama huu wa kupeana kazi kwa kuangalia sura. Hali ni mbaya utadhani utumishi wa umma umekuwa kama mchakato wa kuchumbiana na kupeleka posa. Kama huyu bwana asingekuwa kang'ang'ania ofisi kwa upendeleo, kuna watu wenye uwezo wangekuwepo hapo na wanachapa kazi!!

Leo hii, watoto wa masikini wamechapa kazi wakasoma na kuwa na vyeti safi, ila kupewa kazi ni kimbembe. Na pale wanapopata kazi, huko kazini wanaishia kuwa punda wa kudunda mzigo uliotukuka na kuwapandisha wababaishaji vyeo !!

Natamani nihame hii nchi kwa muda...if it were possible anyway!!
 
Last edited by a moderator:
The Principal Judge, Mr Fakih Jundu, has defended his appointment, dismissing as baseless claims by Singida East legislator, Mr Tundu Lissu, that he was unconstitutionally given the post.

The Principal Judge, Mr Fakih Jundu Mr Lissu (Chadema) told the National Assembly session in Dodoma last month, that Justice Jundu was appointed by President Jakaya Kikwete to the position at the time when he had already retired.

Justice Jundu told a news conference in Dar es Salaam that claims by Mr Lissu were baseless and challenged the MP to produce evidence on the illegality of his appointment. "All procedures were followed in my appointment," he stressed, but admitted that he was 63 years old.

Justice Jundu, however, declined to give details on the issue, saying that whoever needed more information on the matter should make efforts to consult relevant authorities. According to Article 101(1) of the constitution, a High Court Judge should go on retirement after attaining the age of 60 years.

However, under Article 101(3) the president may extend the service of a judge who is beyond 60 years on public interest, provided that judge accepts the extension in writing. Earlier, Judge Jundu officiated at the ceremony where Mr John Rugalema Kahyoza took oath of office following his recent appointment as the Deputy Senior Registrar of the High Court. Before his appointment, Mr Kahyoza was Registrar of the Commercial Division of the High Court.
 
hujui! Kuna jaji anasoma open university sasa hivi. Alikuwa na diploma, post graduate diploma na mastaz ya utawala. Mheshimiwa akamgonga ujaji.

Mkuu naomba uwe makini na maelezo yako! Hapo kwenye red; tafadhali sema UJAJI WA RUFAA na sio ujaji wa kawaida. Huyu akiamua ule kitanzi unakula hivi hivi tunaona ukiacha wajane na mayatima. Mola tusaidie.
 
The Principal Judge, Mr Fakih Jundu, has defended his appointment, dismissing as baseless claims by Singida East legislator, Mr Tundu Lissu, that he was unconstitutionally given the post. The Principal Judge, Mr Fakih Jundu Mr Lissu (Chadema) told the National Assembly session in Dodoma last month, that Justice Jundu was appointed by President Jakaya Kikwete to the position at the time when he had already retired. Justice Jundu told a news conference in Dar es Salaam that claims by Mr Lissu were baseless and challenged the MP to produce evidence on the illegality of his appointment. "All procedures were followed in my appointment," he stressed, but admitted that he was 63 years old. Justice Jundu, however, declined to give details on the issue, saying that whoever needed more information on the matter should make efforts to consult relevant authorities. According to Article 101(1) of the constitution, a High Court Judge should go on retirement after attaining the age of 60 years. However, under Article 101(3) the president may extend the service of a judge who is beyond 60 years on public interest, provided that judge accepts the extension in writing. Earlier, Judge Jundu officiated at the ceremony where Mr John Rugalema Kahyoza took oath of office following his recent appointment as the Deputy Senior Registrar of the High Court. Before his appointment, Mr Kahyoza was Registrar of the Commercial Division of the High Court.

Teh teh teh teh! Hebu mlio karibu naye mshaurini huyo Jaji akae kimya. Asipokuwa makini atamharibia hata Rais aliyemteua. Wakati mwingine kukaa kimya nayo ni busara. Hivi kwa akili yake anadhani atashindana na hoja za Lissu?

Kwa hivi vinchi vyetu uchwara vilivyojaa kila aina ya vitimbi hako ka-statement:
provided that judge accepts the extension in writing kanachekesha kweli na inavyoelekea ndio "mstari" anaosimamia kuhalalisha hoja yake. Such kind of loopholes should be fixed in the new Constitution.
 
Hakujibu hoja hata moja ya Tundu Lissu. Nami naungana na wadau wengine wa maendeleo kwa kuuliza " KWA NINI AONGEZEWE MKATABA WAKATI WATU WENGINE WA KUFANYA KAZI HIYO WAPO?" au huyu jaji kiongozi ni SO SPECIAL kiasi kwamba hatakiwi kustaafu kwa sababu anafanya kazi ambayo wengine hawawezi kuifanya?

"Kipengele cha dini kiingizwe kwenye sensa". TAFAKARI
 
Mkuu naomba uwe makini na maelezo yako! Hapo kwenye red; tafadhali sema UJAJI WA RUFAA na sio ujaji wa kawaida. Huyu akiamua ule kitanzi unakula hivi hivi tunaona ukiacha wajane na mayatima. Mola tusaidie.

Kwa hiyo, mtu asiye na degree ya Sheria kapewa uajaji wa mahakama ya rufaa yenye uweze kutoa hukumu ya kifo kwa mtu ye yote na mtu mzima na degree yake kichwani anakaa JF anamtetea Kikwete siku nzima.

 
Mimi ningemwona Jundu ana hoja kama angejibu hoja za Lisu kuhusu yeye moja baada ya nyingine badala ya kujibu Kisiasa. Kama Je kwa Umri alionao bado anazo sifa za kuwa Jaji Kiongozi? Ukomo wa Umri wa Jaji Kiongozi ni miaka mingapi, na yeye yupo within?
 
kwani hii ilitokea mkuuu???

mkuu henge ndo umeshuka leo kutoka sayari ya mars nini? jaji wa mahakama ya rufaa ya tz aitwaye mbarouk salim mbarouk fr6 zenji kumbe ana diploma ya law ya ud na bachelor of arts. sasa hivi ndo anaitafuta LLB pale pa professor mbwete(open university)
 
Wakuu,
Jaji kiongozi wa mahakama ya Tanzania Fakh Jundu amejibu tuhuma zilizotolewa na msemaji wa wizara ya Sheria na katiba tundu Lissu, kuwa si kweli.

Ninamnukuu,
Akizungumza baada ya kumuapisha Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, John Kahyoza, kushika wadhifa huo jana, Jaji Jundu alisema yuko katika nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria.

Alisema Rais ana mamlaka ya kuwaongezea muda majaji baada ya wao wenyewe kukubali.

“Taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu majaji, imenisikitisha sana. Kwa sababu hatuna nafasi ya kwenda kujitetea. Na kuhusu mimi kuendelea kuwa kwenye kiti hiki kwa mkataba bandia ni suala la uzushi, ambalo halina ukweli,” alisema Jaji Jundu na kuongeza:

“Vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo, waanike huo mkataba niliosaini kuendelea kuwa na wadhifa huu.”

My take; Jaji hakujibu hoja za tundu Lissu hata mmoja, kweli Lissu ni Kiboko.
Source Nipashe.



Habari kamili. Hii hapa.
Jaji Mkuu: Nimekasirishwa






Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, amesema amesikitishwa na kitendo cha majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kutuhumiwa bungeni, kwa kuwa hawana nafasi ya kwenda kwenye chombo hicho kujitetea.

Miongoni mwa tuhuma zinazodaiwa kutolewa bungeni na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, dhidi ya majaji hao, ni pamoja na iliyomhusu yeye mwenyewe (Jaji Jundu) ya kuendelea kuwa kwenye kiti hicho kwa kutumia mkataba bandia.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, alitoa tuhuma hizo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo, Mathias Chikawe.

Akizungumza baada ya kumuapisha Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, John Kahyoza, kushika wadhifa huo jana, Jaji Jundu alisema yuko katika nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria.

Alisema Rais ana mamlaka ya kuwaongezea muda majaji baada ya wao wenyewe kukubali.

“Taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu majaji, imenisikitisha sana. Kwa sababu hatuna nafasi ya kwenda kujitetea. Na kuhusu mimi kuendelea kuwa kwenye kiti hiki kwa mkataba bandia ni suala la uzushi, ambalo halina ukweli,” alisema Jaji Jundu na kuongeza:

“Vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo, waanike huo mkataba niliosaini kuendelea kuwa na wadhifa huu.”

Hata hivyo, alisema Mahakama ya Tanzania haiwezi kufanya mabishano ambayo hayana msingi kwa kuwa yote yaliyozungumzwa yamesikilizwa upande mmoja.

Tuhuma hizo zinazodaiwa kutolewa na Lissu dhidi ya majaji wanane wa Mahakama Kuu, mmoja wao akiwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania pamoja na Jaji Jundu.

Baadhi ya majaji wanatuhumiwa kuteuliwa wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma na wanapewa ‘zawadi’ ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu, ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni.

Wengine wanatuhumiwa kuteuliwa huku wakiwa wagonjwa mahututi, ambapo inadaiwa kuwa hawakuwahi kuandika hukumu hata moja kabla ya mauti kuwafika.

Majaji wengine wanatuhumiwa kwa kutoandika hukumu na hivyo kuwa wacheleweshaji wakubwa wa kesi katika Mahakama Kuu na wengine kwa kupewa mkataba mpya baada ya kustaafu kama Jaji wa mahakama hiyo.

Majaji wengine wanatuhumiwa kwa “kushinikiza au kushawishi kushughulikia au kuamua kwa upendeleo mashauri yaliyowahusu jamaa au rafiki zao na kuwaandalia sababu za rufaa baadhi ya washitakiwa waliotiwa hatiani na mahakama za mahakimu.

Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa “kuidhalilisha” Mahakama na “kuwadhalilisha majaji” (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); “kuwavunjia heshima majaji” (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); “kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji” (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); “kufedhehesha Mahakama na majaji” (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

Aidha, Msemaji wa Kambi ya Upinzani alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na “kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote” (Mangungu).

Kwa upande wake, Waziri Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba “... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na Tume ya Uajiri wa Mahakama. Zaidi ya hayo labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna… hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii.”

Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba.

Lissu alikataa kufuta kauli hiyo na Mwenyekiti wa kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi.

Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hilo.

Hata hivyo taarifa zilizovuja kutoka kwenye kamati hiyo zilieleza kile alichowasilisha Lissu kuwa ni kufafanua tuhuma moja baada ya nyingine na kuwataja majaji hao kwa majina na walivyoteuliwa au kushindwa kuwajibika kwa mujibu wa viapo vya kazi yao.

Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Lissu alisema, “Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana ‘uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.”

Ripoti ya kamati hiyo hajawekwa hadharani, ingawa kuna hisia kwamba utetezi wa Lissu siyo tu umefungua mambo mapya bali umewafanya waliokuwa wanamkejeli na kupuuza kuanza kuwaza mara mbili juu ya misimamo yao ya awali.




CHANZO: NIPASHE
Lissu ana mtindio wa ubongo, la sivyo analipwa hela nyingi sana kuimba taarabu bungeni.
 
Back
Top Bottom