Jafo kupokelewa kishujaa kisarawe!!!

salehe

Member
Mar 16, 2008
83
30
jana usiku nilikuwa nasikiliza tbc taifa nikasikia wananchi wapo wanapanga mikakati ya kumpokea mbunge wao kishujaa baada ya kutoa hoja ile ya fao la kujitoa!!! Nikaanza kushanga! Hoja kama hizo mbona zinztolewa nyingi sana na upinzani lakini hawapendelei misifa ya hivyo????
 
Hao wazaramo wamekosa kazi!!!!!!!! nini kikubwa alichofanya??? sheria ilikuwa tayari imegomewa na wafanyakazi na tayari Migodi ilishaanza kupata hasara hata kama wabunge wasingejadili bado serikali ingefanya kama ilivyofanya kwenye sheria ya kukusanya maoni ya katiba
 
Hata mimi ningekuwa Dar ningeenda kumpokea maana kitu walicho kuwa wametufanyia CCM hakikubaliki kabisa....
 
Mimi ngoja niondoke hapa maana nahisi harufu ya ban hapa kwani huyo jafu ndio nani??alishawahi changia nini??bungeni mpaka aitwe shujaaa???ngoja niondoke ban inanukia.......................
 
Kwani nani waliopitisha hiyo sheria ya mafao?Si ni hao wagonga meza,maana ndo wengi.Sijaona cha ajabu alichofanya,maana shinikizo lilikuwa kubwa toka kwa wafanyakazi,serikali walibanwa kila kona.Hao wapiga kura wake wanaelewa wanachoshabikia,ni wangapi watafaidika na hiyo sheria?Muhimu ilikuwa kujadili ajali zinazotokea kila wakati na kusababisha maafa(hoja ya LISU-ajali ya meli Zanzibar).
 
jana usiku nilikuwa nasikiliza tbc taifa nikasikia wananchi wapo wanapanga mikakati ya kumpokea mbunge wao kishujaa baada ya kutoa hoja ile ya fao la kujitoa!!! Nikaanza kushanga! Hoja kama hizo mbona zinztolewa nyingi sana na upinzani lakini hawapendelei misifa ya hivyo????
hao wananchi watakuwa wanaandaliwa kumpokea,na itakuwa kwa g'harama kubwa sana!!!!!idia ilishatolewa na mnyika yeye kadandia kwa mbele.nahisi atakuwa aliitwa na spika akaambiwa atoe hiyo hoya walau kumfanya nae asikike.
 
Naunga mkono mawazo ya wanakisalawe ikiwezekana apitie na huku kwetu tulisukume gari lake hadi kisalawe!
 
Tatizo lenu wapinzani mmesahau mila. Sisi tumemuweka maji marefu mjengoni ili awaroge wapiga kura wetu, tukienda majimboni wanasahau shida zao zote
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, afanyaye jema bila kujali itikadi yake inapaswa asifiwe Jafo anastahili mapokezi hayo, mbona Zitto kabwe kipindi kile alipofukuzwa bungeni alipokea kama shujaa na hakuna aliyemnanga! au jema linafanywa na wapinzani tu! hapana kwa hili THUMB UP Jafo you diserve mapokezi hayo!
 
Mimi ngoja niondoke hapa maana nahisi harufu ya ban hapa kwani huyo jafu ndio nani??alishawahi changia nini??bungeni mpaka aitwe shujaaa???ngoja niondoke ban inanukia.......................

walikuwa wamezoea former mb Janguo akiwarushia matusi na kejeli nyingi lakini kwa huyu kijana wamefika ni FULL KUTABASAMU!!
 
jana usiku nilikuwa nasikiliza tbc taifa nikasikia wananchi wapo wanapanga mikakati ya kumpokea mbunge wao kishujaa baada ya kutoa hoja ile ya fao la kujitoa!!! Nikaanza kushanga! Hoja kama hizo mbona zinztolewa nyingi sana na upinzani lakini hawapendelei misifa ya hivyo????

acha hizo wewe... mtu yeyote yule akifanya kitu kizuri yatupasa tumpongeze, bilakujali hitikadi ya chama wala langi... kwanza kabla ya yote mh. Jafo nishuja wakuigwa bila kujali hitikadi ya chama chake... sio wewe umekalia ushabiki tu, inatakiwa utambue kitukimoja tu kwamba alichokuwa anakifanya Mh. jafo si kwa maslahi yake binafsi nasi kwa maslahi ya chama chake bali amefanya hivyo kwa maslahi ya wa Tanzania wote.... naomba utambue hivyo.
 
Watu wa Kisarawe wana matatizo mengi likiwemo la kuuwawa vijana wao waliodaiwa kuvamia msitu wa Kazimzumbwi.Sijawahi kumsikia mbunge wao akileta hoja ya serikali kuwaadabisha waliohusika na tukio hilo,pia Kisarawe wamekuwa wakilalamika kutapeliwa ardhi na wawekezaji waliokuja kuwekeza kwenye kilimo cha jatirofa.Huyu mbunge amecheza mchezo wa kisiasa kushupalia hoja ambayo vuguvugu la kudai ibadilishwe ilitoka nje ya bunge kwa sababu wao kwa uzembe wao waliipitisha bila kuangalia madhara yake kwa wananchi wa kawaida
 
Mmmmh mwanawane, hawa wajomba nomaa kweli kweli,! Wanalipika, linawashinda wakikosolewa wanakimbilia kuliweka sawa na kisha kujiita shujaa wakati hoja iliibuliwa na mtu mwingine? Hivi hansard za Bunge hazioneshi ni Mbunge gani aliyeshughulikia hoja maalumu ya kupinga fao la kujitoa? Ushujaa wa Jafu ungekuja kama angeweza kuwashawishi wana migodi kukubaliana na hoja ya silikali ya Wao M ya kufuta fao la Withdrawal? Shame to Jafu and his Wao M members kwa kulikoroga na kushindwa kulinywa kisha kujidai mashujaa baada ya wapinzani kuwaweka sawa. Kazi kweli kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom