J.K Nyerere na siasa za maji taka

Kwanini baba? Hili neno baba limekaa kikanisa kanisa. Mimi siliafiki hata kidogo. Ubaba wa Taifa ndio nini? Hatuna haja ya baba wa Taifa. Tanzania haikuasisiwa na Nyerere pekee ni makubaliano ya watu wawili Nyerere na Karume sasa inakuwaje baba awe Nyerere na Karume awe nani?

Tatizo ni 'kikanisa kanisa' au!? Acha udini wewe binti,halafu inawezekana haujui vizuri kwanin Nyerere anaitwa Baba wa taifa ndio maana unamchanganya na karume!
 
Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?

" Kambona , ah, ah!

Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"



Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.


MY TAKE:


Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.

Naomba kuwakilisha mada.

Sijawahi kumfikiria Nyerere kuwa a great leader hata kabla ya kujua siri zake nyingi.He had just too many shortfalls for my liking.Baada ya kumjua vizuri ndio nika-realize kwamba he was not a true son of Africa.Only and I repeat only Patrice Lumumba and Kwame Nkrumah were true sons of Africa.The rest including Nyerere,Stalin,Mao Tsetung,Hitler, Mandela etc.were and are mere puppets of the Illuminati.
 
Sijawahi kumfikiria Nyerere kuwa a great leader hata kabla ya kujua siri zake nyingi.He had just too many shortfalls for my liking.Baada ya kumjua vizuri ndio nika-realize kwamba he was not a true son of Africa.Only and I repeat only Patrice Lumumba and Kwame Nkrumah were true sons of Africa.The rest including Nyerere,Stalin,Mao Tsetung,Hitler, Mandela etc.were and are mere puppets of the Illuminati.
So, to you a true son of Africa is one who was killed before he even set foot in the President's office and one who was overthrown before he realized his vision. You too, are a true son of Africa!
 
How come watetezi wakuu wa CCM (Kadogoo, MS, FF, Allydou etc.) wanakua against Nyerere katika kila jambo? CCM ipi wanaiwakilisha? Kuna ule msemo maarufu wa kuhalalisha rushwa kwamba "Kila mtu anakula ofisini kwake" upo everywhere serikalini. Ina maana hao nao wametumwa na Kikwete kula rushwa na kuiba mali ya umma??
 
Tatizo ni 'kikanisa kanisa' au!? Acha udini wewe binti,halafu inawezekana haujui vizuri kwanin Nyerere anaitwa Baba wa taifa ndio maana unamchanganya na karume!


Anaitwa na nani? mbona anajulikana kama Dikteta na anafananishwa na Madikteta wakubwa kama Hitler.
 
Sasa mbona Tanganyika haipo na Zanzibar ndio ipo? Au mume alikuwa si rizki?!

Zanziba haina sarafu.

Zanzibar haina bendera.

Zanzibar ni mahali pa kupumzikia na madem zetu, tukimaliza kupigana mikasi tunarudi zetu Bara.

kama saa hizi nina ham kweli kuja kulala Mlandege Lodge.
 
Mimi sijawahi usikia huo wimbo, na wewe kama uliusikia je ni Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa anaimba au ni walimu wako ndiyo walikuwa wanakuimbisha ?
Mitazamo ya Mwalimu ndio iliyoweza kuwekwa kwenye nyimbo mbalimbali zilizokua zinaimbwa mashuleni na hata kwenye kumbi za starehe. Kwa kifupi... the song had the node from the top. To great thinkers ule wimbo wa Jumbe analia oooh lia.... ulikua unamsema Jumbe makamo wa wakati ule au nani
 
tuliosoma miaka ya themanini hatukuimba wimbo huu wewe mzuka nini, au uliimbia shule za msingi za malawi?
Miaka ya themanini tumeimba sana nadhani wewe ndio aukuepo kila nikimkumbuka huyu mzee na roho yake mbaya nasikitika sana
 
Kwahiyo ulitaka aupige marufuku...??, Si ungekuja ukasema jamaa alikuwa Dikteta..., na ule wa nduli Iddi Amini vipi nao ungepigwa marufuku au wenyewe poa tu..

Kwani alipiga marufuku vingapi hata iwe ajabu hilo!

Kuruhusu nyimbo za namna hiyo kusambaa mashuleni haijakaa vyema.

Kambona alikuwa na watoto, wapwa, Tanzania, wangejiskiaje watoto wenzao wakiwabully kuwa baba ya ameolewa?
 
Ndio hapo utagundua "CCM" to those types,means something very different from what Nyerere,Kawawa,Kingunge, Msekwa, me,you and everybody else here know(or knew). Najua utakua umeliona sana hili pia ,kwamba CCM hii hii pengine itamaanisha kitu kingine tofauti kabisa kwa hawa jamaa after 2015.....(ofcourse subject to some occurences....you know what I mean). Na katika sura nyingine tena you can almost certainly tell kwamba muungano wetu huu ukaja kumeguka tuu (maana kinachofuatia "mpasuko" huu ni mmeguko tu!!),,,hatutaziona tena hizi types.
How come watetezi wakuu wa CCM (Kadogoo, MS, FF, Allydou etc.) wanakua against Nyerere katika kila jambo? CCM ipi wanaiwakilisha? Kuna ule msemo maarufu wa kuhalalisha rushwa kwamba "Kila mtu anakula ofisini kwake" upo everywhere serikalini. Ina maana hao nao wametumwa na Kikwete kula rushwa na kuiba mali ya umma??
 
Mimi niliwahi kuwa "kishoka" wa TANESCO. Kulikua na nyimbo zetu fulani hivi,zile tukiziimba wakati tunanyanyua nguzo za umeme au wakati tunavuta waya, basi kazi ilikua inanoga sana. Kuna mtu amewahi kuzisikia? Ningezi-quote kama alivyofanya mwanzisha sred,lakini haziandikiki hapa....zingesomeka ********** zote tangu verse mpaka chorus. Kwakuwa hizi tulikua tukiimba hata wakati tukifanya kazi mitaani tena mbele ya watoto wadogo,....nani alaumiwe hapa? Au waziri wa nishati wakati huo...teh teh, ironically alikua Mkuu JK mwenyewe.

Sredi nyingine bwana sjui hata kwanini zinawekwa humu...hivi hakuna jukwaa jingine kweli? Ni kama kuna effort mahsusi kabisa za ku-undermine JF jukwaa la siasa. Mods....your challenge!
Kwani alipiga marufuku vingapi hata iwe ajabu hilo!

Kuruhusu nyimbo za namna hiyo kusambaa mashuleni haijakaa vyema.

Kambona alikuwa na watoto, wapwa, Tanzania, wangejiskiaje watoto wenzao wakiwabully kuwa baba ya ameolewa?
 
Kwani alipiga marufuku vingapi hata iwe ajabu hilo!

Kuruhusu nyimbo za namna hiyo kusambaa mashuleni haijakaa vyema.

Kambona alikuwa na watoto, wapwa, Tanzania, wangejiskiaje watoto wenzao wakiwabully kuwa baba ya ameolewa?

Angepiga marufuku binafsi ningemuona kazidi where do we draw the line....., Binafsi naona hiyo hatua ingekuwa imezidi mipaka..., Thats life jamaa alitaka kumpindua akashindwa..., Sasa unategemea zitungwe nyimbo za kumsifia..., Thats poitics am afraid anywhere you go.., thats how it goes..,

By the way sidhani kama huo wimbo uliimbwa mashuleni na kama uliimbwa basi makosa yalikuwa ni ya waalimu kuruhusu huu wimbo (na sio kumlaumu President).., tukiendelea hivi naona tutaanza kumlaumu hata kwa vita vya Uganda, na majanga ya njaa yaliyotukumba...
 
Wacha hiyo, Nyerere huwezi kumdhihaki kwa sababu zisizo na sababu, alikuwa ni kiongozi bora hakuna mfanowe mpaka sasa. Kambona alikuwa anataka ubepari nyerere ujamaa, ndo tofauti yao na ndicho kilichomkimbiza kambona nje. Kama mpaka sasa nchi haipo na haikuwa tayari kwa ubepari, vipi wakati ule? si ndio ilikuwa bado kabisa? zaidi ya hayo nyerere hakutunga nyimbo za mchakamchaka, ni wananchi wenyewe. Muache nyerere apumzike kwa amani, kazi aliyoifanya ni nzuri na inatosha na inaeleweka kwa kila mtu duniani sio tanzania tu.
 
Hivi kumbe ni kweli kwamba upo mpango mahususi unaosukwa kwa utaalamu wa juu kumvua Nyerere Ubaba wa Taifa. Kaeni chonjo.
 
naomba kuuliza Nyerere anaelezwa hakufanya kazi kubwa kupigania uhuru, je walimchagua kuongoza TANU waliwezaje kumchagua mtu ambaye hakuwa na vision ya kutuletea uhuru? Oscar kambona pia alikuwa katibu mkuu wa TANU na mtu wa dini moja na Nyerere mbona sijawahi kusikia kwamba alikimbia nchi kwa sababu ya tofauti ya dini na Nyerere? au Oscar alikuwa dini tofauti? naomba kueleweshwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom