Iundwe sheria ya kuwaadhibu abiria wanaosimama ndani ya daladala!

Rich Dad

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
748
133
Wanaharakati wote watakubaliana na mimi kwamba haki mbalimbali zinavunjwa kila siku kupitia usafiri wetu wa public, hasa ndani ya jiji za dar es salaam.
Haki za watoto ( hasa wanafunzi), wakina mama wanadhalilishwa kila siku kutokana na misongamano ndani ya daladala zetu. Watu wanabanana mpaka wanashindwa kupumua.
Mbali na hilo, inapotokea ajali watu wengi wanaachwa eidha majeruhi au wanapoteza maisha kabisa.
Kwa upande mwingine, ni sifa mbaya kwa taifa letu hasa ukizingatia ya kwamba ncho za wenzetu wamesha implement decent public transportation system ambao unapendwa na kutumiwa na watu wa kada mbalimbali. Lakini kwetu Tanzania looh ukianzia na upandaji wa gari ni aibu...watu wanakimbilia kama ng'ombe.
Nawashauri wabunge waiulize serikali ni lini itapitisha pamoja na kuisimamia sheria ya kuwaadhibu abiria wanaosimama ndani ya daladala.
Hatuwezi kuendelea kukaa kimya huku watu wakiteseka na usafiri wa public wao wakifurahia kufunga baadhi ya barabara pale wanapopita na VX zao.
Vile vile sheria hii itailazimisha serikali kufanya haraka kuimarisha njia mbadala za usafiri wa mass. Mfano reli za masafa mafupi ndani ya majiji, mradi wa mabasi yaendayo kasi, upanuzi wa barabara zetu, ferry kutoka Tegeta mpaka city centre.
Nawasilisha wadau!!!
 
Nadhan,sheria itawatia hatiani sana wakaz wa maeneo haya,kwa jijin dar,GONGO LA MBOOO.......T......O,MBAGARA,TANDIKA,MBEZI,KIMARA,TEGETA,KAWE,
 
Nadhan,sheria itawatia hatiani sana wakaz wa maeneo haya,kwa jijin dar,GONGO LA MBOOO.......T......O,MBAGARA,TANDIKA,MBEZI,KIMARA,TEGETA,KAWE,
Sheria inaweza kuonekana mbaya, lakini mwisho wa siku ni kuwasaidia abiria wenyewe hasa ukizingatia watu wa maeneo uliyoyataja wanasimama kwa muda mrefu mno ndani ya hizi daladala. Cha msingi ni kwamba sheria ikisimamiwa vizuri, hakuna ambaye atakubali kuingia hatiani kiuzembe. Lakini najua kigugumizi cha serikali kinatoka wapi, ni kwamba kuundwa na kusimamiwa kwa sheria hii kutaibua madai mengi dhidi ya serikali. Mfano, kuna possibility kubwa ya wafanyakazi kuchelewa kufika maofisini na sababu itakuwa ni usafiri.
 
Operator wa gari ndo yupo responsible kwa kuhakikisha idadi ya watu ni sawa na viwango sio abiria.
 
Mkuu nadhani hii issue hujafikilia vizuri...

Wakileta hio sheria wakati abiria ni wengi kuliko vyombo vya usafiri ni nani atakayeumia... (nadhani hapa watu wengi watachelewa makazini na mashuleni)

The only way kumaliza hili tatizo ni kuwa na sufficient vyombo vya usafiri ili vyombo viwe vingi zaidi ya wasafiri hapo kutakuwa hakuna shida ya kubanana
 
Ikumbukwe pia kwamba yapo mabasi ambayo yametengenezwa maalum kuruhusu abiria kusimama...hata asia na kwingineko watu wanasimama kwenye mabasi treni n.k
 
Sheria inaweza kuonekana mbaya, lakini mwisho wa siku ni kuwasaidia abiria wenyewe hasa ukizingatia watu wa maeneo uliyoyataja wanasimama kwa muda mrefu mno ndani ya hizi daladala. Cha msingi ni kwamba sheria ikisimamiwa vizuri, hakuna ambaye atakubali kuingia hatiani kiuzembe. Lakini najua kigugumizi cha serikali kinatoka wapi, ni kwamba kuundwa na kusimamiwa kwa sheria hii kutaibua madai mengi dhidi ya serikali. Mfano, kuna possibility kubwa ya wafanyakazi kuchelewa kufika maofisini na sababu itakuwa ni usafiri.
ndugu weeee kwani sheria ya kufunga mikanda imefanikiwa??????hutujui sie watu wa zima moto????
 
Ikumbukwe pia kwamba yapo mabasi ambayo yametengenezwa maalum kuruhusu abiria kusimama...hata asia na kwingineko watu wanasimama kwenye mabasi treni n.k
unaweza kuulinganisha na usimamaji wa mabasi yetu.....au????????
 
Wewe ktk dunia hii umeona wapi ktk nchi yoyote iliyoendelea metro mass transit ikawa chini ya watu binafsi wababishaji tena mmoja mmoja? Hii city mass transit ilitakiwa kuwa chini ya UDA na tunavyoongea UDA ilitakiwa iwe na network ya mabasi na light railway kwenye routes zooote hapa mjini. Daladala zilitakiwa zipaki mbali ya jiji na ziende ambako UDA haifiki hukoo Kinyerezi nk
 
mh naunga mkono hoja.LAKINI nadhani ntarudi kijijini kwetu lembeni
kulima ,huko hakuna foleni .KWA jiji hili maisha yatanishinda
make navuta picha ya jioni na asubuhi usafiri
unavyokuwa matata hahaaa.........ni kweli
ni kwaajili ya maisha yetu lakini ukitazama kwa
undani saana mmm
ni vigumu kuliko ngamia kuingia kwenye
tundu la sindano walahi.
sirkali ingetengeza hayo matreni yao ndo walete hiyo sheria jamani
 
mi naona ingesaidia kwa kias flani mfano kupunguza vifo vya watu weng punde itokeapo ajali pia gari ikiwa na abiria wa wastani ingepunguza ongezeko ka magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya hewa mf. Tb na km sheria hiyo itapita itakuwa kero sn hasa dar sbb abiria ni wengi sn na magari ni machache. WABORESHE KWANZA BARABARA NA MAGARI YAWE KIWANGO NDO WALETE SHERIA HII
 
Back
Top Bottom