IT ilivyokuwa msaada mkubwa kwangu - Read and get motivated

herman3

JF-Expert Member
Feb 7, 2015
509
659
Habari napenda leo ku_share story ya namna ambavyo IT imekuwa backup kubwa sana kwangu kila ninapokwama.

Mimi sio IT kwa kuingia darasani lakini nimejifundisha mwenyewe in a hard way. Mwaka 2015 nikiwa nimemaliza Diploma ya kilimo napambania ajira bila mafanikio nilipost hapa JF kuwa nafanya development ya mobile apps kwa watu ambao wanamiliki blog na wanapenda kutengenezewa mobile apps za blog zao, baada ya siku chache nikapokea simu ya moja ya iliyokuwa miongoni mwa blog kubwa za michezo, hapo ndio ilikuwa deal la kwanza ambalo nilipata kutokana na kujifunza apps dev kwa njia ngumu (hapa napenda kusema kuwa JF ya sasa sio ile ya zamani, hapo zamani JF ilikuwa rahisi kupost kitu na kupata solution, JF ya leo watu wamejaa masihala mengi). Nilifanya ile kazi kwa bei ya 500,000 ambayo ilikuja kwa wakati ambao nilikuwa sina hela na ninapaswa kuhudhuria interview ya kazi so ujuzi wa IT ulinibeba sana maana bila hivyo nisingeweza kabisa kwenda kwenye hiyo interview na ashukuriwe Mungu niliipata ile kazi na moja ya vitu ambayo vilinibeba ni ku_prove uwezo wangu kupitia kazi niliyofanya ya kutengeneza app ya blog hiyo iliyokuwa maarufu kwa sports.

Baada ya kuanza kazi 2016, nilipitia kipingi kigumu kwa kuwa mshahara ulikuwa haukidhi mahitaji yangu yote. katika kujitafuta zaidi nikaja na app iliyojulikana kama OnlineTV app ambayo naamini wengi baadhi yenu humu wamewahi kuwa watumiaji wa ile app kati ya December 2016 hadi 2017 mwishoni ambayo ilikuwa miongoni mwa trending apps za kutazama mpira. Kiukweli ile app ilikuwa msaada mkubwa kuniwezesha kiuchumi maana nifanya monetization ya matangazo ya Google so nikawa napata wastani wa 2M-2.5M kwa mwezi kutoka kwenye app plus mshahara wa kazini nikawa nafunga hesabu nzuri kila mwezi. Lakini baadaye mambo hayakwenda sawa, nilifunga operation za OnlineTV app.

Baada ya hapo, nikakomaa na kazi tuu ya ajira, lakini 2023 ajira ikaisha so nikaamua kurudi tena rasmi kwenye njia yangu ya kipato ambayo hunikwamua kila ninapo kwama (IT). Hapo nikaja na app ya kuwasaidia wafanya biashara wadogo na wakati kusimamia taarifa za biashara zao ambayo wanailipia kila mwezi. Hivi sasa imepita miezi 6 tangu nimalize ajira na app hii ina miezi 3 tuu ila imekuwa ikinipa uhakika wa maisha na wakati huo huo imekuwa msaada kwa wafanya biashara ndani na nje ya Tanzania. Sasa nimeisajili kama biashara rasmi na nimeweka wafanyazi 2 kusaidia customer care na kwa level ambayo nimefika sitaki kazi tena maana IT imekuwa njia sahihi ya mafanikio kwangu.

Napenda kuwashauri vijana wengine ambao mko interested na IT Do it with all your heart, believe in the solution you build, and consistency is the key to success. Online kuna pesa nyingi sana zinakusubiri wewe.

Ahsanteni.
 
Mkuu kwa hiyo mpaka sasa hujagusa class zaidi ya kujisomea online tu

Maana binafsi nilijitahidi sana lakini naona kujisomea mwenyewe tutorial za mtandaoni kama ngumu hivi
Sijagusa darasa lolote la IT, nimekomaa online mwenyewe, nimesoma kilimo, ila toka nimalize 2015 hadi muda huu nipo kwenye field ya IT kwa sababu ya kujisomea mwenyewe.

baadhi ya site ambazo zimekuwa msaada mkubwa ni w3schools, stackoverflow, udemy pamoja na youtube. Kila nilipokwama nilitengeneza post na kuuliza stackoverflow.
 
Safi sana mzee
 
OnlineTV app ambayo naamini wengi baadhi yenu humu wamewahi kuwa watumiaji wa ile app kati ya December 2016 hadi 2017 mwishoni ambayo ilikuwa miongoni mwa trending apps za kutazama mpira.

Heko mkuu...

Hivi hii ndio ile app tozo ilikuwa buku 2?
 
Ujakutana na steji IT ila hii ya hapa ni ya kawaida tu hongera.
ukienda USA ndio utaona IT yeru ni candycrash
Nimekutana na developers wengi wazuri, kwenye interaction mbalimbali kwenye developers forums, so najua kabisa kuwa mimi sio developer wa viwango vikubwa, lakini at my level IT inaniwezesha kuishi bila wasiwasi.
 
Heko mkuu...

Hivi hii ndio ile app tozo ilikuwa buku 2?
Yes, Ilikuwa na logo hii

1708622604242.png
 
Kwanza nikupe pongezi kubwa sana kwa kuwa na akili. Umeandika mambo ambayo ni ya msingi sana na nlitamani vijana wengi wasome huu uzi na wakutafute uwasaidie kiushauri.

nafurahi napoona kuna watu wana akili hii hapa JF. Kipindi hiki JF iliharibika sana kulikuwa na uingizaji holela wa members. Ambao umeathiri sana mada za JF. Mimi nlishajichokea na huu uzee na majukumu. Siku hizi kuna vilaza wengi humu wanakuja nyuzi za kipuuzi hazina tija. Unakuta kijana anaanzisha uzi kuwa Ommie anapata wapi pesa mbona anaishi... Unashangaa hizi tabia mbona wanawake wameacha inakuaje walio leave group wanaendeleza?

MIMI NAKUSHAURI PATA MUDA ONGEA NA VIJANA WENZIO. MKAE CHINI MSAIDIANE WAACHE TABIA YA KUTAFUTA "CONNECTION" NA MADEMU. Hii ni moja ya thread nzuri kwa mwaka huu siyo zile nazoanzisha mimi sometimes za kipuuzi.
 
Ahsante sana.
Vijana wengi hawaamini kwenye kile wanachofanya. JF ya zamani kuna watu nawafahamu walipost wanatafuta kazi na walipata connection za ajira kupitia JF, ila hii JF ya sasa ukijichanganya kupost kitu serious umeisha, utapata comment nyingi za ovyo.
 
Kwanza nikupe pongezi kubwa sana kwa kuwa na akili. Umeandika mambo ambayo ni ya msingi sana na nlitamani vijana wengi wasome huu uzi na wakutafute uwasaidie kiushauri.

nafurahi napoona kuna watu wana akili hii hapa JF. Kipindi hiki JF iliharibika sana kulikuwa na uingizaji holela wa members. Ambao umeathiri sana mada za JF. Mimi nlishajichokea na huu uzee na majukumu. Siku hizi kuna vilaza wengi humu wanakuja nyuzi za kipuuzi hazina tija. Unakuta kijana anaanzisha uzi kuwa Ommie anapata wapi pesa mbona anaishi... Unashangaa hizi tabia mbona wanawake wameacha inakuaje walio leave group wanaendeleza?

MIMI NAKUSHAURI PATA MUDA ONGEA NA VIJANA WENZIO. MKAE CHINI MSAIDIANE WAACHE TABIA YA KUTAFUTA "CONNECTION" NA MADEMU. Hii ni moja ya thread nzuri kwa mwaka huu siyo zile nazoanzisha mimi sometimes za kipuuzi.
Fungus pm, hiyo ya biashara ni app au web
 
Back
Top Bottom