Ismail Jussa amtukana Sitta, Nyerere na wa Tz Bara!

Nimesikiliza kwa umakini wa hali ya juu hotuba ya Ismail Jusa akimjibu Samwel Sitta. Kwa kweli wanasiasa wa aina ya Ismail Jusa kwa kweli ni hatari kwa Amani, mshikamano na Muungano wa Tanzania na ni hatari kwa Taifa. Mimi sijui hii nchi inakwenda wapi ....wakiongea watu wengine maneno hayo ya JUSA nadhani wangefunguliwa kesi nyingi tu.... JUSA ni nani katika nchi hii ? Polisi walitakiwa wamkamate right away baada ya mazungumuzo hayo....Sijui nchii hii inakwenda wapi ?

Grounds za kukwamatwa:

1. Hate Speech/uchochezi

2. Matusi

Hizi tu zinatosha yeye kwenda jela kwa muda kidogo....

Kuwa na busara, unaanzisha mada isio na mashikio, kwani kasema kitu gani, naona una bwabwaja tu. Nukulu alicho kukera
 
Kusema kweli lugha alotumia Ismail Jussa kama kiongozi wa CUF nadhani amefanya makosa makubwa sana ktk lugha. Ni mtu hatari sana ktk siasa za nchi na pengine anaiweka Zanzibar mahala pabaya zaidi..Sii tu kamtukana Sitta bali kamwita hata Marehemu Nyerere kwa dharau kubwa huku akimsifia Karume kwa hoja ambazo hazifahamu...Huyu mtu hajui lolote kuhusu Muungano wala Mapinduzi isipokuwa ni mmoja wa watu wanaochukia Muungano na hata Mapinzudi leo anajifanya mpenzi mkubwa wa Mapinduzi ya Zanzibar...

Angekuwa mtu kutoka baraza la Mapinduzi sidhani kama angetumia lugha hii na ajabu sana huyu huyu alikuwa akiwatukana kina Karume sasa maajabu ktk Hotuba hii namwona akimpa sifa...Na sijui kama amefikiria kwa nini hakumuuliza Nyerere maswali haya wakati akiwa hai amesubiri hadi kafa ndio anayasema..Haya yetu macho na siasa za Chuki!
 
Nawaambia hivi, ili kumuenzi Nyerere kwa yooooote aliyoyafanya, mazuri na mabaya, pamoja na huu Muungano inabidi muuendeleze, hivi hapo kuna tusi lipi? si kaambiwa mjinga, sasa hilo nalo tusi? Hivi Sitta ana ujanja upi? maskini ya Mungu, mimi namuoena sana huruma yule mzee, kwanza katukanwa na chama chake kuondolewa uspika. Halafu CCM walipojuwa kuna mjadala waa Muungano wa kumsukumizia yeye, si wanajuwa huyu kabaki CCM ana malengo, sasa niambieni, huyo atawapata Wazanzibar akiutaka Urais, kwa hayo wanayoyaongea? hakubaliki mawee! habari zake kwenye siasa kwisha.

Nawahakikishia vyama vya upinzani, jimbo la huyu mzee 2015 ni lao pengine hata kabla. Kwisha kazi yake kisiasa hana pakutokea. Alicheza turufu zake vibaya.
 
Kumbuka, likija suala la Muungano Wazanzibar woote wanakuwa ni wamoja, huo ndio uzalendo. Na umemsikia Jussa akisema, inawauma sana kuona Wazanzibar wamekuwa kitu kimoja na mlitaka ile "divide and rule" wameistukia. Unajuwa nani aliwastua? Prof Haroub Othman.
 
Ninakubaliana na wewe Bi. FF kuwa neno linaweza kuwa tusi au lisiwe kutokana na "tune and context" ya linapotumika. Mimi neno mjinga hapa nimelichukulia kuwa ni tusi kutokana na yote mawili. Inawezekana pia neno analolihisi mwengine kuwa ni tusi mimi nikaliona ni tusi, mfano ni pale Jussa aliposema kwenye hotuba hii: "Sisi hatuhitaji kubebwa. Sisi kazi yetu si kubebwa bali ni wabebaji", hapa neno kubebwa linaweza kuwa tusi.

Kuhusu Reference ni Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Ama kuhusu suala la Sitta kutoka nafasi ya uspika hadi uwaziri wa Afrika Mashariki kuwa ni ujinga au uerevu, hilo mimi siwezi kulisemea hata kidogo kwani sina ujuzi wa kujua maslahi yake katika sehemu moja au nyengine.

Kumbuka, hakuondolewa na hapohapo akapewa uwaziri.
 
Kumbuka, likija suala la Muungano Wazanzibar woote wanakuwa ni wamoja, huo ndio uzalendo. Na umemsikia Jussa akisema, inawauma sana kuona Wazanzibar wamekuwa kitu kimoja na mlitaka ile "divide and rule" wameistukia. Unajuwa nani aliwastua? Prof Haroub Othman.
Wee unaamini maneno hayo....Huyu Jussa hajui kilichotokea na wala haielewi Mapinduzi wala Muungano yalitokana na nini isipokuwa mjinga mmoja ambaye kabeba dhamana asoijua...wanaume hawa hapa awatazame vizuri..
 
Last edited by a moderator:
Wee unaamini maneno hayo....Huyu Jussa hajui kilichotokea na wala haielewi Mapinduzi wala Muungano yalitokana na nini isipokuwa mjinga mmoja ambaye kabeba dhamana asoijua...wanaume hawa hapa awatazame vizuri..

Sidhani hata kama na wewe unauelewa Muungano.

Babu mwenyewe unamsikia hapo, alikuwa hajui, Jee, ni nani alikuwa anajuwa? Nyerere.
 
Sidhani hata kama na wewe unauelewa Muungano.
Nauelewa kuliko Jussa maana huyu alikuwa upande wa pili....hawa wote Karume na Babu walikuwa bara wakati wa Mapinduzi Je, anajua mipango na kilichofanyika kabla? Hapo alipo hajui hata Pan africanism ilikuwa na malengo gani..
 
Kapatikana, kutoka kuwa mhimili mmoja wa dola mpaka kuwa una "report" kwa waziri wa mambo ya nje, kama si kupatikana ni nini? Alikuwa ana uwezo wa kumnyamazisha hata Waziri Mkuu Bungeni, hata Rais anakuwa chini yake anapokuwa bungeni. Dahhh, mimi namuona ni mjinga sana kuendelea kubaki CCM.

Da Foxy
Uongzi, Siasa na Demokrasia Havitaki hasira, unatakiwa uwe mvumilivu, mwenye subra yahaliya juu, busara na Hekima tele.
Na hayo ndo yatakufanya kiongozi wa kuaminika na kutumainiwa. Kwa hiyo mitihani ikikutokea/kumtokea kiongozi wa kisiasa na hata asie wa kisiasa au hata katika mambo yetu ya kawaida tukizingatia hayo mambo manne hapo juu yana weza kusaidia, kabla ya kutoa maamuzi yetu.
 
Nauelewa kuliko Jussa maana huyu alikuwa upande wa pili....hawa wote Karume na Babu walikuwa bara wakati wa Mapinduzi Je, anajua mipango na kilichofanyika kabla? Hapo alipo hajui hata Pan africanism ilikuwa na malengo gani..

Wewe hodari kwa kuujuwa Muungano kuliko Jussa. Mada ni: Sitta mjinga - Jussa.
 
Da Foxy
Uongzi, Siasa na Demokrasia Havitaki hasira, unatakiwa uwe mvumilivu, mwenye subra yahaliya juu, busara na Hekima tele.
Na hayo ndo yatakufanya kiongozi wa kuaminika na kutumainiwa. Kwa hiyo mitihani ikikutokea/kumtokea kiongozi wa kisiasa na hata asie wa kisiasa au hata katika mambo yetu ya kawaida tukizingatia hayo mambo manne hapo juu yana weza kusaidia, kabla ya kutoa maamuzi yetu.

Kama ni hivyo basi na hili la ujinga na upumbavu asichukulie mtu yeyote kama ni tusi, achukulie kuwa ni siasa na demokrasia. Kwanini yote yaweze kustahamilika, watu wanachapana mpaka makonde, mpaka risasi, virungu, mabomu, yote hayo ni sawa, lakini anapooneshwa sitta "ujinga" na "upumbavu" wake (Jussa) iwe mwao? kwanini? kwa kuwa Jussa ni chaguo la Kikwete kwenye Ubunge?

Kashaitwa mjinga, sasa nyinyi mnasemaje ni mjanja au mjinga Sitta kuung'ang'ania muungano?
 
Wewe hodari kwa kuujuwa Muungano kuliko Kussa. Mada ni: Sitta mjinga - Jussa.
Dada swala hapa ni hotuba ya Jussa ndio inajadiliwa hata kichwa cha mada kinajieleza..Haya ni matusi makubwa sana kwetu sote!... Usipende sana kumtetea mtu alofanya makosa makubwa japokuwa mimi sio mwana CUF lakini as a politician Jussa hakutakiwa kabisa kuyasema haya maana anaitenganisha bara na visiwani na kuwafanya wafuasi wa CUF bara kujiona hawatakiwi..

Halafu huwezi kumtukana mwalimu ktk nchi ambayo bado inampa heshima zote kama Mtawala iwe hata Mkapa au JK maadam wewe ni kiongozi ndani ya serikali ilotokana na muungano huo. Hutakiwi - bali unazungumza kwa mazuri ya Muungano wenyewe unataka uwe wa aina gani?.na hata mabaya unayaweka ktk maslahi na sii watu unaowatumikia kisiasa...

Sote tunaelewa kilichofanyika Zanzibar, weka madai yako kwa misingi ya kuelemisha watu, mara amwite Sitta mjinga kisha ajiite yeye mwenyewe mjinga akielimika.. yaani upuuzi mtupu..

Kuhusu swala la Babu umeuliza kwamba alikuwa hayupo - alikuwa Bara Dar es Salaam... Sasa kama anavyosema JK unatakiwa kuchanganya na za kwako kama mbayuwayu. Aliyepindua na ambaye anajua ni Okello yuko hapo hapo waliposimama, imekuaje Babu ndiye msemaji mkuu na wamekutana vipi hapo hadi Babu aseme alikuwa hajui? ...It's politics dadaangu!
 
Dada swala hapa ni hotuba ya Jussa ndio inajadiliwa hata kichwa cha mada kinajieleza..Haya ni matusi makubwa sana kwetu sote!... Usipende sana kumtetea mtu alofanya makosa makubwa japokuwa mimi sio mwana CUF lakini as a politician Jussa hakutakiwa kabisa kuyasema haya maana anaitenganisha bara na visiwani na kuwafanya wafuasi wa CUF bara kujiona hawatakiwi...
Halafu huwezi kumtukana mwalimu ktk nchi ambayo bado inampa heshima zote kama Mtawala iwe hata Mkapa au JK maadam wewe ni kiongozi ndani ya serikali ilotokana na muungano huo. Hutakiwi - bali unazungumza kwa mazuri ya Muungano wenyewe unataka uwe wa aina gani?.

Sote tunaelewa kilichofanyika Zanzibar, weka madai yako kwa misingi ya kuelemisha watu, mara amwite Sitta mjinga kisha ajiite yeye mwenyewe mjinga akielimika.. yaani upuuzi mtupu..

Kuhusu swala la Babu umeuliza kwamba alikuwa Bara, sasa kama anavyosema JK unatakiwa kuchanganya na za kwako kama mbayuwayu. Aliyepindua na ambaye anajua ni Okello yuko hapo hapo waliposimama, imekuaje Babu ndiye msemaji mkuu na wamekutana vipi hapo hadi Babu aseme alikuwa hajui...

Sitta kuung'ang'ania muungano ni ujanja au ujinga? kwangu mimi naona ni ujinga tu. Hakuna tusi hapo. Tushawaona chadema wakitukana majukwaani zaidi ya hivyo. Kumuita mtu mwizi ambae hauna ushahidi sio tusi hilo?
 
Haya ndio matusi tena ya nguoni:
igunga.jpg

Sitta kuung'ang'ania muungano ni ujanja au ujinga? kwangu mimi naona ni ujinga tu. Hakuna tusi hapo. Tushawaona chadema wakitukana majukwaani zaidi ya hivyo. Kumuita mtu mwizi ambae hauna ushahidi sio tusi hilo?
Sitta hang'ang'anii muungano bali lilikuwa jukumu lake kujibu hoja.. Bungeni unapouliza swali la ziada lazima mjumbe mwakilishi alijibu na kama umemsikia akisema Pinda hakuwepo, hivyo Sitta alikaimu nafasi ile.

Na kwa utovu wa adabu huyu Jussa hajui kwamba anayoyasema Pinda au Sitta sii maneno yake mwenyewe bali yanatokana na mfumo uliopo kisheria. Sii maneno ya Sitta hata kama angesimama Nahodha kama ndiye Waziri mkuu ama kaimu lazima angejibu kulingana na msimamo wa serikali hizi mbili. Majibu yake yangekuwa kinyume cha vile wengi (wazanzibar) walivyotegemea kwani hii sio mara ya kwanza kuhojiwa bungeni.. Kumbuka tume zote zilizokwisha fanyika kuhusiana na swala la Muungano tume tisa (9) na hakujapatikana ufumbuzi..

Kwa hiyo kumwita mtu mwizi wakati ndio ukweli wenyewe haiwezi kubadilisha kitu.. Nitakwambia hawa kina Jussa wanafikiri nini. wanachotaka wao ni kwamba ziwepo serikali tatu na Pato likipatikana ligawanywe sawa kwa uuwiano wa nchi mbili (nusu kwa nusu) wakati bara ina population zaidi ya milioni 40 wao wakiwa chini ya mbili sijui hata kama moja inafika..Haya mengine yoote ni danganya toto wanataka zaidi na zaidi kutoka bara ama muungano ufe..

Hii akili kweli ati fungu kubwa linaenda bara wakati wanajua tofauti kubwa zilizopo..Kwa hiyo hata kama tutaunda serikali tatu na Zanzibar ikakusanya mapato yao kama wanavyofanya hadi sasa.. pato lao ni lao lakini matatizo ya mgawanyo wa fungu la Taifa ktk states toka Federal litazua upya matatizo yale yale kwa sababu hawa watu sii kwamba wanalilia haki ya Wazanzibar bali wanataka muungano ufe wao kwa sababu wana uwezo na fedha watawale kama Sultan wawapake dada zetu chokaa uso mzima angalau waonekane weupe maana wanatisha na weusi wao..
 
Hadithi ndefu isyo na mppango, kama kawa.

Mimi nasema Sitta ni mjinga kama alivyosema Jussa, hivi mtu mjanja atakaa atetee Muungano? oooh, eti anajibu hoja. Kujibu hoja ndio utajibu usichokiamini? Unanchekesha! Kuung'ang'ania Muungano ni ujinga, tuliingizwa mkenge na Nyerere kwa matakwa ya kanisa katoliki. Sasa Wabara hatuutaki na Waunguja hawautaki, yoyote anaeung'ang'ania mimi namuona mjinga tu.
 
Kukubali kutokubaliana na hekima kuliko kutumia maneno makali na matusi. Ndugu yangu Jussa naamini kabisa atakubaliana na mimi kwa hilo.
 
Nawaambia hivi, ili kumuenzi Nyerere kwa yooooote aliyoyafanya, mazuri na mabaya, pamoja na huu Muungano inabidi muuendeleze, hivi hapo kuna tusi lipi? si kaambiwa mjinga, sasa hilo nalo tusi? Hivi Sitta ana ujanja upi? maskini ya Mungu, mimi namuoena sana huruma yule mzee, kwanza katukanwa na chama chake kuondolewa uspika. Halafu CCM walipojuwa kuna mjadala waa Muungano wa kumsukumizia yeye, si wanajuwa huyu kabaki CCM ana malengo, sasa niambieni, huyo atawapata Wazanzibar akiutaka Urais, kwa hayo wanayoyaongea? hakubaliki mawee! habari zake kwenye siasa kwisha.

Nawahakikishia vyama vya upinzani, jimbo la huyu mzee 2015 ni lao pengine hata kabla. Kwisha kazi yake kisiasa hana pakutokea. Alicheza turufu zake vibaya.

Labda unataka kuuliza "Sitta ana werevu upi?" Maana "ujanja" ni sifa mbovu tu kama ujinga. Nikisema wewe unaonekana mjanja-mjanja bila shaka ni sifa mojawapo ya vibaka.
 
Back
Top Bottom