TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

R.I.P mwandishi wa habari hakika sina maneo mengi ila naomba chadema wachukue hatua na mimi binafsi niko tayari kwa lolote vinginevyo itakuwa ni upumbavu kila mkutano wacdm watu wanauwawa.
 
Ili mradi kinachoendelea kwenye wizara mbalimbali ni UOZO kuliko mazuri yanayohitajika mwa manufaa ya wananchi, basi kususia kuandika habari za wizara ya mambo ya ndani ni sawa na kususia kuandika uozo wa wizara hiyo....ni sawa na kuacha maovu ya wizara hiyo yaote mizizi....ningekuunga mkono endapo ungesema kwamba sasa ni wakati wa vyombo vya habari kuuvalia njuga uozo wa wizara hiyo na kuuanika kila uchao......kwamba, kila toleo litokalo, basi ndani ni uozo wa wizara hiyo!

Uko sahihi mkuu. Ngoja ninyooshe kidogo kuwa habari zote nzuri wasiandike bali zile mbaya ruksa na ikiwezeskana hata zile mbaya za wizara nyingine ruksa na in total mbaya kwa serikali ruksa. Wananchi wanatakiwa wafahamu kwa undani jinsi gani serikali yao kupitia jeshi la polisi linaua vijana wao. With this, marks the end of SSM.
 
Dr Slaa aliposema nchi haitatawalika nilidhani ni jazba na hasira za kukosa urais ambao anauota siku zote,lakini sasa hivi ninapata picha kamili ya dhamira yake.Anatumia kila njia kuhalalisha ujambazi wake wa siasa kufikia malengo yake,shime watanzania tukatae siasa za aina hii, Dr Slaa ni Foday Sankoh mwengine anatoa kafara watu ili afanikiwe katika malengo yake.Nilishangaa kuona wanafanya party kwa mchungaji Msigwa baada ya mauaji ya Morogoro sitostaajabu sasa hivi akiwa anakunywa mvinyo kujipongeza kwa kifo cha Daudi Mwangosi.Roho za watanzania hawa zitakuandama popote uendako..

Mungu anafahamu unachokitetea ndani ya ccm.
 
Mie siandiki kitu leo. Ila ninachukua mda kumtafakari yule ***** aliyesema ana degree ya sheria.
.
 
CHADEMA...tunaomba msitishe M4C.. Kiroho safi kabisa.
Tuache Unafiki.
 
KWAHISANI YA MZEE WA MATUKIO(Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima)

IMG_1935.JPG


IMG_1917.JPG


IMG_1943.JPG


IMG_1983.JPG


Gari%2Bya%2Bkamanda%2Bwa%2B%2Bpolisi%2Bmkoa%2B%2Bwa%2BIringa%2BMIchael%2BKamuanda%2Bakiongoza%2Bmsafara%2B%2Bwa%2BFFU.JPG


Daud%2BMwangosi%2B%2Bkulia%2Benzi%2Bza%2B%2Buhai%2Bwake.JPG

Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake

ofisi%2Bya%2BChadema%2BNyololo%2Bikifuk%2Bmoshi%2B%2Bwa%2Bmabomu.JPG


Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo


Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .


Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.


Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .


Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .


Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.


Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.


Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.


" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza


Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.


"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.


Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.


Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .


Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.


"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.


Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
MWISHO
 
A government big enough to give you everything you want is big enough to take away everything you have.
Jamani haka kanchi ketu ni kadogo sana sasa inakuwaje hii serikali haitupi kile tutakacho na bado inachukua kile tulichonacho. Mwandishi wa watu hana hatia amepumzishwa pole watanzania na familia yake kwa ujumla
 
Dr Slaa aliposema nchi haitatawalika nilidhani ni jazba na hasira za kukosa urais ambao anauota siku zote,lakini sasa hivi ninapata picha kamili ya dhamira yake.Anatumia kila njia kuhalalisha ujambazi wake wa siasa kufikia malengo yake,shime watanzania tukatae siasa za aina hii, Dr Slaa ni Foday Sankoh mwengine anatoa kafara watu ili afanikiwe katika malengo yake.Nilishangaa kuona wanafanya party kwa mchungaji Msigwa baada ya mauaji ya Morogoro sitostaajabu sasa hivi akiwa anakunywa mvinyo kujipongeza kwa kifo cha Daudi Mwangosi.Roho za watanzania hawa zitakuandama popote uendako..

Nilidhani una kitu cha kuandika, acha ushabiki wa kishirikina. Kwa hiyo watoa kafara ni polisi si ndio?
 
R.I.P bro.SIKU ZOTE HAKI HUCHUKIWA NA WENGI,DAMU YAKO NA Y A WANA HARAKATI WALIOTANGULIA HAZIJAMWAJIKA BURE.USHINDI NI LAZIMA UPATIKANE.
 
watu wanataka umaarufu mdau,,,,,,polisi na chadema wote wanatafuta popularity,unadhan RPC HAPENDI KUPANDISHWA CHEO ZAID YA HIKO????NA HAO WATU WA CHADEMA PIA WAPO KAZINI,,,,,,,ILA RAIA WA KAWAIDA NDIO TARGET YAO,,,,,,,SIJAWAH KUSIKIA AU KUONA KIONGOZ WA CHADEMA AMEKWANGURIWA WALAU NA RISAS,WALA POLISI KUPIGWA HATA JIWE,TANGU ARUSHA,TARIME,MORO HADI LEO IRINGA,INA MAANA HAWA WANAJUANA,,,,,,POLIS N CHADEMA,ndo maana yule jamaa wa morogoro alisema SISI WENYE GWANDA WAMETUACHA WAMEENDA KUMUUA MTU ASOYEHUSIKA,REFER SINGIDA PIA

Huyu Kamanda wa sasa wa Iringa NDIE YULE ALIYEONGOZA MAUAJI YA WABODA BODA SONGEA, MAUAJI NI JADI YAKE. JE HUO UMAARUFU HAUMTOSHI? TO HELL POLICCM!
 
nchi ikiingia vitani c.c.m watalumiwa kwa kuwatumia polisi kuzuia mikutano harali ya kichama. c.c.m munachochea hasira kwa raia halafu mukiua munaanza kusinhizia na kutoa uongo. polisi na jua hawataki haya isipokwa makamanda wamepewa maagizo wafanye hivyo. mskini polisi;
 
Dr Slaa aliposema nchi haitatawalika nilidhani ni jazba na hasira za kukosa urais ambao anauota siku zote,lakini sasa hivi ninapata picha kamili ya dhamira yake.Anatumia kila njia kuhalalisha ujambazi wake wa siasa kufikia malengo yake,shime watanzania tukatae siasa za aina hii, Dr Slaa ni Foday Sankoh mwengine anatoa kafara watu ili afanikiwe katika malengo yake.Nilishangaa kuona wanafanya party kwa mchungaji Msigwa baada ya mauaji ya Morogoro sitostaajabu sasa hivi akiwa anakunywa mvinyo kujipongeza kwa kifo cha Daudi Mwangosi.Roho za watanzania hawa zitakuandama popote uendako..

hujitambui we *****!
 
sio siri chadema hata kama hamhusiki ni rahisi kabisa kuunganisha hizi vurugu na haya maandamano kumbukeni kuwa watanzania wengi hawajaelimika na msifananishe hata kidogo maandaman yenu na yale yaliyotokea kule misri kwa sababu zifuatazo:
. Maandamano ya misri yalikuwa yanaongozwa na wananchi wa kati( middle class)
.maandamano ya cdm yanahusu vijana ambao hawajui watapata nini siku ya mwisho
masaburi kazini!....
 
Hawa polisi sasa its too much,wanashindwa kupambana na mafisadi wanapambana na raia wema.R.i.p mwandishi wetu.
 
Back
Top Bottom