Asanteni Jeshi la Polisi Wanawake Mkoa wa Manyara

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Pongezi nyingi ziwafikie Polisi wote wanawake Mkoa wa Manyara. Mmefanya jambo la utu. Kuwemo kwenye magwanda ya kijeshi hakujawaondolea moyo wa huruma.

Asanteni sana. Nimeguswa mno na hilo mlilomfanyia huyo mama mjane.

Najua mliwashirikisha askari wa vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, lakini kwa kuwa ni nyie ndiyo mlioratibu, ni sahihi kusema ni tukio lililoandaliwa na Jeshi la Polisi wanawake Mkoa wa Manyara.

Mmeonesha mfano bora unaofaa kuigwa. Mungu awabariki sana wote mlioshiriki kwa namna Moja au nyingine kulifanikisha jambo hilo la baraka kwa mama mjane.

Asanteni sana askari wetu wanawake. Asanteni sana Jeshi la Polisi!

Tumefurahi sana🙏
 

Attachments

  • MJANE_ABUBUJIKWA_MACHOZI_BAADA_YA_ASKARI_WA_KIKE_MANYARA_KUMFANYIA_TUKIO(240p).mp4
    21.3 MB
Mwingine amefanikisha jambo lake kuichonokoa cctv na mumewe kucharangwa mapanga!
 
Back
Top Bottom