TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

Hakuna namna magamba yanaweza kuichonganisha CDM na wananchi kwani wananchi walio wengi sasa wameelimika wanajua kuwa chadema haimiliki mabomu wala hainajeshi na kwanini watu wafe wakiwepo polisi tu?
 
RIP Daud mwangosi,
Nimeumizwa sana na taarifa hizi ambazo mpaka sasa hazieleweki tukio lilivyokuwa lakini itoshe kusema kuwa amekufa.

M.Byabato
Channel ten Kagera
 
Nadhani bado hujanielewa. Soma taratibu nilichoandika. Kwa muda polisi wamekuwa wanaua raia (in general) lakini sasa wanaanza kugeukia waandishi wa habari. Na hapa ndipo hali inazidi kuwa tete maana sio tu wanataka kuuwa raia, ila wanataka kuzuia hata taarifa za mauaji zisiandikwe - (kill wana habari).

thanks, ngoja nikasome upya
 
  • Thanks
Reactions: FJM
IMG_1878.JPG


Kamanda wa mauaji Iringa Michael Kamuhanda!
Eti mkuu wa polisi mkoani...kashiba rushwa hadi shati halimtoshi, shenzi type!
 
[ msifananishe hata kidogo maandaman yenu na yale yaliyotokea kule Misri kwa sababu zifuatazo:
. maandamano ya misri yalikuwa yanaongozwa na wananchi wa kati( middle class)
.maandamano ya cdm yanahusu vijana ambao hawajui watapata nini siku ya mwisho[/QUOTE]
Mkuu umeona mbali, thts ndivyo inavyopaswa kujudge mambo na sio kukurupuka tu!
 
Hakika chadema nawasihi lazima kitu kifanyike, hii haikubaliki. Naamini kwa vichwa vyenu, this is too much....!
RIP my friend Mwangosi!
 
Nashauri waandishi wa habari muungane na wamiliki wa vyombo vya habari msiandike kabisa habari za Wizara ya Mambo ya ndani na zile za SSM. Kweli kifo hiki hakikuwa cha lazima, tear gas zilitosha tu kuwakimbiza hao CDM. Ogopeni damu, polisi, hizo damu zitawalilia. Mtalaanika. Naogopa mno kifo sembuse kuua. So sad.

unazungumzia waandish wa habari wa nchi gani wewe????hebu toa ufafanuz???kama ni tanzania hilo usilitegemee
 
Kama wao wanafanya hivi badala ya kulinda raia,washtakiwe wapi?



Sio washitakiwe mkuu hawa polisi wanaishi mitaani kwetu chakufanya nikuviziana tu, kwa nondo, kwa sululu si tunalalanao. Hawawezi kuchukuliana hatua wao kwa wao.
 
watu wanataka umaarufu mdau,,,,,,polisi na chadema wote wanatafuta popularity,unadhan RPC HAPENDI KUPANDISHWA CHEO ZAID YA HIKO????NA HAO WATU WA CHADEMA PIA WAPO KAZINI,,,,,,,ILA RAIA WA KAWAIDA NDIO TARGET YAO,,,,,,,SIJAWAH KUSIKIA AU KUONA KIONGOZ WA CHADEMA AMEKWANGURIWA WALAU NA RISAS,WALA POLISI KUPIGWA HATA JIWE,TANGU ARUSHA,TARIME,MORO HADI LEO IRINGA,INA MAANA HAWA WANAJUANA,,,,,,POLIS N CHADEMA,ndo maana yule jamaa wa morogoro alisema SISI WENYE GWANDA WAMETUACHA WAMEENDA KUMUUA MTU ASOYEHUSIKA,REFER SINGIDA PIA
Dada Bajabiri inaelekea Arusha hukuangalia au ulikuwa unamlisha mtoto?
 
unazungumzia waandish wa habari wa nchi gani wewe????hebu toa ufafanuz???kama ni tanzania hilo usilitegemee
Mkuu nime-assume wana umoja kwa hiyo mambo ya njenje sikuyafikiria!!! Ila pia sikuwaza kuwa kuna vyombo vya habari kama magazeti ya serikali, na TBC zote kuwa ni pro SSM, na pia magazeti kama ya New habari Corporation ni fisadi ambao wanaogopa CDM. The list is long but tufika wakati hata kwa muda waandishi wasitishe huduma. Ingekuwa nchi za wenzetu wangetoa msimamo. Ngoja tusikie MOAT na MCT kama watasema chochote.
 
Hiv askari siku hiz kazi yao ipi, kwenye uharif huwa hawatokei ila wanaongoza kwa kuomba rushwa, kuuwa raia wasio na hatia na kuanzisha vurugu. Hili jeshi halina faida hata kidogo bora lisingekuwepo km wameongezewa jukumu la kuua raia basi itangazwe. wauaji wakubwa
 
IMG_1878.JPG


Kamanda wa mauaji Iringa Michael Kamuhanda!
Eti mkuu wa polisi mkoani...kashiba rushwa hadi shati halimtoshi, shenzi type!

kweli huyu KAMANDA,,,,,,DUH ANAFANYA MAZOEZ KIAS KWAMBA HAD SHAT HALIMTOSHI
 
Kama walikuwa wanafungua ofisi kijijini nani aliwaita hao polisi? Walitokea wapi? Nani kamada wa kikosi hicho? Walikuwa wangapi?

Wanachama wa CDM au watu wote kwenye eneo walikuwa wangapi? Wanafanya nini?

Polisi wanatoa amri ya kutawanyika kwa sababu gani? Je walipata muda gani kuandika hilo tambara?

Je walitoa amri au ni baada ya kuwasiliana na uongozi?



JAKAYA MRISHO KIKWETE damu hii ya watanzania itakudai, usijifanye hujui, honi husikii yanayotokea. KAMA UMESHINDWA KULINDA WANANCHI ACHIA NGAZI KIUNGWANA

(Mod naomba hata nitukane kimoyo moyo labda hasira yangu itapingua kwa serikali hii uaji)
 
Pole kwa familia ya marehemu Daudi Mwangosi.
Jeshi la policcm limeamua kuwaua wananchi wasio na hatia wakidhani kwa kufanya hivyo watainusuru ccm na kifo mwaka 2015.
Natarajia kuona makali ya kalamu za wanahabari katika tukio hili. Hawa jamaa wamewatumia sana na sasa wameamua kuanza kuwaua.
 
Back
Top Bottom