Iringa: Mwanafunzi afa kwa kujaribu kutoa mimba

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
[h=3]BREAKINGNEWS.........MWANAFUNZI ATUKWA AMEKUFA KWA KUTOA MIMBA KTK CHUMBA CHA MWANAFUNZI WA CHUO[/h]
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Iringa aliyetambuliwa kwa jina la Yasinta Kasuga amekutwa amekufa eneo la Ngome katika Manispaa ya Iringa akiwa ndani ya chumba cha kijana ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini mjini Iringa.

Taarifa za mashuhuda wa tukio hilo ambao wameteta na mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima wamedai kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akifika katika nyumba ya mwanafunzi huyo mara kwa mara na wamekuwa wakiishi kama mke na mume japo wote ni wanafunzi.

Hivyo walisema kuwa kutokana na mazoea hayo walichukulia watu hao kama ni wapenzi na kuwa hata siku ya tukio walipotapa taarifa ya mwanafunzi huyo kufa walitegemea kijana huyo kuwajulisha ila cha kushangaza kijana huyo hakupata kuonekana kabisa na badaal yake kuutelekeza mwili wa mwanafunzi huyo katika chumba chake.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla (pichani) limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa katika chumba hicho walikuta dripu na dawa nyingine ambazo zinaonyesha kuwa mwanafunzi huyo kifo chake kimetokana na kutaka kujaribu kutoa mimba
 
Nimesikiliza story nzima kutoka radio ebony fm asubuhi hii. Kifupi ni kwamba baada ya msichana kubain kuwa ana mimba aliomba ruhusa aende nyumbani kwa matibabu kwa ugonjwa mwingne. Mara baada ya kupata ruhusa, aliamua kwenda kwa jamaa huyo na walishauriana watoe. Ni baada ya wiki 2 tangu atoke shuleni. Baada ya kutoa mimba hali yake ilikuwa mbaya hvyo kuwa kwa mshkaji huyo akiwa anapata matibabu. Mara baada ya kufariki dunia jamaa akakimbia na kuufungia mwili wa marehemu ndani. Alipofika kusikojulikana aliamua kumpigia mama mwenye nyumba na kumwambia 'FUNGUA NDANI KWANGU NA UCHUKUE MZIGO' mara baada ya mama huyo kufungua ndo akakuta mwili wa mwanafunzi huyo huku kukiwa na madrip na madawa mengine. Mpaka ss baba wa marhm pamoja na kaka yake wamefika shuleni. Taarifa zaidi badae baada ya ndugu hao kujadiliana na uongozi wa shule. Taarifa hii ni kwa mujibu wa walimu wawili waliohojiwa na radio hiyo asubuhi hii.
 
Biblia Takatifu inasema USIZINI,lakini pia inasema WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA,HOSEA 6:1 nakuendelea
 
Naomba wahusika waingilie hili swala banah shule ya IRINGA girls inaongoza kwakutoa mimba!!!!!
 
nini kimeharibu sifa ya hii shule? zamani tukiwa wanafunzi binafsi nikiwa mkwawa ilikuwa nadra kuwapata hawa wanafunzi labda j2 ambapo kuna makutano ya YCS pale kihesa zaidi ya hapo hatuwaoni walikuwa geti kali hata disco ilikuwa mbinde kuwaona na walikuwa na sifa ya nidhamu,labda uongozi mbovu na wanafunzi wenyewe kizazi hiki kupenda ngono kuliko masomo.
namlaumu mwanafunzi wa tumaini kufanya nae mapenzi bila kinga kwani mabinti wadogo bado hawana uwezo wa kungamua madhara yatokanayo.wacha akaozee jela na future yako imeishia hapo.lazima ahukumiwe kwa manslaughter kwani alikusudia hivo na kama hakudhamiria angempeleka hospital.

Ebanaah wale watt wanapenda ngono kuliko kitabu yaani wanarukishwa ukuta usipime wanaogopa mimba kuliko ukimwi!!! Siyo utani ila kuna week kabla ya Christmass nlikuta watt wa Iringa gals kama 6 na uniform wakiingia guest na majamaa bad enough wazee wakubwa ambao ni sawa na baba zao au zaidi!!! Usipime ukimwi wa iringa mnihukumu ila ukimwi iringa ni kutokana na vyuo vya RUCO na TUMAINI am sure 70% wanalo hili tatizo la upungufu wa kinga mwilini....
 
Sometimes malipo ni hapahapa duniani but May God forgive her, na huyo kaka atakimbia kokote lakini he will remain haunted forever mpaka mwisho wake!
 
Sometimes malipo ni hapahapa duniani but May God forgive her, na huyo kaka atakimbia kokote lakini he will remain haunted forever mpaka mwisho wake!
dhambi zote za huyu mdada naomba abebeshwe mvulana..yeye ndio source ya kila kitu
 
Back
Top Bottom