Mpendwa hizi zote ni mifano ya fikra zinazoitwa conspiracy theories.
Kwa jumla hizi zote zinadai kuwepo kwa jamii za kisiri zinazojaribu kutawala dunia.
Na kwa jumla nadharia hizo zote ni fuja na ujinga - pamoja na nadharia yako kuhusu Wayahudi.
Zote hazilingani na dunia halisi bali na haja ya kisaikolojia ya aina fulani ya watu.
Zote zimeshachunguliwa na kuonekana si kweli.
zote zinarudi kwa madai mapya na kupata watu wanaoziamini kwa sababu wanataka kuamini.
Hivyo nadharia hizi zinacheza kwenye uwanja wa aina ya "imani" na hazifikiwi kirahisi na akili.
Mfano bora ni link uliyoleta kuhusu ile "Microsoft empire". Ni takataka tupu. Hakuna ukweli hata kidogo ya kwamba mamake alikuwa Myahudi.
(Mimi sioni ubaya wowote kuwa na mama myahudi lakini si kweli kuhusu Gates!)
Ni rahisi sana kuchungulia dai hili na kupata habari juu ya wazazi wake na mababu.
Ila tu watu kama wewe wanataka "kuamini" na hawachungulii.
Au ulijaribu kutumia dakika 1 tu kuchungulia kama dai hili ni kweli?
Sidhani. Badala yake unaendelea kufuata links za hao vichaa na kusoma uwongo mwinmgi na baadaye unakuja hapa kutangaza "Ninavyojua..."
Sidhani ya kwamba unajua kitu kuhusu mambo haya.
Kipala!
Una-crush kila hoja inayotolewa na wachangiaji kwenye huu uzi bila kutoa suluhisho au wewe unavyofikiri,Mimi ninavyojua kila kitu kinachotokea hapa duniani kina mwanzo wake(kuna watu nyama kila jambo) na hao watu wana ajenda zao/yao kuanzia vita ya kwanza,ya pili,ushoga,vita za Iraq.iran,libya syria na instability yote kwenye jumuia za kiislam,etc.Mi sidhani hv vita vinatokea tu,kuna jambo hapa,Unajua kuwa jina EUROPE ni la kishetani na kwa ajili ya shetani?Unajua pia Vatican ndio engineer mkuu wa shetani, nambo yote yanayotokea duniani kwa sasa yamepangwa huko kabla hayajatokea?