Ipyana Malecela (10 years on) - RIP

Status
Not open for further replies.
Duh!

Ipy daima tutakukumbuka yaani nakumbuka tulionana muda mfupi kabla ya mauti kukufika, nakumbuka ulitokea kwenye mkutano uliokuchagua kuwa Mwenyekiti wa UVCCM siku ya jumamosi ukaja Mgulani JKT hall kwenye harusi ya rafiki yetu sote tukakushangilia na ukahaidi kuwafuata maharusi hotelini asubui ukawape supu kwani ulitaka kuchinja mbuzi asubui yake ilikuwa mida ya saa 6:30 usiku sitokaa ni sahau asubui yake tukapigiwa simu kuwa umetutoka, wengi wetu kwenye ile group yetu hatukuaamini tulidhani ni uongo lakini tulipofika upanga tukakuta ni kweli umetangulia mbele ya haki, ni vigumu sana kuamini kuwa ulitutoka ingawa yalisemwa mengi sana juu ya kifo cha Ipy ila Mwenyezi Mungu pekee ndie ajuae.

:rip: Ipy.... RIP Brother daima tunakukumbuka miaka 10 imepita ila ni kama juzi umetutoka,

Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahala pepma peponi Amen.
 
kibongo zaidi hata kama mtu humjui wewe ni kutoa salamu za pole tu..

RIP Ippy.
 
nilisoma nae Obay primary and they were living just opposite the school kama unaenda st peters,so tulikuwa tunavuka tu barabara kwenda kucheza kwao. he was older thn me alikuwa darasa moja mbele. then life separated us tukaja kukutana ukubwani kidogo, but he was still a brother to me, and a good guy. i rembember vikao vyetu vya jioni pale cocobeach back in the 1990s na washkaji wa obay, chole road na masaki.

RIP Ipi.......
 
Jamaa nilipiga nae kwata pale Ruvu JKT miaka ile ya 83/84. Alikuwa mtu safi sana ila kifo akijui hayo................may be angekuwa fisadi la kutupa...... no body knows lakini alikuwa kijana powa.

Ndugu Kaa la Mto, miaka uliyoitaja hapo juu (1983-84) Ippy alikuwa darasa la sita na la saba Oysterbay. Nadhani ulimaanisha mwaka 1993-94.

Nilisoma na Ippy Oysterbay miaka ya 1978-1984. Alikuwa mcheshi, mtani na asiebagua marafiki. Alipenda kushirikiana na watu wa rika mbalimbali bila majivuno wala kejeli. Na alikuwa rafiki wa kila mtu na alipendwa sana na walimu wote shuleni pale.

Mungu ailaze roho ya Ippy Mkwawi Malecela mahali pema peponi. Amen
 
sawa hata mimi nasikitika sana kwa kifo chake. Ila mbona mafanikio yake ya kijamii ambayo kama ni mazuri hayatajwi?Mchangiaji anasema alikuwa mtu wa watu halafu hafafanui wala hata kutaja mafanikio yake. Nakupa mfano mtu anaposema mtu wa watu. Ehud Barak ambaye kwa sasa ni waziri mkuu-1972 akiwa na miaka 19 aliwaokoa waisrael 200 waliokuwa ndani ya ndege ya sabena iliyotekwa nyara mjini tel aviv. 1973 alikuwa shujaa , aliongoza vizuri kikosi cha vifaru na ni mmoja wa makomando waliosababisha kukomboa mfereji huo. Mwaka 1976 alishiriki katika kikosi cha makomandoo wa Israel walikwenda kuwaokoa ndugu zao pale entebe. Yeyey ndiye aliyechukua uongozi mara baada ya netanyahu kupigwa risasi. hapo alipata medali ya ushujaa pale entebe. Hapo nimekufafanulia vizuri sifa za Ehud na hata wewe mwenyewe umemfahamu vizuri na kumpenda.

Sasa unapotaka watu tukuunge mkono kuhusu Ippy na ushujaa wake huna budi kufafanua accomplishments zake kwa umma. kama ni nzuri, tupo tayari hata kumpatia jina katika mitaa mbali mbali ili akumbukwe daima.
Mkuu tunaambiwa alikuwa mtu fresh hana noma mtu muungwana.....lakini mafanikio yake hayatajwi.....binafsi sioni kama kuna mafanikio ya kujivunia kwa Ippy....kaacha nini ambacho leo hii tumkumbuke zaidi ya ile kinachozungumzwa "alikuwa mtu fresh" zaidi ya member mmoja kusema walikuwa wakigombania mademu!!

Umetoa mfano mzuri mkuu....

Kuna watu leo hii uko walipo watakuwa peponi kwa kile walichotufanyia watanzania...
 
Familia ya Mzee Malecela imepitia mambo magumu sana. Pole sana Mzee na familia kwa yote mliyoyapitia.

Majuzi Nov Mzee alipoteza mjukuu, binti mkubwa tu, an adopted baby of Dr Mwele of NIMR. Sina ujasiri wa kukebehi jambo hili au kufanya mzaha maana kipimo cha uchungu wao wanakijua wao hasa zaidi kuliko sisi.

Faraja ya Mungu iwafunike. Songeni mbele msikate tamaa!
 
Mkuu tunaambiwa alikuwa mtu fresh hana noma mtu muungwana.....lakini mafanikio yake hayatajwi.....binafsi sioni kama kuna mafanikio ya kujivunia kwa Ippy....kaacha nini ambacho leo hii tumkumbuke zaidi ya ile kinachozungumzwa "alikuwa mtu fresh" zaidi ya member mmoja kusema walikuwa wakigombania mademu!!

Umetoa mfano mzuri mkuu....

Kuna watu leo hii uko walipo watakuwa peponi kwa kile walichotufanyia watanzania...
Mkuu ndani ya chama cha magamba, hayo yanawapa influence ndani ya chama, then wanaongoza chama na hatimaye nchi.

It has been happening for 50 years and counting...
 
MziziMkavu,

Kifo chake hakikuwa na utata: Wana familia wanajua/walijua kilichomua mtoto/ kaka yao na ndio maana Dr. John Malecela hakutaka mwili wa mwanae ufanyiwe uchunguzi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ndani ya chama cha magamba, hayo yanawapa influence ndani ya chama, then wanaongoza chama na hatimaye nchi.

It has been happening for 50 years and counting...

Assume kama Nyerere naye angewalea watoto wake kwa style kama wanavyolelewa waliomfuata. May be Makongoro nyerere angkeuwa kwa sasa Ni waziri wa mambo ya Nje anayesubiri kupokea Kijiti cha JMK.

Kwa hiyo jmushi siyo 50 years . It has been happening for 30 years and counting
 
Point taken
 
Mkuu tunaambiwa alikuwa mtu fresh hana noma mtu muungwana.....lakini mafanikio yake hayatajwi.....binafsi sioni kama kuna mafanikio ya kujivunia kwa Ippy....kaacha nini ambacho leo hii tumkumbuke zaidi ya ile kinachozungumzwa "alikuwa mtu fresh" zaidi ya member mmoja kusema walikuwa wakigombania mademu!!

Umetoa mfano mzuri mkuu....

Kuna watu leo hii uko walipo watakuwa peponi kwa kile walichotufanyia watanzania...

Jamani this guy was young mnataka awe aliacha nn khaaa! Alichoacha ni mfano mzuri sana wa jinsi watu tunatofautiana tuna karama tofauti! Yeye ndo alianza mbio za siasa labda mngeachiwa hicho mnachoona kingeandikwa kwenye kumbukumbu du! Mi binafsi sikumjua bali kwa kusoma hapa nimejua alikuwa mtu wa aina gani! Mkae mkijua watu wengine wamezaliwa ivo tu kukubalika kuogopwa si kwa kupiga no. . Mi mmojawapo! Mezeni hilo we do differ wangapi hapa wamemuongelea kwa mazuri ukaliona hilo la kugombea vibinti? Duuu we think so differently. .
 
Ilikuwa mwaka 2002 wakati akisherehekea ushindi wake wa uenyekiti wa vijana wa ccm mkoa wa dar,alikufa ghafla.Ni kati ya vifo vilivyonishangaza,naomba mwenye habari yoyote kuhusu mkasa huo aniongezee hapa maana kuna kitabu naandaa kuhusu magambaz.
 
Bila shaka sikuwa kwenye ulingo wa siasa kipindi hicho ila jina hilo siyo geni masikioni pangu!

Shaka ondoa watau watakuja bila shaka.
CCM NI JANGA KWA TAIFA LETU!

Mwisho wao waja hakika!
 
Bila shaka sikuwa kwenye ulingo wa siasa kipindi hicho ila jina hilo siyo geni masikioni pangu!

Shaka ondoa watau watakuja bila shaka.
CCM NI JANGA KWA TAIFA LETU!

Mwisho wao waja hakika!

Umeongea kwa uchungu sana mkuu,...ucjali yana mwisho mkuu
 
Pasco
Ile ajali aliyoipata Senyagwa ilisikitisha sana.....na hasa kama unakumbuka kisa chake kilivyoanzia.......RIP Senyagwa, RIP Catherine, RIP Ipyana.....
Yeah, nakumbuka hiyo story nikiwa shule, kitu kama mama yao aliwaruhusu "waibe" gari ya mzee Malecela wakati huo Malecela akiwa safarini kikazi nje ya nchi, na Senyagwa akatoka na wasichana wa UD Hall 3 na rafiki zake wengine wakaenda kujirusha, wakala mzinga wakati wakirudi.

Sijui kama walikuwa wamepiga maji au vipi. Wakati huo kuwa na gari ilikuwa ujiko sana, hata foleni kulikuwa hakuna kwa jinsi yalivyokuwa machache.
 
......Mama yao (RIP), alipendekeza wapelekwe na dereva..........lakini walikataa......kilichotokea wakati wanarudi ndio hivyo tena....... RIP my friend Senyagwa na Catherine
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom