Ipyana Malecela (10 years on) - RIP

Status
Not open for further replies.
sawa hata mimi nasikitika sana kwa kifo chake. Ila mbona mafanikio yake ya kijamii ambayo kama ni mazuri hayatajwi?

Mchangiaji anasema alikuwa mtu wa watu halafu hafafanui wala hata kutaja mafanikio yake. Nakupa mfano mtu anaposema mtu wa watu. Ehud Barak ambaye kwa sasa ni waziri mkuu-1972 akiwa na miaka 19 aliwaokoa waisrael 200 waliokuwa ndani ya ndege ya sabena iliyotekwa nyara mjini tel aviv. 1973 alikuwa shujaa , aliongoza vizuri kikosi cha vifaru na ni mmoja wa makomando waliosababisha kukomboa mfereji huo. Mwaka 1976 alishiriki katika kikosi cha makomandoo wa Israel walikwenda kuwaokoa ndugu zao pale entebe. Yeyey ndiye aliyechukua uongozi mara baada ya netanyahu kupigwa risasi. hapo alipata medali ya ushujaa pale entebe. Hapo nimekufafanulia vizuri sifa za Ehud na hata wewe mwenyewe umemfahamu vizuri na kumpenda.

Sasa unapotaka watu tukuunge mkono kuhusu Ippy na ushujaa wake huna budi kufafanua accomplishments zake kwa umma. kama ni nzuri, tupo tayari hata kumpatia jina katika mitaa mbali mbali ili akumbukwe daima.
 
Jamaa nilipiga nae kwata pale Ruvu JKT miaka ile ya 83/84. Alikuwa mtu safi sana ila kifo akijui hayo................may be angekuwa fisadi la kutupa...... no body knows lakini alikuwa kijana powa.

Hiyo miaka ipo sawa? Jamaa alikuwa mbele yangu miaka miwili pale Oyster Bay primary na JKT nilienda 93 operation miezi sita. Nadhani umechanganya miaka
 
aisee jamaa walimchagua tu ccm wakampa mambo malecela alikataa tamaa sana na ccm kwa wakati huo akijua yeye next
Mungu akuweke I.M pema peponi
Jamaa ni mpiganaji alikuwa gangwe mfano alikuwa Mtu wa

watoto Sana.kichwani Slyo good kama Dada zake.na tulikutana tena college uk. Naamini angeweza siasa. Kama angejitenga na. Kinje.he was big with upole mwingi.good lad.
 
Wati wazuri na kipenzi cha watu Mungu huwachukua haraka kuliko wale wabaya na maadui wakubwa wa watu.
 
sawa hata mimi nasikitika sana kwa kifo chake. Ila mbona mafanikio yake ya kijamii ambayo kama ni mazuri hayatajwi?

Mchangiaji anasema alikuwa mtu wa watu halafu hafafanui wala hata kutaja mafanikio yake. Nakupa mfano mtu anaposema mtu wa watu. Ehud Barak ambaye kwa sasa ni waziri mkuu-1972 akiwa na miaka 19 aliwaokoa waisrael 200 waliokuwa ndani ya ndege ya sabena iliyotekwa nyara mjini tel aviv. 1973 alikuwa shujaa , aliongoza vizuri kikosi cha vifaru na ni mmoja wa makomando waliosababisha kukomboa mfereji huo. Mwaka 1976 alishiriki katika kikosi cha makomandoo wa Israel walikwenda kuwaokoa ndugu zao pale entebe. Yeyey ndiye aliyechukua uongozi mara baada ya netanyahu kupigwa risasi. hapo alipata medali ya ushujaa pale entebe. Hapo nimekufafanulia vizuri sifa za Ehud na hata wewe mwenyewe umemfahamu vizuri na kumpenda.

Sasa unapotaka watu tukuunge mkono kuhusu Ippy na ushujaa wake huna budi kufafanua accomplishments zake kwa umma. kama ni nzuri, tupo tayari hata kumpatia jina katika mitaa mbali mbali ili akumbukwe daima.

Ushujaa ni relative; siyo kila shujaa awe na accomplishment kubwa sana kama vile kijeshi au za kiuchumi. Anaweza kuwa na accomplishments za kawaida tu katika jamii yake. Asingekuwa nazo huenda asingekumbukwa na wanaomfahamu.

Vile vile ningekuomba uvute kumbukumbu yako tena vizuri. Ingawa ni Kweli Baraka alishiriki katika operations nyingi za kikomandoo dhidi ya magaidi, ukweli ni kuwa hakusihiriki kwenye operation Thunderbolt kule Entebbe ingawa alishiriki katika kuplani mission ile kutokana na uzoefu wake wa kupambana na magaidi na vile vile kutokana na position yake wakati huo kama Deputy Chief of Intelligence akiwa na cheo cha Kanali.

Yoni Netanyahu ndiye aliyekuwa kamanda wa kikosi kilichokwenda Entebbe akiwa na cheo cha Luteni Kanali; lakini kiongozi mkuu wa misheni hiyo alikuwa na General Dan Shomron ambaye ndiye aliyekuwa anatoa command akiwa kwenye war room kwenye basement ya makao makuu ya IDF huko Tel Aviv. Isingewezekana Kanali Barak aongozwe na Luteni Kanali Netanyahu. Kuna vitabu kadhaa vilivyoandikwa kuhusiana na tukio hilo wakati ule kwa mfano Ninty minutes at Entebbe, Operation Thuderbolt, The Entebbe Rescue na vinginevyo; vile vile kuna documentary na movie kadhaa zilizotengezwa; vyote bado vinapatikana online. Baada ya kifo cha Yoni, mtu aliyechukua command ile alikuwa ni Meja Moshe Betser
 
Tulikuwa tunakwenda tosamaganga sec kucheza basketball na wa Tito's za mjini na tunawafunga.pia tumewaringishia Tito's mwisho wa match ni ngumi mtindo mmoja.ma bus tuliokodi wanatuacha tunapiga azimio la arusha tunarudi kwa mguu na totos zetu na ushindi mjini usiku km kama 15.
 
Jamaa nilipiga nae kwata pale Ruvu JKT miaka ile ya 83/84. Alikuwa mtu safi sana ila kifo akijui hayo................may be angekuwa fisadi la kutupa...... no body knows lakini alikuwa kijana powa.

well ukiacha hiyo comment yako ya ufisadi hujakosea sana,wewe unamuongelea senyagwa samwel malecela ambaye ni kaka yake huyo ipyana na yeye kwa bahati mbaya alifariki 1984 au 1985 kwa ajali ya gari akiwa 1st udsm foe naye alikuwa born leader na mtu poa sana.kwa wote nawapa a big rip????
 
Jamaa alikuwa school mate wangu na rafiki highlands sec school iringa.baba yake mkuu mkoa.tulikuwa tunagombania vidada kwa kwenda mbele.rip rafiki

Eti kaka Ritz umesoma na akima Dani na Stanle Napiya pale Midlands High School.
 
Jamaa alikuwa school mate wangu na rafiki highlands sec school iringa.baba yake mkuu mkoa.tulikuwa tunagombania vidada kwa kwenda mbele.rip rafiki

Eti kaka tz1 umesoma na akima Dani na Stanle Napiya pale Midlands High School.
 
Simfahamu lakini nadhani kufa angali kijana ni pigo kwa Taifa lolote lile, kwani vijana hao ndio ambao future ya taifa inategemea; hasa kwa vile alikuwa ni kiongozi capable. Siku nyingi zimepiga kiasi kuwa majina nimeyasahu lakini mwaka 1981 nilikuwa jeshini Ruvu na mmoja wa watoto wa Malecela wakati akiwa waziri wa mawasiliano; alikuwa kijana mwungwana ingawa sina uhakika kama ndiye huyo.

Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu

Kichuguu sio tuu hauna uhakika kama huyo, bali pia hauna uhakika kama ulikuwa JKT mwaka 1981!.

Huyu unayemdhania ndio yeye siye!.
 
Mungu amlaze mahala pema kijana Ippy. Nakumbuka kama alikuwa anajiandaa kigombea Uongozi UVCCM lakini akafariki ghafla.

Alishagombea na kupata uongozi wa ccm vijana,lakini tukiwa kwenye maandalizi ya party ya kumpongeza tuliyoiandaa pale leaders club ambayo ilikua aje kuwa mgeni rasmi,yeye alipitia pahala kwenye shughuli za kichama asubuhi ya siku ile,sasa akarejea nyumbani akabadili magwanda yao yale ya ccm ndio aje kwenye party akiwa "ameoga",akiongozana na msafara wake yeye pamoja an katibu wake ccm vijana,walipita nyumbani kwake,akawaacha wengine chini akapanda juu kwenda kubadili nguo...hakushuka tena mpaka leo...kufuatia tukio lile kuna watu walitajwa tajwa kuhusika na kifo chake akiwemo Londa,meya wa zamani wa kinondoni na watu wengine waliosemekana kukerwa na ippy kupata nafasi hiyo huku akiwaacha watu waliokimbiza sana mwenge..na waliosotea chama kitambo
 
Jamaa alikuwa school mate wangu na rafiki highlands sec school iringa.baba yake mkuu mkoa.tulikuwa tunagombania vidada kwa kwenda mbele.rip rafiki

Baba yake aliwahi kuwa Balozi, Waziri na wakati huo mkuu wa mkoa lakini jamaa alikuwa Highlands! Bado tulikuwa tuna vimelea vya mwalimu wakati huo na ndio nakumbuka kuna watoto wa mabalozi walirudishwa Tz toka ughaibuni wakaja kwenye shule za serikali. Lakini sasa hao tunawapata kweli? Ukifanya research ya watoto wa WAKUBWA ni wangapi utawapata kwenye shule zetu za huko iringa, Mbeya ama Kigoma?
 
Jamaa nilipiga nae kwata pale Ruvu JKT miaka ile ya 83/84. Alikuwa mtu safi sana ila kifo akijui hayo................may be angekuwa fisadi la kutupa...... no body knows lakini alikuwa kijana powa.
Kaa la Moto, uliyepiga naye kwata hapo Ruvu 83/84 siye yeye bali ni kaka mtu aliyemaliza Tambaza PCM akaibuka na Div 1 kali na akajoin UDSM!.
Ila na huyu kaka mtu naye ni RIP.
RIP Ippy!.
 
sawa hata mimi nasikitika sana kwa kifo chake. Ila mbona mafanikio yake ya kijamii ambayo kama ni mazuri hayatajwi?

Mchangiaji anasema alikuwa mtu wa watu halafu hafafanui wala hata kutaja mafanikio yake. Nakupa mfano mtu anaposema mtu wa watu. Ehud Barak ambaye kwa sasa ni waziri mkuu-1972 akiwa na miaka 19 aliwaokoa waisrael 200 waliokuwa ndani ya ndege ya sabena iliyotekwa nyara mjini tel aviv. 1973 alikuwa shujaa , aliongoza vizuri kikosi cha vifaru na ni mmoja wa makomando waliosababisha kukomboa mfereji huo. Mwaka 1976 alishiriki katika kikosi cha makomandoo wa Israel walikwenda kuwaokoa ndugu zao pale entebe. Yeyey ndiye aliyechukua uongozi mara baada ya netanyahu kupigwa risasi. hapo alipata medali ya ushujaa pale entebe. Hapo nimekufafanulia vizuri sifa za Ehud na hata wewe mwenyewe umemfahamu vizuri na kumpenda.

Sasa unapotaka watu tukuunge mkono kuhusu Ippy na ushujaa wake huna budi kufafanua accomplishments zake kwa umma. kama ni nzuri, tupo tayari hata kumpatia jina katika mitaa mbali mbali ili akumbukwe daima.

kwa vijana walioishi uingereza miaka ya 90 ndio wanaujua msaada wake,aliwasaidia vijana wengi pande zile kwa kuwa tu ni watanzania.hapo ndio utu wake wa watu unapoingia..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom