Ipi sahihi kumwita jina lake au Baba/mama fulani?

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,542
12,404
Waungwana habari za jioni!
Leo nikiwa napumzika baada ya mihangaiko ya kutwa nzima nilipata wasaa wa kukaa na kupumzisha koo kwa kupata moja moto moja baridi!

Tukiwa tunabadilishana mawazo na jamaa zangu hoja ikazuka ipi ni sahihi mkiwa kwenye ndoa hasa pale mkiwa na watoto, je ni sahihi kumwita mke/mume wako jina lake la kwanza au la mwisho au umwite kwa jina la baba/mama nanii!

Utata ukawa wengine wanadai si sahihi kabisa kumwita mwenzi wako kwa jina lake kama mna watoto instead mwite kwa Baba/Mama nanii kwa kuwa ndio heshima.

Nikasema ngoja nilete hii hoja hapa nipate usahihi maana hapa ni jungu kuu!

Naomba kuwasilisha kwa michango.
 
Mfano: Baba anaitwa = Andendekisye MwaipunguMama anaitwa =Atupakisye MwakaswesweMtoto wao anaitwa - Tumpe MwaipunguSwali kuhusu mama: Je, tumwite Mama Mwaipungu au tutumie jina la mtoto na kumwita Mama Tumpe?
 
Mfano: Baba anaitwa = Andendekisye MwaipunguMama anaitwa =Atupakisye MwakaswesweMtoto wao anaitwa - Tumpe MwaipunguSwali kuhusu mama: Je, tumwite Mama Mwaipungu au tutumie jina la mtoto na kumwita Mama Tumpe?

Haha haaa utata sasa hapo!
 
inaonyesha heshima zaidi mkiitana baba/mama fulani; mkiitana majina yenu ni rahisi hata watoto kuwaita hivyohivyo na hivyo kuonekana wanawakosea adabu
 
Mke wangu/mume wangu. . .
MAMA/BABA (fuladni). . .
Anna/Frank. . .
Ni vizuri watu wakiulizana/angalia lipi linampendeza mwenzake kwasababu tunatofautiana. Binafsi lolote naona sawa kwasababu yote yana kitu special ndani yake.
 
mie naprefrer kuita majina halisi.
Asha / Musa

na watoto nimewatajia majina yetu halisi kesho na keshokutwa watoto yakiwapata ya kuwapata wajue majina kamili ya wazazi wao.

Sio mtoto anaulizwa baba yakoanaitwa nani anajibu 'baba asia' mama yako anaitwa nani mtoto anajibu 'mama asia'
 
Back
Top Bottom