Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,937
- 46,690
Suala la Katibu Mwenezi wa Taifa wa CCM, Makonda kuwaitisha, kuwataka majibu na kuwapa maelekezo mbalimbali viongozi wakubwa wa nchi limekuwa gumzo kubwa.
Wengine wakisema hana mamlaka hayo na wengine wakisema anayo.
Bado ni utata kama Katibu mwenezi wa chama mkoa anaweza kumuita na kumpa maelekezo Mkuu wa Mkoa, RPC, Menejea wa mkoa wa TANESCO, TARURA, TANROAD, Mganga mkuu wa mkoa n.k vivyo hivyo pia kwa katibu mwenezi wa Wilaya, Kata na Mtaa/Kijiji.
Iliwahi kutokea huko nyuma katika mkoa wa Arusha katibu mwenezi wa kata alimpigia simu daktari wa Zahanati siku ya sikukuu akimtaka kufika kazini hali iliyopelekea kurushiana maneno na kufokeana sana kati yao na kupelekea gumzo hadi lililopelekea Rais wa chama cha madaktari wa wakati huo kutoa kauli.
Sasa kuondoa sintofahamu hii na utata huu kinachotakiwa ni Msemaji wa Serikali, Matinyi pamoja na Waziri wa TAMISEMI, Mchengerwa kutoka hadharani na kutoa kauli ya pamoja na thabiti nafasi ya wenezi wa chama na mipaka ya mamlaka yao kwa watendaji wa serikali katika kila ngazi.