Inflation rate kwenye uwekezaji wa Mifuko ya UTT

Mech

Member
Nov 13, 2017
96
210
Wakuu habari,

Kuna uzi nilishawahi kuusoma humu ndani juu ya uwekezaji kwenye mifuko ya UTT. Kuna ndugu aliuliza ni kiasi gani anapaswa kuwekeza ili aweze kupata return ya Tshs 250,000 kila mwezi. Jibu likawa ni anapaswa kuwekeza Tshs 30M.

Maswali yangu ni:

a) Je huyo ndugu, akiwekeza hiyo Tshs 30M na kila mwezi akiwa anachukua 250,000, baada ya miaka 5 ijayo hiyo Tshs 30M aliyowekeza haiwezi kutafunwa na Inflation rate?.

b) Kama Tshs 30M haiathiriwi na inflation rate, je ni mbinu gani ambazo zinatumika kulinda thamani ya Tshs 30M ibaki pale pale?.

Kwa yeyote yule mwenye uelewa juu ya hili naomba atupe elimu.

Asanteni.
 
Unajua maana ya inflation rate?

Itatafunwaje na infalation rate wakati UTT wanatoa wastani wa 12% return kwa mwaka na inflation kwa nchi yetu ni around 3% annually?
Wanatoa return ya 12% kwa mwaka, ambayo ni sawa na 1% kwa mwezi. Lakini hiyo 1% ambayo UTT wanaitoa kila mwezi kama faida ya uwekezaji, huyu ndugu anaitoa na kuitumia. Hii ina maana anaacha ile Tshs 30M yake. Sasa hii Tshs 30M anayoiacha si itatafunwa na hiyo 3%?

Au hapa imekaaje?
 
Wanatoa return ya 12% kwa mwaka, ambayo ni sawa na 1% kwa mwezi. Lakini hiyo 1% ambayo wanaitoa kila mwezi, jamaa anaitoa na kuitumia. Hii ina maana anaacha ile Tshs 30M yake. Sasa hii Tshs 30M anayoiacha si itatafunwa na hiyo 3%?

Au hapa imekaaje?
Sasa mzee unataka hela uitafune na ibaki na thamani hio hio kila mwaka? Kama hutaki itafunwe ile hela uwe unairudisha kule kule, au simply zaidi, uwe unarudisha 3% za inflation kwenye uwekezaji, then % iliyobaki ndio unakula, simple as that
 
Nimekuelewa mkuu. Ila hii inflation rate unaisoma wapi mkuu. Maana nimejaribu kugoogle Tanzania inflation rate imeniletea 4.3%
 
Swali makini sana.
Mimi ninavyojua huo mfuko ww Bond fund hiyo pesa unakula na hiyo 30 yako baada ya miaka 3 itaendelea kuongezeka hata kidogo na sio kupungua. Na bado unaweza kuitoa yote kuanzia miezi mitatu ukiwa umeshaiweka.

Kama kunautofauti na ufafanuzi wa kina, nitajifunza kitu kipya.
 
Wakuu habari,

Kuna uzi nilishawahi kuusoma humu ndani juu ya uwekezaji kwenye mifuko ya UTT. Kuna ndugu aliuliza ni kiasi gani anapaswa kuwekeza ili aweze kupata return ya Tshs 250,000 kila mwezi. Jibu likawa ni anapaswa kuwekeza Tshs 30M.

Maswali yangu ni:

a) Je huyo ndugu, akiwekeza hiyo Tshs 30M na kila mwezi akiwa anachukua 250,000, baada ya miaka 5 ijayo hiyo Tshs 30M aliyowekeza haiwezi kutafunwa na Inflation rate?.

b) Kama Tshs 30M haiathiriwi na inflation rate, je ni mbinu gani ambazo zinatumika kulinda thamani ya Tshs 30M ibaki pale pale?.

Kwa yeyote yule mwenye uelewa juu ya hili naomba atupe elimu.

Asanteni.
Kwenye bond fund, pamoja na kuwa na option ya kupata gawio la kila mwezi, hata kama utaamua kuichukua, kuna element ya capital gain unayoipata kutokana na ongezeko la bei ya kipande.

Hivyo ndani ya hiyo miaka mitano unayosema, kama utaamua kuuza vipande vyako, utaviuza kwa bei itakayokuwa sokoni kipindi hicho. Hiyo bei itakuwa ime "account for inflation". Hivyo utapata zaidi ya TZS 30m uliyowekeza.
 
Kwenye bond fund, pamoja na kuwa ba option ya kupata gawio la kila mwezi, hata kama utaamua kuichukua, kuna element ya capital gain unayoipata kutokana na ongezeko la bei ya kipande.

Hivyo ndani ya hiyo miaka mitano unayosema, kama utaamua kuuza vipande vyako, utaviuza kwa bei itakayokuwa sokoni kipindi hicho. Hiyo bei itakuwa ime "account for inflation". Hivyo utapata zaidi ya TZS 30m uliyowekeza.
Shukrani sana, nimepata elimu
 
Kwenye bond fund, pamoja na kuwa na option ya kupata gawio la kila mwezi, hata kama utaamua kuichukua, kuna element ya capital gain unayoipata kutokana na ongezeko la bei ya kipande.

Hivyo ndani ya hiyo miaka mitano unayosema, kama utaamua kuuza vipande vyako, utaviuza kwa bei itakayokuwa sokoni kipindi hicho. Hiyo bei itakuwa ime "account for inflation". Hivyo utapata zaidi ya TZS 30m uliyowekeza.
Hiki ndio ninachokifahamu
 
Sio kila kitu kwa watu wote.

Weka BANK iyo million 30 kisha baada ya miaka 5 itakuwa ile ile million 30?.

Asante.
KAZI ni kipimo Cha utu
 
Nimekuelewa mkuu. Ila hii inflation rate unaisoma wapi mkuu. Maana nimejaribu kugoogle Tanzania inflation rate imeniletea 4.3%
in very simple term , kama inflation rate ni 4.3%pa na wewe unapata 12%pa maana yake net income (12% -4.3% )
ila kama ukipata pahali uwekezaji wako unakupa 4 3% net bas hapo unakuwa unalinda thamani ya fedha yako tuu isipotee ila huna unachopata.ndiyo. maana mabenki yanatakiwa angalau yatulipe 4.3% kama riba ya deposit zetu.
 
Wanatoa return ya 12% kwa mwaka, ambayo ni sawa na 1% kwa mwezi. Lakini hiyo 1% ambayo UTT wanaitoa kila mwezi kama faida ya uwekezaji, huyu ndugu anaitoa na kuitumia. Hii ina maana anaacha ile Tshs 30M yake. Sasa hii Tshs 30M anayoiacha si itatafunwa na hiyo 3%?

Au hapa imekaaje?
Mkiambiwa msome, mnasema hakuna Ajira,...hivi hesabu ndogo kama hiyo nayo ngumu🤔?....🚮

Haya mwambie, awe anachukua 200,000/_,..Hiyo 50,000 ita-cover inflation...
 
Mkiambiwa msome, mnasema hakuna Ajira,...hivi hesabu ndogo kama hiyo nayo ngumu?....

Haya mwambie, awe anachukua 200,000/_,..Hiyo 50,000 ita-cover inflation...
Umejibu kimhemko sana.

Tatizo lako umesoma uzi ili ujibu takataka zilizokujaa kichwani na sio kujifunza upate kuelewa.

Point haikuwa kutoa riba ya 12% na inflation rate ya 4.3%. Point ilikuwa nje ya hiyo 7.7% ambayo unaipata as return, ni namna gani value ya Tshs 30M inabaki pale pale?,

Sasa kwa kuwa una akili mgando bado upo pale pale kwenye return ya 7.7%. Kasome post #9 upate kujifunza kitu, nilikuwa nategemea mtiririko wa maelezo kama haya ambayo watu watajifunza zaidi juu ya huu uwekezaji na sio ujinga wako wa kujifanya mwamba wa hesabu. Na huenda hesabu zenyewe unazohisi unazijua ni kwa sababu ulibahatisha kupata "B" O'level ndio inayokupa kiburi. Halafu hesabu yenyewe ilikuwa Basic Mathematics. Sasa sijui ingekuaje kama ndio ungekuwa umepata "A" kwenye Additional, Advanced & Applied Mathematics .

Nirudi kwenye mada, kwa sasa UTT imekuwa ni mada kubwa sana kwenye upande wa uwekezaji. Hivyo niliianzisha hii mada ili watu waliobobea kwenye mambo ya uchumi wadadavue aina hii ya uwekezaji, na watu wengine tupate kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu Mutual funds with correlation to other factors. Nilitumia Inflation rate as one factor ila kuna factor nyingi sana zinazoweza kuaffects hizi Mutual funds, je ww mtaalamu wa hesabu unazijua?. Au kujua kutoa hiyo Interest ya 12% na inflation rate ya 4.3% ndio unahisi umemaliza kila kitu (Hii si hesabu ya mtoto wa darasa la kwanza)?.

Hii ni siri nakupa "Ukiona swali lililoulizwa ni jepesi sana hata mtoto mdogo anaweza kulijibu kiurahisi, usikurupuke kujibu ili uonekane mwamba, utaaibika kwa kuonyesha ujinga wako, maswali ya aina hiyo huwa yanakutaka ufikirie nje ya box."
 
Wewe ndo umekurupuka, na AKILI zako za kirikiuu...ulishaona wapi utoe faida ya pesa yako uliyowekeza, 12%, na bado investment yako ibaki fixed bila kuathiriwa na inflation ilihari annual return unakula?.... unatumia matako kufikiri 🤔🚮🚮🚮
 
Wewe ndo umekurupuka, na AKILI zako za kirikiuu...ulishaona wapi utoe faida ya pesa yako uliyowekeza, 12%, na bado investment yako ibaki fixed bila kuathiriwa na inflation ilihari annual return unakula?.... unatumia matako kufikiri
Sawa mimi nina akili kirikuu, haya wewe mwenye akili nyingi, hebu tueleze ni factors gani nyingine zinaweza kuaffect Mutual funds ikiwa hiyo interest ya 12% na Inflation rate ya 4.3 remain constant ili sisi wenye akili ndogo tujifunze kwako.

Muda mwingine uwe unaficha upumbavu wako, unajisifu mtaalamu wa hesabu na huwezi kung'amua mambo. Ngoja nikusaidie kwa kutumia akili zangu ndogo za ukirikuu.

a) Kwenye uzi nimeandika muhusika anachukua Tshs 250,000 ikiwa amewekeza Tshs 30M. Hii ni sawa na kusema kila mwezi jamaa anachukua Interest ya 0.83% badala ya 1% ambayo anapewa kila mwezi (12% kwa mwaka).

b) Sasa kila mwezi jamaa ataacha reserve ya 0.17% kwenye gawio lake la mwezi, ila hii 0.17% ambayo muhusika atakuwa anaiacha, itakuwa multiplied mara dufu due to compounding effect (8th wonder of world), ambayo ndio itaenda kucover hiyo Inflation rate.

c) Jamaa anaweza kuchukua Tshs 250,000 kila mwezi na value ya hela yake 30M ikaongezeka. Swali inaongezekaje, ndio lilikuwa lengo la huu uzi.

d) Post #9 imetoa mwanga hiyo Tshs 30M inaongezekaje.

N.B

1. Kama umesoma uzi vizuri, ulikuwa na maswali mawili, swali a) na swali b). Lengo kuu la huu uzi lilikuwa ni swali b) na sio swali a).

2. Majibu yako yanaonyesha jinsi gani wewe ni mbumbumbu ambaye hujui kitu, na bado hautaki kujifunza.

3. Vitu kama hujui uwe unakaa kimya, ufiche upumbavu wako. Nilikupa tittle kwamba huenda O'level ulibahatisha kupata "B" hesabu ila jinsi unavyong'amua mambo nina uhakika ulikula "F+".

4. Majibu yote uliyokuwa unareply umejibu kwa kutumia mihemko na matusi juu ila ulichokuwa unafanya ni kuonyesha upuuzi wako.

Nakupa siri ya 2: "Jifunze kukaa kimya, hamna mtu atajua wewe ni mpumbavu".
 
Back
Top Bottom