Waziri Dkt. Ashatu Kijaji: Zalisheni bidhaa zenye ubora unaohitajika sokoni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ametoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa zote za viwandani kuongeza jitihada za uzalishaji wa bidhaa kwa ubora unaohitajika sokoni na kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali nchini.

"Tanzania ina viwanda 25 vinavyozalisha chuma na bidhaa za chuma kama nondo, mabomba, misumari na seng’enge. Viwanda 16 vinauwezo wa kuzalisha nondo tani 750,000 kwa mwaka ambapo mahitaji nchini ni tani 550,336 na ziada ya tani 199,664 huuzwa nje ya nchi." - Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara

"Tanzania ina viwanda 14 vyenye uwezo wa kuzalisha tani 10,850,000 za saruji kwa mwaka . Mahitaji ya ndani ya nchi ni tani 7,100,000, ziada ya tani 3750,000 inauzwa nje ya nchi hususani nchi za Congo, Rwanda, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji." - Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara

"Uzalishaji wa sukari nchini 2023/24 umeimarika kwa kuwa Tanzania ina viwanda vikubwa 5 vya kuzalisha sukari vikiwemo TPC, Kagera Kilombero, Mtibwa na Bagamoyo vyenye uwezo wa kuzalisha tani 75,000 kwa mwezi. Mahitaji ni tani 38,000 na ziada ya tani 37,000" - Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara

"Mwenendo wa bei za bidhaa muhimu Julai 2023 imeonesha bei ya mahindi, unga wa mahindi, mchele, maharage, viazi mviringo na unga wa ngano imeshuka, bei ya sukari na mafuta ya kupikia ni himilivu, bei ya saruji imeongezeka kidogo, nondo na bati ni himilivu" - Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara

"Natoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa zote za viwandani kuongeza jitihada za uzalishaji wa bidhaa kwa ubora unaohitajika sokoni na kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali nchini" - Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara

"Hatutovumilia kuona mzalishaji, msambazaji au muuzaji wa bidhaa yoyote ile akiongeza kiholela bei ya bidhaa yoyote ile bila sababu ya msingi" - Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara.

"Nawaelekeza Maafisa Biashara wote Nchini waliopo kwenye Halmashauri zetu kuhakikisha mnasimamia ipasavyo bei za bidhaa, ni jukumu letu kuwalinda wazalishaji na walaji pia" - Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara.

F15OgDOXsAMd7Ep.jpg
F15L0rgXoAERGlV.jpg
F15IelZXsAE7RYb.jpg
 
Back
Top Bottom