Inakuwaje mtu anamaliza form six na hajui chuo akasome kozi gani

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,183
3,547
wadau wangu wa elimu ya tanzania nimekuwa nikipokea maoni mengi ya vijana wengi waliomaliza form six wananiuliza
ni kozi gani nzuli inalipa na wengine wakiniuliza nikasome kozi gani ila swali langu ni kwamba inakuwaje mtu anamaliza form six hajui akasome kozi gani
 
Elimu ya tz haikuandai kupata kazi bali inakufundisha kusoma na kuandika, suala la kazi gani baada ya wewe kumaliza shule serikali yetu haijali.
 
Elimu ya tz haikuandai kupata kazi bali inakufundisha kusoma na kuandika, suala la kazi gani baada ya wewe kumaliza shule serikali yetu inajali kwa watu wachache maalum walioandaliwa kwa lengo fulani, mfano mzuri ni Malima na Januari Makamba.
 
kuna mtu alisoma hgl aliniuliza kama anaweza kusoma telecommunications udsm aliniambia amepata divisio1 ya point 9
dahh nikashangaa
 
my observation ni kwamba asilimia kubwa [japo sina exact figures] ya waajiriwa wanafanya kazi tofauti na taaluma zao except for technical jobs like medicine etc.

Kwa hiyo lengo la muuliza swali labda ni kwamba kozi gani inalipa zaidi kwenye market kiajira na kimapato

Lakini pia ukweli ni kwamba Elimu yetu haituandai wala kutujenga kudadisi, kutatua matatizo, kujiajiri nk
 
wadau wangu wa elimu ya tanzania nimekuwa nikipokea maoni mengi ya vijana wengi waliomaliza form six wananiuliza
ni kozi gani nzuli inalipa na wengine wakiniuliza nikasome kozi gani ila swali langu ni kwamba inakuwaje mtu anamaliza form six hajui akasome kozi gani

Kwanza wewe umemaliza form ipi? mbona hata Kiswahili kukiandika ipaswavyo hujui? sio "nzuli" ni nzuri.
 
Ndoto zetu nyingi huwa zinakuwa determined na matokeo na uamuzi wa serikali..Kwa mfano unaweza ukawa na ndoto za kusoma PCM ukapangiwa HGL and vv..Na sasa issue ya mkopo ndo imemaliza kabisa, mtu unaomba kozi yenye uhakika wa kupewa mkopo..So mi sishangai kuulizwa hl swali la nisome nini.
 
Muulize wanamuziki wa bongo fleva na studio wanazo record uone kama hawazijui?ni wa puuzi sana hawafuatilii mambo ya maana wao ni ku shake tu!
 
Back
Top Bottom