Inakuaje!

tamaa ndo zinasababisha haya yote m2 wangu na uaminifu na marumbano ya hapa na pale ndan ya ndoa ndo hupelekea haya kutokea so usishangae sana wanasema asilimia 80 ya walio kwny ndoa hawawez kuhimili mikimiki ya kutoelewana kwa muda mrefu. Ndo husababisha haya kutokea ila tatzo kubwa ni TAMAA
 
Superman kitaaluma unamaanisha experience au uwezo wa kumsoma mtu kisaikolojia??Michango ya kishabiki naamini ni ile isiyo na sababu!Yani mtu anasema tu sio vizuri bila kujua kwanini sio vizuri..kwa niliyoona hapa wengi wametumia upeo wa juu kutetea na kuelezea wanayoamini!Nwy tuendelee na mada!
 
AD is there any place nilosema kuwa yeye kutoka kwake kunasaidia ndoa anayoicheat?? nimetumia neno COWARD yaani mtu asiye na ujasiri wa kuamua lililo sahihi kwake i.e. kama hampendi aliye naye amuache no matter the consequences!

mmhh
hiyo ni mimi nilikuwa najiwazia mwenyewe tuuuu ..
kivipi mtu kutoka nje ya ndoa inasaidia ndoa ??
Hapo kwenye blue nakuunga mkono na asante sana..
 
HAhahahahahahahahah, poooole sana Lizzy,

Umeongea na hao watawa wakakueleza changamoto zao? There is no free lunch...Popote utakapoamua kwenda lazima utalipa nauli tu.. Tofauti ni amount utakayolipa!
Hahaha nauli ya utawa i can afford..ya kua singo tu i can afford..ya mchumba wa milele i can afford ila ya kitanzi nadhani mwisho wa siku naweza kuishia jela!Bora nikae pembeni!
 
Lizzy,

Kwa sisi ambao tumeshatoka na wake za watu naomba tusichangie maana tunaweza kuwa revealed!

Pasaka Njema

BE....Kweli wewe ni real!! Laiti wengi wetu tunagekuwa tunayasema yale yanatoa picha halisi za jinsi tulivyo na tunavyotena. Akina Lizzy na AD wangekuwa na amani.

DC

Babu DC umeona eh? Usijeshangaa huyu akawa condemned kwa hii post yake ambayo wengi wanawezaichukulia juu juu..ukweli unaouma ni kuwa hawa wanaokemea kwa kusimamia vidole gumba na kulaani wengi wao wanayafanya haya..ndio maana ninasema ni vema kina Lizzy na AD wakajua situation halisi ili wakijaingia ngomani wasijekufa kwa presha au kupata strokes wakingali makinda. Tatizo tunataka tuwapambie ukumbi kwa kuziba mashimo kwa vitambaa vizuri vya kupendeza bila kuwapa tahadhari ya wapi pa kukanyaga wapi pa kuacha kwa kuwa ukumbi una mashimo...nawaambia watakapoanguka sisi ndio tutakaokuwa tumewaangusha kwa kutotaka kuwaeleza ukweli juu ya hali halisi................ ingawa haimaanishi kuwa watakuwa wamejua kila kitu la hasha but at least wanayo ramani......a sketched map for that matter.

Jamani jioni njema.
 
Hivi inakuaje mwanamke anaondoka nyumbani kwake anamuaga mume wake ambae ni mzuri as in hamnyanyasi na anajitahidi siku zote kumfanyia mke yaliyo mema..alafu anaenda kukutana na kimada wake ambae nae ni mume wa mtu ambae nae mke wake anajitahidi kumfanyia yaliyo mema?Yani wote wanavunja ahadi zao kwanza kwa kutoka nje ya ndoa zao alafu wanafikia kutamani mpaka kutembea na mume/mke wa mwingine!Watu hawa ambao kuna watu wanawaangalia kama 'rolemodels' kwenye maswala ya maisha tuwachukulieje?

Kuoa au kuolewa siyo kigezo au kikwazo cha kutoka nje ya ndoa au mahusiano
inakuaje hivi?.....inakuwa hivi......kwanza ujiulize ni kwanini watu wanaoana...kuoa
au kuolewa?...je,wanaoa au kulewa na watu halisi wanaowahitaji?kwa kiasi gani wamemshirikisha mungu?....je, wamezingatia nyakati muafaka za kuoa au kuolewa?
je, wamezingatia kanuni na desturi za mahusiano?

okey.....sisi kama ''rolemodels'' tunatakiwa kujifunza tu kumbe kuna vitu kama
hivi na wengi wetu watafanya hivi na wao watakuwa ''rolemodels'' wa matendo
haya.......
 
MJ nimekusoma kikamilifu!Ila kwakweli inabidi tujifunze kuishi na maamuzi yetu...ikishindikana kabisa tuanze upya!

Nyamayao..MJ na Mzee DC asanteni kwakutupa moyo na mafunzo tuliopo nje.Woga upo na nadhani utaendelea kuwepo mpaka tutakapoona matumaini kidogo linapokuja swala la ndoa!Kwa sasa ngoja tuendelee kujifunza na kujitayarisha (just incase tukishawishika siku moja) kutoka kwa mliotutangulia!
 
Hivi inakuaje mwanamke anaondoka nyumbani kwake anamuaga mume wake ambae ni mzuri as in hamnyanyasi na anajitahidi siku zote kumfanyia mke yaliyo mema..alafu anaenda kukutana na kimada wake ambae nae ni mume wa mtu ambae nae mke wake anajitahidi kumfanyia yaliyo mema?Yani wote wanavunja ahadi zao kwanza kwa kutoka nje ya ndoa zao alafu wanafikia kutamani mpaka kutembea na mume/mke wa mwingine!Watu hawa ambao kuna watu wanawaangalia kama 'rolemodels' kwenye maswala ya maisha tuwachukulieje?

Lizzy,

Nimejitahidi kwa juu juu kufuatilia mada yako..nimeona umeleta kama changamoto, lakini mwisho wa siku imekuwa kama kisu kwako,
kwamba hakuna waaminifu duniani..

Kwa haraka haraka, wengi waliochangia kwa namna moja ama nyingine hawajaingia kwenye ndoa, pili, hata waliochangia hii mada na wapo kwenye ndoa, idadi yao ni ndogo ya wewe kupata ukweli halisi..

Kwa hiyo usikatwishe tamaa na maoni ya watu humu ndani, wana-represent percentage ndogo sana ya wanandoa walioko mtaani..
Yes, kuna watu sio waaminifu, wengine by nature, au mazingira n.k
Ila wako wengi tu ni waaminifu..
Ningeshauri, upunguze ku-conceptualize things, later on, u may have a very negative picture of what a proper marriage should be..
yaani utakuwa kama mtu aliyeumwa na nyoka, ukiguswa na jani unaruka..Focus more on the positive sides, trust in the Lord,

Inawezekana tukawa tunadharau uwezo wa Mungu,ambaye ndio aliyeanzisha mahusiano baina ya mke na mume...kwamba He was wrong, bcoz marriages seem not to work out..
Faithfulness is connected to the fear of God..( If you cant fear God, who else?)..na Mungu anakupa wa kufanana na wewe (ukiwa mwanamifu ni more likely utapata mwaminifu mwenzio)..but you have to be careful..(usiendeshwe na hisia)
 
Hahaha nauli ya utawa i can afford..ya kua singo tu i can afford..ya mchumba wa milele i can afford ila ya kitanzi nadhani mwisho wa siku naweza kuishia jela!Bora nikae pembeni!

Mhhh Lizzy,

Ni vizuri kama unaweza kutambua ipi itakuwa nafuu kati hizo nauli. Hata hivyo mzigo wa hiyo nauli ni cumulative...Sina hakika kama unaweza kuulewa vizuri (with certainty) sasa. Hata hivyo kwa level uliyofikia si mbaya!
 
Hivi inakuaje mwanamke anaondoka nyumbani kwake anamuaga mume wake ambae ni mzuri as in hamnyanyasi na anajitahidi siku zote kumfanyia mke yaliyo mema..alafu anaenda kukutana na kimada wake ambae nae ni mume wa mtu ambae nae mke wake anajitahidi kumfanyia yaliyo mema?Yani wote wanavunja ahadi zao kwanza kwa kutoka nje ya ndoa zao alafu wanafikia kutamani mpaka kutembea na mume/mke wa mwingine!Watu hawa ambao kuna watu wanawaangalia kama 'rolemodels' kwenye maswala ya maisha tuwachukulieje?

Lizzy naomba nirudie tena ule usemi ambao siku zote huwa napenda kuwaeleza dada zangu,
ntaongelea kwa mwanaume ambae ametchepuka nje, kwa upande wa akina mama,
wanaotoka nje sijui sababu!
lakini kwetu sisi akina baba ambao tunapenda quick relief baada ya kuzozana na wako mwandani, hii yawezekana kwa namna fulani ikawa inasaidia ingawa sio kwa wanaume wote.
Isitoshe, kutoka nje sio kwamba mkeo humpendi wajameni,
ndo maana mwisho w siku sijengi kibanda kule, ni lazima nirudi home,
na hata kama ikitokea hayo mahusiano kwisha, sijutii kivile................

joto kweli....ngoja nikanyimwagie maji bafuni, narudi.........
Baba Enock anaweza akaendelea hapo nilipoishia..................
 
dahhh
kwa kweli tuajiwekea Mentality mbaya sana kichwani..
very soon kutakuwa hakuna tofauti ya kuwa na ndoa au kuwa Single..
na maana halisi ya ndoa haitakuwepo..

AD,

If you can afford it...baki single.

Ila mimi niliwahi kuwaeleza hapa hapa kuwa hata ungeniamsha ndotoni...ni heri kuuubeba huu mzigo wa ndoa kuliko kubaki single. Tatizo ni kwamba sijui yeye bibi anaonaje! But I am better off katika ndoa kuliko kuishi maisha ya kutanga tanga kama njiwa! No please...Nauli ya kwenye ndoa so far (with more than 10 yrs) ndo the cheapest kwangu!
 
BE....Kweli wewe ni real!! Laiti wengi wetu tunagekuwa tunayasema yale yanatoa picha halisi za jinsi tulivyo na tunavyotena. Akina Lizzy na AD wangekuwa na amani.

DC

DC/Nyamayao/Lizzy:

Honestly, maisha ya ndoa hayana formula. Haya maeno "... kumfanyia mke yaliyo mema.." yana maana pana sana..

Kwa kipimo changu naamini Mama Enock "namfanyia yaliyo mema", lakini jambo tunalosahau ni kuwa, Ni vigumu sana "kusoma ubongo wa mwanadamu na kutambua ni mambo gani ambayo yeye anayaona kuwa mema".. Na hapo ndipo tatizo kubwa linapoanzia..

Kwa mfano, ninaye rafiki yangu mmoja humtendea mke wake yafuatayo:
- Akitoka kazini, straight home
- Kila siku ya mapumziko hukaa na mkewe 24/7
- Mara kwa mara zawadi za aina mbalimbali umnunulia (weekly)
- Unywa pombe akiwa na mke wake tu
- Simu za mkononi ni shared property
- e.t.c, e.t.c, e.t.c

Siku moja nilimwambia naenda Unguja kikazi, akaniambia angenituma nimletee zawadi kwa ajili ya mkewe, but, mkewe alikuwa amesafiri kwenda Unguja pia...

The next evening nafika Unguja, nikachukua, chumba Marsons Hotel, na straight nikaingia mtaani (Mercury then Garage), to my astonishment, nlimkuta kaunta pale Garage akila laivu denda na jamaa ambaye ni jirani yetu maeneo ya Bunju...! And, above all walikuwa wamepanga chumba kimoja..!!!

Ni vigumu kukubalika, lakini mara zote, jaribu kufahamu ni nini ambacho mwenzio ana-"perceive" kuwa ni "chema" kutoka kwake mwenyewe, do not assume - assumptions za kutenda mema ndiyo zinafanya watu wanatoka na wake/waume za watu...
 
Mhhh Lizzy,

Ni vizuri kama unaweza kutambua ipi itakuwa nafuu kati hizo nauli. Hata hivyo mzigo wa hiyo nauli ni cumulative...Sina hakika kama unaweza kuulewa vizuri (with certainty) sasa. Hata hivyo kwa level uliyofikia si mbaya!
Ngoja nibaki kwenye bus nililomo kwa sasa..nikiona umuhimu wa kubadili kituo au usafiri hapo baadae mahesabu ntapiga wakati huo huo!Until then...let me enjoy what i have instead of mourning for what i don't!
 
Back
Top Bottom